NI
KUTOKUJUA WA SHERIA???
INATOKEA
AFRIKA TU, DUNIA NZIMA HAITOKEI!!
by rahim kassonga
FIFA
imepatwa na wasiwasi mkubwa kuhusu Timu za Afrika kuvunja Sheria na kuchezesha
Wachezaji wasiostahili kwenye Mechi za Mchujo za Kombe la Kombe la Dunia na
sasa wanataka kulishughulikia tatizo hilo ipasavyo.
Wasiwasi
huo umetangazwa na Mkurugenzi wa Mashindano wa FIFA Mustapha Fahmy hapo Jana.
Katika
Mechi 8 za Mchujo za Kombe la Kombe la Dunia Kanda ya Afrika Matokeo ilibidi
yafutwe baada ya Timu kuchezesha Mchezaji asiestahili ama kwa Sheria za Uraia
au kuwa Kifungoni kufuatia kupewa Kadi katika Mechi za nyuma.
Kwenye
Mechi zote hizo 8, Matokeo yalifutwa na Pointi 3 na Bao 3 kupewa Wapinzani wa
Timu iliyokiuka Sheria na hilo lilileta athari kubwa kwenye Timu husika na
Makundi yao.
Fahmy
amesema: “Tumepatwa wasiwasi na hili ambao ni ukiukwaji wa wazi wa Sheria
ambazo ziko wazi. Na hili limetokea katika Bara moja tu Duniani…Afrika. Mengine
kama Ulaya, Asia na Marekani ya Kusini hamna hata tukio moja.”
Fahmy
amesema kuwa inabidi wao kutafakari nini kimetokea na kutafuta ufumbuzi ili
makosa haya yasijirudie tena.
Tukio
la mwisho la ukiukwaji huu wa Sheria ni baada ya Cape Verde kuifunga Tunisia
Bao 2-0 huko Tunis na kutwaa ushindi wa Kundi lao na hivyo kutinga Raundi ya
Mwisho ya Mtoano lakini ikagundulika walimchezesha Mchezaji ambae alitakiwa
kuwa kwenye Kifungo cha Mechi 4.
Cape
Verde wakafutiwa ushindi na Tunisia, ambao Kocha wao Nabil Maaloul, alijiuzulu
baada ya kipigo hicho, kupewa Pointi 3 na Goli 3 na hivyo wao kufuzu kuingia
aundi ya Mwisho ya Mtoano ambayo itatoa Timu 5 kwenda Brazil.
Tunisia
watacheza na Cameroun kwenye Raundi hiyo.
Cha
ajabu ni kuwa, kwenye Kundi hilo hilo la Cape Verde na Tunisia, ni hao hao Cape
Verde walionufaika walipofungwa 4-3 na Equatorial Guinea na baadae kupewa
ushindi baada ya Equatorial Guinea kumchezesha Mchezaji asiestahili kwenye
Mechi hiyo.
No comments:
Post a Comment