Wednesday, 21 August 2013

Haya ndo mashitaka matatu aliyosomewa Sheikh Ponda mahakamani leo



Kiongozi wa Jumuiya na Taasisi za Kiislamu Tanzania, Sheikh Issa Ponda leo amepandishwa kizimbani katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Mfawidhi mkoa wa Morogoro kujibu mashitaka matatu yanayomkabili ambayo ni kutotii amri halali, kutoa maneno yenye nia ya kuharibu imani za dini na kushawishi  kutenda kosa. 
 
Sheikh Ponda amefikishwa mjini Morogoro na helkopta ya jeshi la polisi majira ya saa tano asubuhi  chini ya ulinzi mkali ambapo askari waliimarisha ulinzi kwa muda wote huku kikosi cha kutuliza ghasia FFU wakiwa na silaha mabomu na mbwa ambapo hali hiyo imesababisha kusimama kwa baadhi ya shughuli zingine za kiofisi katika ofisi zilizopo jirani na mahakama ya hakimu mkazi wakati kesi hiyo ikiendelea ...


Akisoma shataka mbele ya hakimu mkazi Richard Kabate , wakili mkuu wa serikali kanda ya Morogoro Benard  Kongola amedai kuwa shekh Ponda anadaiwa kutenda makosa hayo matatu Agosti 10 mwaka huu majira ya jioni katika viwanja vya shule ya msingi kiwanja cha ndege manispaa ya Morogoro.

Katika shitaka la kwanza la shekhe Ponda anadaiwa kutotii amri halali ambapo shitaka la pili anadaiwa kutoa maneno yenye nia ya kuharibu imani za dini kwa kutoa maneno kuwa serikali iliamua kupeleka jeshi  Mtwara kushughulikia suala la vurugu iliyotokana na gesi kwa kuwaua na kuwatesa wananchi kwa sababu asilimia 90 ya wakazi wa Mtwara ni Waislamu. 


Shitaka la tatu linalomkabili shekh Ponda ni kushawishi na kutenda kosa ambapo anadaiwa kuwa alitoa maneno ya ushawishi kwa kuwataka  waislaam wasikubali uundwaji wa kamati za ulinzi na usalama za misikiti kwani zinaundwa na Bakwata ambao ni vibaraka wa CCM na serikali, na kama kamati hizo zitajitokeza aliwaamuru wafunge milango na madirisha ya misikiti kuwapiga.
 

Baada ya kusomewa mashitaka hayo shekh Ponda anayetetewa na mawakili wasomi Barthoromew Tarimo na Ignas Punge  alikataa mashataka yote matatu na hivyo upande wa mashitaka kupinga dhamana kwa madai kuwa shekh Ponda anatumikia kifungo cha nje na kwamba hakutakiwa kufanya kosa, hata hivyo anakabiliwa na makosa mengine.
 
Upande wa mashitaka umedai kuwa upelelezi umekamilika na kesi hiyo itasomwa tena Agosti 28  mwaka huu ambapo mstakiwa amerudishwa rumande kwa helkopta jijini Dar es salaam.

 
 

Tuesday, 20 August 2013

Picha na habari kamili kuhusu vurugu zilizotokea jijini mwanza leo


 

MAANDAMANO ya amani yaliyokuwa yameandaliwa na chama cha demokrasia na maendeleo(chadema) yamegeuka shubiri kwa wakazi wa jiji la Mwanza baada ya kuibuka mapambano makali baina ya waandamanaji hao na jeshi la polisi mkoani Mwanza na kusababisha polisi kutumia nguvu kuwatawanya wafuasi wa chama hicho.

 

Maandamano hayo ya amani ambayo yalianzia katika eneo la Buzuruga nje kidogo ya jiji la Mwanza yalikuwa  yakiongozwa na wabunge Highness Kiwia wa Ilemela  pamoja na Ezekiel Wenje kuelekea katika viwanja vya Furahisha na yalilenga kumshinikiza Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, Ernest Ndikilo kutoa barua zinazodaiwa kuandikwa na ofisi ya Waziri Mkuu Tamisemi kuwarejesha madiwani watatu waliotimuliwa katika Manispaa ya Ilemela kutokana na kushindwa kuhudhuria vikao vitatu mfululizo.

