Dereva Sergio Perez amesisitiza kuwa hahofii mustakabali
wake wa baadae na kampuni McLaren, japokuwa team hiyo imeweka bayana mpango wao
wa kumleta dereva Fernando Alonso kwa ajili ya kumbadilisha nae
Mkuu
wa team ya McLaren
Martin Whitmarsh ameweka bayana nchini Singapore kwenye Singapore Grand Prix
kwamba team inataka kuona mabadiliko chanya toka Perez kabla ya kumpa mkataba
mwingine mwakani.
Na kuongeza kuwa
mtu ambaye anatakiwa kwa kuchukua nafasi yake ni dereva mmexixo Alonzo ambaye
alishasema kwamba asingependa kurudi kwenye timu hyo hivi karibuni
Perez alisema
hajahusishwa kuhusu suala hilo na anauhakika atakuwepo kwenye timu ya Mc Laren
mwakani
Aliongeza kuwa,
unatakiwa kufanya kazi kwa bidii kwenye timu yoyote utakayokuwepo, siku zote
unatakiwa kufanya vema zaidi na kitaalam
Akizungumzia
kuhusu kauli ya bosi wake amesema kuwa, kauli hiyo ya Whitmarsh ni kauli ya
kumwamsha ili aongeze juhudi
"ndio kitu
ninachofanya na najaribu kutoa kitu nilichonacho kwa ufanisi wa hali ya juu,
umekuwa wakati mgumu msimu huu kwetu sote, lakini kila siku nasema maisha yangu
ya baadae hapa yapo sawa
Nitakuwepo hapa
mwaka ujao na ngoja tuone, ninaimani tutarudi na kupigania ubingwa mwaka ujao
No comments:
Post a Comment