Monday, 18 November 2013

KATAVI SPORTS BONANZA


by rahim kassonga
Tamasha kubwa la aina  yake na la kwanza la michezo limefanyika leo wilayani Mpanda mkoani Katavi kwa kushirikisha michezo  mbalimbali ikiwemo,mpira wa miguu kwa wanawake,wanaume na watoto,mpira wa pete,mpira wa wavu,riadha ,kukimbia na magunia,kufukuza kuku,mbio za walemavu na kushindana kunywa soda.
Tamasha  hilo lililofanyika katika viwanja vya azimio lilianza saa tatu asubuhi na kumalizika saa kumi na mbili jioni ambapo kamanda wa polisi mkoa wa katavi,Dhahiri Kidavashari ndiye alikuwa mgeni rasmi ambapo alitia baraka katika tamasha hilo kwa kupiga penati na kumfunga muhandisi Frank John wa Tanroad.
Katika hotuba yake kamanda Kidavashari alisisitiza kuwa michezo ni afya,michezo ni ajira lakini pia michezo inaleta undugu kwani inawakusanya watu pamoja na  kuongeza kuwa kama michezo ikitumika vizuri inapunguza uhalifu.
kikosi cha msakila
kikosi cha shule ya Uhuru
timu ya Msakila na Uhuru wakikaguliwa na waamuzi





Afisa michezo halmashauri ya mji-Revocatus Kalunde akifungua Bonanza
waamuzi wa mchezo wa ufunguzi, Daudi (kushoto), Ngalla (katikati) na Kaburu (kulia) wakiingia uwanjani tayari kwa mchezo wa ufunguzi
vijana wa msakila wakisalimiana kabla ya mchezo
kibatari nishati, the super MC akisherehesha



mchezaji wa Msakila akimiliki mpira
vijana wa Msakila wakimpongeza mwenzao baada ya kufunga goli
wanafunzi wa Msakila wakishangilia baada ya mpira kwisha na kuibuka washindi
Ulinzi ulikuwa wa kutosha


timu ya netiboli ya halmashauri ya wilaya ikifanya mazoezi kabla ya kuanza kwa mchezo huo

pasha..pasha..pasha

Timu ya vijana ikipokea maelekezo toka kwa mwalimu wao
MAELEKEZO
Timu za netiboli zikipokea maelekezo kabla ya kuanza kwa mchezo

KIVUMBI KIMEANZA
huwezi amini hadi mapumziko walikuwa wamefungana 16-16





Mkubwa ni mkubwa, mwishowe Halmashauri ya wilaya waliibuka na ushindi

SARAKASI
mambo ya sarakasi pia yalikuwepo, ilikuwa noumaaa sanaaaaaaaaaaaaaaa


WATU WENGIIIIIIIIIIIII
watoto kwa wakubwa, wanawake kwa wanaume


KUFUKUZA KUKU
mtu aliondoka na bonge la jogoo, ilikuwa nouma sanaa, weka mbali na watoto

wanaume wakijiandaa kufukuza kuku

refarii akitoa maelekezo

kuku anapasha
KAZI IMEANZA HATARIIIIIIIIIIIIIIIIIIII

HATIMAE JAMAA KAJIPATIA KITOWEO, kiroho safi




BURUDANI KADHAA ZILITO;EWA, mshikamano arts group nao waliwasha moto




RIADHA MITA 400 KINAMAMA  ilikuwa sooo,





HATARII SANAAA, jamaa akionesha mautundu kwa kucheza na baiskeli huwezi amini, mshikaji alivyotembelea tairi moja


KWENYE VOLLEYBALL NAKO PALIKUWA HAPATOSHI
veta na katavi walioneshana kazi




WEKA MBALI NA WATOTO, mbio za magunia zilifunika

kazi imeanza
huyu jamaa nouma sana, achana nae

soka la wanawake
AMSHA POPO, watoto wakipiga viduku













Tuesday, 12 November 2013

HUYU NDIO MSANII WA TAARABU ALIYEFARIKI DUNIA LEO.

by zangii ze icon


Marehemu Nyawana Fundikira enzi za uhai wake.

Msanii wa taarab nchini anayejulikana kwa jina la Nyawana Fundikira aliyetamba na wimbo wa 'Nipo Kamili Nimejipanga', amefariki dunia  kwa ugonjwa wa malaria.




Nyawana amefariki akiwa kwake maeneo ya

Mwananyamala B na mwili wake sasa umepelekwa kuhifadhiwa Hospitali ya Mwananyamala, Dar.

