Mtangazaji wa Mpanda
FM Radio aliyerusha live tamasha kutokea Katumba
Wednesday, 11 September 2013
TAMASHA LA ROSE MUHANDO NDANI YA MNYAKI KATUMBA (MAKAZI YA WAKIMBIZI)
Wednesday, 21 August 2013
Haya ndo mashitaka matatu aliyosomewa Sheikh Ponda mahakamani leo
8/19/2013
habari za kitaifa
Kiongozi wa Jumuiya na Taasisi za Kiislamu Tanzania, Sheikh Issa Ponda leo amepandishwa kizimbani katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Mfawidhi mkoa wa Morogoro kujibu mashitaka matatu yanayomkabili ambayo ni kutotii amri halali, kutoa maneno yenye nia ya kuharibu imani za dini na kushawishi kutenda kosa.
Sheikh Ponda amefikishwa mjini Morogoro na helkopta
ya jeshi la polisi majira ya saa tano asubuhi chini ya ulinzi mkali
ambapo askari waliimarisha ulinzi kwa muda wote huku kikosi cha kutuliza
ghasia FFU wakiwa na silaha mabomu na mbwa ambapo hali hiyo
imesababisha kusimama kwa baadhi ya shughuli zingine za kiofisi katika
ofisi zilizopo jirani na mahakama ya hakimu mkazi wakati kesi hiyo
ikiendelea ...
Akisoma shataka mbele ya hakimu mkazi Richard Kabate , wakili
mkuu wa serikali kanda ya Morogoro Benard Kongola amedai kuwa shekh
Ponda anadaiwa kutenda makosa hayo matatu Agosti 10 mwaka huu majira ya
jioni katika viwanja vya shule ya msingi kiwanja cha ndege manispaa ya
Morogoro.
Katika shitaka la kwanza la shekhe Ponda anadaiwa
kutotii amri halali ambapo shitaka la pili anadaiwa kutoa maneno yenye
nia ya kuharibu imani za dini kwa kutoa maneno kuwa serikali iliamua
kupeleka jeshi Mtwara kushughulikia suala la vurugu iliyotokana na gesi
kwa kuwaua na kuwatesa wananchi kwa sababu asilimia 90 ya wakazi wa
Mtwara ni Waislamu.
Shitaka la tatu linalomkabili shekh Ponda ni
kushawishi na kutenda kosa ambapo anadaiwa kuwa alitoa maneno ya
ushawishi kwa kuwataka waislaam wasikubali uundwaji wa kamati za ulinzi
na usalama za misikiti kwani zinaundwa na Bakwata ambao ni vibaraka wa
CCM na serikali, na kama kamati hizo zitajitokeza aliwaamuru wafunge
milango na madirisha ya misikiti kuwapiga.
Baada ya kusomewa mashitaka hayo shekh Ponda
anayetetewa na mawakili wasomi Barthoromew Tarimo na Ignas Punge alikataa mashataka yote matatu na hivyo upande wa mashitaka
kupinga dhamana kwa madai kuwa shekh Ponda anatumikia kifungo cha nje na
kwamba hakutakiwa kufanya kosa, hata hivyo anakabiliwa na makosa
mengine.
Tuesday, 20 August 2013
Picha na habari kamili kuhusu vurugu zilizotokea jijini mwanza leo
MAANDAMANO ya amani yaliyokuwa yameandaliwa na chama cha demokrasia na maendeleo(chadema) yamegeuka shubiri kwa wakazi wa jiji la Mwanza baada ya kuibuka mapambano makali baina ya waandamanaji hao na jeshi la polisi mkoani Mwanza na kusababisha polisi kutumia nguvu kuwatawanya wafuasi wa chama hicho.
Maandamano hayo ya amani ambayo yalianzia katika eneo la Buzuruga nje kidogo ya jiji la Mwanza yalikuwa yakiongozwa na wabunge Highness Kiwia wa Ilemela pamoja na Ezekiel Wenje kuelekea katika viwanja vya Furahisha na yalilenga kumshinikiza Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, Ernest Ndikilo kutoa barua zinazodaiwa kuandikwa na ofisi ya Waziri Mkuu Tamisemi kuwarejesha madiwani watatu waliotimuliwa katika Manispaa ya Ilemela kutokana na kushindwa kuhudhuria vikao vitatu mfululizo.
