Bondia FATAKI toka Mpanda juzi alishushia kipigo cha nguvu bondia Tadeo toka Dar es salaam kwa kumtwanga kwa KO katika raundi ya pili tu tena sekunde za mwanzoni.
Pambano hilo ambalo ni la kwanza kufanyika mkoani Katavi lilisimamiwa na shirikisho la ngumi za kulipwa nchini TPBO.
Said Kassim Chaku ambaye pia ni katibu wa TPBO ndio alikuwa mwamuzi wa pambano hilo ambalo lilitangulia na mapambano mengine mawili na burudani mbalimbali zikiwemo muziki toka kwa vijana wa mkoani katavi na mchezo wa TAI CHI
Majaji wa mapambano yote matatu walikuwa ni Steven Monela bondia na mwanajeshi mstaafu na Rey Mwanauta wote kutoka Katavi
maandalizi ya pambano glove zikiwa tayari kwa ajili ya pambano |
ulingo uliandaliwa vema |
wasanii D-touch na D-zela wakifanya yao |
Ally Bizo akishambulia jukwaa |
mkurugenzi wa Pamoja FM Emmanuel mallack akitoa neno |
Balbel King akifanya yake |
Balbel King |
Bondia kulwa akijiandaa kucheza pambano la utangulizi na Benjamini |
Benjamin akiwa tayari kumkabili kulwa |
Refarii said Chaku akitoa maelekezo kwa mabondia kabla ya pambano |
Ngumi jiwe shurti ukunje sura- chezea masumbwi wewe |
Konde sharti litokee mbali |
sio kama nakwepa bali navuta kasi ya konde |
MC kelly B akijumlisha hesabu na refa CHAKU |
benjamin ameshinda kwa pointi 39 dhidi ya 38 za mpinzani wake kwenye uzito wa unyoya |
Pambano la pili ambapo Oswald mwenye bukta nyekundu akipambana na Elfaz mwenye Blue |
refa yupo makini kwelikweli |
Oswald aliibuka kidedea kwa pointi 40 dhidi ya 36 za mpinzani wake |
mambo ya TAI CHII |
Radical Mnyama akifanya unyama jukwaani, funika mbayaaaaa |
kazi ilikuwepo Radical aliwasha moto vibaya yaani mpaka baaaasiiiiii |
mwana Kabende Fataki akiingia na wapambe wake |
Add caption |
Simon Tadeo kama Tyson atoki katikati anakufuata tu |
Makonde yaliendelea |
Tadeo akijaribu kuinuka bila ya mafanikio baada ya kupokea konde nene toka kwa Fataki |
King FATAKI akitia mbwembwe baada ya kumaliza mpinzani wake kwenye raundi ya pili |
refa akitangaza mshindi |
Steven Monela kocha wa Fataki akimpongeza kijana wake |
Ndondi sio ugomvi, baada ya kubondwa mnakuwa marafiki kama kawa, fair play |
Fataki akipongezwa na mashabiki wake |
Fataki akiwashukuru mashabikimkwa sapoti yao |
La Captain akiwa kazini |
wasanii radical na ally bizo wakimpongeza kaka yao fataki |