Wednesday, 1 October 2014

ILIVYO NGUMU SIMBA SC KUEPUKA KUUA KIPAJI CHA MANYIKA JR WANAJUA KABAL FARAJ NA ABUU HASHIMU


MWAKA 2001, waliokuwa makocha wa timu za taifa za vijana, Mnigeria Ernest Mokake na mzalendo Juma Matokeyo (wote marehemu) walifanikiwa kuibua vipaji vingi, ambavo vilikuwa tegemeo la taifa kwa karibu muongo wote uliopita.
Miongoni mwa nyota waliobuliwa ni kipa Juma Kaseja, viungo Haruna Moshi ‘Boban’, Nico Nyagawa na mshambuliaji Mussa Hassan Mgosi.
Kaseja akiwa na wenzake hao baada ya kung’ara na timu ya taifa ya vijana chini ya umri wa miaka 17, kwa uwezo wao wakasajiliwa na timu za Ligi Kuu.
Peter Manyika kipa chipukizi wa Simba SC anayehitaji kukuza kiwango chake, lakini anakabiiwa na changamoto ya ushindani wa namba dhidi ya makipa wazoefu, Ivo Mapunda na Hussein Sharrif 'Cassilas'
Kaseja alikwenda Moro United, Haruna alikwenda Coastal Union ya Tanga wakati Mgosi na Nico walikwenda Mtibwa Sugar.
Mwishoni mwa mwaka 2002, Kaseja akasajiliwa Simba SC na kuanza kudaka msimu wa 2003. Simba SC ilimsajili Kaseja baada ya aliyekuwa kipa wao hodari enzi hizo, Mwameja Mohamed kustaafu.
Mwameja alistaafu vizuri akiiacha Simba SC na mataji matatu, Kombe la Tusker, ubingwa wa Ligi Kuu ya Muungano na Kombe la Kagame au Klabu Bingwa Afrika Mashariki na Kati.
Katika msimu wake wa kwanza, Kaseja aliifikisha Simba SC Fainali ya Kombe la Kagame mjini Kampala, Uganda, ikafungwa 1-0 katika fainali na wenyeji SC Villa.
Tangu hapo, Kaseja akawa ‘Simba One’ na akaiongoza vyema klabu hiyo katika Ligi ya Mabingwa Afrika akiifikisha hatua ya makundi kwa mara ya kwanza na ya mwisho hadi sasa.
Kabla ya hapo, klabu ya Tanzania kuwahi kucheza hatua ya makundi ya Ligi ya Mabingwa Afrika ilikuwa Yanga SC mwaka 1998.
Kaseja amekuwa kipa kipenzi cha wana Simba na tegemeo kwa muongo wote uliopita- kabla ya mwaka 2009 kuhamia Yanga SC kwa Mkataba mnono wa mwaka mmoja, ambao ulipoisha akarejea Msimbazi.
Amedaka Simba SC na kuendelea kuipa mataji hadi mwaka jana alipotemwa na kwa bahati nzuri akasajiliwa tena Yanga SC.
Kaseja ameingia kwenye orodha ya makipa wenye mafanikio Tanzania akiwa ameshinda mataji na klabu mbili kubwa, Simba na Yanga pamoja na timu ya taifa.
Juma Kaseja kushoto aliiongoza Simba SC kucheza hatua ya makundi Ligi ya Mabingwa Afrika katika msimu wake wa kwanza 2003 kabla ya gwiji wa klabu hiyo 