Polisi wenye silaha pamoja na askari kanzu walianza kutanda katika eneo hilo la Furahisha wakiongozwa na Mkuu wa upelelezi wa makosa ya jinai Mkoa wa Mwanza RCO Konyo ambaye alikuwa akitumia gari lenye namba za usajili DK 068EXV aina ya Toyota Land Cruiser
Maandamano hayo ambayo awali yalionekana kana kwamba yangelimalizika salama yaliwasili katika viwanja vya Furahisha majira ya saa 5.38 huku yakiongozwa na gari la polisi lenye namba za usajili za nchi ya Uganda 779 UAG likiwa nimesheheni polisi wenye silaha nzito ikiwa ni pamoja na mabomu ya machozi na bunduki pamoja na askari kadhaa ambao walikuwa katikati ya maandamano hayo.
Baada ya maandamano hayo kuwasili katika viwanja vya Furahisha kwa amani,waandamani hao ambao walikuwa na mabango mbalimbali yaliyosomeka kuwa :‘Matata hatutaki uendelee kuwa Meya wa Ilemela rudia kazi yako ya awali,.... na jingine Jaji Sumari tumechoka kuahirisha mara kwa mara kesi dhidi ya Matata ....na jingine lililosomeka kuwa RD Ndikilo tunahitaji barua za kurejeshwa kwa madiwani wetu.
Hata hivyo tofauti na ilivyokuwa imetangazwa kuwa maandamano hayo ya amani yangelipokelewa na Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Ernest Ndikilo,hakukuwa na kiongozi yoyote wa Serikali ambaye alikuwepo uwanjani hapo kupokea maandamano hayo.
Kufuatia kutoonekana kwa kiongozi yoyote wa Serikali,viongozi wa chadema pamoja na wabunge wao walikutana kwa faragha kwa dakika kadhaa kwa ajili ya kujua hatima ya maandamano hayo ambapo Mbunge wa Nyamagana Ezekiel Wenje alipanda jukwaani saa 6.45 na kuwaeleza maelfu ya waandamanaji kuwa wameamua kumtuma Mbunge wa Ilemela Highnes Kiwia kwenda ofisini kwa Mkuu wa Mkoa wa Mwanza kuchukua majibu kwa ajili ya kuwaletea wananchi walioandamana juu ya hatima ya madiwani hao.
Hata hivyo saa moja baadae Mbunge huyo alisimama jukwani na wakuwaeleza waandamani hao kuwa simu ya Mbunge Kiwia ilikuwa haipatikani hivyo kuwataka kuandamana kwenda kwa Mkuu wa mkoa wa Mwanza kujua kulikoni na hapo ndipo hali ya hewa ilipochafuka.
Jeshi la polisi baada ya kuona wandamanaji hao wameanza kuelekea katika ofisi za Mkuu wa mkoa liliwataka kutawanyika ambapo waandamanaji hao walikaidi ndipo jeshi la polisi lilipoamua kutumia mabomu ya machozi kuwatawanya wafuasi hao.
Vurugu hizo ambazo zilianza majira ya saa 7.30 zilisababisha kufungwa kwa baadhi ya barabara kutokana na waandamanji hao kuweka vizuizi vya mawe na kuchoma matairi,ambapo pia maduka na ofisi mbalimbali zililazimika kufungwa kwa muda kupisha vurugu hizo.
Baadhi ya wananchi ambao walikuwa wakitumia usafiri wa umma walionekana wakishuka kupitia katika madirisha ya magari hayo na kukimbia kwa hofu ya kujeruhiwa na mabomu pamoja na mawe ambayo yalikuwa yakirushwa na waandamanji hao kwa jeshi la polisi.
MKUU WA MKOA WA MWANZA ALONGA.
Mkuu wa mkoa wa Mwanza akizungumza na Mbunge Kiwia pamoja na viongozi wa chadema ofisini kwake alisema kuwa ameshangazwa na uvumi huo kuwa ofisi yake imekalia barua za kurejeshwa kwa madiwani Abubakar Kapera(Nyamanoro),Dan Kahungu(Kirumba) pamoja na Marietha Chenyenge(Ilemela).