Marehemu Nyawana alizaliwa mwaka 1977 katika Hospitali ya Taifa Muhimbili na kupata elimu yake katika shule mbalimbali kuanzia Msingi, Sekondari na elimu ya juu.

Shule ya Msingi Zanaki ndipo alipopata elimu yake mwaka 1983 na kuhitimu mwaka 1989, wakati ile ya Sekondari alisoma Masjid Quba mwaka 1992 na kumalizia Al Haramain.

Baada ya hapo alisomea Uhadhiri kabla ya kumaliza na kusomea masomo ya Uandishi wa Habari na Utangazaji, ambapo pia alishiriki shindano la urembo na kunyakua taji la Miss Tabora, mwaka 1996.

Mbali na sanaa ya uimbaji, pia Nyawana ni mwandishi na mtangazaji, aliyefanya vyema mno, hasa kwa kutangaza vipindi vya taarabu, katika redio kadhaa, ikiwamo ile ya Voice of Tabora.

Baadhi ya nyimbo alizorekodi marehemu ni pamoja na 'Nipo Kamili Nimejipanga' na 'Umesharoga Wangapi', nyimbo ambazo zilitangaza na kuonyesha kipaji chake halisi.

Baadhi ya makundi ya taarab aliyowahi kufanya nayo kazi marehemu ni, Kings Modern Taarab na Tanzania Moto Modern Taarab, maarufu kama T-Moto.

MSANII PROFESA JAY APATA AJALI MBAYA YA GARI.


by zangii ze icon
Taarifa zilizotufikia hivi punde ni kwamba Mwanamuziki wa Hip hop, Joseph Haule 'Profesa Jay' amepata ajali ya gari baada ya kuparamia kifusi akijaribu kumkwepa mtu eneo la Kimara-Baruti, jijini Dar wakati akitoka nyumbani kwake Mbezi! Prof hajaumia sana katika ajali hiyo japo gari lake limeharibika.

PICHA;TIZAMA PICHA ZA UZINDUZI WA ALBUM YA MAKUHANI CHOIR JANA MAKANYAGIO

 by zangii ze icon
zangwinyo korobwinyo ....hatareee sana cheki nyomi mtu wangu

sema wewe....ni ful upako mpendwa....twende kazi
ilikuwa shangwe za ukweeee
ILIKUWA NI SIKU YA UZINDUZI WA ALBUM MPYA YA KWAYA HAPA MPANDA,


INAITWA MAKUHANI KWAYA,MGENI RASMI ALIKUWA MKURUGENZI WA RADIO MPANDA FM NA KWAKUWA ALIKUWA NJE YA NCHI KWA MATIBABU,ALIWAKILISHWA VEMA NA MENEJA KITUO GERLAD SETTY SEDEKIA 

AKIWA SAMBAMBA NA TEAM YA WAANDISHI WA HABARI MAHIRI TOKA 97.0 MPANDA FM SAUTI YA KATAVI 


RAHIM KASSONGA,BENEDICT KUZWA ,ALINANUSWE EDWARD NA TUNNU LUGOMBE AMBAYE ALIKUWA NDIYE MC WA SHUGHULI PALE KANISANI JIONEE PICHA HAPA
meneja kituo cha redio mpanda fm akikaribishwa na mchungaji na waumini kanisani


kwakutulia ....muite baba wawili ..kiroho safi  


mc tunu lugombe...bibi...amshaaaa popooo....
jambooo...makanyagioooo...haya nipo hapa kwa niaba mkurugenzi...amin mitha


mgeni rasmi...twakuomba uje uongee na wana katavi...huyu ndo mc bibi tunu

.....naahidi kwa niaba ya mkurugenzi wa mpanda fm..kutoa milioni mbili na nusu za ku shuti video yenu...pia promo kali ndani ya 97.0 voice of katavi....sedekia setty baba wawili



changizo likaendelea....



tuka pata risala kwa ufupi....



burudani.....




tuka maliza na kuondoka......


Thursday, 7 November 2013

Victoria Kimani amshambulia hater baada ya kumuita "Brainless Rihanna Copycut"


BY ZANGII ZE ICON
Mwanamuziki Victoria kimani, dada wa Rapper Bamboo ambae kwasasa anafanya vizuri na wimbo wake "Mtoto" amejikuta akipeleka majeshi kwa mtu mmoja ambae ni shabiki lakini ni hater ambae alithubutu kumwambia "hana akili"  kwa kuiga mavazi aliyokuwa ameyavaa Rihanna (Mexican Gangster) wakati wa haloween


Victoria Kimani kwenye haloween 2013