Friday, 11 October 2013

MPANDA FM RADIO NDANI YA MAHAFALI KATUMBA

Na: rahim kassonga (La Captain)

UONGOZI WA MPANDA FM RADIO, WAALIKWA KAMA WAGENI RASMI KWENYE MAHAFALI HUKO TAMBAZI (makazi ya wakimbizi katumba)

msafara wa Mpanda FM radio ukiwa kwenye ofisi za mkuu wa makazi katumba, kwa ajii ya kujitambulisha na kupata kibali cha kuingia makazi

Tunu Lugombe akifanya yake wakati Mpanda FM radio wakisubiri hatua za  ofisi ya makazi




Babuu the suka akipoza mtambo wake baada ya kuvunja rekodi ya kutembea dakika 18 Mpanda -Katumba

Msafara wa Mpanda FM radio upo Tambazi-Katumba kwenye shule ya msingi Tambazi 
Mgeni rasmi, meneja wa Mpanda FM radio akiingia eneo la tukio

waalikwa Mpanda FM radio wakiwa meza kuu, tayari kwa kuanza ratiba za mahafali yaliyofana sana

meza kuu wapili kulia ni mkuu wa shule, katikati mgeni rasmi

baadhi ya wanafunzi wa Tambazi na waagwa

wanafuzi wa Tambazi wakifuatilia kwa makini utaratibu mzima

baadhi ya wahitimu

wanaTambazi na baadhi ya wanafunzi waliohudhuria mahafali hiyo

mchungaji akifungua mahafali kwa maombi

wananchi wa Tambazi wakisikiliza kwa makini maneno toka meza kuu

mkuu wa shule akitambulisha watumishi wake kwa mgeni rasmi

mtangazji wa Mpanda radio akituma tukio hilo live radioni, huku akipata ulinzi mkali toka kwa bodyguard (kassonga)

Captain kassonga akiwa kazini

meneja wa mpanda FM radio na Tunu Lugombe wakiwa meza kuu

waagwa wa shule ya msingi Tambazi 2013, wakitoa burudani

mapanga shaaaaaaaa, pia yalikuwepo

waagwa akiyakata mapanga

burudani za kutosha zilikuwepo

pozi za graduuuuuuu

ngonjera nazo hazikuwa nyuma

wanafunzi darasa la kwanza hadi la tatu akiburudisha kwa ngonjera

watangazaji wa Mpanda FM radio wakifuatilia burudani kwa makini

meneja wa Mpanda FM radio akiwa makini na matukio ya graduuuuu

pozi la menejaaaaaaaaaaaaaaaa

MC wa tukio hilo alikuwa na makeke mengi na kutoa burudani ya aina yake hapa akiwa kwenye poziiii

wanafunzi waagwa akitoa burudani

sio kama wamechoka bali ni pozi la umakini wa matukio

burudani zilipochanganya, meza kuu ilishindwa kujizuia kwa kucheka

wahitimu wakisoma risala kwa mgeni rasmi

mgeni rasmi akijiandaa kupokea risala

mgeni rasmi akipokea risala toka kwa waagwa

baada ya kusoma risala, waagwa aliondoka kwa kustua kijoti na kutoa burudani babu kubwa

mgeni rasmi akiipitia risala na kunong'ona kitu na tunu lugombe

mgeni rasmi anatoa zawadi ya mwanafunzi bora kwa upande wa taaluma

mtoto wa mwalimu lazima awe na akili, hapa mtoto wa mwalimu na mama yake akipokea zawadi 

bodyguard yupo makini na kazi yake

mwanafunzi aliyepokea zawadi ya usafi akipongezwa na walimu wake na kupewa zawadi ya  vyoda

zawadi zikiendelea kutolewa

meza kuu ilipomaliza kutoa zawadi

kutoa zawadi kazi hadi kiu!!!!!!!!!