Kaseja alipata bahati ya aina yake, kutoka U17 kwenda Moro United ambako aliaminiwa na kupewa nafasi akang’ara hadi kuonekana Simba SC alikoingia na kufanya vizuri hadi sasa anaitwa gwiji.
Katika kikosi cha sasa cha Simba SC, wachezaji 11 wanapokuwa uwanjani, kwenye benchi anakuwapo kipa mmoja chipukizi, anaitwa Peter Manyika.
Huyo ni mtoto wa kipa maarufu na bora wa zamani nchini, Manyika Peter aliyewika Taifa Stars na klabu za Yanga SC na Mtibwa Sugar.      
Manyika mdogo ana umbo zuri la ukipa, anajua kudaka na unaweza kumuita hodari awapo langoni.
Lakini katika Simba SC, ni kipa wa tatu baada ya Ivo Mapunda na Hussein Sharrif ‘Cassilas’.
Huyo huwezi kumfikiria kudaka leo wala kesho, labda itokee bahati mbaya sana wakati huu ambao kipa namba moja, Ivo ni majeruhi, na Cassilas naye apate udhuru wa kuumia au kusimamishwa.
Lakini kama haitatokea bahati mbaya hiyo- ina maana Manyika mdogo ataendelea kudaka mazoezini tu na labda mwishoni mwa mwaka ataidakia Simba B katika Kombe la Uhai.
Amepitia kwenye msingi mzuri wa soka akianzia kuwa kipa namba moja wa U17 na kipa namba moja wa U20- na uwezo wake umewavutia wengi.
Kabali Faraj alikuwa kipa namba moja wa U20 ya nchi ambayo ilikuwa inaundwa na akina Mbwana Samatta na Thomas Ulimwengu, wakati huo huo kipa wa kwanza wa timu ya vijana ya Simba SC. Alikuwa miongoni mwa nyota waliokuwa wakiibukia vizuri wakati huo na akatabiriwa kufika mbali.
Na wakati huo, kikosi cha kwanza cha Simba SC kilikuwa ina makipa Kaseja na Ally Mustafa ‘Barthez’ ambao wote sasa wapo Yanga SC- leo hii Samatta na Ulimwengu wakiwa TP Mazembe, sijui Kabali yuko wapi. Hasikiki tena kwenye viwanja vya soka.
Abuu Hashim ameipa mataji Simba B na alidaka vizuri timu hiyo ikicheza na timu za wakubwa za Ligi Kuu zikiwemo Mtibwa Sugar na Azam FC katika michuano ya BancABC mwaka juzi na kuipa timu Kombe hilo lililofanyika mara moja.
Baada ya hapo, akapandishwa Simba A na kuna wakati alipewa mechi za Ligi Kuu na kudaka vizuri. Leo sijui yuko wapi Abuu.
Ukweli ni kwamba ni vigumu mno kwa chipukizi kuanzia timu kubwa na kufanikiwa- wachache sana wanaofanikiwa, kwa sababu viongozi wetu hawana subira.
Mbaya zaidi klabu zetu kubwa hazifikirii sana kumpandisha mchezaji, ingawa Simba SC na Azam FC kwa sasa wanajaribu hiyo- ukiwa kipa wa pili au wa tatu, daima utaendelea kuchukuliwa hivyo. 
Kipa wa kwanza akiyumba kidogo, watu hawafikirii kipa wa pili au wa tatu, wanatafuta kipa mwingine kutoka nje na ndiyo maana leo Kabal na Abuu hawapo Simba SC kuna Ivo na Cassilas.
Ili kukuza kiwango chake, Manyika mdogo anahitaji kupata mechi za kucheza akusanye uzoefu, nafasi ambayo ni vigumu kuipata Simba SC kwa sasa. Lakini huyo ni kipa ambaye ukiondoa Simba yenyewe, Azam na Yanga SC- klabu nyingine yoyote ya Lgi Kuu itatamani huduma zake.
Ni juu yao Simba SC kumtoa kwa mkopo mchezaji huyo akapate uzoefu timu nyingine, au kuendelea kuwa naye ili baadaye ije kumtupia virago kama ilivyokuwa kwa Kabal Faraj na Abuu Hashimu. 

