Mbeya
Wanafunzi wa Shule
ya Sekondari Lupata, inayomilikiwa na Jumuiya ya Wazazi (CCM) wilayani Rungwe
wamefanya vurugu na kuliteketeza kwa moto bweni la wavulana wakipinga kitendo
cha wanafunzi wenzao watatu kusimamishwa masomo kwa utovu wa nidhamu.
Kamanda wa Polisi
wa Mkoa wa Mbeya, Diwani Athuman, amesema vurugu hizo zilitokea juzi majira ya
saa 2:00 usiku baada ya wanafunzi waliosimamishwa masomo kuwahamasisha wenzao
kupinga adhabu hiyo.
Kamanda Diwani
amesema tukio hilo limesababisha uharibifu mkubwa wa mali za shule hiyo ingawa
moto huo haukusababisha madhara.
Amesema chanzo cha
vurugu hizo ni kutokana na wafunzi hao; Joseph Robert (18) mwanafunzi wa kidato
cha nne, Mwita Chacha (17) mwanafunzi wa kidato cha tatu wote wakazi wa
Kitunda, Dar es Salaam kusimamishwa masomo kwa utovu wa nidhamu.
Amesema mwanafunzi
mwingine anayehusika katika kuhamasisha wenzao kufanya vurugu hizo ni Daniel
David (18) anayesoma kidato cha tatu na mkazi wa Ipinda, wilayani Kyela.
Kutokana na tukio
hilo, amesema wanafunzi 15 wakiwamo waliosimamishwa masomo wanashikiliwa na
polisi kwa ajili ya mahojiano zaidi.
Arusha
Wadau wa utalii kutoka halimashauri
ya Wilaya ya longido wamekutana mjini arusha katika mkutano wa Siku Mbili wenye
lengo kuu la kutathimini na kutambua mchango wa Rasilamali zinazo wazunguka
wafugaji wa haliamashauri hiyo katika kujiletea uchumi kwa njia nyingine
tofauti na ile iliyozoeleka
Mkutano huo wa Wadau hao wa Utalii
kutokandani ya Halimashauri ya Wilaya ya longido ambao ulifunguliwa na Afisa wa
Mazingira ya Ikolojia kutokea mamlaka ya Hifadhi za Taifa Bwana
Alibert Mziray ambapo amesema kuwa kuna umuhimu mkubwa wa kujua jinsi ya kutumia Rasilimali zilizopo hasa kwa Wafugaji hao wa Loliondo.
Amesema kuwa jamii hizo zinatakiwa
kutambua kuwa kuna umuhimu mkubwa wa
kutambua kuwa mazingira ya asili yaliyowazunguka wafugaji wa kiasili yana
umuhimu mkubwa na ushirikiano nao hivyo inabidi wangalie jinsi gani
watashirikiana na mazingira yao katika maisha yao ya kila siku.
pamoja na hayo mkutano huo
uliwakuatanisha wadau hao wa utalii unatarajia kujadili na kupata njia muafaka
za kumsaidia mfugaji wa kiasili katika kufanya ufugajiwake uwe na tija ya
kiuchumi sambamba na kuwafanya wafugaji hao kutotegemea mifugo na kuangalia
njia nyingine za kiuchumi zitakazo wafanya wapate maendeleo.
Kwa sasa hivi mradi wa BFFS wilayani
longido wamefanikiwa kuwafikia zaidi ya wamasai 300 ambapo zaidi ya asiliamia
90 ni wanawke ambapo wamefanikiwa kwa awmu ya kwanza kuwapatia mkopo wa zaidi
ya milioni 90 kwa vikundi zaidi ya 30 ambapo wamelenga kwa awamu ya pili
kuvipatia vikundi vipatavyo 48 mkopo wa kuwasaidi kaya hizo za wafugaji.
Arusha 16/05/2013
MKE wa waziri mkuu Mama Tunu Pinda amewaasa
Makatibu Muhtasi na kuwataka wazingatie maadili ya taaluma yao ya uhazili ili
kuongeza ufanisi wa majukumu ya kazi zao.
Ametoa wito hu o leo wakati akifungu Kongamano la
Tatu la Makatibu Muhtasi (Tanzania Personal Secretaries Association – TAPSEA)
kwenye ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa Arusha (AICC), Jijini Arusha.
Kongamano hilo la siku mbili, limehudhuriwa na
Makatibu Muhtasi zaidi ya 1,500 kutoka mikoa yote nchini, na baadhi ya
wawezeshaji kutoka Kenya, Uganda na Rwanda.
Amewataka waongeze jitihada za kukimarisha Chama
cheo ili hatimaye TAPSEA iweze kuenea Mikoa yote na kuwa Chombo
kitakachosimamia miiko na maadili ya fani ya Uhazili.
Amesema majukumu ya makatibu muhtasi siyo kupiga
chapa pekee na kuongeza kwamba, kama chama cha kitaaluma, TAPSEA lazima
iendeleze jitihada za kubadili mtazamo huo ili jamii iweze kutambua umuhimu wa
nafasi ya makatibu muhtasi katika taasisi mbalimbali za umma na za sekta
binafsi.