RC Ndikilo alisema kuwa Serikali imekuwa ikifanya kazi zake kwa maandishi na sio kwa kufuata maneno ya mtaani na kueleza kuwa hana barua yoyote toka ofisi ya Waziri Mkuu inayomualifu kuhusu kuwarejesha madiwani hao baada ya kukata rufaa.
“We Mbunge kuna siku ulinipigia simu ukiniuliza juu ya kuwepo kwa barua hizo nami nilikujibu kuwa kwa kuwa uko hapo Bungeni Dodoma ambapo pia kuna ofisi ya Waziri Mkuu nilikujibu kuwa ni muhimu ukawaona viongozi wakuu wa Tamisemi ikiwa ni pamoja na Waziri Mkuu,pia nilikushauri kuwa wakupe japo nakala ya barua hiyo”,alisema RC Ndikilo.
“Lakini cha kushangaza nimekuwa nikisikia maneno ya ajabu kuwa nimeficha barua za madiwani hao,ikumbukwe kuwa madiwnai hao hawakukata rufaa kwangu bali walikata rufaa ngazi ya juu kabisa,ili kukata mzizi wa fitina naomba kati ya tarehe 26 hadi 27 wewe Mbunge pamoja na mimi twende TAMISEMI kukutana na viongozi ili kukata mzizi wa fitina na tuje tuwaeleze wananchi ukweli uliopo”,alisema RC Ndikilo.
Kuhusu suala la Meya Henry Matata kutoondolewa madarakani RC Ndikilo alisema kuwa hawezi kulizungumzia suala hilo kwa kuheshimu mamlaka ya mahakama na kuwataka chadema kuvuta subira hadi pale mahakama itakapotoa maamuzi yake.
KAULI YA MBUNGE KIWIA.
Akizungumza katika ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Mwanza,Kiwia alisema kuwa waliamua kuitisha maandamano hayo kutokana na kuelezwa na Waziri Hawa Ghasia kuwa tayari barua hizo zimeishatumwa mkoani Mwanza.
“Mheshimiwa Mkuu wa mkoa hawa madiwani waliosimamishwa ni wawakilishi wa wananchi,wamekaa nje kwa miezi saba sasa na uchaguzi wa Meya haukuwa halali ndio maana tuliamua kuitisha maandamano kwa ajili ya kuhakikisha madiwani hawa wanarejeshwa.
RPC MANGU.
Akizungumza kwa simu juu ya kutokea kwa vurugu zilizosababisha kupigwa kwa mabomu ya machozi,Kamanda wa polisi mkoa wa Mwanza Ernest Mangu alisema kuwa polisi walifanikiwa kudhibiti vurugu hizo na hadi sasa hawezi kusema ni wananchi wangapi ambao walikamatwa kuhusu vurugu hizo.










Mtandao wa Kagame wadai kuwa Mama Salma Kikwete ni Mnyarwanda
Baada ya kukurupa na madai kwamba Rais Kikwete si mtanzania halisi na kwamba ni mtu mwenye asili ya Burundi, mtandao huo umekuja na kioja kipya....
Taarifa iliyotolewa jana tarehe 19/08/2013 na mtandao huo inadai kwamba mke wa Rais Kikwete aitwaye Mama Salma Kikiwete ni mnyarwanda wa kabila la wahutu ( mhutu )..
Katika maelezo yake, mtandao huo umeenda mbali na kudai kuwa Mama Salma Kikwete ni binamu wa rais wa zamani wa Rwanda, Juvenal Habyarimana na ndo maana rais Kikwete alitoa ushauri wa mazungumzo ya amani kati ya Kagame na waasi....
.............................................................
HII NDO POST YAO WALIYOTOA
---------------------------------------------
New details obtained by News of Rwanda
may give insight into why Tanzania’s President Jakaya Kikwete came out
as the sole global leader sympathetic to Rwandan FDLR rebels based in DR
Congo jungles since 1994.
According to secret US State Department
cables published by whistle-blowing site Wikileaks, President Jakaya
Kikwete’s wife fondly known in Tanzania as “Mama Salma Kikwete” is a
cousin of former Rwanda leader Juvenal Habyarimana. The shocking details
are contained in a cable sent to Washington on Thursday May 5th, 2005,
by Shabyna Stillman, a senior diplomat at the US embassy in Dar es
Salaam.