 

Polisi wenye silaha pamoja na askari kanzu walianza kutanda katika eneo hilo la Furahisha wakiongozwa na Mkuu wa upelelezi wa makosa ya jinai Mkoa wa Mwanza RCO Konyo ambaye alikuwa akitumia gari lenye namba za usajili DK 068EXV aina ya Toyota Land Cruiser

 

Maandamano hayo ambayo awali yalionekana kana kwamba yangelimalizika salama yaliwasili katika viwanja vya Furahisha majira ya saa 5.38 huku yakiongozwa na gari la polisi lenye namba za usajili za nchi ya Uganda  779 UAG likiwa nimesheheni polisi wenye silaha nzito ikiwa ni pamoja na mabomu ya machozi na bunduki pamoja na askari kadhaa ambao walikuwa katikati ya maandamano hayo.

 

Baada ya maandamano hayo kuwasili katika viwanja vya Furahisha kwa amani,waandamani hao ambao walikuwa na mabango mbalimbali yaliyosomeka kuwa :‘Matata hatutaki uendelee kuwa Meya wa Ilemela rudia kazi yako ya awali,.... na jingine Jaji Sumari tumechoka kuahirisha mara kwa  mara kesi dhidi ya Matata ....na jingine  lililosomeka kuwa RD Ndikilo tunahitaji barua za kurejeshwa kwa madiwani wetu.

 

Hata hivyo tofauti na ilivyokuwa imetangazwa kuwa maandamano hayo ya amani yangelipokelewa na Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Ernest Ndikilo,hakukuwa na kiongozi yoyote wa Serikali ambaye alikuwepo uwanjani hapo kupokea maandamano hayo.

 

Kufuatia kutoonekana kwa kiongozi yoyote wa Serikali,viongozi wa chadema pamoja na wabunge wao walikutana kwa faragha kwa dakika kadhaa kwa ajili ya kujua hatima ya maandamano hayo ambapo Mbunge wa Nyamagana Ezekiel Wenje alipanda jukwaani saa 6.45 na kuwaeleza maelfu ya waandamanaji kuwa wameamua kumtuma Mbunge wa Ilemela Highnes Kiwia kwenda ofisini kwa Mkuu wa Mkoa wa Mwanza kuchukua majibu kwa ajili ya kuwaletea wananchi walioandamana juu ya hatima ya madiwani hao.

 

Hata hivyo saa moja baadae Mbunge huyo alisimama jukwani na wakuwaeleza waandamani hao kuwa simu ya Mbunge Kiwia ilikuwa haipatikani hivyo kuwataka kuandamana kwenda kwa Mkuu wa mkoa wa Mwanza kujua kulikoni na hapo ndipo hali ya hewa ilipochafuka.

 

Jeshi la polisi baada ya kuona wandamanaji hao wameanza kuelekea katika ofisi za Mkuu wa mkoa liliwataka kutawanyika ambapo waandamanaji hao walikaidi ndipo jeshi la polisi lilipoamua kutumia mabomu ya machozi kuwatawanya wafuasi hao.

 

Vurugu hizo ambazo zilianza majira ya saa 7.30 zilisababisha kufungwa kwa baadhi ya barabara kutokana na waandamanji hao kuweka vizuizi vya mawe na kuchoma matairi,ambapo pia maduka na ofisi mbalimbali zililazimika kufungwa kwa muda kupisha vurugu hizo.

 


Baadhi ya wananchi ambao walikuwa wakitumia usafiri wa umma walionekana wakishuka kupitia katika madirisha ya magari hayo na kukimbia kwa hofu ya kujeruhiwa na mabomu pamoja na mawe ambayo yalikuwa yakirushwa na waandamanji hao kwa jeshi la polisi.

 

MKUU WA MKOA WA MWANZA ALONGA.

