MSANII wa filamu nchini Elizabeth Michael 'Lulu' akanusha taalifa za
kuzushiwa za kuchumbiwa na kukalibia kuolewa muda mchache zilizoandikwa
na moja ya chombo cha habari jijini.
Lulu amekanusha taarifa hizo ambazo zimeandikwa na gazeti moja la udaku
kuwa anatarajia kuolewa hivi karibuni huku wazazi wake wakiwa tayari
wameshapokea mahali.
Akizungumza na katika mahojiano , muigizaji huo
ameweka wazi kuwa ameshangazwa na habari hizo ambapo baadhi ya magazeti
mengi ya udaku ndiyo yamekuwa yakimwandika kile wanachojisikia.
Aliweka wazi kuwa hajachumbiwa na mwanaume yoyote yule na siku ikitokea
amechumbiwa basi kila mtu atajua kwani halitakuwa jambo la kificho tena.
"Sijajua wao wameipata wapi hiyo habari kutoka chanzo kipi, kila kukicha
kumekuwa na habari mtu akijisikia kuandika tu anaandika bila hata ya
kufikiria leo wameandika nimechumbiwa, kesho wataandika nimeolewa, tena
wataandika nimeachwa, kila watakalo lihisi kuandika wanaandika" alieleza
Lulu.
Aliweka wazi kuwa kuchumbiwa kuolewa ni vitu ambavyo vimeumbiwa
binadamu, vipo kama ukiwa na mpango wa mwenyezi mungu nitachumbiwa.
No comments:
Post a Comment