Tuesday, 1 July 2014

Nikki Mbishi aeleza sababu za kuisogeza mbele project ya Ufunuo na collabo aliyofanya na Collo


Rapper wa Tamaduni music, Nikki Mbishi ambaye aliwafanya mashabiki wake waisubiri kwa hamu siu ya June 16 ambayo ilikuwa inaonekana kwenye akaunti zake za Twitter na jina project yake ya ‘Ufunuo’.
Nikki Mbishi ameeleza kuwa tarehe hiyo ilikuwa tarehe ya kuzaliwa ya mwanae Malcom amapo alikuwa ameiweka kama siku muhimu kwake.
Hata hivyo rapper huyo ameeleza kuwa alilazimika kutotoa Ufunuo siku hiyo kwa kuwa rapper mwenzake One The Incredible alikuwa amepanga kauchia mradi wake June 11 kwa hiyo ratiba ingekuwa nzuri kibiashara.
“Ile tarehe ilikuwa tarehe ya kuzaliwa kwa Malcom kwa hiyo niliiweka tu vile lakini nilikuwa najua siwezi kufanya hivyo kwa sababu One pia alitangaza kutoa kazi yake. Kwa hiyo One angetoa tarehe 11 mwezi wa 6 na mimi nikatoa tarehe 16 mwezi wa 6 ingekuwa sio biashara ni utoto kwa kuwa tungekuwa tunashindana sisi wenyewe kuuza.” Amesema Nikki Mbishi.
Hata hivyo, kutokana na sababu zilizo juu ya uwezo wao, One The Incredible pia alishindwa kutoa kazi yake kama ilivyopangwa.
Nikki Mbishi amewaahidi mashabiki wake kuwa mwisho wa mwaka huu ni lazima aitoe albam ya Ufunuo kwa ajili yao.
Katika hatua nyingine, Nikki ameeleza kuhusu collabo waliyofanya na King wa Rap Kenya, Collo kuwa ilikuwa ngoma waliyofanya pamoja mwaka jana na imekaa pending kwa muda mrefu huku kichwani kwake kukiwa na mipango tofauti na kwamba hana uhakika kama ataichia hivi karibuni.

No comments:

Post a Comment