Mkuu wa mkoa wa Mwanza akizungumza na Mbunge Kiwia pamoja na viongozi wa chadema ofisini kwake alisema kuwa ameshangazwa na uvumi huo kuwa ofisi yake imekalia barua za kurejeshwa kwa madiwani Abubakar Kapera(Nyamanoro),Dan Kahungu(Kirumba) pamoja na Marietha Chenyenge(Ilemela).

 

RC Ndikilo alisema kuwa Serikali imekuwa ikifanya kazi zake kwa maandishi na sio kwa kufuata maneno ya mtaani na kueleza kuwa hana barua yoyote toka ofisi ya Waziri Mkuu inayomualifu kuhusu kuwarejesha madiwani hao baada ya kukata rufaa.

 

“We Mbunge kuna siku ulinipigia simu ukiniuliza juu ya kuwepo kwa barua hizo nami nilikujibu kuwa kwa kuwa uko hapo Bungeni Dodoma ambapo pia kuna ofisi ya Waziri Mkuu nilikujibu kuwa ni muhimu ukawaona viongozi wakuu wa Tamisemi ikiwa ni pamoja na Waziri Mkuu,pia nilikushauri kuwa wakupe japo nakala ya barua hiyo”,alisema RC Ndikilo.

 

“Lakini cha kushangaza nimekuwa nikisikia maneno ya ajabu kuwa nimeficha barua za madiwani hao,ikumbukwe kuwa madiwnai hao hawakukata rufaa kwangu bali walikata rufaa ngazi ya juu kabisa,ili kukata mzizi wa fitina naomba kati ya tarehe 26 hadi 27 wewe Mbunge pamoja na mimi twende TAMISEMI kukutana na viongozi ili kukata mzizi wa fitina na tuje tuwaeleze wananchi ukweli uliopo”,alisema RC Ndikilo.

 

Kuhusu suala la Meya Henry Matata kutoondolewa madarakani RC Ndikilo alisema kuwa hawezi kulizungumzia suala hilo kwa kuheshimu mamlaka ya mahakama na kuwataka chadema kuvuta subira hadi pale mahakama itakapotoa maamuzi yake.

 

KAULI YA MBUNGE KIWIA.

Akizungumza katika ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Mwanza,Kiwia alisema kuwa waliamua kuitisha maandamano hayo kutokana na kuelezwa na Waziri Hawa Ghasia kuwa tayari barua hizo zimeishatumwa mkoani Mwanza.

 


“Mheshimiwa Mkuu wa mkoa hawa madiwani waliosimamishwa  ni wawakilishi wa wananchi,wamekaa nje kwa miezi saba sasa na uchaguzi wa Meya haukuwa halali ndio maana tuliamua kuitisha maandamano kwa ajili ya kuhakikisha madiwani hawa wanarejeshwa.

 


RPC MANGU.

Akizungumza kwa simu juu ya kutokea kwa vurugu zilizosababisha kupigwa  kwa mabomu ya machozi,Kamanda wa polisi mkoa wa Mwanza Ernest Mangu alisema kuwa polisi walifanikiwa kudhibiti vurugu hizo na hadi sasa hawezi kusema ni wananchi wangapi ambao walikamatwa kuhusu vurugu hizo.




















Mtandao wa Kagame wadai kuwa Mama Salma Kikwete ni Mnyarwanda


 Mtandao  wa  News  of  Rwanda  umeendelea  kutuchokonoa  watanzania  ili  kuupima  msimamo  wetu.....

Baada  ya  kukurupa  na  madai  kwamba  Rais  Kikwete  si  mtanzania  halisi  na  kwamba  ni  mtu  mwenye  asili  ya  Burundi, mtandao  huo  umekuja  na  kioja  kipya....

Taarifa  iliyotolewa  jana  tarehe  19/08/2013  na  mtandao  huo  inadai  kwamba  mke  wa  Rais  Kikwete  aitwaye  Mama  Salma  Kikiwete  ni   mnyarwanda   wa  kabila  la  wahutu ( mhutu )..


