Sunday, 19 May 2013

Korea Kaskazini yarusha makombora ya masafa mafupi

Raia mmoja wa Korea Kusini akifuatilia kwenye televisheni urushaji wa makombora uliofanywa na Korea Kaskazini.Raia mmoja wa Korea Kusini akifuatilia kwenye televisheni urushaji wa makombora uliofanywa na Korea Kaskazini.
ukubwa wa habari
Korea Kusini inasema Korea Kaskazini imefyatua makombora matatu ya masafa mafupi katika bahari ya East Sea ambayo pia hujulikana kama Sea of Japan.

Wizara ya Ulinzi ya Korea Kusini inasema imegundua kurushwa kwa makombora mawili Jumamosi asubuhi, na jingine lilirushwa nyakati za mchana.

Msemaji wa wizara hiyo, Kim Min-seok anasema azma ya Kaskazini haiko bayana. Anasema jeshi la Korea Kusini linafuatilia kwa karibu urushaji mwingine wowote na uwezekano wa uchokozi.

Shirika la habari la Japan, Kyodo limeripoti kuwa afisa mmoja wa Japan amethibitisha kuhusu majaribio hayo na kusema makombora hayakuangukia katika maji ya Japan.

Maendeleo haya yamekuja katika kipindi cha mawasiliano ya kidiplomasia yanayolenga kupunguza mivutano. Mapema mwaka huu, Pyongyang ilitishia kufanya mashambulizi ya nyuklia kwa Korea Kusini na Marekani kufuatia  mazoezi ya kijeshi ya kila mwaka kati ya Marekani na Korea Kusini na vikwazo vya Umoja wa Mataifa vilivyowekewa kaskazini baada ya majaribio yake ya tatu ya nyuklia mwezi Februari.

No comments:

Post a Comment