BREAKING NEWS: EBOLA YATUA NCHINI MAREKANI


Ugonjwa wa Ebola bado unapasua vichwa vya wanasayansi walio wengi katika kuutafutia chanjo ama tiba ili kukabiliana nao, ingawa mpaka sasa walau kuna matumaini ya dawa ya Zimapp.

Mgonjwa wa kwanza ametambuliwa nchini Marekani eneo la Dallas, Texas mahali amabako utafiti wa kilimo unafanyika .

Mgonjwa huyo aliyegunduliwa bado hajatambuliwa na ametengwa kwa uchunguzi ili kumfuatilia na kuepusha kuambukiza watu wengine.Mtu huyo ametambuliwa jinsi yake kuwa ni mwanamume na alipata uambukizo nchini Liberia na hii ni baada ya kuonesha dalili zote za ugonjwa huo.

Mwanamume huyo anaripotiwa kuondoka nchini Liberia mapema mwezi September na kufika mjini Texas siku iliyofuatia bila ya kuonesha dalili za uambukizo wa virusi hatari vya ugonjwa wa Ebola.Mkurugenzi wa ufuatiliaji magonjwa na udhibiti nchini Marekani Thomas Frieden aliwaambia waandishi habari mapema wiki hii kwamba wote waliotembelea nchini Liberia waligundulika na virusi vya ugonjwa huo nchini Marekani

Mpaka sasa watu zaidi ya 3,000 wamefariki dunia huko Africa Magharibi, na baadhi ya wafanyakazi wa kujitolea kutoka nchini Marekani wamepata ahueni baada ya kurejeshwa nchini Mwao pindi walipogundulika kuwa na dalili za awali za ugonjwa huo.

via bbc

HIVI ULIIPATA ISHU YA RAILA ODINGA KUTIWA BAKORA???

Hali ya taharuki iliibuka katika mkutano wa hadhara katika jimbo la Kwale nchini Kenya, baada ya mwanamume mmoja kwenda ukumbini na kuanza kutandika bakora kiongozi wa upinzani Raila Odinga pamoja na wanasiasa wengine.
Raila alikuwa amejiunga na kikundi cha wanawake waliokuwa wanacheza densi ya kitamaduni kuwatumbuiza wageni, pamoja na gavana wa jimbo la Kwale Pwani ya Kenya Salim Mvuruya katika mkutanmo wa kisiasa.
Walikuwa wameambatana na viongozi wengine, wakiwemo, Seneta Juma Boy, Hassan Omar, Agnes Zani, James Orengo, Johnstone Muthama na wengineo.
Mwanamume huyo alimshambulia Odinga ambaye ni waziri mkuu wa zamani na kumchapa mara mbili kabla ya kumgeukia gavana wa jimbo hilo na pia kumchapa mara mbili. Hata hivyo mwanamume huyo alishindwa nguvu na walinzi wa Raila Odinga.
Polisi walithibitisha kuwa walimkamata mwanamume huyo na kumwachilia baada ya kugundua kuwa alikuwa na matatizo ya kiakili.
Haijulikani kwa nini mwanammume huyo alimshambulia Raila ila baadhi wabnasema ni kwa sababu alighadhabishwa pale waziri mkuu alipocheza densi na mwanamke aliyesemekana kuwa mke wake ambaye alikuwa katika kikundi cha wanawake waliokuwa wanawatumbuiza wageni waheshimiwa.
Viongozi waliofika walilazimika kusitisha densi hiyo kabla ya mwanamume huyo kushindwa nguvu.

