SIKU moja
baada ya kukumbana na kipigo cha mabao 3-0 kutoka kwa Yanga, Kocha Mkuu wa
Rhino, Jumanne Chale amesema wako baadhi ya wadau we mkoa we Tabora wanachangia
timu hiyo kutofanya vizuri.
Chale
amesema amekuwa akishangazwa na kuona baadhi ya mashabiki au wadau wa soka
katika mkoa huo wakifanya kila juhudi kuzisaidia timu za wageni.
“Wanaona
Yanga, Simba au timu nyingine ndiyo wanapaswa kuzisaidia. Lakini wanasahau wao
wako hapa Tabora.
“Hata kuziona
timu nyingine ni kwa kuwa Rhino iko ligi kuu. Ikiteremka wataziona wapi Yanga
na Simba, kweli inanishangaza sana,” alisema akionyesha kutokukubaliana na
suala hilo.