Monday, 16 December 2013

MWANA KABENDE FATAKI ASHUSHA KIPIGO KIKALI KWA BONDIA TOKA DAR

by rahim kassonga (La captain)

Bondia FATAKI toka Mpanda juzi alishushia kipigo cha nguvu bondia Tadeo toka Dar es salaam kwa kumtwanga kwa KO katika raundi ya pili tu tena sekunde za mwanzoni.

Pambano hilo ambalo ni la kwanza kufanyika mkoani Katavi lilisimamiwa na shirikisho la ngumi za kulipwa nchini TPBO.

Said Kassim Chaku ambaye pia ni katibu wa TPBO ndio alikuwa mwamuzi wa pambano hilo ambalo lilitangulia na mapambano mengine mawili na burudani mbalimbali zikiwemo muziki toka kwa vijana wa mkoani katavi na mchezo wa TAI CHI

Majaji wa mapambano yote matatu walikuwa ni Steven Monela bondia na mwanajeshi mstaafu na Rey Mwanauta wote kutoka Katavi
maandalizi ya pambano glove zikiwa tayari kwa ajili ya pambano

ulingo uliandaliwa vema

wasanii D-touch na D-zela wakifanya yao

Ally Bizo akishambulia jukwaa


mkurugenzi wa Pamoja FM Emmanuel mallack akitoa neno 

Balbel King akifanya yake

Balbel King

Bondia kulwa akijiandaa kucheza pambano la utangulizi na Benjamini


Benjamin akiwa tayari kumkabili kulwa



Refarii said Chaku akitoa maelekezo kwa mabondia kabla ya pambano


Ngumi jiwe shurti ukunje sura- chezea masumbwi wewe






Konde sharti litokee mbali

sio kama nakwepa bali navuta kasi ya konde

MC kelly B akijumlisha hesabu na refa CHAKU

benjamin ameshinda kwa pointi 39 dhidi ya 38 za mpinzani wake kwenye uzito wa unyoya


Pambano la pili ambapo Oswald mwenye bukta nyekundu akipambana na Elfaz mwenye Blue

refa yupo makini kwelikweli




Oswald aliibuka kidedea kwa pointi 40 dhidi ya 36 za mpinzani wake

mambo ya TAI CHII

Radical Mnyama akifanya unyama jukwaani, funika mbayaaaaa

kazi ilikuwepo Radical aliwasha moto vibaya yaani mpaka baaaasiiiiii

mwana Kabende Fataki akiingia na wapambe wake

Add caption

Simon Tadeo kama Tyson atoki katikati anakufuata tu

Makonde yaliendelea

Tadeo akijaribu kuinuka bila ya mafanikio baada ya kupokea konde nene toka kwa Fataki

King FATAKI akitia mbwembwe baada ya kumaliza mpinzani wake kwenye raundi ya pili

refa akitangaza mshindi

Steven Monela kocha wa Fataki akimpongeza kijana wake

Ndondi sio ugomvi, baada ya kubondwa mnakuwa marafiki kama kawa, fair play


Fataki akipongezwa na mashabiki wake



Fataki akiwashukuru mashabikimkwa sapoti yao



La Captain akiwa kazini 





wasanii radical na ally bizo wakimpongeza kaka yao fataki

Wednesday, 4 December 2013

TABU LEY ROCHEREAU : PROFILE

by zangii ze icon


Tabu Ley: Mshumaa uliozimika kimyakimya *Aacha watoto 68 akiwa na miaka 76

JINA KAMILI : Pascal-Emmanuel Sinamoyi Tabu, ni mwanamuziki nguli wa Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo (DRC).

JINA LA KIMUZIKI : Maarufu kwa jina la Tabu Ley Rochereau.

MWANAMUZIKI WA AINA GANI? Alikuwa ni mwanamuziki wa miondoko ya Afrika ya aina ya Rhumba

AMEFARIKI : Amefariki Dunia Novemba 30, mwaka huu

AMEZALIWA : Tabu Ley alizaliwa Novemba 13, kati ya mwaka 1937 katika mji wa Bagata kwenye nchi iliyokuwa ikijulikana kama Congo ya Ubelgiji (Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo).

ANAWATOTO WANGAPI? Anawatoto 68 ambao amezaa na wanawake tofautitofauti.

SAFARI YAKE YA MUZIKI : Alikuwa kiongozi wa bendi ya muziki wa dansi iitwayo Orchestre Afrisa International na alikuwa mmoja wa waimbaji wa Afrika wenye mvuto na mtunzi mahiri.

ALIFANYA VITU GANI KUBORESHA MUZIKI WAKE : Akiwa pamoja na mpiga gita mashuhuri Dkt. Nico Kasanda, Tabu Ley alikuwa mwasisi wa mtindo wa soukous (Rumba ya Afrika) na muziki wake aliufanya kuwa wa kimataifa kwa kutia vionjo vya muziki wa asili wa Congo na rhumba la Cuba, Caribbean na Latin America.

MTU MASHUHURI WA CONGO : Tabu Ley au ukipenda Rochereau, anaelezewa kama 'mtu mashuhuri' wa Congo ambaye, pamoja na Rais Mobutu Sese seko, waliweka historia ya Afrika katika karne ya 20."