The US embassy was giving update on the
selection of Mr Jakaya Kikwete to be the CCM flag-bearer in the
presidential election late that year. “For years, observers of the Great
Lakes conflicts have considered Kikwete to be virulently pro-Hutu,”
reads the cable, in part.
“Kikwete’s marriage to a cousin of
former Rwandan President Juvenal Habyarimana may have fueled these
rumors, which are now fading as the Burundi conflict winds down,” adds
the cable, signed by Stillman.
According to the US embassy, Mr
Kikwete’s love affair with “Hutus” could be seen in his spirited support
for Burundian rebels at the time fighting former President Pierre
Buyoya.
Since 1995, up until 2005 when Mr.
Kikwete was foreign affairs minister of Tanzania, rumours have swelled
around him suggesting he sided massively with the ethnic extremist
establishment. It is this system that planned and executed the genocide
against Tutsis in 1994, and fled across to Zaire and other parts of the
world.
It is alleged, around 1996, Mr Kikwete
suggested publicly that “Hutus” need to be armed to fight off the
government in Kigali at the time. A book published by virulent critic of
President Paul Kagame and historian Gérard PRUNIER writes that Tanzania
did offer to train troops for Seth Sendashonga.
A former leader of the Rwanda Patriotic
Front (RPF), for whom he was a minister in the government set up after
the rebel movement’s victory over the army and the militias responsible
for the genocide in 1994, Mr. Sendashonga was murdered in Nairobi,
Kenya, on 16 May 1998 by, according to PRUNIER, “unknown assailants.”
Fast forward to May 26, 2013, President
Jakaya Kikwete goes public with a suggestion that the government of
President Kagame in Rwanda negotiates with rebels of the Democratic
Forces for the Liberation of Rwanda (FDLR). The group was formed in May
2000, but its members had been roaming DRC forests ever since they lost
power in Kigali.
The suggestion by a head of state of
Tanzania, a country that had long been considered a friendly nation to
Rwanda, caught many by surprise. Since then, the two countries are
embroiled in a bitter war of words.
The ex-Rwandan Juvenal Habyarimana died on the evening of April 6th,
1994, after his plane was shot down by extremist members of inner
circle who did not want the peace talks with the RPF rebels. In the same
plane was Burundian counterpart Cyprien Ntaryamira and French pilots.
The death of the French crew has been
the centre of legal battles in France and the United States. A French
judicial inquiry did confirm that the plane was brought down by a
missile fired from a military camp next to Habyarimana’s home near the
airport.
Monday, 5 August 2013
Meneja masoko na meneja wa mpanda fm Gerrrald Seth Sedekia akiwa ofisini kwake na mtangazaji wa mpanda fm Fatuma Amas
Mkurugezi wa kituo cha radio mpanda fm Ndg Kanji aliyevaa tshet ya NMB akiwa baadhi ya asikari uwanja wa ndege (mpanda air port) wakimlaki waziri mkuu wa jamhuri ya muungano wa Tanzani
ofisi za uwanja wa ndege wa mpanda
Mkurugezi wa kituo cha radio mpanda fm Ndg Kanji aliyevaa tshet ya NMB akiwa baadhi ya asikari uwanja wa ndege (mpanda air port) wakimlaki waziri mkuu wa jamhuri ya muungano wa Tanzani
ofisi za uwanja wa ndege wa mpanda
| Gerald Seth Sedekia meneja masoko mpanda fm |
Wednesday, 31 July 2013
CHADEMA HAINA UBAVU WA KUMKATAA TENDWA
OFISI ya Msajili wa Vyama vya Siasa, imesema Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) hakina ubavu wa kumkataa au kutomtambua John Tendwa kuwa ndiye msajili wa vyama vya siasa nchini.
Kauli hiyo ilitolewa jana na Naibu Msajili wa Vyama vya Siasai, Rajab Baraka alipozungumza na MTANZANIA kuhusu kauli iliyotolewa na Katibu Mkuu wa Chadema, Dk. Wilbroad Slaa aliyedai chama hicho hakimtambui John Tendwa kuwa ndiye msajili wa vyama vya siasa.
