Mshindi wa tuzo za Grammy, Alicia Keys amepata mchongo kwa mara ya kwanza na kuiuza bidhaa ya urembo ambapo amesainiwa kuwa kisura kwenye perfume ya Givenchy.
Mwimbaji wa label ya Chocolate City, Victoria Kimani amewashirikishwa Ommy Dimpoz na Diamond kwenye wimbo wake anaotarajia kuuachia May 14, unaitwa bokodo ‘Prokoto’.
Wakali hao wameutengeneza wimbo huo kwa kuunganisha lugha mbili ambazo ni Kiswahili na Kiingeza ili kutengeneza kitu ambacho kuwashika mashabiki wao kwa ujumla.
Prokoto haina maana ila ni neno tu la kutunga ambalo limetumika kama alivyozoea kufanya Dully Sykes kwenye nyimbo zake nyingi.
“Prokoto ni jina la kubuni tu ambalo itakuwa style mpya ya uchezaji, watu wataona itakavyotoka video ambayo tunatarajia kushoot very soon.” Ommy Dimpoz ameiambia Bongo5.
Ommy Dimpoz ameeleza kuwa ‘Prokoto’ ni wimbo mkali sana wa kuchezeka ambao anaamini kwa kutumia lugha hizo mbili wimbo huo utaishika Afrika nzima.
Victoria Kimani yuko Tanzania na inawezekana akawa anaendelea na mchakato wa kushoot video ya Prokoto..