JINA ALILOPEWA KUTOKANA NA KAZI YAKE : Kutokana na umahiri wake katika muziki wa rhumba, Tabu Ley aliwahi kupewa jina la "Elvis wa Afrika" na gazeti la 'Times' la Los Angeles nchini Marekani.

MBALI NA MUZIKI ALIKUWA MWANASIASA : Baada ya kuangushwa utawala wa Mobutu, Tabu Ley pia aliingia katika siasa.

JUMLA YA NYIMBO ALIZOTUNGA : Wakati wa enzi zake, Tabu Ley aliweza kutunga nyimbo mpaka 3,000 na kutoa albamu 250.

ALIANZA MUZIKI LINI?: Tabu Ley au Rochereau, alianza kazi ya muziki mwaka 1956 wakati alipoimba pamoja na Joseph Kabasele Yampanya 'Pepe Kalle' akiwa na bendi yake ya African Jazz.

Baada ya kumaliza kidato cha sita, Tabu Ley aliamua kuwa mwanamuziki wakati wote. Tabu Ley alitoa wimbo uitwao 'Cha Cha' kusherehekea uhuru wa Congo kutoka Ubelgiji mwaka 1960.

ALIFANYA MUZIKI NA WASANII GANI? Wimbo huu wa 'Cha Cha' ulitungwa na Pepe Kalle, ambapo ulimpaisha Tabu Ley na kupata umaarufu kwa haraka sana. Tabu Ley alibaki na bendi ya African Jazz mpaka mwaka 1963 wakati yeye na Dkt. Nico Kasanda walipounda bendi yao, African Fiesta.

ALIFUNGUA BENDI: Miaka miwili baadaye, Tabu Ley na Dkt. Nico walisambaratika na Tabu Ley akaunda bendi yake ambayo ilikuwa ikijulikana kama African Fiesta National, na pia ilijulikana kama African Fiesta Flash.

Bendi ya African Fiesta National ilikuwa moja ya bendi zenye mafanikio makubwa katika historia ya muziki wa Afrika, ikirekodi nyimbo kali kama 'Afrika Mokili Mobimba'.

WIMBO GANI ULIOVUNJA REKODI YA MAUZO ? Wimbo Wa 'Afrika Mokili Mobimba' ilivunja rekodi ya mauzo kwa kuuza nakala milioni moja mwaka 1970.

Wakati huo, Papa Wemba na Sam Mangwana walikuwa miongoni mwa wanamuziki waliotakatisha kundi la African Fiesta National.

JINA GANI LA JUKWAA ALILOCHUKUA? Tabu Ley alichukua jina la jukwaa la 'Rochereau' kutoka kwa Generali wa Jeshi la Ufaransa, Pierre Denfert-Rochereau, ambaye alisoma naye shule moja na kulipenda jina lake.

SAFARI YA BENDI : Mwaka 1970, Tabu Ley aliunda bendi ya Orchestre Afrisa International, Afrisa ikiwa ni mchanganyiko kati ya jina Afrika na Isa, alama ya muziki wake.

Akiwa pamoja na Franco Luambo Makiadi wa TPOK Jazz, Afrisa ikawa moja ya bendi kubwa barani Afrika. Walirekodi vibao kama 'Sorozo', 'Kaful Mayay', 'Aon Aon', na 'Mose Konzo'.

ALIVUMBUA VIPAJI VIPYA : Katikati ya miaka ya 1980, Tabu Ley aliweza kugundua kipaji cha mwanadada mwimbaji na mcheza shoo, M'bilia Bel, ambaye alichangia sana kuipaisha bendi ya Orchestre Afrisa International.

M'bilia Bel alikuwa mwimbaji mwanamke wa kwanza wa muziki wa soukous, ambaye alijipatia umaarufu Afrika yote.

MAISHA YA MAPENZI : Tabu Ley na M'bilia Bel baadaye walifunga ndoa na kupata mtoto mmoja. Mwaka 1988 Tabu Ley alimuibua mwanamuziki mwingine wa kike ajulikanaye kama Faya Tess.

Kuona Faya Tess ananyanyuka kwa kasi,  M'bilia Bel aliamua kuondoka katika bendi hiyo na kuendelea kufanya vizuri katika kazi za muziki akiwa kivyake.

Baada ya M'bilia Bel kuondoka, mvuto wa bendi ya Afrisa pamoja na ule wa wapinzani wao TPOK Jazz uliendelea kufifia kutokana na mashabiki kugeukea mtindo mpya wa muziki wa soukous wenye kasi zaidi.

Baada ya utawala wa Rais Mobutu Sese Seko kuanzishwa katika Congo, Rochereau akachukua jina la 'Tabu Ley' kama sehemu ya kampeni ya Mobutu kuwafanya wananchi wa Zaire kuwa na majina ya asili.

SABABU ZILIZOMFANYA ATOROKE: Hata hivyo, mwaka 1988 Tabu Ley alitoroka na kwenda kuishi uhamishoni nchini Ufaransa.

Mwaka 1985, Serikali ya Kenya ilipiga marufuku muziki wa kigeni kuchezwa kwenye Redio ya Taifa.

