Hahahahaaaaaaaa! Nimefurahi sana kwa maswali yako na nimelazimika kukujibia hapa japo wewe umeni in box! Huenda wako wengi wenye maswali kama yako dhidi yangu!
Ki ukweli hata mimi niliisikia hiyo radio interview kama uliivyoiita! Lakini mimi naamini ukitukanana na mtoto wote mtaonekana mna akili za kitoto! Mimi naamini kila palipo na nia njema moyoni kuna mkono wa mungu Na kuhusu Mshikamano Arts Group hawajapoa kama unavyodhani,wanaendelea na harakati kama kawaida kwa sababu fulsa walizonazo kama kundi ni nyingi na zinaongezeka kila siku! Ingawa nimedokezewa kuwa “eti”kuna jitihada za wazi kuwadhoofisha hapa mjini (hahahahaaaa!) Niandikapo post hii wako katika ziara ya maonesho maalumu mkoani Rukwa,walianzia Kakese Mpanda tarehe 7/11 ingawa baadhi yao walilazimika kubakia mpanda kwa ajili ya sherehe za LATCU then wakawafuata wenzao, lakini pia wamefanikiwa kutengeneza tamthiria itakayokuwa ikiruka Azam Two kwa jina la MOTO WA YAKA wakishirikiana na Dodo Arts ya Dar-es-salaam kila siku ya alhamis saa tatu usiku,pia kwa mara ya kwanza wameweza kutengeneza komedi ambayo tunaamini itakuwa gumzo hapa mjini! Na mengine mengi ambayo yako sirini,
Kuhusu makundi ya sanaa mimi sijawahi kuwa na bifu na kundi lolote kwa sababu mimi ni mwanaharakati wa masuala ya kijamii na vijana ndio issue yangu kuu! Nashirikiana na kundi la Mshikamano kwa kua ndio kundi ninalofanya nalo kazi lakini nimejaribu mara kadhaa kuwaunganisha wasanii hapa katavi ili washirikiane na kufanya sanaa kuwa kazi yao na si kuendekeza majungu!
Kimsingi nimekuwa nikiwahimiza wasanii wa mshikamano kufanya sanaa kama mradi wao wa maendeleo na si kufanya sanaa ya mashindano ya nani zaidi! Ukiona mtu anafanya sanaa ili akushinde na aonekane mbele ya jamii kwamba yeye ni mkali kuliko wewe huyo hajitambui achana nae we fanya vizuri ili ulipwe vizuri na kazi yako ndio itakutangaza na jamii itajua nani zaidi hata bila kupiga kelele maana hatuuzi sura ila tunauza kazi yetu ya sanaa ili tujikwamue kiuchumi pia!
Kwa kawaida kundi huwa haliyumbi wanaoyumba ni wanakikundi ndio maana hata Tanzania ipo ingawa mawaziri wana badilika kila mara kutokana na sababu mbalimbali! Mimi kazi yangu ni kuratibu kazi ya vijana na kuhakikisha ndoto zao zinatimia,
Nawasisitiza wasanii wote wa mkoa wetu wa katavi kukaa chini na kufikilia zaidi ni jinsi gani wanajikwamua kiuchumi ili wamudu viwango vya kazi zao na kuleta tija waachane na wababaishaji wachache wanaopenda sifa na kujikweza! Na pia wawe na moyo wa kusameheana kwani riziki ya mtu huja kupitia mtu mwingine hivyo nikijenga chuki na wewe sijui mungu amepanga uwe nani kesho! Pia tutendeane vile vimpendezavyo mungu ili mkono wake uwe mbele ya kazi zetu!
Asante sana na mungu akubariki, ada ya mja hunena “uungwana ni vitendo”
|
MSHIKAMANO KAZINI |
NI HAYO TUU KAZI KWENU WADAU TOA COMENT YAKO HAPA CHINI
No comments:
Post a Comment