Qatar
imesisitiza kuwa inaweza kuandaa dimba la Kombe la Dunia mwaka wa 2022 katika
majira ya joto, hata wakati Shirikisho la FIFA likiendelea kuwekewa mbinyo wa
kuhamisha tamasha hilo hadi msimu wa baridi
Taifa
hilo lenye utajiri wa nishati, ambako nyuzijoto hufikia sentigredi 45 ilipewa
kibali cha kuandaa Kombe la Dunia miaka mitatu iliyopita katika uamuzi wa
kushangaza.
Qatar
inasema inaweza kukubali kuhamisha dimba hilo hadi msimu wa baridi lakini
ikasisitiza kuwa licha ya joto kali, inaweza kuandaa Dimba la Dunia msimu wa
joto kwa kujenga viwanja vyenye hewa ya baridi kwa kutumia teknolojia mpya
inayojali mazingira.
Namna
ambavyo mashabiki wataweza kukabiliana na joto, nje ya viwanja, bado ni suala
linalotia wasiwasi na Rais wa FIFA Sepp Blatter hivi karibuni amesema lilikuwa
kosa kupanga kinyang'anyiro hicho cha msimu wa joto, katika taifa la jangwa.
Rais
wa Shirikisho la Soka barani Ulaya UEFA, Michel Platini pia amethibitisha kuwa
mashirikisho 54 wanachama wa UEFA wamekubaliana kwa kauli moja kuhusu wazo la
kuhamisha dimba hilo la Qatar, hadi msimu mwingine wa mwaka
Lakini
nayo kamati andalizi ya Qatar imejaribu kuondoa wasiwasi hiyo, kwa kusema
teknolojia ya kuleta hewa ya baridi, kwa kutumia solar, katika maeneo ya umma,
nje na ndani ya viwanja, huenda ikatatua shida hizo.
No comments:
Post a Comment