by rahim kassonga
Tamasha kubwa la aina yake na la kwanza la michezo limefanyika leo wilayani Mpanda mkoani Katavi kwa kushirikisha michezo mbalimbali ikiwemo,mpira wa miguu kwa wanawake,wanaume na watoto,mpira wa pete,mpira wa wavu,riadha ,kukimbia na magunia,kufukuza kuku,mbio za walemavu na kushindana kunywa soda.
Tamasha hilo lililofanyika katika viwanja vya azimio lilianza saa tatu asubuhi na kumalizika saa kumi na mbili jioni ambapo kamanda wa polisi mkoa wa katavi,Dhahiri Kidavashari ndiye alikuwa mgeni rasmi ambapo alitia baraka katika tamasha hilo kwa kupiga penati na kumfunga muhandisi Frank John wa Tanroad.
Katika hotuba yake kamanda Kidavashari alisisitiza kuwa michezo ni afya,michezo ni ajira lakini pia michezo inaleta undugu kwani inawakusanya watu pamoja na kuongeza kuwa kama michezo ikitumika vizuri inapunguza uhalifu.
|
kikosi cha msakila |
|
kikosi cha shule ya Uhuru |
|
timu ya Msakila na Uhuru wakikaguliwa na waamuzi |
|
Afisa michezo halmashauri ya mji-Revocatus Kalunde akifungua Bonanza |
|
waamuzi wa mchezo wa ufunguzi, Daudi (kushoto), Ngalla (katikati) na Kaburu (kulia) wakiingia uwanjani tayari kwa mchezo wa ufunguzi |
|
vijana wa msakila wakisalimiana kabla ya mchezo |
|
kibatari nishati, the super MC akisherehesha
|
|
mchezaji wa Msakila akimiliki mpira |
|
vijana wa Msakila wakimpongeza mwenzao baada ya kufunga goli |
|
wanafunzi wa Msakila wakishangilia baada ya mpira kwisha na kuibuka washindi |
|
Ulinzi ulikuwa wa kutosha |
|
timu ya netiboli ya halmashauri ya wilaya ikifanya mazoezi kabla ya kuanza kwa mchezo huo |
|
pasha..pasha..pasha |
|
Timu ya vijana ikipokea maelekezo toka kwa mwalimu wao |
MAELEKEZO
Timu za netiboli zikipokea maelekezo kabla ya kuanza kwa mchezo
KIVUMBI KIMEANZA
huwezi amini hadi mapumziko walikuwa wamefungana 16-16
|
Mkubwa ni mkubwa, mwishowe Halmashauri ya wilaya waliibuka na ushindi |
SARAKASI
mambo ya sarakasi pia yalikuwepo, ilikuwa noumaaa sanaaaaaaaaaaaaaaa
WATU WENGIIIIIIIIIIIII
watoto kwa wakubwa, wanawake kwa wanaume
KUFUKUZA KUKU
mtu aliondoka na bonge la jogoo, ilikuwa nouma sanaa, weka mbali na watoto
|
wanaume wakijiandaa kufukuza kuku |
|
refarii akitoa maelekezo |
|
|
|
kuku anapasha |
KAZI IMEANZA HATARIIIIIIIIIIIIIIIIIIII
HATIMAE JAMAA KAJIPATIA KITOWEO, kiroho safi
BURUDANI KADHAA ZILITO;EWA, mshikamano arts group nao waliwasha moto
RIADHA MITA 400 KINAMAMA ilikuwa sooo,
HATARII SANAAA, jamaa akionesha mautundu kwa kucheza na baiskeli huwezi amini, mshikaji alivyotembelea tairi moja
KWENYE VOLLEYBALL NAKO PALIKUWA HAPATOSHI
veta na katavi walioneshana kazi
WEKA MBALI NA WATOTO, mbio za magunia zilifunika
|
kazi imeanza |
|
huyu jamaa nouma sana, achana nae |
|
soka la wanawake |
AMSHA POPO, watoto wakipiga viduku
No comments:
Post a Comment