Saturday, 30 November 2013
BAADA YA KUFUKUZWA KWA KUFANYA NGONO NDANI YA GARI YA WEMA SEPETU..PRODUZA HUYO AMENENA MAZITO NA MADUDU YA WEMA SEPETU NA KAMPUNI YAKE
BY ZANNGII ZE ICON
Baada ya juzi kati kuripotiwa habari ya aliyekuwa producer ama
mtengenezaji wa vipindi vya Wema Sepetu Chidi Mohamed kufukuzwa kazi
kutokana na kulitumia gari la kampuni kama sehemu yake ya kuvunjia amri
ya sita na wadada wa mjini, hatimaye katika pitapita zetu za mtandaoni
tuliweza kukutana na kauli ya producer huyo akizungumzia habari hiyo ya
yeye kufukuzwa kazi kwenye kampuni ya Endless Fame ya wema sepetu.
Chidi mwenyewe anasema kuwa habari hizo si za kwel na ni kwamba
wote walioandika wamepanga kumchafua tuu kwa kuogopa kuwa anaweza
kuyaniika mambo mazito yanayoendelea huko endless Fame
Kwa mujibu wa chidi anasema kuwa yeye ameondoka kwenye Kampuni
hiyo siyo kwa sababu ya uzinzi ngani ya gari kama ilivyoripotiwa bali ni
kutokana na sababu hizi kuu mbili.
1. Ameona hamna jipya na wala hamna maendeleo yoyote ndani ya Kampuni hiyo ndio maana ameamua kuondoka
2. Wafanyakazi wa Endless Fame hawalipwi
kabisa ndio maana yeye akaamua kujitoa kwani anafanya kazi bure na pia
sio yeye peke yake aliyeondoka bali kuna wafanyakazi zaidi ya watatu
walioondoka kwenye kampuni hiyo ila nashangaa ni kwanini wameamua
kumchafua yeye?
Bado tunafanya mawasiliano na Endless Fame ili tujue kama daia haya ni ya kweli au la......
Thursday, 28 November 2013
UKWELI WA ISHU YA SNURA NA MRISHO NGASSA.
BY ZANGII ZE ICON
Ni picha ambazo zimekua zikizungumziwa kwenye mitandao ya kijamii na hata kwenye mitandao
mingine ya habari nchini Tanzania zikimwonyesha mchezaji wa Yanga Mrisho Ngassa akiwa mapenzini na mwimbaji Snura wa bongofleva.
Snura anasema mwanzo wa hizi picha kusambaa ni baada ya kupoteza simu yake, namnukuu akisema ‘hizo picha hazina uhusiano wowote unaounganishwa kimapenzi kati yangu na Ngassa ila ni sehemu ya vipande vya movie yangu inaitwa ‘Majanga’ ambayo nimeanza kuifanya na Ngassa amecheza ndani yake kwenye scene za mapenzi, yani Snura kwenye movie amecheza kama binti mrembo anaerukiarukia Wanaume’
‘Simu yangu ilipotea ndio maana wamezipata hizo picha, wakati tunashoot tulikua tunapigapiga tu hayo mapicha, mi sikuwa nataka kuzitoa kabisa manake movie yenyewe bado naifanya nusunusu kutokana na kukosa muda, hii ishu imeniletea sana matatizo manake mwingine anakua haamini unachokiongea na hakuna kitu kinauma kama kuongea ukweli alafu mtu anasema unadanganya’ – Snura
Kwa kumalizia Snura anasema ‘Ngassa alinipiga muda mfupi tu baada ya picha kuanza kusambaa akauliza mbona hizi picha zinasambaa hivi Snura? nikamwambia usinielewe tofauti babaangu kwa sababu mimi mwenyewe sikutaka zitoke, picha nilizopiga nyinginyingi tu wakati tunatengeneza movie ila naona watu wameona hizi ndio nzuri kwa skendo’
mingine ya habari nchini Tanzania zikimwonyesha mchezaji wa Yanga Mrisho Ngassa akiwa mapenzini na mwimbaji Snura wa bongofleva.
