Sunday, 23 March 2014

KOCHA RHINO ALIA WANATABORA WANAWAMALIZA


by kassonga




SIKU moja baada ya kukumbana na kipigo cha mabao 3-0 kutoka kwa Yanga, Kocha Mkuu wa Rhino, Jumanne Chale amesema wako baadhi ya wadau we mkoa we Tabora wanachangia timu hiyo kutofanya vizuri.

Chale amesema amekuwa akishangazwa na kuona baadhi ya mashabiki au wadau wa soka katika mkoa huo wakifanya kila juhudi kuzisaidia timu za wageni.


“Wanaona Yanga, Simba au timu nyingine ndiyo wanapaswa kuzisaidia. Lakini wanasahau wao wako hapa Tabora.
“Hata kuziona timu nyingine ni kwa kuwa Rhino iko ligi kuu. Ikiteremka wataziona wapi Yanga na Simba, kweli inanishangaza sana,” alisema akionyesha kutokukubaliana na suala hilo.

Tuesday, 4 March 2014

HIZI NDIO SHULE ZETU KATAVI MPANDA PICHA MOJA YA SHULE KATA YA KABUNGU WILAYA YA MPANDA

                                            Haya ndio madarasa ya shule ya Kabungu
                                           Hili ndio darasa zuri kuliko yote na ni la awali ( CHEKECHEA )
                                          Ofisi ya walimu. mwalimu akiendelea na kazi za kiofisi
                                             Vyoo vinavyoonekana kuto kutumika muda mrefu





Wednesday, 26 February 2014

LIGI YA MKOA WA KATAVI YAMALIZIKA; ZAWADI ZAKABIDHIWA

by rahim kassonga (La Captain)

Ligi ya mkoa wa katavi imemalizika hii leo, kwa mchezo mmoja ambao ulikuwa wa kukamilisha ratiba baada ya jana timu ya Mpanda United kuibuka bingwa wa ligi hiyo baada ya kufikisha jumla ya point 10 katika ligi ndogo ya mzunguko wa pili ambayo ilikuwa na jumla ya timu tano.

kombe la bingwa wa mkoa

kaimu katibu mkuu wa karefa (katikati ) akiwa na mgeni rasmi Galius Mgawe
 Katika mchezo wa leo ambao uliwakutanisha Majalila FC toka Ifukutwa  na timu ya Mbugani ya Kakese, Mbugani waliendelea kuthibitisha kuwa vibonde wa mzunguko wa pili baada ya kukubali kipigo cha goli 4 -0.


kocha wa majalila akitoa maelekezo kwa wachezaji wake
 Magoli ya Majalila leo yalifungwa na WEMA SADOCK  aliyefunga magoli 2 ktk dakika ya 27 na 55, wakati mengine yalifungwa na MAULID SAID dk 47 na HILALI SAID 86.


mchezaji wa majalila akipiga faulo

mashabiki wakifurahia burudani ya mpira
 Mbugani walipata penati katika dk za mwishoni za mchezo lakini katika hali isiyotegemewa jalala MAULID alipaisha penati hiyo na kuifanya mbugani kushindwa kupata hata goli moja katika mzunguko wa pili ikiruhusu magoli 15 baada ya kufungwa 5 na timu za majalila na Polisi Katavi goli 1 dhidi ya Mpanda Utd na magoli 4 dhidi ya Majalila


wachezaji wa mbugani wakiwa wamekata tamaa baada ya kukosa penati
 Baada ya mchezo ya mchezo huo timu zote zilikabidhiwa mpira mmoja mmoja na bingwa kukabidhiwa kikombe na mgeni rasmi GALIUS MGAWE ambaye pia ndio aliyetoa zawadi hizo
kapteni wa mbugani akipokea zawadi kutoka kwa mgeni rasmi

shije luvinza kapeni wa majalila akipokea mpira 

mwakilishi wa washindi wa pili timu ya makanyagio akipokea mpira

mwakilishi wa polisi akipokea mpira

mwakilishi wa mpanda united akipokea mpira


Geofrey Augustino maarufu kama KANYOKA akiwa amebeba kombe la ubingwa wa mkoa
MSIMAMO WA LIGI YA KATAVI MZUNGUKO WA PILI

1
MPANDA UNITED
10
2
POLISI KATAVI
7
3
MAKANYAGIO FC
5
4
MAJALILA FC
4
5
MBUGANI FC
0
kapteni wa mpanda united akipokea kombe toka kwa mgeni rasmi

Monday, 17 February 2014

OPEN LOVE VALLENTINE SPECIAL BONANZA@AZIMIO STADIUM TIZAMA PICHA HAPA ( BY ZANGII ZE ICON)

WATANGAZAJI WA MPANDA FM NA PAMOJA FM WALIO UNDA KIKOSI CHA WANA MEDIA WAKIWA KATIKA PICHA YA PAMOJA UWANJA WA AZIMIO

PAMOJA NA MVUA KUBWA KUNYESHA WADAU WALI JITOKEZA KWA WINGI KUSHIRIKI BONANZA LA VALENTINE

MENEJA WA MPANDA FM GERLAD SETTY SEDEKIA AKIWA ANA SHUHUDIA MECHI KALI YA WADAU NA WATANGAZAJI SAMBAMBA NA WATANGAZAJI WA PAMOJA FM MR ZOZI NZ MR KAFILIKA

WATANGAZAJI WA PAMOJA FM WALIO JITOKEZA KUSHUHUDIA TAMASHA

ZANGII NA DJ DON DALA
GOOOOOOOOOOOOO...WATANGAZAJI WAKISHANGILIA GOLI LAO LA USHINDI KWA STAILI YAO...HATAREEE SANA

Sunday, 26 January 2014

JUAN MATA: NI RASMI, NI MCHEZAJI MANCHESTER UNITED

KUTAMBULISHWA RASMI JUMATATU JIONI!!