Baada ya Tabu Ley kutunga wimbo 'Twende Nairobi', aliouimbwa na M'bilia Bel, kumsifu Rais wa Kenya wakati huo, Daniel Arap Moi katazo hilo mara moja likaondolewa.

Mapema 1990 Tabu Ley aliishi kwa muda mfupi Kusini ya California nchini Marekani. Alianza kutengeneza muziki wake kuwa wa kimataifa zaidi na kuingiza lugha ya Kingereza na kuongeza staili za kucheza kuwa za kimataifa zaidi kama vile Samba.

Rochereau aliona kupata mafanikia kwa kutoa albamu kama Muzina, Exil Ley, Africa worldwide na Babeti soukous.

Utawala wa Mobutu ulipiga marufuku albamu yake ya mwaka 1990 iitwayo 'Trop, C'est Trop' ambayo aliiona kama inamchafua. Mwaka 1996, Tabu Ley alishiriki katika albamu iitwayo Gombo Salsa iliyotolewa na bendi ya Africando.

Wimbo wa 'Paquita' kutoka albamu ya Gombo ni moja ya wimbo uliowahi kurekodiwa mwishoni mwa miaka ya 1960 na bendi ya African Fiesta.

Wakati Rais Mobutu Sese Seko alipoondolewa madarakani mwaka 1997, Tabu Ley alirudi Kinshasa na kupewa Uwaziri katika serikali mpya ya Rais Laurent Kabila.

Kutokana na kifo cha Laurent Kabila, Tabu Ley kisha alijiunga na Bunge teule la mpito lililoundwa na Joseph Kabila, mpaka lilipovunjwa baada ya kuundwa kwa taasisi za mpito.

CHEO ALICHOPATA : Novemba 2005, Tabu Ley aliteuliwa kuwa Kaimu Gavana Kinshasa, nafasi aliyopewa kutokana na chama chake cha Congolese Rally for Democracy, kutokana na makubaliano ya amani 2002.

AMESHWAHI KUWA WAZIRI : Tabu Ley aliyewahi pia kuwa Waziri wa Utamaduni, inasemekana amezaa watoto 68 na wanawake tofauti tofauti, akiwemo rapa mashuhuri wa Ufaransa, Youssoupha.

Rochereau amekufa akiwa na umri wa miaka 76 katika Hospitali ya Mtakatifu Luc mjini Brussels, Ubelgiji ambako alikuwa akipata matibabu ya ugonjwa wa kiharusi uliomkumba mwaka 2008.

BREAKING NEWS : MAHAKA YA RUFAA IMERIDHIA HUKUMU YA KAJALA


Mahakama ya Rufaa kanda ya Dar imeridhia hukumu iliyotolewa na Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu ya faini ya sh. milioni 13 na kumuachia huru staa wa filamu za kibongo, Kajala Masanja.

Kajala sasa yupo huru baada ya kulipa faini hiyo ambapo hivi karibuni mumewake Faraji Agostini amekata rufaa ingawa teyari imeshapingwa. Faraji anatumikia kifungo cha miaka mitano katika hukumu ya kesi ya kutakatisha fedha haramu iliyotolewa mapema wiki hii.