Katika madai yake Dk. Slaa alidai Tendwa anakipendelea CCM katika kutoa haki ya demokrasia na hatendi haki kama mlezi wa vyama vyote vya siasa nchini.
Dk. Slaa alisema hayo wiki iliyopita alipokuwa akizungumza na waandishi wa Habari na kusisitiza hata katika barua zao za mawasiliano kwenda kwa ofisi ya msajili chama hicho hakitumii jina la John Tendwa.
Kwa mujibu wa Dk. Slaa, Chadema kinaitambua ofisi ya Msajili wa Vyama tu lakini hakimtambui Tendwa kuwa ndiye msajili wa vyama vya siasa nchini.
“Hatumpelekei hata barua huyu hatunzi sheria siyo mtu wa kulea vyama ni mlezi wa chama kimoja, hayuko serious na hatushirikiani naye mpaka aondoke madarakani.
“Tukiandika barua hatuweki jina lake lakini tunaitambua ofisi yake, hata yeye mwenyewe analijua hilo na akijibu barua zetu haweki jina lake,” alidai Dk. Slaa.
Akijibu hoja hizo, Naibu Msajili alisema Chadema hawana ubavu wa kutomtambua Tendwa kwa sababu amewekwa kisheria na ofisi yake ipo kisheria.
Alisisitiza Tendwa ataendelea kuwa mlezi wa vyama vyote na siyo chama kimoja kama inavyodaiwa na kuvitaka vyama vyote kuheshimu sheria iliyomuweka madarakani msajili huyo.
Mtanzania.
TANZANIA YAMJIBU RAIS KAGAME....YADAI IPO TAYARI KWA LOLOTE NA AKITHUBUTU ITAMCHAPA KAMA MTOTO

Kauli hiyo ya kwanza nzito imetolewa jana na Wizara ya Mambo ya Nje ya Ushirikiano wa Kimataifa kufuatia taarifa ya matamshi makali yanayodaiwa kutolewa na Rais Paul Kagame wa Rwanda, dhidi ya Rais Jakaya Kikwete na kutishia kuishambulia Tanzania.
Akizungumza na Tanzania Daima jana jijini Dar es Salaam, Msemaji wa wizara hiyo, Mkumbwa Ally, alisema ingawa Serikali ya Tanzania hadi sasa inajua haina ugomvi wowote na Rwanda, lakini amekiri kuwapo kwa kile alichokiita ‘kupishana lugha’ kwa Rais Jakaya Kikwete na Paul Kagame.
Mkumbwa alikiri Serikali ya Tanzania kunasa matamshi yanayodaiwa kutolewa na Rais Kagame katika moja ya hotuba zake aliyoitoa Juni 30, nchini kwake wakati akihutubia katika hafla moja ya vijana.
Kwa mujibu wa hotuba hiyo, ambayo kwa wiki sasa imesambazwa katika baadhi ya mitandao ya kijamii, Kagame anadaiwa kusikika akitoa matamshi ya vitisho dhidi ya Rais Kikwete, kwamba anamsubiri katika wakati aujuao na kumchapa.
Baadhi ya maneno yanayodaiwa Rais Kagame aliwaambia vijana waliokutana katika mkutano wao uliojulikana kama ‘Youth Konnect’ na kufadhiliwa na mke wake, Janet Kagame, yanasema: “Huyu mtu mliyemsikia akiwa upande wa Interahamwe na FDLR na akashauri majadiliano….majadiliano?”
Aidha, Kagame anadaiwa kusema kuwa hatakuwa tayari kujadili jambo hilo, isipokuwa atamsubiri Rais Kikwete sehemu muafaka na ‘kumtandika’.
“Sitapoteza muda wangu kumjibu Kikwete, inajulikana maana kuna mahali hataweza kuvuka…haiwezekani,” alikaririwa akisema Rais Kagame, akilenga kumtisha Rais Kikwete.
Mbali na Kagame, baadhi ya viongozi kadhaa wa serikali ya Rwanda wamekuwa wakimshambulia Rais Kikwete wakimpachika majina ya kejeli ya; “Rais mhurumia magaidi, wauaji wa kimbari, mkorofi na mwenye dharau.”