WAZEE WALALAMIKIA KUNYANYAPALIWA NA WAHUDUMA WA AFYA

Wazee wakiwa kwenye kongamano la wazee kwenye ukumbi wa mikutano wa Halmashauri ya Mpanda kujadili changamoto zinazowakabili wakati wa kupatiwa matibabu.
.
Wahudumu wa Afya wameendelea kuwanyanyapaa wazee wawapo hospitalini kupata huduma ya Afya kwa kuwaacha wakae asubuhi hadi jioni ,huku wenyewe wakifanya kazi zao nyingine.
Pia wakitibiwa na Daktari mara nyingi huambiwa wakatafute dawa madukani hata kama zipo hospitalini na ukiuliza kwa nini hujibu hawahitaji usumbufu.
Hayo yameelezwa na Katibu wa Shirika la Wazee saidia lenye makao yake Wilayani Kasulu Mkoani Cotlida Kokupima wakati akiwasilisha salamu za wazee kutoka Mkoani kigoma kwenye kongamano la wazee lililofanyika Mjini Mpanda Mkoa wa Katavi.
Bibi Kokupima ameeleza changamoto zinazowakabiliwa wazee katika maeneo mbalimbali zikiwemo na manyanyaso hayo wanayofanyiwa wazee wakiwa katika Zahanati,Vituo vya Afya Pamoja na Kwenye Hospitali mbalimbali hapa nchini.
Changamoto hizo ni kuwa wakienda kutibiwa na wakishaandikiwa dawa wanaambiwa hazipo waende wakanunue madukani wakati mwingine wanakuwa hawana hela matokeo yake wanarudi nyumbani kulala bila kupata dawa na mwisho ni kufa.
Changamoto ya usafiri kutoka nyumba hadi kufika kwenye huduma za jamii hasa matibabu kwa wazee wenye umri mkubwa ni taabu,hawana uwezo wa kuzifuata dawa dukani hata kama watakuwa na fedha.
Kwa Upande wake mwakilishi wa shirika la Afya la Wazee Duniani Athman Daniel ameeleza kuwa shirika lake kwa kusaidiana na wadau mbalimbali na wazee limeweza kuchangia kuisukuma serikali kuona uwezekano wa kuwapatia wazee malipo ya uzeeni na mchakato unaenda vizuri na wakati wowote suala hilo litafanikiwa.
Akizungumzia Halmashauri ya Mpanda amesifu juhudi zilizofanywa katika kuwahudumia wazee kwa kutenga chumba cha kiliniki ya wazee na wanapatiwa huduma hapo.
Kauli mbiu ya mwaka huu ni “WAZEE WASIACHWE NYUMA TUJENGE JAMII SHIRIKISHI KUPITISHA SHERIA YAO.