Snura anasema mwanzo wa hizi picha kusambaa ni baada ya kupoteza simu yake, namnukuu akisema ‘hizo picha hazina uhusiano wowote unaounganishwa kimapenzi kati yangu na Ngassa ila ni sehemu ya vipande vya movie yangu inaitwa ‘Majanga’ ambayo nimeanza kuifanya na Ngassa amecheza ndani yake kwenye scene za mapenzi, yani Snura kwenye movie amecheza kama binti mrembo anaerukiarukia Wanaume’
‘Simu yangu ilipotea ndio maana wamezipata hizo picha, wakati tunashoot tulikua tunapigapiga tu hayo mapicha, mi sikuwa nataka kuzitoa kabisa manake movie yenyewe bado naifanya nusunusu kutokana na kukosa muda, hii ishu imeniletea sana matatizo manake mwingine anakua haamini unachokiongea na hakuna kitu kinauma kama kuongea ukweli alafu mtu anasema unadanganya’ – Snura
Kwa kumalizia Snura anasema ‘Ngassa alinipiga muda mfupi tu baada ya picha kuanza kusambaa akauliza mbona hizi picha zinasambaa hivi Snura? nikamwambia usinielewe tofauti babaangu kwa sababu mimi mwenyewe sikutaka zitoke, picha nilizopiga nyinginyingi tu wakati tunatengeneza movie ila naona watu wameona hizi ndio nzuri kwa skendo’
WAZEE KATAVI WASHAURI SERIKALI KUENDELEA NA OPERESHENI TOKOMEZA UJANGILI
by isack gerlad
Wazee
Mkoani Katavi wameshauri Serikali kuendelea na operation tokomeza
ujangili kwa kuwa imesadia kwa kiasi kikubwa kuokoa rasilimali za Taifa
zilizokuwa zikiteketea kutokana na baadhi ya watu wachache waliokuwa
wakijihusisha na ujangili wa kuhujumu rasilimali hizo.
Wakiongea
kwenye Mkutano Maalum wa majadiliano na Wazee wakiwa na Mkuu wa Wilaya
Mpanda Paza Mwamlima wamezungumzia juu ya wahamiaji haramu nao
wanajihususha kwa njia moja au nyingine na katika vitendo vya ujangili
na uharibifu wa mazingira wamesema hali hiyo ikiendelea uharibifu wa
rasilimali za Taifa kama wanyama pori na mistu, na uharibifu wa
mazingira hali inayoashiria kutoweka kwa rasilimali za taifa.
Kwa
upande wake Mkuu huyo wa Wilaya ya Mpanda Paza Mwamlima amesema katika
operation tokomeza ujangili iliyofanyika Mkoani Katavi katika
Wilaya ya Mpanda Kata moja ya Mwese pekee jumla ya silaha 250
zilikamatwa hiyo inaonesha ni namna gani watu wanaishi na silaha ambazo
hutumika kwa vitendo vya ujangili hivyo amewaomba wazee hao kusaidia kwa
njia moja au nyingine kuwafichua watu wa namna hiyo wanaojihusisha na
uharifu, akaongeza kuwa wazee ni tunu ya Taifa na amani katika nchi
Wazee wanasaidia katika kuimarisha amani.
Awali
katika risala yao wazee walimweleza Mkuu wa Wilaya kuwa wanakabiliwa na
changamoto mbalimbali ikiwemo ukosefu wa usafiri wa kuwafikia wenzao
walioko mbali kutoka makao makuu ya wilaya na Mkoa kuwafikia wazee
wenzao walioko wilaya ya Mlele na Kata za Inyonga, mamba. Majimoto,
kasansa kibaoni ,usevya mwamapuli,mbede,ikuba, Nsenkwa, Ilelea, Ilunde
na Utende
Pia
alitaja wazee wengine walioko katika kata za mwese, karema ,ikola,
Mishamo katuma Kapalamsenga na sibwesa pamoja na maeneo mengine imekuwa
tatizo kuwafikia hivyo wanaomba kusaidiwa kutatua changamotohiyo.
Changamoto
nyingine waliyozungumzia ni wazee kutohudumiwa ipasavyo hususani
wanpokuwa wakipatiwa matibabu katika Hospitali wakaeleza kuwa
wanakumbana na vikwazo vingi,pia wakaomba kusamehewa na mambo mengine
kama kulipia umeme na huduma nyingine.
