Monday 18 November 2013

KATAVI SPORTS BONANZA


by rahim kassonga
Tamasha kubwa la aina  yake na la kwanza la michezo limefanyika leo wilayani Mpanda mkoani Katavi kwa kushirikisha michezo  mbalimbali ikiwemo,mpira wa miguu kwa wanawake,wanaume na watoto,mpira wa pete,mpira wa wavu,riadha ,kukimbia na magunia,kufukuza kuku,mbio za walemavu na kushindana kunywa soda.
Tamasha  hilo lililofanyika katika viwanja vya azimio lilianza saa tatu asubuhi na kumalizika saa kumi na mbili jioni ambapo kamanda wa polisi mkoa wa katavi,Dhahiri Kidavashari ndiye alikuwa mgeni rasmi ambapo alitia baraka katika tamasha hilo kwa kupiga penati na kumfunga muhandisi Frank John wa Tanroad.
Katika hotuba yake kamanda Kidavashari alisisitiza kuwa michezo ni afya,michezo ni ajira lakini pia michezo inaleta undugu kwani inawakusanya watu pamoja na  kuongeza kuwa kama michezo ikitumika vizuri inapunguza uhalifu.
kikosi cha msakila
kikosi cha shule ya Uhuru
timu ya Msakila na Uhuru wakikaguliwa na waamuzi





Afisa michezo halmashauri ya mji-Revocatus Kalunde akifungua Bonanza
waamuzi wa mchezo wa ufunguzi, Daudi (kushoto), Ngalla (katikati) na Kaburu (kulia) wakiingia uwanjani tayari kwa mchezo wa ufunguzi
vijana wa msakila wakisalimiana kabla ya mchezo
kibatari nishati, the super MC akisherehesha



mchezaji wa Msakila akimiliki mpira
vijana wa Msakila wakimpongeza mwenzao baada ya kufunga goli
wanafunzi wa Msakila wakishangilia baada ya mpira kwisha na kuibuka washindi
Ulinzi ulikuwa wa kutosha


timu ya netiboli ya halmashauri ya wilaya ikifanya mazoezi kabla ya kuanza kwa mchezo huo

pasha..pasha..pasha

Timu ya vijana ikipokea maelekezo toka kwa mwalimu wao
MAELEKEZO
Timu za netiboli zikipokea maelekezo kabla ya kuanza kwa mchezo

KIVUMBI KIMEANZA
huwezi amini hadi mapumziko walikuwa wamefungana 16-16





Mkubwa ni mkubwa, mwishowe Halmashauri ya wilaya waliibuka na ushindi

SARAKASI
mambo ya sarakasi pia yalikuwepo, ilikuwa noumaaa sanaaaaaaaaaaaaaaa


WATU WENGIIIIIIIIIIIII
watoto kwa wakubwa, wanawake kwa wanaume


KUFUKUZA KUKU
mtu aliondoka na bonge la jogoo, ilikuwa nouma sanaa, weka mbali na watoto

wanaume wakijiandaa kufukuza kuku

refarii akitoa maelekezo

kuku anapasha
KAZI IMEANZA HATARIIIIIIIIIIIIIIIIIIII

HATIMAE JAMAA KAJIPATIA KITOWEO, kiroho safi




BURUDANI KADHAA ZILITO;EWA, mshikamano arts group nao waliwasha moto




RIADHA MITA 400 KINAMAMA  ilikuwa sooo,





HATARII SANAAA, jamaa akionesha mautundu kwa kucheza na baiskeli huwezi amini, mshikaji alivyotembelea tairi moja


KWENYE VOLLEYBALL NAKO PALIKUWA HAPATOSHI
veta na katavi walioneshana kazi




WEKA MBALI NA WATOTO, mbio za magunia zilifunika

kazi imeanza
huyu jamaa nouma sana, achana nae

soka la wanawake
AMSHA POPO, watoto wakipiga viduku













No comments:

Post a Comment