Mkumbwa hata hivyo alisema Serikali ya Tanzania haina sababu ya kuingia katika vita na Rwanda, kwa sababu tu ya ushauri alioutoa Rais Kikwete wa kuitaka ikutane na wapinzani wake wanaoishi ndani ya nchi ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC), kujadiliana kuhusu amani ya nchi za Maziwa Makuu.
Alisema msimamo wa Tanzania utabaki kuwa uleule wa kuitaka nchi hiyo ikubali kukaa meza moja na wapinzani wake, ili kumaliza migogoro inayoendelea katika nchi hizo za maziwa makuu, ambao unaungwa mkono na jumuiya ya kimataifa na SADC.
“Unajua mgogoro wa DRC na Rwanda hauwezi kumalizika bila ya nchi hizo kukaa meza moja na wapinzani wao ili kupata suluhu ya kudumu,” alisema Mkumbwa.
Aliwataka Watanzania kuwa watulivu na kuendelea na kazi zao kama kawaida, kwani serikali yao iko makini katika kulinda mipaka yake.
Chanzo cha mzozo
Msuguano baina ya nchi hizi mbili ulianza siku chache tu baada ya kumalizika kwa kikao cha viongozi wa nchi za Maziwa Makuu na ambacho kilihudhuriwa pia na Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Ban Ki-Moon, chini ya uenyekiti wa Rais wa Uganda, Yoweri Museveni.
Rais Kikwete wakati akimtaarifu Rais Museveni kile walichokuwa wamekijadili katika kikao hicho kwa vile aliketi kwa muda kwa kuwa alichelewa kuwasili, alisema ni vema serikali za Rwanda na Uganda zifungue mlango wa mazungumzo na waasi wao na akaanza kutaja majina ya vikundi vya uasi vya nchi hiyo vilivyopo nchini DRC.
Habari zinasema kauli ya Rais Kikwete iliungwa mkono na Rais Museveni akisema: “Bila mazungumzo hatutafika popote pale”.
Hata hivyo, matamshi hayo yalijibiwa kwa ukali na serikali ya Rwanda, kiasi cha kumlazimu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Bernard Membe, kutoa tamko bungeni.
Kwa kauli yake, Membe alisema serikali ilikuwa imeshangazwa na shutuma hizo za Rwanda kwani halikuwa jambo baya kutoa ushauri uliolenga kuleta mapatano na kuepusha umwagaji zaidi wa damu wa wananchi.
Akaongeza kuwa, ilikuwa ni wajibu wa Serikali ya Rwanda kuupokea ama kuukataa, na wala si kutoa maneno ya kejeli na vitisho.
Kauli ya Zitto
Akizungumzia kauli hiyo ya vitisho, mwanasiasa machachari hapa nchini na Naibu Katibu Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Zitto Kabwe, alisema ushauri wa Rais Kikwete kwa Rwanda ulikuwa wa busara mno na akashangaa kuona nchi hiyo jirani ikitoa vitisho, kejeli, dharau na ukosefu wa adabu kwa Kikwete.
Katika moja ya tamshi lake alilolitoa jana katika mitandano ya kijamii, Zitto ambaye ni Mbunge wa Kigoma Kaskazini (CHADEMA) alisema Marekani wanaongea na waasi wa kundi la Taliban, hivyo hakuna dhambi kwa Rwanda pia kufanya hivyo.
“Pia kama hutaki ushauri si unakataa tu, sasa kuanza kurushiana maneno ya nini tena? Hutaki ushauri basi.
Maneno ya kila siku ya nini? Tangu Kikwete amesema kule Addis, hajasema tena. Membe (waziri) akajibu Dodoma Tanzania haijasema tena. Kigali inasema mambo haya kila siku kwa ajili ya nini?
“Taliban na Al Qaeda si wale wale? Wale watoto waliozaliwa mwaka 1994 na wakimbizi wa Kihutu waliopo Kongo nao ni wauaji? Tufikiri vizuri mambo haya. Kuna ‘genociders’ wasakwe, wakamatwe wahukumiwe. Kuna watu wana haki kabisa ya kutaka kushiriki kwenye siasa za Rwanda na wanazuiwa, wameshika silaha. Hawa lazima wakae meza moja wakubaliane,” alisema Zitto.