waagwa akisikiliza nasaha kwa makini na nidhamu ya hali ya juu

waagwa akishangilia nasaha nzuri toka kwa mgeni rasmi Meneja wa Mpanda FM radio

mwanafunzi huyu alikuwa burudani na kuwavutia wengi kwani
alikuwa mcheshi, akihusika kila tukio, bingwa wa viduku lakini pia aliwafunika wanafunzi wenzake wote
kitaaluma .....kweli wanawake wanaweza

meneja wa Mpanda FM radio Gerard Seti Sedekia akitoa hutuba kwenye mahafali

menejaaaaa, tabasam hilooooooooooo

mkuu wa shule na meneja Seti wakiwa tayari kwa picha ya pamoja na kupokea zawadi toka  waagwa

hapa katika picha ya pamoja

    meneja baada ya kupokea zawadi toka kwa waagwa


serikali mpo wapi?????   oneni shule yenu hii imeisahau? darasa hili ni baadhi ya madarasa machache yanayohitaji ukarabati shuleni Tambazi

usafiri wetu

wazazi wakibebelea zawadi tayari kuwapa waagwa

mtangazaji wa mpanda fm radio akiwa kwenye tanki la maji ambalo linatumika kuvunia maji ya mvua na huu ni mfano wa kuigwa kwa shule zingine

ni kama utaliii


pozi la bodyguardddddddddddd





Tuesday, 8 October 2013

kikosi bora cha Ubelgiji kupata kutokea

by rahim kassonga
kikosi cha Ubelgiji, kwangu mimi ndio kikosi bora kupata kutokea

kama ulikua hukijui, ndio hiki hapaa

vp? maoni yako

Monday, 7 October 2013

SHAHIDI KATIKA KESI YA RUSHWA MTWARA AHUKUMUMIWA KIFUNGO CHA MIAKA MIWILI JELA KWA KUSEMA UONGO MAHAKAMANI



Bw. ISSA BAKARI MATWANI Katibu wa CCM Tawi la Naulongo Kata ya Naliendele Manispaa ya Mtwara, Mkoani Mtwara, amehukumiwa kifungo cha miaka 2 gerezani au kulipa faini la shilingi laki moja kufuatia Mahakama kubaini kuwa kwa makusudi alikana maelezo aliyokuwa ameyatoa TAKUKURU katika shauri la Rushwa kwenye uchaguzi wa Diwani mwaka 2010.
Bwana ISSA BAKARI MATWANI alikuwa shahidi muhimu kwenye shauri la Na. 85/2011 kati ya Jamhuri dhidi ya SALMA HAMIS CHITOPE ambapo akiwa Katibu wa CCM Tawi la Naulongo Kata ya Naliendele Mtwara mnamo mwezi Mei, 2010 aliandaa orodha ya majina ya mgao wa Rushwa kwa ajili ya mgombea kiti cha Udiwani Kata ya Naliendele Bi. SALMA HAMIS CHITOPE ambaye aliibuka mshindi
Awali Bw. ISSA BAKARI MATWANI aliandikisha maelezo yake TAKUKURU na kukiri kuandaa orodha hiyo ya mgao wa Rushwa kwa wapiga kura na hivyo kufanywa shahidi muhimu katika shauri hilo -baada ya Mtuhumiwa Bi SALMA HAMIS CHITOPE kukamatwa akiwa na orodha ya majina ya mgao wa Rushwa kabla ya kufikishwa Mahakamani
Katika hali isiyo ya kawaida, akiwa anatoa ushahidi Mahakamani mnamo 23/5/2012 Bw. ISSA BAKARI MATWANI mbele ya Hakimu Mkazi Mheshimiwa Ernest Mbungu, alikana maelezo yote aliyoyatoa kwa Maafisa wa
TAKUKURU wakati wa uchunguzi ; hivyo kuifanya Mahakama kukosa nafasi ya kutathmini ushahidi wake.
Upande wa Jamhuri ukiongozwa na mwendesha mashtaka wa TAKUKURU Sospeter S. Tyeah uliiomba Mahakama imwone shahidi kama aliyegeuka Mahakamani (hostile) ili hatua za kisheria zichukuliwe dhidi yake. Hatimaye, baada ya Mahakama kuridhika na mazingira ya ushahidi huo ilikubaliana na upande wa mashtaka na kumtangaza ISSA BAKARI MATWANI kuwa ni shahidi kigeugeu (hostile)
Kufuatia hatua hiyo ya Mahakama, Jamhuri ilifungua shauri Na 135/2012 dhidi ya BAKARI ISSA MATWANI katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Mtwara 5/9/2012 kwa kosa la kutoa maelezo ya uongo (perjury) kwa Afisa Uchunguzi wa TAKUKURU akiwa chini ya kiapo.
Shauri hili ambalo lilivuta hisia za wakazi wengi wa Manispaa ya Mtwara na wanachama wa CCM na vyama vingine, lilifikia tamati hivi karibuni ambapo Hakimu Mkazi wa Mahakama ya Mtwara, Mheshimiwa Joseph Fovo alimtia hatiani Bw. ISSA B. MATWANI kwa kosa la kutoa ushahidi wa uongo Mahakamani huku akizuia Mahakama kutenda haki katika shauri ambalo TAKUKURU kwa niaba ya Jamhuri ilikuwa ikimshtaki Diwani SALMA HAMIS CHITOPE.
Baada ya kumkuta ana hatia, Mahakama ilimhukumu Bw. ISSA BAKARI MATWANI kwenda jela miaka miwili ama kulipa faini ya Tshs. 100,000/= (Laki moja tu) ili iwe fundisho kwa wote wanotoa maelezo ya uongo wakiwa chini ya kiapo na kuidanganya Mahakama katika ushahidi wanao ufahamu.
IMETOLEWA na:-
AIDAN A. NDOMBA
MKUU WA TAKUKURU (M)
MTWARA.................................06.09.2013

