Tuesday, 21 October 2014

Msanii YP wa TMK Wanaume Family afariki dunia


YP
                                                           YP (kulia)

Msanii wa kundi la TMK Wanaume Family, YP amefariki dunia usiku wa jana katika hospitali ya Temeke baada ya kusumbuliwa kwa muda mrefu na ugonjwa wa kifua.
 kiongozi wa kundi hilo, Said Fela, amethibitisha msiba huo na kusema ratiba kamili itatoka leo mchana.
“Mpaka sasa hivi bado hatujaandaa ratiba, tunasubirika kaka yake kwa sababu huyo mtu kafariki usiku hospitali. Kwahiyo ndugu zake wakishakuja ndo watasema tunazikaje, kwa sababu alikuwa mkristo. Kwahiyo kwenye saa 7 mchana ratiba itakuwa tayari,” amesema Fela.
“Tatizo alikuwa anaumwa kifua muda tu, lakini alishaanza kunywa dozi lakini majuzi akazidiwa na tukampeleka hospitali. Jana ndo mwenyezi Mungu kampenda zaidi akamchukua. Wazazi wa marehemu wapo Keko pale, lakini wazazi wake baba na mama walifariki ila ndugu zake wapo, na kuna kibanda waliachiwa na wazazi wake, kwahiyo msiba utakuwa Keko.”

MUONGOZAJI WA FILAMU BENII OTIENO AFARIKI DUNIA



 
Mdogo wa aliyekuwa muigizaji na muongozaji wa filamu marehemu George Otieno ‘Tyson’ aitwaye Benson Okumu Otieno 'Benii' enzi za uhai wake.
Mdogo wa aliyekuwa muigizaji na muongozaji wa filamu marehemu George Otieno ‘Tyson’ aitwaye Benson Okumu Otieno 'Benii' amefariki dunia ghafla katika Hospitali ya Jeshi ya Lugalo, Dar mchana leo. Msiba upo Sinza Vatican
Benii alikuwa muigizaji na muongozaji wa filamu mbalimbali nchini. Mipango ya mazishi ya kumpeleka kwao Kenya

ALIYEUAWA NA KOMANDOO WA JWTZ MSIBA WAKE WAZIZIMA


INAUMA sana! Baadhi ya ndugu waliokuwa wakiuaga mwili wa Aron Kihundwa (28) kwenye Hospitali ya Taifa Muhimbili, Dar walijikuta wakidondoka na kuzimia kufuatia uchungu wa kumpoteza mpendwa wao huyo aliyedaiwa kuuawa na Komandoo wa Jeshi la Wananchi wa Tanzania, Octavian Mgowele.
Aron Kihundwa akiwa mahututi hospitali kabla ya kifo chake.
Tukio hilo lilijiri wiki iliyopita na kumfanya Mchungaji  Elaina Msuya wa Kanisa la KKKT aliyekuwa akiongoza misa ya kumuombea marehemu huyo, kuingilia kati na kusema mwili usiendelee kuagwa ili kuzuia watu kuzidi kuzimia.
Komandoo Octavian Mgowele mwenye cheo cha Luteni wa Kikosi cha 94 KJ Ngerengere, Morogoro, Oktoba 13, mwaka huu alidaiwa kumuua Aron kwa kumpiga kipigo kibaya.Tukio hilo lilidaiwa kutokea kwenye baa iitwayo Mbondela iliyopo Yombo - Buza maeneo ya Kipera, jijini Dar kwa madai kwamba alikuwa akimbughudhi mke wa komandoo huyo.
Taarifa toka kwa mtu aliyekwepo kwenye baa hiyo zinasema siku hiyo mjeshi huyo alikaa meza moja na mkewe ambaye alitoka kufunga naye ndoa jana yake. Pia kwenye meza hiyo  alikaa Aron huku wakiendelea kunywa bia ambapo mnunuaji mkuu alikuwa komandoo.
Marehemu Aron Kihundwa enzi za uhai wake.
Ikadaiwa kuwa, kuna wakati komandoo alikwenda kaunta aliporudi alishangaa kumkuta mkewe amehama katika kiti alichomuacha.Chanzo hicho kikaendelea kusema komandoo huyo alimuuliza mkewe kisa cha kuhama kiti, naye akamjibu; si huyu rafiki yako ananisumbua.’
Wakati huo, marehemu alikuwa anauchapa usingizi kutokana na kulewa.
“Marehemu akiwa usingizini alishtukia komandoo akimwadhibu bila kujua sababu ni nini hadi akamjeruhi.
”Baada ya kumpiga sana hadi kumjeruhi tulimchukua marehemu na kumpeleka Kituo cha Polisi Chang’ombe (Dar) na kupewa PF3, tukamkimbiza Hospitali ya Temeke,  ilipofika saa kumi usiku wa kuamkia kesho yake alifariki dunia.
“Aron ni rafiki yake sana komandoo, hata siku ya ndoa yake, yeye ndiye aliyempambia gari la harusi na ukumbi. Siku ya tukio ilikuwa ni sherehe ya kuvunja kamati.
“Hatujajua ni kwa nini komandoo aliamua kumpiga Aron kiasi kile, mambo ya kuambiwa na mwanamke siyo ya kuyafanyia kazi kama haukushuhudia ama hauna uthibitisho,” alisema shuhuda huyo.
Marehemu Aron alizikwa Oktoba 18, mwaka huu kijijini kwao Kyengia Wilaya ya Siha mkoani Kilimanjaro.