Mama Tunu Pinda amesema kuwekeza katika
teknolojia ni jambo muhimu lakini teknolojia pekee haiwezi kuleta mabadiliko
chanya katika kuboresha huduma na kuongeza tija
Mama Tunu Pinda pia amezindua TAPSEA SACCOS na
kuwataka makatibu muhtasi hao wajiunge kwa wingi ili kutunisha mfuko wa chama
chao.
Mapema, akimkaribisha kuzungumza na washiriki wa
mkutano, Mlezi wa TAPSEA Dk. Mary Nagu ambaye pia ni Waziri wa Nchi, Uwekezaji
na Uwezeshaji aliwataka wawe waaminifu katika kuijenga TAPSEA SACCOS ili
hatimaye ifikie hatua ya kuwa benki yao maalum kama ilivyo kwa Chama cha Walimu
nchini.
Naye Naibu Waziri wa Katiba na Sheria, Bi. Angela
Kairuki ambaye pia mshauri wa Kisheria wa TAPSEA aliwataka washiriki wa
kongamano hilo kuzingatia maadili kwa kutunza siri za ofisi wanazozitumikia.
Arusha 16
Jeshi la Polisi mkoani Arusha limekanusha taarifa ya
kuachiwa huru kwa mtuhumiwa wa ujangili Bw. Frank William Silangei
maarufu kwa jina la “Ojung’s Mwarusha” mkazi wa Ngaramtoni Kibaoni.
Fatma amasi
Kamanda wa polisi mkoa wa Arusha Liberatus Sabas
amesema kuwa mtuhumiwa huyo mwenye umri wa miaka 32 hivi sasa yuko
mahabusu na taratibu za kumfikisha mahakamani zinaendelea kufanyika.
Kamanda Sabas ameeleza kuwa mtuhumiwa
Silangei hajaachiwa huru kama ilivyoripotiwa
Kamanda Liberatus Sabas amesema Serikali kupitia
Jeshi la Polisi itaendelea na
jitihada zake za kuhakikisha kuwa vitendo vyote vya ujangili vinatokomezwa na
yeyote atakayehusika na vitendo hivyo atachukuliwa hatua za kisheria.
Wakurugenzi
wa Upelelezi wa makosa ya jinai kutoka nchi 25 barani Afrika wametakiwa kutumia
vizuri mafunzo ya Operesheni za pamoja ili kuweza kukabiliana na uhalifu
ikiwemo vitendo vya ugaidi na uhamiaji haramu vinavyojitokeza katika nchi za
Afrika Mashariki na Kusini mwa Afrika kwa kasi hivi sasa.
Aziza seif
Hayo
yamesemwa na Mkurugenzi wa
Upelelezi wa Makosa ya Jinai Nchini DCI Robert Manumba wakati akizungumza na
waandishi wa habari baada ya kufungua Mafunzo kwa Wakurugenzi wa Upelelezi wa
Makosa ya Jinai kutoka Umoja wa Wakuu wa Polisi Kusini mwa Afrika (SARPCCO)
Pamoja na Umoja wa Wakuu wa Polisi Afrika Mashariki (EAPCCO) kuhusu
kufanya operesheni za pamoja kukabiliana na uhalifu unaovuka mipaka.
DCI
Manumba amesema uhalifu unaofanyika hapa nchini na ukanda huu wa Afrika
Mashariki ndio huo huo unaotokea katika nchi nyingine hivyo ushirikiano na
kubadilishana taarifa kutasaidia kutambua na kuweka mikakati thabiti ya kuweza
kudumisha amani na usalama katika bara la Afrika.
Kwa upande
wake Mkuu wa Polisi wa Kimataifa INTEPOL kanda ya Afrika Mashariki kutoka
Nchini Kenya Bw.Rego Francis amesema Majeshi ya Polisi yana wajibu wa kutoa
elimu ya kutosha kwa wananchi ili waweze kutoa taarifa za uhalifu mapema
kwa vyombo vya usalama ili ziweze kufanyiwa kazi mapema kabla ya matukio
kutokea.
Naye
Mkuu wa Kitengo cha Polisi wa Kimataifa (INTEPOL) Tanzania Kamishna Msaidizi wa Polisi Gustavus Babile
amesema Mafunzo hayo ya siku mbili lengo lake ni kubadilishana uzoefu na
kupeana mbinu na kuweka mikakati ya kufanya operesheni zitakazoweza
kuutokemeza uhalifu.
Babile
amesema kupitia mafunzo hayo wataweza kuandaa Operesheni zenye mafanikio
zitakazoweza kushirikisha nchi nyingi katika kukabiliana na Ugaidi, Madawa ya
kulevya, wahamiaji haramu, wizi wa magari na uhalifu wa aina nyingine unaotokea
hapa Afrika.
Mafunzo
hayo yanafanyika baada ya kumalizika kwa Mkutano wa kumi na nane wa Wakuu wa Polisi
kusini mwa Afrika ambapo katika maazimio
yaliyofikiwa ni pamoja na kufanya operesheni za pamoja baina ya SARPCCO na
EAPCCO.