Mtangazaji wa Mpanda
FM Radio aliyerusha live tamasha kutokea Katumba
Waandaaji wa tamasha hilo,
wakiongozwa na meneja wa Mpanda FM Radio (mwenye suti), walinzi wa usalama
wakijaribu kuweka utaratibu sawa wakati Rose Muhando akitaka kushuka kwenye
gari yake huku mamia ya mashabiki wakiwa wamerizunguka gari lake
Gari iliyombeba Rose Muhando ikiingia
kwenye uwanja wa Mnyaki, hapa ni nje ambapo baadhi ya watu walikuwa wakisubiri
kumwona Rose kwanza ndio waingie
Baadhi ya wapenzi wa muziki wa injili
na Rose Muhando waliofika mapema uwanjani hapo kujionea burudani ya kusifu na
kuabudu kwa njia ya nyimbo
wana-makazi ya wakimbizi katumba waliohudhuria
Rose Muhando akienda kumpa zawadi
binti aliyemvutia, alimkabidhi tshs 20,000 taslimu ili akanunue viatu. Kitendo
hicho na promo alizompa binti huyo vilisababisha kutunzwa na watu wengi
aliporudi kucheza mara ya pili kwa kuitwa tena na Rose, na kwa hesabu ya haraka
haraka binti huyo aliyekuwa na bahati siku hiyo aliondoka na kiasi
kisichopungua tshs 45,000/-
Mtangazaji wa Mpanda FM Radio akiteta
kitu na Mkurugenzi wake wakati Rose Muhando akifanya vitu vyake stejini
Rose akiwa na binti aliyemvutia kwa
kujitoa kwake na jinsi alivyoweza kucheza nae wakienda sawa bila kuwa na aibu
Ni kama amesusa baada ya DJ kuchanganya mambo na kuzima
muziki huku Rose akiwa katikati ya burudani na mzuka ndio umepanda
No comments:
Post a Comment