MICHEPUKO BADO NI SHIDA TANZANIA AFUMWA NA MKE WA MTU


Kijana mmoja aliyefahamika kwa jina la Marck Costantine (24), mkazi wa mtaa wa Kitangiri jijini Mwanza amenaswa ‘live’ gesti akiwa na mke wa kigogo mmoja (jina kapuni), aitwaye Mwanaidi wakijiandaa kuvunja amri ya sita.
Baada ya fumanizi kati ya Serengeti boy aliyefahamika kwa jina la Marck Costantine na mke wa kogogo. Tukio hilo lilijiri Septemba 18, mwaka huu kwenye gesti moja maarufu iliyoko mitaa ya Kitangiri baada ya kigogo huyo kupewa ‘ubuyu’ kwamba anaibiwa mali yake ndipo akaandaa mtego na kufanikiwa kumnasa kijana huyo alipokutwa kwenye chumba namba 4 cha gesti hiyo akijiandaa kuserebuka. “Kigogo alipopewa mchoro huo na wambea, siku ya tukio alimshtua Mwenyekiti wa Mtaa wa Kitangiri, Maginga Patroba, wakatia timu katika gesti hiyo, wakawakuta wachepukaji hao wakiwa kitandani huku Marck akiwa tayari ameshachojoa nguo, Mwanaidi akiwa bado,” kilisema chanzo chetu na kuongeza:
Akisainishwa kulipishwa faini. “Kigogo aliamuru wahudumu wagonge mlango ili wahusika wasishtuke, walipofungua ndipo mwenyekiti sabamba na kigogo huyo wakazama ndani.”
Mwanaidi alipoona flashi za kamera ya mapaparazi zikiwamulika, alianza kuangua kilio mbele ya mumewe kumuomba awasamehe lakini kigogo huyo alimtaka kijana huyo amlipe fidia ya shilingi milioni moja kama adhabu ya kutembea na mke wake.
Kutokana na hali ya uchumi ya kijana huyo kutokuwa nzuri, hakuweza kulipa kiasi hicho cha pesa badala yake aliomba kupewa muda wa kulipa pesa hizo. 
Barua ya makubaliano ya kulipwa pesa kwa kigogo huyo shilingi laki tano. Chini ya uangalizi wa mwenyekiti, Marck aliandika barua ya makubaliano jinsi ya kulipwa kwa kiasi hicho cha pesa kwa kigogo huyo na iwe kama fundisho kwake kuachana na tabia za kutembea na wake za watu. 
Kwa upande mwingine, mwenyekiti Patroba alikiri kumfahamu Marck na kudai ni kijana wa mtaani kwake na kumuonya asirudie mchezo huo mchafu. 
Mke huyo wa Kigogo aliyefahamika kwa jina moja la Mwanaidi akiwa analia akiomba msamaha kwa mumewe. 
“Namfahamu huyu kijana nimeshangazwa na kitendo hiki anachokifanya kwani ni vitendo ambavyo havikubaliki katika jamii hivyo kama kiongozi wa mtaa huunitaendelea kutoa ushirikiano ili kuukomesha tabia kama hizi za kuvunja miji ya watu,’’ alisema Patroba.

THE MAGAZETI YA BONGO LEO WEDNESDAY /JUMATANO 1/10/2014 LIVE!!


.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.

.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.

