Mwimbaji wa label ya Chocolate City, Victoria Kimani amewashirikishwa Ommy Dimpoz na Diamond kwenye wimbo wake anaotarajia kuuachia May 14, unaitwa
Wakali hao wameutengeneza wimbo huo kwa kuunganisha lugha mbili ambazo ni Kiswahili na Kiingeza ili kutengeneza kitu ambacho kuwashika mashabiki wao kwa ujumla.
Prokoto haina maana ila ni neno tu la kutunga ambalo limetumika kama alivyozoea kufanya Dully Sykes kwenye nyimbo zake nyingi.
“Prokoto ni jina la kubuni tu ambalo itakuwa style mpya ya uchezaji, watu wataona itakavyotoka video ambayo tunatarajia kushoot very soon.” Ommy Dimpoz ameiambia Bongo5.
Ommy Dimpoz ameeleza kuwa ‘Prokoto’ ni wimbo mkali sana wa kuchezeka ambao anaamini kwa kutumia lugha hizo mbili wimbo huo utaishika Afrika nzima.
Victoria Kimani yuko Tanzania na inawezekana akawa anaendelea na mchakato wa kushoot video ya Prokoto..
|
Thursday, 8 May 2014
Maana ya wimbo mpya wa Victoria Kimani aliowashirikisha Ommy Dimpoz na Diamond 'Prokoto' unatoka May 14
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment