WASANII wa filamu nchini bado wanaendelea kupokea kipato kidogo kutoka
kwa wasambazaji wa filamu hali iinayopelekea kudumaza soko la filamu
nchini, huku kupelekea wasanii hao kuwa na kipato cha chini.
Hayo yalibainishwa na msanii wa filamu za maigizo nchini Kulwa Kikumba
'Dude' ambapo aliweka wazi kuwa tasnia hiyo inaonekana kukuwa siku hadi
siku ingawa wasanii hao bado wanaonekana kuwa masikini kutokana na
kipato wanachopata.
Aliweka wazi kuwa mfumo mbaya wa mauzo ya filamu nchini ndio chanzo
pekee kinachodidimiza kazi za wasanii hao huku baadhi yao wakikosa soko
la filamu hali inayochangia baadhi yao kupotea katika tasnia hiyo.
Alibainisha kuwa wapo baadhi ya wasanii wanaendelea kunufaika kutokana
na kazi zao lakini walio wengi wanaendelea kudidimia hadi hapo mfumo wa
usambazaji utakapobadilika ndipo ahueni itakapopatikana kwa wasanii
wengine.
" Sisi wasanii tumekosa ushirikiano kutokana na baadhi ya wasanii
kunufaika na kazi hizo huku wengi kunyonywa na wasambazaji , ila kama
tungeweza kushirikiana wasanii wote tukawa tunauza filamu kwa bei
zinazolingana na ubora na ghrama ya filamu tungefika mbali" alibainisha
Dude
No comments:
Post a Comment