Wazee
wakiwa kwenye kongamano la wazee kwenye ukumbi wa mikutano wa
Halmashauri ya Mpanda kujadili changamoto zinazowakabili wakati wa
kupatiwa matibabu.
.
Wahudumu
wa Afya wameendelea kuwanyanyapaa wazee wawapo hospitalini kupata huduma
ya Afya kwa kuwaacha wakae asubuhi hadi jioni ,huku wenyewe wakifanya
kazi zao nyingine.
Pia
wakitibiwa na Daktari mara nyingi huambiwa wakatafute dawa madukani
hata kama zipo hospitalini na ukiuliza kwa nini hujibu hawahitaji
usumbufu.
Hayo
yameelezwa na Katibu wa Shirika la Wazee saidia lenye makao yake
Wilayani Kasulu Mkoani Cotlida Kokupima wakati akiwasilisha salamu za
wazee kutoka Mkoani kigoma kwenye kongamano la wazee lililofanyika Mjini
Mpanda Mkoa wa Katavi.
Bibi
Kokupima ameeleza changamoto zinazowakabiliwa wazee katika maeneo
mbalimbali zikiwemo na manyanyaso hayo wanayofanyiwa wazee wakiwa katika
Zahanati,Vituo vya Afya Pamoja na Kwenye Hospitali mbalimbali hapa
nchini.
Changamoto
hizo ni kuwa wakienda kutibiwa na wakishaandikiwa dawa wanaambiwa
hazipo waende wakanunue madukani wakati mwingine wanakuwa hawana hela
matokeo yake wanarudi nyumbani kulala bila kupata dawa na mwisho ni
kufa.
Changamoto
ya usafiri kutoka nyumba hadi kufika kwenye huduma za jamii hasa
matibabu kwa wazee wenye umri mkubwa ni taabu,hawana uwezo wa kuzifuata
dawa dukani hata kama watakuwa na fedha.
Kwa
Upande wake mwakilishi wa shirika la Afya la Wazee Duniani Athman Daniel
ameeleza kuwa shirika lake kwa kusaidiana na wadau mbalimbali na wazee
limeweza kuchangia kuisukuma serikali kuona uwezekano wa kuwapatia wazee
malipo ya uzeeni na mchakato unaenda vizuri na wakati wowote suala
hilo litafanikiwa.
Akizungumzia
Halmashauri ya Mpanda amesifu juhudi zilizofanywa katika kuwahudumia
wazee kwa kutenga chumba cha kiliniki ya wazee na wanapatiwa huduma
hapo.
Kauli mbiu ya mwaka huu ni “WAZEE WASIACHWE NYUMA TUJENGE JAMII SHIRIKISHI KUPITISHA SHERIA YAO.
No comments:
Post a Comment