Mmoja
wa wazee aliyejitambulisha kwa jina la John Kisalala aliomba eneo la
kusaidia wazee matibabu liwekewe utaratibu mzuri ili kuondoa usumbufu
kwa wazee hao ikiwa ni pamoja na kuondolewa usumbufu wa kulipia huduma
ya maji, umeme na huduma nyingine kwa kuwa wazee hao wamelitumika taifa
kwa muda mrefu na sana na sasa wanatakiwa kuhudumiwa.
Akizungumzia
operation tokomeza ujangilia na operation kimbunga wazee hao wameshauri
washirikishwe katika zoezi hilo kwa kuwa wazee wanawatambua watu ambao
sio wazawa wao wanawatambua watu ambao siyo raia halali.
Naye
Benezite Mwanauta akizungumzia uharibifu wa mazingira na rasilimali za
taifa amewalaumu wafungaji wa kabilia la kisukuma kwa kukataa miti hovyo
huku watu waliopewa dhamana wakiwa wanaangali bila kuchukua hatua
yeyote huku mazingira yakiendelea kuharibika suala hilo lisipochukuliwa
hatua na umuhimu wa kipeke huenda katavi ikageuka jangwa walishauri
hatua za makusudi zichukuliwe ili kunusuru uharibifu huo.
sikiliza hapa
http://www.hulkshare.com/356bxvkxsp1c
HUYU NDIO MSANII WA VITUKO SHOW ALIYEPIGWA NA MKE WAKE KIPIGO CHA PAKA MWIZI.
by zangii ze icon
Anatambulika kwa
HUYU ndiye msanii niliyemzungumzia wiki iliyopita kuhusu kichapo alichopewa kama mnavyomuona hapo pichani.
Anatambulika kwa
jina
''Kazi Kijeba''.. MSANII kutoka kundi la BONGO SUPERSTAR'S
COMEDY linalorusha kipindi chake maarufu hapa nchini (VITUKO SHOW)
Kinachorushwa katika runinga ya CHANNEL TEN Kundu hili limeweka kambi
ya takribani miaka miwili mkoani Tanga.
Nafikiri chazo cha habari cha wiki iliyopita hakikufafanua kisa kwa kina,tuliweza
kuongea na msanii huyu na kugundua kwamba aliyemdunda kumbe alikuwa
mpenzi wake anaeishi maeneo ya usagara Jijini Tanga, Na sio mara moja
alishawahi kumpiga tena mara ya kwanza wakaachana baadae kama mnavyojua
mapenzi, Si wakarudiana tena?.. Ila hii ya sasahivi hakuwa na nia njema
maana alimpigia kelele za mwizi hatimaye msanii huyu kunusurika kufa
aliokolewa na muuza bucha baada ya kukimbilia buchani..! Ama kweli
wanawake wa sikuhizi noma...! Yani weka jiwe niweke kigingi.
HAYA NDIO MAJANGA YALIYOMKUTA TUNDA MAN HUKO TABORA HIVI KARIBUNI.
by zangii ze icon
Msanii wa kizazi kipya - Tunda Man pichani alijikuta akishangiliwa sana na kupata wakati mgumu wa kujipenyeza popote aliposhuka kwenye
gari siku ya tarehe 23.11.2013 kwenye tamasha la uzinduzi wa somo la TEHAMA mkoani Tabora katika uwanja wa Al-hassan Mwinyi, jeshi la polisi lilitakiwa kutoa msaada kwa msanii huyo kwani wanafunzi wengi wa shule za msingi waliohudhuria tamasha hilo walimzonga hali iliyotatanisha ikiwa watadondoka na kuanza kukanyagana.
[chini utaitazama video hiyo-KWA KIASI WALIHARIBU HATA UTARATIBU WA UCHUKUAJI WA VIDEO HIYO KWA SHAUKU YA KUMWONA MSANII WAO]
Akitathimini fadhira za wanafunzi kumshangilia...
wakati akiondoka na kuwaaga
Wanafunzi hawakuridhika na walizidi kulizonga gari wakati akiondoa na ilikuwa vigumu kuwazuia.