Saturday, 5 October 2013

KAKAO CHA TATU CHA KAMATI YA USHAURI (RCC) MKOANI KATAVI

 by rahim kassonga


KAKAO CHA TATU CHA KAMATI YA USHAURI (RCC) MKOANI KATAVI 
chaadhimia kuboresha sekta mbalimbali mkoani Katavi 
Dkt.Rajabu Lutengwa  mwenyekiti wa kikao hicho akifungua kikao




baadhi ya wajumbe wa mkutano huo uliofanyika kwenye ukumbi wa idara ya maji mjini Mpanda wakisiliza kwa makini hoja toka kwa mwenyekiti


mwenyekiti wa kikao hicho Dr Rajabu Rutengwe akijibu hoja za wajumbe 




ukumbi wa idara ya maji ambapo ndio kikao hicho kilifanyikia



wajumbe wakisiliza kwa makini mada toka kwa wawasilishaji

miongoni mwa wajumbe waliohudhuria kikao hicho


Katibu tawala wa mkoa, ambaye pia ndio alikuwa katibu wa kikao  hicho

wajumbe wa kikao cha RCC wakisikiliza mada


RPC mkoa wa Katavi kamanda Dhahiri Kidavashari akifuatilia kwa makini  mikhutasari  ya  kikao hicho

wajumbe wa kikao wakinakili dondoo muhimu za kikao hicho

mjumbe wa kikao hicho akichangia jambo

mjumbe wa kikao akichangia jambo kwenye kikao hicho

kamanda Kidavashari akitoa maoni yake kwenye kikao hicho



kamanda Kidavashari, akiweka maiki sawa kwa ajili ya kutoa maoni yake kwenye kikao hicho

technolojia haikuwa nyuma kwenye kikao hicho

manufaa ya EPZA yakiainishwa kupitia technolojia ya projector












mmoja wa watoa mada akisisitiza jambo kwenye kikao hicho

baadhi ya wajumbe wa kikao


Wednesday, 2 October 2013

KOMBE LA DUNIA: GHANA YAITA WAKONGWE KUIKABILI EGYPT

by kassonga


Kocha wa Ghana Kwesi Appiah amewaita kwenye Kikosi chake cha kuikabili Egypt hapo Oktoba 15 huko Kumasi ambapo Mshindi ndie anapewa Tiketi ya kwenda Brazil Mwakani kucheza Fainali za Kombe la Dunia, Wakongwe Sulley Muntari na Kipa Richard Kingson kwenye Kikosi cha Wachezaji 25.


Muntari, mwenye Miaka 29 na anachezea AC Milan huko Italy, aliachwa kwenye Kikosi cha Ghana cha Mwezi Septemba kilichoibwaga Zambia na kufuzu kucheza Raundi ya Mwisho ya Mtoano dhidi ya Egypt.

KOMBE LA DUNIA 2014 AFRIKA
Raundi ya Mwisho ya Mtoano
RATIBA:
[kwa saa za kitanzania]
Mechi za Kwanza:
Jumamosi Oktoba 12
19:00 Burkina Faso v Algeria
20:00 Ivory Coast v Senegal
Jumapili Oktoba 13
16:00 Ethiopia v Nigeria
20:00 Tunisia v