Tuesday, 3 December 2013

PATA FURSA YA KUSIKILIZA NGOMA MPYAA TOKA KWA MC GEORGE FT TUNDA MAN-HALI MBAYA

CD COVER YA MKONO HUUMPYAAA
MC GEORGE KATIKA POZI
BONYEZA HAPA KUIPATA UISIKILIZE

Toure ndiye bora zaidi Afrika

by zangii ze icon
Yaya Toure aliteuliwa mara tano kuwania tuzo hili lakini akafanikiwa kushinda mwaka huu
Yaya Toure ametangazwa mshindi wa tuzo ya BBC ya mwaka 2013 ya mchezaji bora zaidi wa soka barani Afrika.
Mchezaji huyo wa Ivory Coast, na ambaye pia ni kiungo wa klabu ya Manchester City ya Uingereza, na ambaye jina lake limekuwepo kwa miaka minne iliyopita katika orodha ya wachezaji wanaowania tuzo, aliwashinda Pierre-Emerick Aubameyang, Victor Moses, John Mikel Obi na Jonathan Pitroipa, katika kuibuka mshindi.
Mchezaji huyo ana umri wa miaka 30.
Orodha fupi ya waliowania tuzo hiyo ilitayarishwa na wataalamu 44 wa soka kutoka kote barani Afrika, na wakizingatia hasa maarifa ya mchezaji, kiufundi, ushirikiano na wenzake katika timu, na kwa kucheza mchezo safi na kwa haki.
Kisha, kupitia idadi kubwa kabisa kuandikishwa kwa wapiga kura, mashabiki waliweza kushiriki katika shughuli hiyo katika mtandao, au kupitia ujumbe wa simu ya mkononi.
Mashabiki hao wameamua kwamba Toure ndiye bora zaidi, kwani katika kipindi cha mwaka mmoja uliopita, raia huyo wa Ivory Coast alicheza kwa bidii, kuonyesha mchezo wa kasi, ubunifu, na vile vile kwa kufunga magoli.
Ingawa mwaka 2013 ulikuwa ni wa ufanisi kwa Toure hasa kwa kupata vikombe, hakuweza kuisaidia nchi yake, wala klabu, kupata kombe lolote lile, lakini bado alionyesha kiwango cha hali ya juu katika mchezo.
Baada ya kuvunjika moyo kwa kushindwa kuutetea ubingwa wao wa ligi kuu ya Premier wa mwaka 2012 akiichezea Manchester City, Toure alirudi uwanjani akijizatiti, na kuimarisha mikwaju yake ya free-kick.
Alitumbukiza wavuni bao, kwa mpira wa kupinda, katika siku ya kwanza ya msimu mpya wa ligi kuu ya Premier, wakati timu yake ilipocheza na Newcastle, na akarudia hayo hayo katika mechi iliyofuata wakati Hull walipowatembelea katika uwanja wao wa nyumbani.
Toure amefunga magoli manne ya kupanga kwa makini shambulio, na hayo yakiwa ni kati ya magoli saba kwa jumla aliyoweza kuifungia klabu ya Man City msimu huu.
Kufikia sasa, mwaka huu wa 2013, Toure ametumbukiza wavuni jumla ya magoli 12; ya klabu na vile vile ya nchi yake, na hiyo ni rekodi nzuri sana kwa mchezaji wa kiungo cha kati.
Mbali na ustadi huo katika kumalizia, Toure ni kiongozi bora katika timu, na maarifa yake yameiwezesha City kufikia sasa kuwa katika nafasi ya nne katika ligi kuu ya England.
Aliisaidia kikamilifu nchi yake ya Ivory Coast kufuzu kwa michuano ya Kombe la Dunia ya mwaka ujao itakayofanyika nchini Brazil.
Timu yake ya Tembo, The Elephants ilihitaji kuusahau mwanzo mbovu hapo awali katika kampeni yao ya michuano ya Kombe la Mataifa ya Afrika, na walipoondolewa katika robo fainali na Nigeria, ambao hatimaye waliibuka mabingwa, na Toure akiwapa matumaini ya kufanya vyema baadaye.
Nje ya uwanja, Toure ameongoza vita dhidi ya ubaguzi wa rangi katika soka, hasa baada ya matusi kuelekezwa kwake katika mechi ya ligi ya klabu bingwa dhidi ya CSKA Moscow, mwezi Oktoba, na akionyesha moyo wa uvumilivu na wa kimichezo unaostahili uwanjani.
Tukio kama hilo linaweza kumvunja moyo mchezaji asiyejiamini, lakini Toure ameendelea kuwa mchezaji wa kipekee tangu wakati huo.
Na katika mwaka wa tano baada ya jina lake kupangwa katika orodha ya wachezaji wanaowania tuzo, hatimaye Toure ametajwa kama mshindi wa tuzo ya mchezaji bora zaidi wa soka barani Afrika.

Saturday, 30 November 2013

PICHA ZA MPANDA FM

TID ALALA MAHABUSU

by zangii ze icon


 
Khaleed Mohamed 'TID'.
Msanii mahiri wa muziki wa kizazi kipya, Khaleed Mohamed 'TID' yupo mahabusu katika Kituo cha Polisi Oysterbay tangu jana usiku baada ya kukamatwa na polisi kwa tuhuma za kumpiga na kumjeruhi msichana anayedaiwa kuwa ni mpenzi wake,  Mariam Nnauye.

BAADA YA KUFUKUZWA KWA KUFANYA NGONO NDANI YA GARI YA WEMA SEPETU..PRODUZA HUYO AMENENA MAZITO NA MADUDU YA WEMA SEPETU NA KAMPUNI YAKE


BY ZANNGII ZE ICON

Baada ya juzi kati kuripotiwa habari ya aliyekuwa producer ama mtengenezaji wa vipindi vya Wema Sepetu Chidi Mohamed kufukuzwa kazi kutokana na kulitumia gari la kampuni kama sehemu yake ya kuvunjia amri ya sita na wadada wa mjini, hatimaye katika pitapita zetu za mtandaoni tuliweza kukutana na kauli ya producer huyo akizungumzia habari hiyo ya yeye kufukuzwa kazi kwenye kampuni ya Endless Fame ya wema sepetu.

Chidi mwenyewe anasema kuwa habari hizo si za kwel na ni kwamba wote walioandika wamepanga kumchafua tuu kwa kuogopa kuwa anaweza kuyaniika mambo mazito yanayoendelea huko endless Fame
Kwa mujibu wa chidi anasema kuwa yeye ameondoka kwenye Kampuni hiyo siyo kwa sababu ya uzinzi ngani ya gari kama ilivyoripotiwa bali ni kutokana na sababu hizi kuu mbili.
1. Ameona hamna jipya na wala hamna maendeleo yoyote ndani ya Kampuni hiyo ndio maana ameamua kuondoka

2. Wafanyakazi wa Endless Fame hawalipwi kabisa ndio maana yeye akaamua kujitoa kwani anafanya kazi bure na pia sio yeye peke yake aliyeondoka bali kuna wafanyakazi zaidi ya watatu walioondoka kwenye kampuni hiyo ila nashangaa ni kwanini wameamua kumchafua yeye?
Bado tunafanya mawasiliano na Endless Fame ili tujue kama daia haya ni ya kweli au la......