Waliopiga kura ya hapana walalamika kutishwa




Dodoma/Dar. Baadhi ya wajumbe wa Bunge la Katiba waliopiga kura za hapana wamelazimika kuondoka Dodoma na kurudi Zanzibar kwa madai ya vitisho walivyopata kutoka kwa wenzao.
Mmoja wa wajumbe hao, Salma Said alisema jana jioni kuwa yeye na wajumbe wenzake wamekataa kuitikia wito wa Mwenyekiti wa Bunge, Samuel Sitta kwenye Kamati ya Mashauriano ili kuhojiwa kuhusu kura hiyo na kutokana na vitisho wanavyopata kutoka kwa wajumbe wenzao wameamua kuondoka Dodoma.
Vitisho hivyo vimeripotiwa muda mfupi baada ya Sitta kuunda Kamati ya Mashauriano ya watu tisa inayoongozwa na Makamu Mwenyekiti, Samia Suluhu Hassan kushughulikia kura hizo zilizopigwa na wajumbe saba zinazoweka njiapanda uwezekano wa kupatikana akidi ya kupitisha Katiba inayopendekezwa.
Wajumbe waliopiga kura za wazi za hapana kwa ibara zote ni Adil Mohamed Adil, Dk Alley Soud Nassor, Fatma Mohamed Hassan, Jamila Ameir Saleh, Salma Hamoud Said, Mwanaidi Othman Twahir na Ali Omary Juma.
Kwa upande wa Tanzania Bara aliyepiga kura ya hapana kwa rasimu nzima ni Mbunge wa Mpanda Kati (Chadema), Said Arfi na wajumbe 30 kutoka Zanzibar wakipiga kura ya siri.
“Baada ya kupiga kura za hapana leo (jana), walijitokeza wajumbe akiwamo (jina tunalihifadhi kwa sasa) wakaanza kutuzongazonga,” alisema Salma.
“Walituambia kuwa tumebaki hadi dakika ya mwisho halafu tunasema hapana kwa rasimu nzima ili kula fedha za bure, wanasema bora tungeondoka na Ukawa (Umoja wa Katiba ya Wananchi).”
Hata hivyo, alipopigiwa simu yake ya mkononi mmoja wa watuhimiwa, alipokea na baada ya mwandishi kujitambulisha alikata simu na alipopigiwa mara ya pili alijibu alisema; “Mimi ni mheshimiwa mwana na niko Sudan.”
Salma alisema miongoni mwa wajumbe hao wakiwamo baadhi ya mawaziri waliwafuata hadi nje ya ukumbi wakiwatishia kuwa watawafanyia hujuma kwa kukataa kuunga mkono rasimu hiyo.
“Sisi tumeamua kuondoka kurudi kwetu, hatutaingia tena bungeni maana hivi vitisho vimezidi sasa,” alisema Salma.
Juhudi za kuwapata wajumbe wenzake kuzungumzia vitisho hivyo hazikuzaa matunda, lakini Katibu wa Bunge hilo, Yahya Khamis Hamad alikiri kupokea malalamiko hayo na kwamba amelichukulia kama suala la kisiasa.
Alisema wajumbe hao hawajasema wametishiwa kufanyiwa kitu gani, bali walimweleza kuwa wameambiwa kuwa wamekaa pale (bungeni) kwa ajili ya kupata pesa.
Kuhusu kukataa kwao kuhudhuria katika Kamati ya Mashauriano, Hamad alisema hawezi kulitolea jibu kwa kuwa litafanya maridhiano yasifanyike.
Kamati ya Maridhiano
Akitangaza kuunda kamati hiyo, Sitta alisema ana suala mbele yake ambalo linahitaji mashauriano chini ya Kanuni ya 54(4) kutokana na baadhi ya wajumbe kupiga kura ya hapana kwa ibara zote.
Kanuni hiyo inasema: “Mwenyekiti baada ya kushauriana na kamati ya uongozi anaweza kuunda kamati ya mashauriano pale linapojitokeza suala linalohitaji mashauriano.
“Baadhi ya wajumbe jana (juzi), walipiga kura za hapana kwa ibara zote, jambo ambalo haliwezekani kuwa hivyo. Kwa kushirikiana na Makamu Mwenyekiti, nimeunda kamati hii ambayo naomba ikafanye kazi leo,” alisema.
Alisema kamati hiyo yenye wajumbe tisa itakayoongozwa na Samia na baada ya kikao chake cha jana itatoa matokeo bungeni. Wajumbe wengine ni Rashid Mtuta, Shamsi Vuai Nahodha, Omary Yusuf Mzee, Mohamed Aboud, Andrew Chenge, Dk Asha-Rose Migiro, Dk Francis Michael na Brigedia Jenerali Hassan Ngwilizi.
