Wawili hao wamerekodi wimbo huo kwenye studio za AM Records chini ya producer Manecky Jumapili iliyopita
Mirror ameiambia Pro-24 Blog kuwa alifanikiwa kumpata Chameleone na kumshirikisha kwenye wimbo wake huo baada ya kukutanishwa na meneja wake (Mirror) waliyekutana na Chameleone kwenye tuzo za KTMA zilizofanyika Jumamosi kwenye ukumbi wa Mlimani City.
Amesema kesho yake alifanikiwa kumsikilizisha baadhi ya nyimbo zake na Chameleone akamshauri warekodi wimbo mpya kabisa.
“Kila kitu tumeshamaliza ni wimbo unasubiri kufanyiwa finishing tu uwe tayari,” amesema.
“ I am so happy kwanza ni ndoto yangu kwasababu Chameleone ni msanii mkubwa ambaye mimi nimeanza kumwangalia, kumsikiliza tokea niko mdogo so nilikuwa na dream kufanya naye kazi siku moja. Nafikiri na yeye pia amenikubali kama ni msanii mchanga ambaye ndio ninatoka sasa hivi. I am so proud kwanza kufanya nyimbo naye na nyimbo ni kali, watu wategemee kitu kikubwa sana,” amesema Mirror.
No comments:
Post a Comment