Thursday, 28 November 2013

UKWELI WA ISHU YA SNURA NA MRISHO NGASSA.

BY ZANGII ZE ICON

Ni picha ambazo zimekua zikizungumziwa kwenye mitandao ya kijamii na hata kwenye mitandao
mingine ya habari nchini Tanzania zikimwonyesha mchezaji wa Yanga Mrisho Ngassa akiwa mapenzini na mwimbaji Snura wa bongofleva.

Snura anasema mwanzo wa hizi picha kusambaa ni baada ya kupoteza simu yake, namnukuu akisema ‘hizo picha hazina uhusiano wowote unaounganishwa kimapenzi kati yangu na Ngassa ila ni sehemu ya vipande vya movie yangu inaitwa ‘Majanga’ ambayo nimeanza kuifanya na Ngassa amecheza ndani yake kwenye scene za mapenzi, yani Snura kwenye movie amecheza kama binti mrembo anaerukiarukia Wanaume’

‘Simu yangu ilipotea ndio maana wamezipata hizo picha, wakati tunashoot tulikua tunapigapiga tu hayo mapicha, mi sikuwa nataka kuzitoa kabisa manake movie yenyewe bado naifanya nusunusu kutokana na kukosa muda, hii ishu imeniletea sana matatizo manake mwingine anakua haamini unachokiongea na hakuna kitu kinauma kama kuongea ukweli alafu mtu anasema unadanganya’ – Snura

Kwa kumalizia Snura anasema ‘Ngassa alinipiga muda mfupi tu baada ya picha kuanza kusambaa akauliza mbona hizi picha zinasambaa hivi Snura? nikamwambia usinielewe tofauti babaangu kwa sababu mimi mwenyewe sikutaka zitoke, picha nilizopiga nyinginyingi tu wakati tunatengeneza movie ila naona watu wameona hizi ndio nzuri kwa skendo’ 

WAZEE KATAVI WASHAURI SERIKALI KUENDELEA NA OPERESHENI TOKOMEZA UJANGILI




MWAMLIMA-DC

Wazee Mkoani Katavi wameshauri Serikali kuendelea na operation tokomeza ujangili kwa kuwa imesadia kwa kiasi kikubwa kuokoa rasilimali za Taifa zilizokuwa zikiteketea kutokana na baadhi ya watu wachache waliokuwa wakijihusisha na ujangili wa kuhujumu rasilimali hizo.
Wakiongea kwenye Mkutano Maalum wa majadiliano na Wazee wakiwa na  Mkuu wa Wilaya Mpanda Paza Mwamlima  wamezungumzia  juu ya wahamiaji haramu nao wanajihususha kwa njia moja au nyingine na   katika vitendo vya ujangili na uharibifu wa mazingira wamesema hali hiyo ikiendelea uharibifu wa rasilimali za Taifa kama wanyama pori na mistu,  na  uharibifu wa mazingira hali inayoashiria    kutoweka  kwa  rasilimali  za taifa.

Kwa upande wake Mkuu huyo wa Wilaya  ya Mpanda Paza Mwamlima amesema katika   operation tokomeza  ujangili iliyofanyika Mkoani  Katavi  katika Wilaya ya Mpanda  Kata  moja  ya Mwese pekee jumla ya silaha 250 zilikamatwa hiyo inaonesha ni namna gani watu wanaishi na silaha ambazo hutumika kwa vitendo vya ujangili hivyo amewaomba wazee hao kusaidia kwa njia moja au nyingine kuwafichua watu wa namna hiyo wanaojihusisha na  uharifu, akaongeza  kuwa wazee ni tunu ya Taifa na amani katika nchi Wazee wanasaidia katika kuimarisha amani.
Awali katika risala yao wazee walimweleza Mkuu wa Wilaya kuwa wanakabiliwa na changamoto mbalimbali ikiwemo ukosefu wa usafiri wa kuwafikia wenzao walioko mbali kutoka makao makuu ya wilaya na Mkoa kuwafikia wazee wenzao walioko wilaya ya Mlele na Kata za Inyonga, mamba. Majimoto, kasansa kibaoni ,usevya mwamapuli,mbede,ikuba, Nsenkwa, Ilelea, Ilunde na Utende
Pia alitaja wazee wengine walioko katika kata za mwese, karema ,ikola,  Mishamo katuma Kapalamsenga na sibwesa pamoja  na maeneo mengine imekuwa tatizo kuwafikia hivyo wanaomba kusaidiwa kutatua changamotohiyo.
Changamoto nyingine waliyozungumzia  ni wazee kutohudumiwa ipasavyo hususani wanpokuwa wakipatiwa matibabu katika Hospitali wakaeleza kuwa wanakumbana na vikwazo vingi,pia wakaomba kusamehewa na mambo mengine kama kulipia umeme na huduma nyingine.
Mmoja wa wazee aliyejitambulisha kwa jina la John Kisalala aliomba eneo la kusaidia wazee matibabu liwekewe utaratibu mzuri ili kuondoa usumbufu kwa wazee hao ikiwa ni pamoja na kuondolewa usumbufu wa kulipia huduma ya maji, umeme na huduma nyingine kwa kuwa wazee hao wamelitumika taifa kwa muda mrefu na sana na sasa wanatakiwa kuhudumiwa.
Akizungumzia operation tokomeza ujangilia na operation kimbunga wazee hao wameshauri washirikishwe katika zoezi hilo kwa kuwa wazee wanawatambua watu ambao sio wazawa wao wanawatambua watu ambao siyo raia halali.
Naye Benezite Mwanauta akizungumzia uharibifu wa mazingira na rasilimali za taifa amewalaumu wafungaji wa kabilia la kisukuma kwa kukataa miti hovyo huku watu waliopewa dhamana wakiwa wanaangali bila kuchukua hatua yeyote  huku mazingira yakiendelea kuharibika suala hilo lisipochukuliwa hatua na umuhimu wa kipeke huenda katavi ikageuka jangwa walishauri hatua za makusudi zichukuliwe ili kunusuru uharibifu huo.
sikiliza hapa
http://www.hulkshare.com/356bxvkxsp1c