Katika  maelezo  yake, mtandao  huo  umeenda  mbali  na  kudai  kuwa  Mama  Salma  Kikwete  ni  binamu  wa  rais  wa zamani wa Rwanda, Juvenal Habyarimana  na  ndo  maana  rais Kikwete  alitoa  ushauri  wa   mazungumzo  ya  amani  kati  ya  Kagame  na  waasi....
.............................................................
HII  NDO  POST  YAO  WALIYOTOA
---------------------------------------------
New details obtained by News of Rwanda may give insight into why Tanzania’s President Jakaya Kikwete came out as the sole global leader sympathetic to Rwandan FDLR rebels based in DR Congo jungles since 1994.

According to secret US State Department cables published by whistle-blowing site Wikileaks, President Jakaya Kikwete’s wife fondly known in Tanzania as “Mama Salma Kikwete” is a cousin of former Rwanda leader Juvenal Habyarimana. The shocking details are contained in a cable sent to Washington on Thursday May 5th, 2005, by Shabyna Stillman, a senior diplomat at the US embassy in Dar es Salaam.

The US embassy was giving update on the selection of Mr Jakaya Kikwete to be the CCM flag-bearer in the presidential election late that year. “For years, observers of the Great Lakes conflicts have considered Kikwete to be virulently pro-Hutu,” reads the cable, in part.

“Kikwete’s marriage to a cousin of former Rwandan President Juvenal Habyarimana may have fueled these rumors, which are now fading as the Burundi conflict winds down,” adds the cable, signed by Stillman.

According to the US embassy, Mr Kikwete’s love affair with “Hutus” could be seen in his spirited support for Burundian rebels at the time fighting former President Pierre Buyoya.

Since 1995, up until 2005 when Mr. Kikwete was foreign affairs minister of Tanzania, rumours have swelled around him suggesting he sided massively with the ethnic extremist establishment. It is this system that planned and executed the genocide against Tutsis in 1994, and fled across to Zaire and other parts of the world.

It is alleged, around 1996, Mr Kikwete suggested publicly that “Hutus” need to be armed to fight off the government in Kigali at the time. A book published by virulent critic of President Paul Kagame and historian GĂ©rard PRUNIER writes that Tanzania did offer to train troops for Seth Sendashonga.

A former leader of the Rwanda Patriotic Front (RPF), for whom he was a minister in the government set up after the rebel movement’s victory over the army and the militias responsible for the genocide in 1994, Mr. Sendashonga was murdered in Nairobi, Kenya, on 16 May 1998 by, according to PRUNIER, “unknown assailants.”

Fast forward to May 26, 2013, President Jakaya Kikwete goes public with a suggestion that the government of President Kagame in Rwanda negotiates with rebels of the Democratic Forces for the Liberation of Rwanda (FDLR). The group was formed in May 2000, but its members had been roaming DRC forests ever since they lost power in Kigali.

The suggestion by a head of state of Tanzania, a country that had long been considered a friendly nation to Rwanda, caught many by surprise. Since then, the two countries are embroiled in a bitter war of words.

The ex-Rwandan Juvenal Habyarimana died on the evening of April 6th, 1994, after his plane was shot down by extremist members of inner circle who did not want the peace talks with the RPF rebels. In the same plane was Burundian counterpart Cyprien Ntaryamira and French pilots.

The death of the French crew has been the centre of legal battles in France and the United States. A French judicial inquiry did confirm that the plane was brought down by a missile fired from a military camp next to Habyarimana’s home near the airport.

Monday, 5 August 2013

Meneja masoko na meneja wa mpanda fm Gerrrald Seth Sedekia akiwa ofisini kwake na mtangazaji wa mpanda fm Fatuma Amas
Mkurugezi wa kituo cha radio mpanda fm Ndg Kanji aliyevaa tshet ya NMB akiwa  baadhi ya asikari uwanja wa ndege  (mpanda air port)  wakimlaki waziri mkuu wa jamhuri ya muungano wa Tanzani

                                                         ofisi za uwanja wa ndege wa mpanda

Gerald Seth Sedekia meneja  masoko mpanda fm