“Hawa watakaa na wale wawili walioniomba kwamba wanataka kusikilizwa kwa nini wamesema hapana kwa kitendo ambacho inaonekana kama wamepoteza muda kukaa bungeni ili kukataa Katiba yote,” alisema.
Alitoa nafasi kwa wajumbe wengine ambao walipiga kura za hapana watakaopenda kwenda katika kamati hiyo kueleza ni kwa nini waliikataa rasimu hiyo.
Hata hivyo, kabla ya kuanza kwa upigaji kura jana, Sitta alisema kuwa hali inakwenda vizuri… “Inshallah hali inakwenda vizuri na dua la kuku halimpati mwewe.”
Kwa mujibu wa Kanuni 36(3). Endapo mjumbe baada ya kukataa ibara za Rasimu ya Katiba, mwenyekiti ataunda kamati ya mashauriano ambayo itasikiliza hoja zake na kupata mwafaka.
Kanuni 36 (4), baada ya kamati ya mashauriano kukutana na kujadili ibara inayobishaniwa, itapeleka taarifa ya matokeo ya mashauriano yake kwenye Bunge Maalumu kwa ajili ya kujadiliwa na ibara hiyo kama ilivyo au baada ya kuandikwa upya kwa kuzingatia taarifa ya Kamati ya Mashauriano.
Endapo theluthi mbili haitapatikana kwa mara ya pili, ibara hiyo itahesabiwa kuwa haikukubaliwa wala kupitishwa na Bunge Maalumu kwa mujibu wa masharti yaliyowekwa na sheria na kanuni hizi.
TEC yamshukia Sitta
Kauli ya Sitta kuwa baadhi ya nyaraka kuhusu mchakato wa Katiba Mpya zinazotolewa na makanisani, “hazina utukufu wa Mungu na ni za kipuuzi” imepondwa na Baraza la Maaskofu wa Kanisa Katoliki Tanzania (TEC), likisema hajui nguvu ya umma.
Akizungumza na gazeti hili jana, Makamu wa Rais wa TEC, Askofu Severine Niwemugizi alisema: “Unadhani tulivyotoa waraka tulikuwa tunawataka waumini wafanye nini? Je, ni kufuata dhehebu lako limesema nini au kufuata kilichomo katika waraka? Wewe (mwandishi) si Mkristo? Jibu hilo.”
Aliongeza, “Wenye mapenzi na nchi hii wamfute kichwani Sitta na huo upuuzi aliosema ni wake mwenyewe. Huyu anadhani kuwa ana akili kuliko mamilioni ya Watanzania waliopendekeza wanataka kujitawala namna gani?”
Sitta alitoa kauli hiyo mjini Dodoma juzi wakati akiwatambulisha viongozi 13 kutoka Jumuiya ya Image ya Kanisa Kuu la Mtakatifu Paulo wa Msalaba ya mjini Dodoma.
Licha ya Sitta kutotaja taasisi husika, lakini Jukwaa la Wakristo Tanzania ndilo lililotoa waraka unaotaka kusitishwa kwa mchakato wa Katiba Mpya na kusambazwa makanisani.
Waraka huo ulitolewa kwa pamoja na TEC, Jumuiya ya Kikristo Tanzania (CCT), Baraza la Makanisa ya Kipentekoste Tanzania (FPCT) na Kanisa la Waadventista Wasabato (SDA).
“Anadhani wanaweza kutunga Katiba ya kuwatawala wananchi. Kauli aliyoitoa ni sawa na kuwapuuza Watanzania na ni sababu ya madaraka tu, maana ndiyo yanayowapa watu wengi kiburi,” alisema.
Askofu huyo alikwenda mbali zaidi na kusema kuwa kauli hiyo ya Sitta maana yake ni kwamba CCM itabaki milele madarakani na Watanzania hawawezi kuwafanya jambo lolote.
“Unajua mtu mwenye kiburi na dharau anayedhani hawezi kuambiwa chochote unatakiwa kumwacha kama alivyo ila Watanzania ndiyo watakaoamua nini wanataka katika maisha yao,” alisema.
Mchungaji wa Kanisa la Maombezi (GRC), Antony Lusekelo alisema: “Bunge la Katiba limemwelemea Sitta na ndiyo maana ameanza kutukana watu.”
Lusekelo maarufu kama Mzee wa Upako alisema kwa jinsi jamii ilivyogawanyika katika mchakato wa kupata Katiba Mpya, ilikuwa jambo la busara kwa makanisa kutaka kusitishwa kwa mchakato huo mpaka makundi yote yanayovutana yafikie mwafaka.
Imeandikwa na Sharon Sauwa, Habel Chidawali na Fidelis Butahe