HUYU NDIO MSANII WA VITUKO SHOW ALIYEPIGWA NA MKE WAKE KIPIGO CHA PAKA MWIZI.

by zangii ze icon

HUYU ndiye msanii  niliyemzungumzia wiki iliyopita kuhusu kichapo alichopewa kama mnavyomuona hapo pichani.


Anatambulika kwa
jina  ''Kazi Kijeba''.. MSANII kutoka kundi la BONGO SUPERSTAR'S COMEDY linalorusha kipindi chake maarufu hapa nchini (VITUKO SHOW) Kinachorushwa katika runinga ya CHANNEL TEN Kundu  hili limeweka kambi ya takribani miaka miwili mkoani Tanga.

Nafikiri chazo cha habari cha wiki iliyopita hakikufafanua kisa kwa kina,tuliweza kuongea na msanii huyu na kugundua kwamba aliyemdunda kumbe alikuwa mpenzi wake anaeishi maeneo ya usagara Jijini Tanga, Na sio mara moja alishawahi kumpiga tena mara ya kwanza wakaachana baadae kama mnavyojua mapenzi, Si wakarudiana tena?.. Ila hii ya sasahivi hakuwa na nia njema maana alimpigia kelele za mwizi hatimaye msanii huyu kunusurika kufa aliokolewa na muuza bucha baada ya kukimbilia buchani..! Ama kweli wanawake wa sikuhizi noma...! Yani weka jiwe niweke kigingi.

HAYA NDIO MAJANGA YALIYOMKUTA TUNDA MAN HUKO TABORA HIVI KARIBUNI.


by zangii ze icon


Msanii wa kizazi kipya - Tunda Man pichani alijikuta akishangiliwa sana na kupata wakati mgumu wa kujipenyeza popote aliposhuka kwenye
gari siku ya tarehe 23.11.2013 kwenye tamasha la uzinduzi wa somo la TEHAMA mkoani Tabora katika uwanja wa Al-hassan Mwinyi, jeshi la polisi lilitakiwa kutoa msaada kwa msanii huyo kwani wanafunzi wengi wa shule za msingi waliohudhuria tamasha hilo walimzonga hali iliyotatanisha ikiwa watadondoka na kuanza kukanyagana.

[chini utaitazama video hiyo-KWA KIASI WALIHARIBU HATA UTARATIBU WA UCHUKUAJI WA VIDEO HIYO KWA SHAUKU YA KUMWONA MSANII WAO]


Akitathimini fadhira za wanafunzi kumshangilia...





wakati akiondoka na kuwaaga




Wanafunzi hawakuridhika na walizidi kulizonga gari wakati akiondoa na ilikuwa vigumu kuwazuia.

