by zangii ze icon
Tabu Ley: Mshumaa uliozimika kimyakimya *Aacha watoto 68 akiwa na miaka 76
JINA KAMILI : Pascal-Emmanuel Sinamoyi Tabu, ni mwanamuziki nguli wa Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo (DRC).
JINA LA KIMUZIKI : Maarufu kwa jina la Tabu Ley Rochereau.
MWANAMUZIKI WA AINA GANI? Alikuwa ni mwanamuziki wa miondoko ya Afrika ya aina ya Rhumba
AMEFARIKI : Amefariki Dunia Novemba 30, mwaka huu
AMEZALIWA : Tabu Ley alizaliwa Novemba
13, kati ya mwaka 1937 katika mji wa Bagata kwenye nchi iliyokuwa
ikijulikana kama Congo ya Ubelgiji (Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo).
ANAWATOTO WANGAPI? Anawatoto 68 ambao amezaa na wanawake tofautitofauti.
SAFARI YAKE YA MUZIKI : Alikuwa
kiongozi wa bendi ya muziki wa dansi iitwayo Orchestre Afrisa
International na alikuwa mmoja wa waimbaji wa Afrika wenye mvuto na
mtunzi mahiri.
ALIFANYA VITU GANI KUBORESHA MUZIKI WAKE :
Akiwa pamoja na mpiga gita mashuhuri Dkt. Nico Kasanda, Tabu Ley
alikuwa mwasisi wa mtindo wa soukous (Rumba ya Afrika) na muziki wake
aliufanya kuwa wa kimataifa kwa kutia vionjo vya muziki wa asili wa
Congo na rhumba la Cuba, Caribbean na Latin America.
MTU MASHUHURI WA CONGO : Tabu Ley au
ukipenda Rochereau, anaelezewa kama 'mtu mashuhuri' wa Congo ambaye,
pamoja na Rais Mobutu Sese seko, waliweka historia ya Afrika katika
karne ya 20."
JINA ALILOPEWA KUTOKANA NA KAZI YAKE :
Kutokana na umahiri wake katika muziki wa rhumba, Tabu Ley aliwahi
kupewa jina la "Elvis wa Afrika" na gazeti la 'Times' la Los Angeles
nchini Marekani.
MBALI NA MUZIKI ALIKUWA MWANASIASA : Baada ya kuangushwa utawala wa Mobutu, Tabu Ley pia aliingia katika siasa.
JUMLA YA NYIMBO ALIZOTUNGA : Wakati wa enzi zake, Tabu Ley aliweza kutunga nyimbo mpaka 3,000 na kutoa albamu 250.
ALIANZA MUZIKI LINI?: Tabu Ley au
Rochereau, alianza kazi ya muziki mwaka 1956 wakati alipoimba pamoja na
Joseph Kabasele Yampanya 'Pepe Kalle' akiwa na bendi yake ya African
Jazz.
Baada ya kumaliza kidato cha sita, Tabu Ley aliamua kuwa mwanamuziki
wakati wote. Tabu Ley alitoa wimbo uitwao 'Cha Cha' kusherehekea uhuru
wa Congo kutoka Ubelgiji mwaka 1960.
ALIFANYA MUZIKI NA WASANII GANI? Wimbo
huu wa 'Cha Cha' ulitungwa na Pepe Kalle, ambapo ulimpaisha Tabu Ley na
kupata umaarufu kwa haraka sana. Tabu Ley alibaki na bendi ya African
Jazz mpaka mwaka 1963 wakati yeye na Dkt. Nico Kasanda walipounda bendi
yao, African Fiesta.
ALIFUNGUA BENDI: Miaka miwili baadaye,
Tabu Ley na Dkt. Nico walisambaratika na Tabu Ley akaunda bendi yake
ambayo ilikuwa ikijulikana kama African Fiesta National, na pia
ilijulikana kama African Fiesta Flash.
Bendi ya African Fiesta National ilikuwa moja ya bendi zenye mafanikio
makubwa katika historia ya muziki wa Afrika, ikirekodi nyimbo kali kama
'Afrika Mokili Mobimba'.
WIMBO GANI ULIOVUNJA REKODI YA MAUZO ? Wimbo Wa 'Afrika Mokili Mobimba' ilivunja rekodi ya mauzo kwa kuuza nakala milioni moja mwaka 1970.
Wakati huo, Papa Wemba na Sam Mangwana walikuwa miongoni mwa wanamuziki waliotakatisha kundi la African Fiesta National.
JINA GANI LA JUKWAA ALILOCHUKUA? Tabu
Ley alichukua jina la jukwaa la 'Rochereau' kutoka kwa Generali wa Jeshi
la Ufaransa, Pierre Denfert-Rochereau, ambaye alisoma naye shule moja
na kulipenda jina lake.