Mwanasiasa huyu alisema kwa sasa serikali za nchi hizo mbili zinatakiwa kuingia katika vita ya kupambana na kuondoa umasikini wa watu wake na si vita ya mtutu wa bunduki.
“Busara itumike kwa viongozi ‘neutral’ kama Uhuru Kenyatta kuwaweka pamoja Kagame na Kikwete wamalize tofauti zao. Haya maneno hayana maana yoyote,” alisema.
Alisema vita haitamuumiza Rais Kagame wala Rais Kikwete na familia zao, bali itaumiza wananchi wa kawaida wa mikoa ya Kagera na Kigoma na mikoa ya mpakani ya Rwanda.
“Vita itaturudisha nyuma sana kwenye juhudi za maendeleo. Vita itazima harakati za kujenga demokrasia nchini. Busara itumike tu,” alisema Zitto.
Tanzania Daima
Wanaokwenda ualimu
Serikali imetangaza majina ya wanafunzi 18,754 waliochaguliwa kujiunga na vyuo vya ualimu vilivyo chini yake ikiwa ni ongezeko la wanafunzi 1,659 ikilinganishwa na 17,095 waliochaguliwa mwaka jana.
Kati ya wanafunzi hao, 11,806 wamechaguliwa kusomea ngazi ya cheti (Grade A) na 6,948 watasoma katika ngazi ya stashahada.
Wanafunzi 363 wamechaguliwa kusoma elimu maalumu kwa ngazi ya cheti huku 57 wakisoma elimu hiyo kwa ngazi ya stashahada.
Akizungumza na mwandishi wetu jana, Msemaji wa
Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi, Ntambi Bunyazu alisema wanafunzi
wanatakiwa kuripoti kwenye vyuo walivyopangiwa kuanzia Agosti 15, mwaka
huu.
“Usajili utafungwa Agosti 25 saa 12:00 jioni,
‘Joining instructions’ (fomu ya maelekezo ya kujiunga) zitatumwa kwa
wahusika kupitia anuani zao.... fomu hizi pia zinapatikana kwenye tovuti
ya Wizara ya Elimu na mafunzo ya Ufundi,” alisema.
Taarifa ya Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi
iliyotolewa baadaye jana ilisema kuwa wanafunzi waliochaguliwa
wanatakiwa kufika vyuoni wakiwa na vyeti halisi vya kidato cha nne na
cha sita vinavyotolewa na Baraza la Mitihani la Tanzania (Necta) , ada
ya muhula wa kwanza Sh100,000 au Sh200,000 kwa mwaka.
Wanatakiwa kuwa na “Sare ya chuo kulingana na
maelekezo ya chuo husika, fedha za tahadhari chuoni na matumizi
binafsi,” inasema taarifa hiyo.
Taarifa hiyo inaeleza pia kuwa wakuu wa vyuo
wanatakiwa kuhakikisha wanafunzi wanaosajiliwa ni wale waliopo kwenye
orodha iliyotolewa na wizara na si vinginevyo.
Wengi wa wanafunzi hawa ni wale waliohitimu kidato
cha nne mwaka 2012 na kidato cha sita mwaka huu. Kwa upande wa wale wa
kidato cha nne, matokeo yaliyotangazwa na Wizara ya Elimu na Mafunzo ya
Ufundi yalionyesha kuwa watahiniwa 159,609 wa shule walifaulu kwa daraja
la kwanza mpaka la nne.
Inaonyesha pia kuwa kwa upande wa Tanzania Bara,
wanafunzi 34,599 walifaulu kwa daraja la kwanza mpaka la tatu na kati
yake waliochaguliwa kujiunga na kidato cha tano na vyuo vya ufundi
walikuwa ni 34,213.
Kwa upande wa matokeo ya kidato cha sita mwaka
huu, watahiniwa waliofaulu mtihani huo walikuwa ni 44,366 kati yao
40,242 wakiwa ni wa shule. Matokeo hayo yanaonyesha pia kuwa, watahiniwa
35,880 ndiyo waliofaulu kwa daraja la kwanza mpaka la tatu.
Kwa mujibu wa Kitabu cha Takwimu cha Wizara ya
Elimu (Best), mwaka 2012 wanafunzi 17,095 walichaguliwa kujiunga na vyuo
mbalimbali vya ualimu nchini.
