Sunday, 22 September 2013

AFRIKA YAIPA WASIWASI FIFA!!


NI KUTOKUJUA WA SHERIA???
INATOKEA AFRIKA TU, DUNIA NZIMA HAITOKEI!!
by rahim kassonga


FIFA imepatwa na wasiwasi mkubwa kuhusu Timu za Afrika kuvunja Sheria na kuchezesha Wachezaji wasiostahili kwenye Mechi za Mchujo za Kombe la Kombe la Dunia na sasa wanataka kulishughulikia tatizo hilo ipasavyo.
Wasiwasi huo umetangazwa na Mkurugenzi wa Mashindano wa FIFA Mustapha Fahmy hapo Jana.
Katika Mechi 8 za Mchujo za Kombe la Kombe la Dunia Kanda ya Afrika Matokeo ilibidi yafutwe baada ya Timu kuchezesha Mchezaji asiestahili ama kwa Sheria za Uraia au kuwa Kifungoni kufuatia kupewa Kadi katika Mechi za nyuma.
Kwenye Mechi zote hizo 8, Matokeo yalifutwa na Pointi 3 na Bao 3 kupewa Wapinzani wa Timu iliyokiuka Sheria na hilo lilileta athari kubwa kwenye Timu husika na Makundi yao.
Fahmy amesema: “Tumepatwa wasiwasi na hili ambao ni ukiukwaji wa wazi wa Sheria ambazo ziko wazi. Na hili limetokea katika Bara moja tu Duniani…Afrika. Mengine kama Ulaya, Asia na Marekani ya Kusini hamna hata tukio moja.”
Fahmy amesema kuwa inabidi wao kutafakari nini kimetokea na kutafuta ufumbuzi ili makosa haya yasijirudie tena.
Tukio la mwisho la ukiukwaji huu wa Sheria ni baada ya Cape Verde kuifunga Tunisia Bao 2-0 huko Tunis na kutwaa ushindi wa Kundi lao na hivyo kutinga Raundi ya Mwisho ya Mtoano lakini ikagundulika walimchezesha Mchezaji ambae alitakiwa kuwa kwenye Kifungo cha Mechi 4.
Cape Verde wakafutiwa ushindi na Tunisia, ambao Kocha wao Nabil Maaloul, alijiuzulu baada ya kipigo hicho, kupewa Pointi 3 na Goli 3 na hivyo wao kufuzu kuingia aundi ya Mwisho ya Mtoano ambayo itatoa Timu 5 kwenda Brazil.
Tunisia watacheza na Cameroun kwenye Raundi hiyo.
Cha ajabu ni kuwa, kwenye Kundi hilo hilo la Cape Verde na Tunisia, ni hao hao Cape Verde walionufaika walipofungwa 4-3 na Equatorial Guinea na baadae kupewa ushindi baada ya Equatorial Guinea kumchezesha Mchezaji asiestahili kwenye Mechi hiyo.

Formula 1 – Perez hahofii kuhusu mustakabali wa baadae na kampuni ya McLaren



Dereva Sergio Perez amesisitiza kuwa hahofii mustakabali wake wa baadae na kampuni McLaren, japokuwa team hiyo imeweka bayana mpango wao wa kumleta dereva Fernando Alonso kwa ajili ya kumbadilisha nae


Mkuu wa team ya McLaren Martin Whitmarsh ameweka bayana nchini Singapore kwenye Singapore Grand Prix kwamba team inataka kuona mabadiliko chanya toka Perez kabla ya kumpa mkataba mwingine mwakani.
Na kuongeza kuwa mtu ambaye anatakiwa kwa kuchukua nafasi yake ni dereva mmexixo Alonzo ambaye alishasema kwamba asingependa kurudi kwenye timu hyo hivi karibuni
Perez alisema hajahusishwa kuhusu suala hilo na anauhakika atakuwepo kwenye timu ya Mc Laren mwakani
Aliongeza kuwa, unatakiwa kufanya kazi kwa bidii kwenye timu yoyote utakayokuwepo, siku zote unatakiwa kufanya vema zaidi na kitaalam
Akizungumzia kuhusu kauli ya bosi wake amesema kuwa, kauli hiyo ya Whitmarsh ni kauli ya kumwamsha ili aongeze juhudi
"ndio kitu ninachofanya na najaribu kutoa kitu nilichonacho kwa ufanisi wa hali ya juu, umekuwa wakati mgumu msimu huu kwetu sote, lakini kila siku nasema maisha yangu ya baadae hapa yapo sawa
Nitakuwepo hapa mwaka ujao na ngoja tuone, ninaimani tutarudi na kupigania ubingwa mwaka ujao

Qatar yawatoa wasiwasi kuhusu Kombe la Dunia 2022



Qatar imesisitiza kuwa inaweza kuandaa dimba la Kombe la Dunia mwaka wa 2022 katika majira ya joto, hata wakati Shirikisho la FIFA likiendelea kuwekewa mbinyo wa kuhamisha tamasha hilo hadi msimu wa baridi 

Taifa hilo lenye utajiri wa nishati, ambako nyuzijoto hufikia sentigredi 45 ilipewa kibali cha kuandaa Kombe la Dunia miaka mitatu iliyopita katika uamuzi wa kushangaza.
Qatar inasema inaweza kukubali kuhamisha dimba hilo hadi msimu wa baridi lakini ikasisitiza kuwa licha ya joto kali, inaweza kuandaa Dimba la Dunia msimu wa joto kwa kujenga viwanja vyenye hewa ya baridi kwa kutumia teknolojia mpya inayojali mazingira.
Namna ambavyo mashabiki wataweza kukabiliana na joto, nje ya viwanja, bado ni suala linalotia wasiwasi na Rais wa FIFA Sepp Blatter hivi karibuni amesema lilikuwa kosa kupanga kinyang'anyiro hicho cha msimu wa joto, katika taifa la jangwa.
Rais wa Shirikisho la Soka barani Ulaya UEFA, Michel Platini pia amethibitisha kuwa mashirikisho 54 wanachama wa UEFA wamekubaliana kwa kauli moja kuhusu wazo la kuhamisha dimba hilo la Qatar, hadi msimu mwingine wa mwaka
Lakini nayo kamati andalizi ya Qatar imejaribu kuondoa wasiwasi hiyo, kwa kusema teknolojia ya kuleta hewa ya baridi, kwa kutumia solar, katika maeneo ya umma, nje na ndani ya viwanja, huenda ikatatua shida hizo.