Friday, 17 May 2013

Askofu Mtega afafanua sababu za kustaafu kwake

Askofu Mkuu Mstaafu wa jimbo Katoliki la Songea, Mhashamu Norbert Mtega
Askofu Mkuu Mstaafu wa jimbo Katoliki la Songea, Mhashamu Norbert Mtega
Askofu Mkuu Mstaafu wa jimbo Katoliki la Songea Mhashamu Norbert Mtega ametoa ufafanuzi juu ya uamuzi wake wa kumuomba Baba Mtakatifu kustaafu na kusema amefanya hivyo kwa maslai ya jimbo kuu Katoliki la Songea baada ya kubaini kuwa afya yake haimwezeshi kumudu majukumu ya kiutawala ya jimbo hilo.
 Askofu Mtega mwenye umri wa miaka 68 amesema licha ya kustaafu kwake ataendelea kufanya majukumu ya kitume kama kawaida na amechagua kuishi Songea baada ya kustaafu huku akitaka wakatoliki wa jimbo hilo wasiwe na wasiwasi na uamuzi wake.
Baada ya saa kadhaa za maombi ya wandishi wa habari waliokua na kiu ya kuzungumza na Askofu huyo juu ya uamuzi wake wa kuomba kustaafu na hatimaye kukubaliwa na Baba Mtakatifu Papa Francis, hatimaye wakakutana nae majira ya jioni, na kwanza ilikua ni kutaka ufafanuzi wa kwa nini amechukua hatua hiyo iliyoshitua watu wengi.
Pili, waandishi wa Habari walitaka kujua kwa nini afanye hivyo wakati umri wake wa kustaafu kwa hiari ambao ni miaka 70 haujafika, wala kustaafu kwa lazima ambao ni miaka 75 hajafikia na tatu, tukataka kujua Askofu Mtega angependa Askofu Ajae afanye nini kwa maslai ya jimbo kuu katoliki la Songea.
Aidha Askofu Mtega amesema hakuna lolote baya lililosababisha yeye astaafu kazi hiyo ya kuhudumia jimbo kuu katoliki la Songea ambalo kiutawala linasimamia majimbo nane ya kusini mwa Tanzania.
Gerson Msigwa, TBC Ruvuma.

No comments:

Post a Comment