"WAPIGWE TU" YA MIZENGO PINDA ITAMFIKISHA KORTINI
KAULI ya Waziri Mkuu, Mizengo Pinda, ya kubariki vyombo vya dola kuendeleza kipigo kwa raia wanaokaidi amri imechukua sura mpya baada ya Kituo cha Sheria na Haki za Bindamu (LHRC) kutangaza kumburuza mahakamani wiki hii kutokana na kushindwa kufuta kauli yake.
Juni 20, mwaka huu, wakati akijibu maswali ya papo kwa hapo bungeni, Waziri Mkuu, Pinda, alivitaka vyombo vya dola kuendelea kuwapiga raia, akisema kuwa hakuna namna nyingine kwani serikali imechoka.
Kauli hiyo imekuwa ikipingwa na wananchi, mashirika ya kutetea haki za binadamu na wanasiasa wakimtaka Waziri Mkuu, Pinda, kuifuta kwa kuomba radhi, wakidai kuwa inachochea uvunjifu wa sheria.
Akitangaza kusudio la kituo hicho kufungua kesi dhidi ya Pinda, Mkurugenzi wa maboresho na utetezi, Harold Sungusia, alisema hadi jana walikuwa tayari wameandaa kusudio la shtaka lao.
Alisema kuwa kisheria kilichowafanya kufikia uamuzi huo ni kutokana na waziri mkuu huyo kukiuka Katiba ya nchi inayozungumzia usawa mbele ya sheria.
“Kitendo alichofanya waziri mkuu cha kuwaruhusu polisi kupiga wananchi hakikubaliki hata kidogo na walitegemea kwamba angeomba radhi kutokana na kauli yake hiyo tangu alivyoshinikizwa kufanya hivyo na makundi mbalimbali.
“Badala yake ameendelea kuwa kimya licha ya mkubwa wake, Rais Jakaya Kikwete, hivi karibuni kukiri kwamba mtendaji wake huyo aliteleza,” alisema.
Sungusia aliongeza kuwa Alhamisi wiki hii wataweka bayana kwa waandishi wa habari ni wapi kesi hiyo itafunguliwa.
Pinda alitoa kauli hiyo tata ambayo imehojiwa na wengi wakati akijibu swali la Mbunge wa Kilwa Kaskazini, Murtaza Mangungu (CCM) aliyehoji kama serikali iko tayari kutoa tamko kuhusu vurugu zilizotokea jijini Arusha, Mtwara na maeneo mengine pamoja na hatua ya vyombo vya dola kutumia nguvu.
Katika majibu yake Pinda alisema kuwa suala la amani linawagusa wote, kwamba jukumu ni kwa viongozi wa kisiasa. Alifafanua kuwa kama viongozi wa kisiasa hawatafika mahali wakakubaliana bila kujali vyama vyao nchi itafika pabaya.
Pinda alifafanua kuwa kwa upande wa serikali lazima wahakikishe kwamba wale wote wanaojaribu kuvunja amani kwa namna yoyote ile kazi waliyonayo ni kupambana kweli kweli kwa njia zozote zinazostahili.
“Mimi naomba sana Watanzania, maana kila juhudi zinazoonekana zinaelekea huko, tunapata watu wengine wanajitokeza kuwa mara unajua…unajua. Acheni serikali itimize wajibu wake, kwa sababu jambo hili ni la msingi na wote tulilinde kwa nguvu zetu zote.
“Mheshimiwa Mangungu umeanza vizuri lakini hapa unasema vyombo vya dola vinapiga watu. Ukifanya fujo unaambiwa usifanye hiki, ukaamua wewe kukaidi, utapigwa tu,” alisema.
Waziri mkuu aliongeza kuwa hakuna namna nyingine, maana lazima watu wakubaliane na serikali kwamba nchi hii wanaiendesha kwa misingi ya kisheria.
“Sasa kama wewe umekaidi, hutaki, unaona kwamba ni imara zaidi, wewe ni jeuri zaidi, watakupiga tu, na mimi nasema wapigwe tu, maana hakuna namna nyingine, tumechoka,” alisema
Tanzania Daima
Subscribe to:
Posts (Atom)