Thursday, 21 November 2013

UNESCO YAITAKA SERIKALI KUZITAMBUA REDIO ZA JAMII NCHINI

DSC05297
Mgeni rasmi Mkurugenzi wa Idara ya Habari (MAELEZO) Assah Mwambene (kushoto) akiwasili katika Hoteli ya New Palm Tree iliyopo Bagamoyo mkoani Pwani kufungua mkutano wa nne wa Mtandao wa vyombo vya habari vya Kijamii nchini (COMNETA) akiwa ameongozana na wenyeji wake Afisa Mipango Taifa wa Kitengo cha Mawasiliano na Habari na mratibu wa miradi ya UNESCO , Yusuph Al-Amin (wa pili kulia), Mwenyekiti wa COMNETA ambaye pia ni Mkurugenzi wa Redio ya Jamii ya Wilayani Karagwe ya FADECO Bw.Joseph Sekiku (wa pili kushoto) na Makamu Mwenyekiti wa COMNETA ambaye pia ni Meneja wa Kituo cha Habari na Mawasiliano cha Telecentre Sengerema FM mkoani Mwanza Bw. Felician Ncheye.
Na.Mwandishi wetu
SHIRIKA la Umoja wa Mataifa la Elimu, Sayansi na Utamaduni,(UNESCO), limeiomba Serikali kutambua mchango wa redio za jamii katika maendeleo nchini na hivyo kufanya nao kazi kwa karibu.
Ombi hilo limetolewa jana na Afisa Mipango Taifa wa Kitengo cha Mawasiliano na Habari na mratibu wa miradi ya UNESCO , Yusuph Al-Amin wakati wa mkutano wa Mtandao wa vyombo vya habari vya Kijamii nchini (Community Media Network of Tanzania – COMNETA)unaofanyika mjini Bagamoyo.
Akizungumza kwenye mkutano huo, Al-Amin aliwapongeza COMNETA kwa kufanikiwa kuanzisha umoja huo ambao awali kulikuwa na vituo viwili tu vilivyokuwa vikitambuliwa na Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA), huku kwa sasa vikifikia vituo zaidi ya 27, kwa nchi nzima ikiwemo Tanzania Bara na Visiwani.
DSC05299
Mgeni rasmi Mkurugenzi wa Idara ya Habari (MAELEZO) Assah Mwambene akibadilishana mawazo na wenyeji wake kabla ya kufungua mkutano wa nne wa COMNETA unaoendelea Bagamoyo mkoa wa Pwani.
Akifafanua zaidi, Al-Amin alisema UNESCO imekuwa ukiisaidia COMNETA kufikia malengo yake kwa kutambua kuwa radio hizo zinafanya kazi katika jamii na zina uwezo mkubwa wa kuifikia jamii inayoizunguka.
“Zaidi ya asilimia 70 ya Watanzania wako vijijini na hawa wanafikiwa kwa karibu zaidi na radio jamii, kwa kupata taarifa za kina na za haraka” alisema Al-Amin.
Alitoa mfano wa Radio ya jamii iliyoko Micheweni, Pemba ambayo uwepo wake umesaidia sana kuleta mabadiliko ya maendeleo wilayani hapo tofauti na ilivyokuwa huko nyuma ambapo wilaya hiyo likuwa nyuma sana kimaendeleo.
‘Vipindi mbalimbali vya kuhamasisha maendeleo vinavyorushwa na redio hii vimesaidia sana kuhamasisha wananchi na sasa mwamko wa maendeleo umekuwa mkubwa hapo Micheweni” alisema, Al-Amin.
DSC05318
Mwenyekiti wa COMNETA ambaye pia ni Mkurugenzi wa Redio ya Jamii ya Wilayani Karagwe ya FADECO Bw.Joseph Sekiku akizungumza na WanaCOMNETA kabla ya kumkaribisha mgeni rasmi Mkurugenzi wa Idara ya Habari (MAELEZO) Assah Mwambene.
Aliwashauri wanachama wa COMNETA, wawe na umoja, mshikamano na kupendana ili kuepuka migogoro inayoweza kuyumbisha ustawi wa chama. “Tunawaomba sana, COMNETA, muwe mfano wa kuigwa kwa kuepuka migongano ya wenyewe kwa wenyewe ikiwamo kugombea madaraka ili kuwa umoja wa mfano kwa katika tasnia ya vyombo vya habari hapa nchini’.
Kwa upande wake, mgeni rasmi katika mkutano huo, Mkurugenzi wa Idara ya Habari (MAELEZO) Assah Mwambene aliupongeza umoja huo na kuwataka kuendelea kuwa daraja muhimu la kuipasha jamii mambo yote ya msingi bila kuvunja misingi ya kitaifa ikiwemo kulinda maslahi ya taifa.
“Kwanza kabisa, niwapongeze, COMNETA kwa kuanzisha umoja wenu huu, na kuwapo kwangu hapa leo kunanifunza mengi, hivyo kwa yale yote mulioniomba nami, nitayafikisha kwa wahusika na kuyafanyia kazi” alisema, Mwambene.
Aidha, akijibu maswali mbali mbali ya wajumbe yaliyokuwa yakitolewa kwenye mkutano huo, Mwambene aliwahakikishia kuwa Serikali inatambua mchango wa vyombo vya habari na inatarajia kupeleka muswada wa sheria ya vyombo vya habari kwenye Bunge lijalo.
“Muswada wa habari upo tayari, tunatarajia utapelekwa Bungeni katika kikao kijacho mwezi Desemba ili kujadiliwa.Tunaamini Kamati husika ya Bunge itawakaribisha wadau wa tasnia ya habari ili kutoa mawazo yao katika muswada huo kabla haujafikishwa bungeni,” alisema.
DSC05335
Mkurugenzi wa Idara ya Habari (MAELEZO) Assah Mwambene akitoa risala wakati akifungua mkutano wa siku nne wa COMNETA unaoendelea mjini Bagamoyo mkoa wa Pwani.
DSC05357

