Kiongozi wa Jumuiya na Taasisi za Kiislamu Tanzania, Sheikh Issa Ponda leo amepandishwa kizimbani katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Mfawidhi mkoa wa Morogoro kujibu mashitaka matatu yanayomkabili ambayo ni kutotii amri halali, kutoa maneno yenye nia ya kuharibu imani za dini na kushawishi kutenda kosa.
Sheikh Ponda amefikishwa mjini Morogoro na helkopta
ya jeshi la polisi majira ya saa tano asubuhi chini ya ulinzi mkali
ambapo askari waliimarisha ulinzi kwa muda wote huku kikosi cha kutuliza
ghasia FFU wakiwa na silaha mabomu na mbwa ambapo hali hiyo
imesababisha kusimama kwa baadhi ya shughuli zingine za kiofisi katika
ofisi zilizopo jirani na mahakama ya hakimu mkazi wakati kesi hiyo
ikiendelea ...
Akisoma shataka mbele ya hakimu mkazi Richard Kabate , wakili
mkuu wa serikali kanda ya Morogoro Benard Kongola amedai kuwa shekh
Ponda anadaiwa kutenda makosa hayo matatu Agosti 10 mwaka huu majira ya
jioni katika viwanja vya shule ya msingi kiwanja cha ndege manispaa ya
Morogoro.
Katika shitaka la kwanza la shekhe Ponda anadaiwa
kutotii amri halali ambapo shitaka la pili anadaiwa kutoa maneno yenye
nia ya kuharibu imani za dini kwa kutoa maneno kuwa serikali iliamua
kupeleka jeshi Mtwara kushughulikia suala la vurugu iliyotokana na gesi
kwa kuwaua na kuwatesa wananchi kwa sababu asilimia 90 ya wakazi wa
Mtwara ni Waislamu.
Shitaka la tatu linalomkabili shekh Ponda ni
kushawishi na kutenda kosa ambapo anadaiwa kuwa alitoa maneno ya
ushawishi kwa kuwataka waislaam wasikubali uundwaji wa kamati za ulinzi
na usalama za misikiti kwani zinaundwa na Bakwata ambao ni vibaraka wa
CCM na serikali, na kama kamati hizo zitajitokeza aliwaamuru wafunge
milango na madirisha ya misikiti kuwapiga.
Baada ya kusomewa mashitaka hayo shekh Ponda
anayetetewa na mawakili wasomi Barthoromew Tarimo na Ignas Punge alikataa mashataka yote matatu na hivyo upande wa mashitaka
kupinga dhamana kwa madai kuwa shekh Ponda anatumikia kifungo cha nje na
kwamba hakutakiwa kufanya kosa, hata hivyo anakabiliwa na makosa
mengine.
No comments:
Post a Comment