SAFARI YA BENDI : Mwaka 1970, Tabu Ley
aliunda bendi ya Orchestre Afrisa International, Afrisa ikiwa ni
mchanganyiko kati ya jina Afrika na Isa, alama ya muziki wake.
Akiwa pamoja na Franco Luambo Makiadi wa TPOK Jazz, Afrisa ikawa moja ya
bendi kubwa barani Afrika. Walirekodi vibao kama 'Sorozo', 'Kaful
Mayay', 'Aon Aon', na 'Mose Konzo'.
ALIVUMBUA VIPAJI VIPYA : Katikati ya
miaka ya 1980, Tabu Ley aliweza kugundua kipaji cha mwanadada mwimbaji
na mcheza shoo, M'bilia Bel, ambaye alichangia sana kuipaisha bendi ya
Orchestre Afrisa International.
M'bilia Bel alikuwa mwimbaji mwanamke wa kwanza wa muziki wa soukous, ambaye alijipatia umaarufu Afrika yote.
MAISHA YA MAPENZI : Tabu Ley na M'bilia
Bel baadaye walifunga ndoa na kupata mtoto mmoja. Mwaka 1988 Tabu Ley
alimuibua mwanamuziki mwingine wa kike ajulikanaye kama Faya Tess.
Kuona Faya Tess ananyanyuka kwa kasi, M'bilia Bel aliamua kuondoka
katika bendi hiyo na kuendelea kufanya vizuri katika kazi za muziki
akiwa kivyake.
Baada ya M'bilia Bel kuondoka, mvuto wa bendi ya Afrisa pamoja na ule wa
wapinzani wao TPOK Jazz uliendelea kufifia kutokana na mashabiki
kugeukea mtindo mpya wa muziki wa soukous wenye kasi zaidi.
Baada ya utawala wa Rais Mobutu Sese Seko kuanzishwa katika Congo,
Rochereau akachukua jina la 'Tabu Ley' kama sehemu ya kampeni ya Mobutu
kuwafanya wananchi wa Zaire kuwa na majina ya asili.
SABABU ZILIZOMFANYA ATOROKE: Hata hivyo, mwaka 1988 Tabu Ley alitoroka na kwenda kuishi uhamishoni nchini Ufaransa.
Mwaka 1985, Serikali ya Kenya ilipiga marufuku muziki wa kigeni kuchezwa kwenye Redio ya Taifa.
Baada ya Tabu Ley kutunga wimbo 'Twende Nairobi', aliouimbwa na M'bilia
Bel, kumsifu Rais wa Kenya wakati huo, Daniel Arap Moi katazo hilo mara
moja likaondolewa.
Mapema 1990 Tabu Ley aliishi kwa muda mfupi Kusini ya California nchini
Marekani. Alianza kutengeneza muziki wake kuwa wa kimataifa zaidi na
kuingiza lugha ya Kingereza na kuongeza staili za kucheza kuwa za
kimataifa zaidi kama vile Samba.
Rochereau aliona kupata mafanikia kwa kutoa albamu kama Muzina, Exil Ley, Africa worldwide na Babeti soukous.
Utawala wa Mobutu ulipiga marufuku albamu yake ya mwaka 1990 iitwayo
'Trop, C'est Trop' ambayo aliiona kama inamchafua. Mwaka 1996, Tabu Ley
alishiriki katika albamu iitwayo Gombo Salsa iliyotolewa na bendi ya
Africando.
Wimbo wa 'Paquita' kutoka albamu ya Gombo ni moja ya wimbo uliowahi
kurekodiwa mwishoni mwa miaka ya 1960 na bendi ya African Fiesta.
Wakati Rais Mobutu Sese Seko alipoondolewa madarakani mwaka 1997, Tabu
Ley alirudi Kinshasa na kupewa Uwaziri katika serikali mpya ya Rais
Laurent Kabila.
Kutokana na kifo cha Laurent Kabila, Tabu Ley kisha alijiunga na Bunge
teule la mpito lililoundwa na Joseph Kabila, mpaka lilipovunjwa baada ya
kuundwa kwa taasisi za mpito.
CHEO ALICHOPATA : Novemba 2005, Tabu
Ley aliteuliwa kuwa Kaimu Gavana Kinshasa, nafasi aliyopewa kutokana na
chama chake cha Congolese Rally for Democracy, kutokana na makubaliano
ya amani 2002.
AMESHWAHI KUWA WAZIRI : Tabu Ley
aliyewahi pia kuwa Waziri wa Utamaduni, inasemekana amezaa watoto 68 na
wanawake tofauti tofauti, akiwemo rapa mashuhuri wa Ufaransa,
Youssoupha.
Rochereau amekufa akiwa na umri wa miaka 76 katika Hospitali ya
Mtakatifu Luc mjini Brussels, Ubelgiji ambako alikuwa akipata matibabu
ya ugonjwa wa kiharusi uliomkumba mwaka 2008.
No comments:
Post a Comment