Akidokeza juu ya yaliyomo ndani ya muswada huo, Mwambene alisema umebainisha wazi ulazima wa wamiliki wa vyombo vya habari kuwakatia bima za afya na usalama kazini waajiriwa wao pamoja na suala la maslahi stahiki kwa waandishi wa habari. Muswada huo pia umependekeza kiwango cha elimu kwa mwandishi wa habari kiwe shahada ya kwanza.
Kwa upande wake, Makamu Mwenyekiti wa COMNETA, Bw. Felician Nchewe aliomba Serikali ivifikirie vyombo vya Jamii nchini, katika kufikia malengo yake.
DSC05408
Afisa Mipango Taifa wa Kitengo cha Mawasiliano na Habari na mratibu wa miradi ya UNESCO, Bw.Yusuph Al-Amin akizungumza mbele ya mgeni rasmi Mkurugenzi wa Idara ya Habari (MAELEZO) wakati wa ufunguzi wa mkutano wa nne wa WanaCOMNETA uliofunguliwa rasmi jana wilayani Bagamoyo mkoa wa Pwani.
“Kwa sasa COMNETA, tumefikia malengo mbali mbali, hivyo tunaiomba sana Serikali ivifikie vyombo hivi vya Jamii, kama ilivyo kwa wenzetu kupitia TCRA, kuvisaidia vituo vya Tele Centre kufikia malengo yao” alisema Nchewe.
Kwa upande wake, Mkufunzi wa radio za Jamii kutoka UNESCO, Mama Rose Hajj Mwalimu alisema mkutano huo wa COMNETA wa siku nne, ni wa kuweka mifumo na mikakati bora ya uendashaji wa vituo hivyo na kuweka maazimio ya kufanyia kazi. Ambapo uliwahusisha Mameneja na Wakurugenzi kutoka radio za Jamii (Community Radio) zilizopo nchini.
Mkutano huo unaendelea katika hoteli ya New Palm Tree Village, Bagamoyo.
DSC05371
Meneja wa Redio Kahama FM Marco Mipawa akichangia maoni yake juu ya sheria ya Magereza wakati wa mkutano wa nne wa COMNETA unaohusisha redio za Jamii nchini uliofadhiliwa na Shirika la UNESCO kupitia mradi wa DEP.
DSC05384
Afisa Habari wa Kitengo cha Habari cha Umoja wa Mataifa (UNIC) Bi. Usia Nkhoma Ledama akitoa maoni yake katika mkutano huo
DSC05303
Baadhi ya washiriki wakisikiliza mada mbalimbali zilizokuwa zikitolewa wakati wa mkutano wa nne wa COMNETA unaoendelea Bagamoyo mkoani Pwani.
DSC05272
Erick Kalunga kutoka Ubalozi wa Uswiss ambao wanadhamini mradi wa SIDA akizungumzia furaha yao kuona miradi wanayofadhili inapiga hatua na kuleta maendeleo kwa jamii.
DSC05432
Mwenyekiti wa Tanzania Telecentre Network (TTN) Bw. Hirnoy Barmeda akizungumzia umuhimu wa Telecentre kwa jamii.
DSC05441
Mkurugenzi wa taasisi isiyo ya kiserikali ya Barmedas na Jamii Foundation Crystal Kigoni akifafanua kuhusu taasisi yao isiyo ya Kiserikali inayojishughulisha na mambo ya ustawi wa Jamiikupitia vyombo vya habari na Teknohama kwa kuibua mambo yanayotokea mitaani kwa jamii inayozunguka Redio za Jamii.
DSC05446
Washiriki wa mkutano wa nne wa COMNETA unaoendelea wilayani Bagamoyo mkoani Pwani.
DSC05453
Mkutano wa nne wa WanaCOMNETA ukiendelea katika hoteli ya New Palm Tree wilayani Bagamoyo mkoa wa Pwani.
DSC05450
Mratibu wa Mtandao wa Jinsia na Habari Tawi la Tanzania (GEMSAT) Bi. Gladness Hemedi Munuo akiongelea usawa wa jinsia katika Uongozi na Utawala kwa Redio za Jamii.
IMG_4988
Mshauri wa UNESCO, Balozi mstaafu Mh. Celestine Liundi akisisitiza umuhimu wa kuhubiri amani kwa redio za Jamii nchini.
DSC05265
Meneja wa mradi wa DEP kutoka UNESCO Courtney Ivins akibadilishana mawazo na Mwenyekiti wa COMNETA ambaye pia ni Mkurugenzi wa Redio ya Jamii ya Wilayani Karagwe ya FADECO Bw.Joseph Sekiku kwenye mkutano wa WanaCOMNETA unaoendelea wilayani Bagamoyo mkoa wa Pwani.
DSC05422
Mkurugenzi wa Idara ya Habari (MAELEZO) Bw. Assah Mwambene katika picha ya pamoja na WanaCOMNETA mara baada ya kufungua mkutano wa nne wa COMNETA wilayani Bagamoyo.
DSC05425
Mkurugenzi wa Idara ya Habari (MAELEZO) Assah Mwambene katika picha ya pamoja na Bodi ya COMNETA.
DSC05420
Mkurugenzi wa Idara ya Habari (MAELEZO) Assah Mwambene (kulia) akibadilishana mawazo na Mshauri wa UNESCO, Balozi mstaafu Celestine Liundi (katikati) pamoja Mkufunzi wa Mafunzo hayo ambaye pia ni Mjumbe ya wadhamini COMNETA Bw. Gervas Mushiro (kushoto)

Monday, 18 November 2013

THE VOICE OF KATAVI: KATAVI SPORTS BONANZA

THE VOICE OF KATAVI: KATAVI SPORTS BONANZA: by rahim kassonga
Tamasha kubwa la aina  yake na la kwanza la michezo limefanyika leo wilayani Mpanda mkoani Katavi kwa kushir...