PICHA JINSI UPIGAJI KURA WA RASIMU INAYOPENDEKEZWA WAENDELEA LEO BUNGENI MJINI DODOMA.

Mjumbe wa Bunge Maalum la Katiba wa upande wa Zanzibar akiweka kura yake ya siri ndani ya sanduku la kuhifadhia kura mara baada ya kukamilisha kupiga kura yake kwa ajili ya Rasimu ya Katiba inayopendekezwa bungeni mjini Dodoma.
Mjumbe wa Bunge Maalum la Katiba wa upande wa Zanzibar akiweka kura yake ya siri ndani ya sanduku la kuhifadhia kura mara baada ya kukamilisha kupiga kura yake kwa ajili ya Rasimu ya Katiba inayopendekezwa bungeni mjini Dodoma.
Mjumbe wa Bunge Maalum la Katiba, Mhe. Shymar Kwegir akiipigia kura Rasimu ya Katiba inayopendekezwa Bungeni hapo leo 30 Septemba, 2014 mjini Dodoma.
Mwenyekiti wa Bunge Maalum la Katiba, Mhe. Samuel Sitta akipiga  kura yake kwa ajili ya Rasimu ya Katiba inayopendekezwa Bungeni hapo leo 30 Septemba, 2014 mjini Dodoma.
BOFYA HAPA KWA PICHA ZAIDI»




Waziri Mkuu wa Tanzania ambaye pia ni mjumbe wa
Bunge Maalum la Katiba, Mhe. Mizengo Pinda akiipigia kura Rasimu
inayopendekezwa



 Makamu wa Pili wa Zanzibar ambaye pia Mjumbe wa Bunge Maalum la
Katiba, Mhe. Seif Ali Idd akiipigia kura Rasimu ya Katiba
inayopendekezwa Bungeni hapo leo 30 Septemba, 2014 mjini Dodoma.





Mjumbe wa Bunge Maalum toka upande wa
Zanzibar, Mhe. Pandu Ameir Kificho naye akiipigia kura Rasimu ya Katiba
inayopendekezwa bungeni mjini Dodoma.



 Makamu Mwenyekiti wa Bunge Maalum la Katiba, Mhe. Samia Hassan
Suluhu akipiga kura yake kwa ajili ya Rasimu ya Katiba inayopendekezwa
Bungeni hapo leo 30 Septemba, 2014 mjini Dodoma.



 Waziri wa TAMISEMI ambaye pia ni Mjumbe wa Bunge Maalum la
Katiba, Mhe. Hawa Ghasia akiipigia kura Rasimu ya Katiba inayopendekezwa
Bungeni hapo leo 30 Septemba, 2014 mjini Dodoma.



 Mjumbe wa Bunge Maalum la Katiba, Mhe. Ummy Mwalimu akiipigia
kura Rasimu ya Katiba inayopendekezwa Bungeni hapo leo 30 Septemba, 2014
mjini Dodoma.



 Mwenyekiti wa Kamati ya Uandishi ya Bunge Maalum la Katiba, Mhe.
Andrew Chenge akipiga kura yake kwa ajili ya Rasimu ya Katiba
inayopendekezwa Bungeni hapo leo 30 Septemba, 2014 mjini Dodoma.



 Waziri wa Katiba na Sheria ambaye pia ni Mjumbe wa Kamati namba
Tano ya Bunge Maalum la Katiba, Mhe. Asha-Rose Migiro akiipigia kura
Rasimu ya Katiba inayopendekezwa Bungeni hapo leo 30 Septemba, 2014
mjini Dodoma.



 Naibu Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo ambaye pia
ni Mjumbe wa Bunge Maalum la Katiba, Mhe. Juma Nkamia akiipigia kura
Rasimu ya Katiba inayopendekezwa Bungeni hapo leo 30 Septemba, 2014
mjini Dodoma.



 Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo ambaye pia ni
Mjumbe wa Bunge Maalum la Katiba, Mhe. Fenella Mukangara akiipigia kura
Rasimu ya Katiba inayopendekezwa Bungeni hapo leo 30 Septemba, 2014
mjini Dodoma.





Wajumbe mbalimbali wa Bunge Maalum la Katiba,wakichangia hoja wakati wa upigaji kura
Rasimu ya Katiba inayopendekezwa Bungeni hapo leo 30 Septemba, 2014
mjini Dodoma.