ANASWA AKIMTEKA MTOTO WA SHULE


HALI bado tete! Polisi wa Kituo cha Magomeni jijini Dar, wamemkamata baba mmoja aliyetambuliwa kwa jina moja la Omar baada ya kupokea kipigo ‘hevi’ kutoka kwa raia wenye hasira kali akihusishwa na utekaji wa denti wa Shule ya Msingi Mwalimu Nyerere iliyopo maeneo hayo.
Denti wa Shule ya Msingi Mwalimu Nyerere, Magomeni (mwenye sare za shule) aliyenusurika kutekwa na njemba inayotambuliwa kwa jina moja la Omar.
Tukio hilo lililokusanya kadamnasi lilijiri wikiendi iliyopita, Magomeni-Kagera, Dar wakati mwanafunzi huyo akitokea shuleni.Kwa mujibu wa mashuhuda, denti huyo alipofika eneo hilo, baba huyo alimsalimia na baada ya kujibiwa salamu yake alianza kumchombeza kwa maneno matamu-tamu.
 Baadhi ya raia wenye hasira kali waliotoa kipigo ‘hevi’ kwa Bw. Omar wakiwa wametanda eneo la tukio.
Akizungumza  denti huyo aitwaye Laila alisema licha ya kuitikia salamu ya jibaba huyo na kumuamkia bado aliendelea kumchombeza na kila alipojaribu kumkwepa ilishindikana.Makamanda wa Polisi waliofika eneo la tukio kumuokoa mtuhumiwa.
Njemba huyo alivuka mipaka na kumshika mkono na kutaka kumvutia ndani ya gari lililokuwa karibu yake ndipo Laila alipoamua kupiga mayowe ya kuomba msaada na hatimaye kuokolewa na wasamaria wema waliokuwa wakipita njia.”
Mtuhumiwa (Omar) akiwa ndani ya gari mara baada ya kipigo.
Mwanafunzi huyo aliendelea kusema: “Alianza kunifuatilia tangu kule, akanisalimia hujambo nikamjibu sijambo, akaniambia tena kwenu hawajambo, nikamjibu hawajambo, akaendelea kuniambia eti, nimfuate akanipe lambalamba, mimi nikakataa kwa sababu mama alinikataza kukubali kupewa lifti na vitu vingine kutoka kwa watu nisiowajua tangu aliposikia habari za watoto kutekwa na Noah nyeusi.Wasamaria wema wakimuokoa mtoto huyo.
“Kila kitu nilimkatalia lakini yeye akawa anaendelea kuniambia maneno yake na kuanza kunivuta ndipo nikaona sasa naenda kufa hivyo ikanibidi nipige kelele ndiyo watu wakatokea na kumkamata kisha kuanza kumpiga mpaka walipofika polisi.”
Mmoja wa wasamaria wema akimuingiza binti huyo kwenye gari kumuondoa eneo la tukio.
tulilizungumza na mtuhumiwa aliyekuwa amehifadhiwa ndani ya gari, alipoulizwa kuhusiana na tuhuma hizo alimuomba paparazi wetu kabla ya yote kwanza amuokoe na kifo kutoka kwa wananchi wenye hasira kali.Binti akiwa kwenye gari mara baada ya kuokolewa.
“Chondechonde ndugu yangu, naomba kwanza mnilindie usalama wangu, hao jamaa wanataka kuniua bila sababu, mimi wala sikuwa na nia mbaya na huyo binti wananizushia tu, nilikuwa namsalimia tu,” alisema Omar kupitia upenyo mdogo wa juu ya dirisha la gari alilohifadhiwa.

Monday, 20 October 2014

Magazeti ya leo October 20 2014 Udaku, Michezo na Hardnews

 Chukua muda wako kupitia kila kilichoandikwa kwenye kurasa za mbele za magazeti ya leo.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.

Matokeo Ya Mechi Za Premier League League 19/10/2014

Matokeo Ya Mechi Za  Premier League League 19/10/2014