Friday, 17 May 2013

Wapenzi wa jinsia moja wabaguliwa Ulaya


Wapenzi wa jinsia moja huhofia kuripoti kwa polisi visa vya dhulma dhidi yao
Muungano wa Ulaya umetoa ripoti kuonyesha kuwa zaidi ya robo ya wapenzi wa jinsia moja waliohojiwa wameshambuliwa ama kutishwa katika miaka mitano iliyopita.
Ripoti hiyo iliandaliwa na wataalamu wa muungano huo kuboresha sera zinazoelekea kutenga watu kutokana na hulka zao za mapenzi.
Watu elfu tisini na tatu wanaoishi Ulaya walihojiwa kuhusu namna wapenzi wa jinsia moja wanavyochukiwa na kutengwa. Majibu yao yaliyowasilishwa kwenye mtandao yalionyesha katika miaka mitano zaidi ya robo walishambuliwa ama kutishwa.
Na shuleni wanafunzi wawili kati ya watatu waliohojiwa walisema kuwa walificha kuwa wao ni wapenzi wa jinsia moja.
Kinachotia wasiwasi ni kuwa zaidi ya nusu yao hawako radhi kuripoti visa vya kushambuliwa kwa polisi kwa sababu wanaamini kuwa hakuna kitakachofanyika.
Wanasiasa na watunga sera mia tatu wanakutana Hague Uholanzi kujadili njia mpya za kuwalinda watu na kuhakikisha kuwa hawashambuliwi hata wakipendelea mapenzi ya jinsia moja.

No comments:

Post a Comment