SIKU chache baada ya kutoka lupango kwa msala wa madawa ya kulevya,
‘video queen grade one’ Bongo, Agnes Gerald ‘Masogange’ ametupia picha
za utupu mtandaoni.
Agnes Gerald ‘Masogange’ katika pozi.
Masogange na mwenzake, Melisa Edward walikamatwa nchini Afrika Kusini
Julai 5, mwaka huu wakidhaniwa kuwa na madawa haramu ya kulevya na
baadaye mahakama kuu ya nchini humo ikawaachia kwa dhamana ikidai unga
waliokutwa nao si madawa ya kulevya bali ni mali ghafi zijulikanazo kama
Methamphetamine.
Baada
ya kuachiwa huru, Masogange anayesifika kwa kuwa na figa matata,
alitupia picha hizo katika mtandao wa Instagram akiwa amevalia sidiria
na nguo ya ndani pekee hali iliyowafanya wafuasi wa mtandao huo
wamshangae huku wengi wakimlaumu kuwa alichokifanya hakifanani na
maadili ya Mtanzania.
Video queen grade one Bongo, Agnes Gerald ‘Masogange’.
“Sasa huu upuuzi gani unatuwekea humu, kwani kila kitu unachofanya ni
lazima sisi tuone? Hivi kwa nini mastaa wa Bongo wanapenda kujirahisi
kiasi hiki?” alihoji mmoja wa wafuasi wa mtandao huo.
Pamoja na wadau wengi kuonesha kukerwa na picha hizo, Masogange
hakujali, aliwajibu kuwa kama hawataki kuziona picha hizo wamuondoe
kwenye listi ya marafiki mtandaoni humo kwani siyo lazima.
“Hii ni akaunti yangu, nina uhuru wa kuweka picha za aina yoyote.
Kama mtu anaona nimemkera basi ‘aniblok’ maana hapa nimevaa mavazi ya
kuogelea sasa mlitaka nivae pensi niogelee nayo? Simuogopi mtu…,”
aliandika Masogange.