MOYES_n_MATA-1Juan Mata amekamilisha Uhamisho wa Dau la Pauni Milioni 37.1 kutoka Chelsea kwenda Manchester United.
Jana Mata alipimwa Afya yake huko Manchester na kusaini Mkataba unaoaminika kuwa unamalizika Juni 2018.
Mata, Miaka 25, anatarajiwa kucheza Mechi yake ya kwanza hapo Jumanne Uwanjani Old Trafford na Cardiff City kwenye Mechi ya Ligi Kuu England.
Akiongea baada ya kusaini Mkataba, Mata alisema: “Umefika wakati wa changamoto nyingine. Nimefurahi mno kuwa sehemu ya awamu nyingine ya historia ya Klabu hii.”
Aliongeza: “Chelsea ni Klabu kubwa na nia Marafiki wengi kule lakini huwezi kuikataa nafasi ya kujiunga na Manchester United. Ninatarajia kumsaidia Meneja na Timu kupata mafanikio zaidi katika Miaka ijayo!”
Mata anakuwa Mchezaji wa pili kusainiwa na Meneja David Moyes baada kumsaini Marouane Fellaini kutoka Everton  Mwezi Septemba kwa Dau la Pauni Milioni 27.5.
Pia, kwa kumsaini Mata, Man United imevunja Rekodi yao ya kusaini Mchezaji kwa Bei ya juu ambayo iliwekwa Mwaka 2008 walipomsaini Dimitar Berbatov kwa Pauni Milioni 30.
Mata atatambulishwa rasmi kama Mchezaji mpya wa Man United Jumatatu Saa 10 na Nusu Jioni, Saa za Tanzania.

WASIFU:
Jina: Juan Manuel Mata García
Kuzaliwa: 28 Aprili 1988 (Miaka 25)
Namba ya Jezi: 10

MH. KIKWEMBE ATOA VIFAA VYA MAABARA SEKONDARI YA MWANGAZA

by rahim kassonga (La Captain

Katika jitihada za kukuza na kuendeleza elimu hususani katika masomo ya sayansi, Mbunge wa viti maalum Mkoa wa Katavi kwa tiketi ya CCM mh. Pudenciana Kikwembe ameipatia shule ya sekondari Mwangaza vifaa vya maabara vyenye thamani zaidi ya milioni mbili zikiwemo kemikali


vifaa hivyo vilikabithiwa ijumaa mchana shuleni mwangaza mbele ya mwenyekiti wa Halmashauri ya mji Mpanda mh Enock Gwambasa, Afisa elimu mji, mkuu wa shule mh. Simon Rubange, walimu na wanafunzi


mh kikwembe akiingia mwangaza sekondari
waeni wakisalimiana, nje ya ofisi ya mkuu wa shule
mh. kikwembe akijiandaa kusaini kitabu cha wageni ofisini kwa mkuu wa shule
baadhi ya wanafunzi ambao waliwawakilisha wenzao kupokea msaada huo
mh. kikwembe akitoka kusalimiana na wanafunzi
mh. kikwembe anasisitiza jambo kuhusu mtalaam wa masomo ya sayansi wa
kujitolea kutoka korea kusini ambaye yupo mwangaza sekondari
Mr. Kim mtaalam wa kujitolea wa masomo ya sayansi kutoka korea kusini akitoa neno la shukranii na usia kwa wanafunzi

mh kikwembe akiwahusia wanafunzi kuhusu shule, likini pia alizungumzia umuhimu wa masomo ya sayansi
baadhi ya vifaa vilivyokabidhiwa

baadhi ya vifaa vilivyokabidhiwa

baadhi ya vifaa vilivyokabidhiwa
baadhi ya vifaa vilivyokabidhiwa
mh. akitafakari jambo na pembeni kushoto ni vifaa alivyovitoa

Mkuu wa shule ya sekondari mwangaza akitoa shukrani zake kwa mh. Kikwembe kabla ya kupokea vifaa

Afisa elimu mji akitoa shukrani zake na kuwahusia wanafunzi hasa wa kike umuhimu wa kusoma na kumtolea mfano mh. Kikwembe kwa ni mwanamke mwenye PHD




Mh Enock Gwambasa , meya akisisitiza jambo kwa wanamwangaza

Mh. Meya akitoa shukrani kwa mh kikwembe

Mh. Pudenciana Kikwembe mbunge viti maalum

baadhi ya walim wakisiliza kwa makini maelekezo na maagizo