Thursday, 21 November 2013
UNESCO YAITAKA SERIKALI KUZITAMBUA REDIO ZA JAMII NCHINI
by zangii ze icon
Mgeni rasmi Mkurugenzi wa Idara ya Habari (MAELEZO) Assah Mwambene
(kushoto) akiwasili katika Hoteli ya New Palm Tree iliyopo Bagamoyo
mkoani Pwani kufungua mkutano wa nne wa Mtandao wa vyombo vya habari vya
Kijamii nchini (COMNETA) akiwa ameongozana na wenyeji wake Afisa
Mipango Taifa wa Kitengo cha Mawasiliano na Habari na mratibu wa miradi
ya UNESCO , Yusuph Al-Amin (wa pili kulia), Mwenyekiti wa COMNETA ambaye
pia ni Mkurugenzi wa Redio ya Jamii ya Wilayani Karagwe ya FADECO
Bw.Joseph Sekiku (wa pili kushoto) na Makamu Mwenyekiti wa COMNETA
ambaye pia ni Meneja wa Kituo cha Habari na Mawasiliano cha Telecentre
Sengerema FM mkoani Mwanza Bw. Felician Ncheye.
Na.Mwandishi wetu
SHIRIKA
la Umoja wa Mataifa la Elimu, Sayansi na Utamaduni,(UNESCO), limeiomba
Serikali kutambua mchango wa redio za jamii katika maendeleo nchini na
hivyo kufanya nao kazi kwa karibu.
Ombi
hilo limetolewa jana na Afisa Mipango Taifa wa Kitengo cha Mawasiliano
na Habari na mratibu wa miradi ya UNESCO , Yusuph Al-Amin wakati wa
mkutano wa Mtandao wa vyombo vya habari vya Kijamii nchini (Community
Media Network of Tanzania – COMNETA)unaofanyika mjini Bagamoyo.
Akizungumza
kwenye mkutano huo, Al-Amin aliwapongeza COMNETA kwa kufanikiwa
kuanzisha umoja huo ambao awali kulikuwa na vituo viwili tu vilivyokuwa
vikitambuliwa na Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA), huku kwa sasa
vikifikia vituo zaidi ya 27, kwa nchi nzima ikiwemo Tanzania Bara na
Visiwani.
Mgeni rasmi Mkurugenzi wa Idara ya Habari (MAELEZO) Assah Mwambene
akibadilishana mawazo na wenyeji wake kabla ya kufungua mkutano wa nne
wa COMNETA unaoendelea Bagamoyo mkoa wa Pwani.
Akifafanua
zaidi, Al-Amin alisema UNESCO imekuwa ukiisaidia COMNETA kufikia
malengo yake kwa kutambua kuwa radio hizo zinafanya kazi katika jamii na
zina uwezo mkubwa wa kuifikia jamii inayoizunguka.
“Zaidi
ya asilimia 70 ya Watanzania wako vijijini na hawa wanafikiwa kwa
karibu zaidi na radio jamii, kwa kupata taarifa za kina na za haraka”
alisema Al-Amin.
Alitoa
mfano wa Radio ya jamii iliyoko Micheweni, Pemba ambayo uwepo wake
umesaidia sana kuleta mabadiliko ya maendeleo wilayani hapo tofauti na
ilivyokuwa huko nyuma ambapo wilaya hiyo likuwa nyuma sana kimaendeleo.
‘Vipindi
mbalimbali vya kuhamasisha maendeleo vinavyorushwa na redio hii
vimesaidia sana kuhamasisha wananchi na sasa mwamko wa maendeleo umekuwa
mkubwa hapo Micheweni” alisema, Al-Amin.
Mwenyekiti
wa COMNETA ambaye pia ni Mkurugenzi wa Redio ya Jamii ya Wilayani
Karagwe ya FADECO Bw.Joseph Sekiku akizungumza na WanaCOMNETA kabla ya
kumkaribisha mgeni rasmi Mkurugenzi wa Idara ya Habari (MAELEZO) Assah Mwambene.
Aliwashauri
wanachama wa COMNETA, wawe na umoja, mshikamano na kupendana ili
kuepuka migogoro inayoweza kuyumbisha ustawi wa chama. “Tunawaomba sana,
COMNETA, muwe mfano wa kuigwa kwa kuepuka migongano ya wenyewe kwa
wenyewe ikiwamo kugombea madaraka ili kuwa umoja wa mfano kwa katika
tasnia ya vyombo vya habari hapa nchini’.
Kwa
upande wake, mgeni rasmi katika mkutano huo, Mkurugenzi wa Idara ya
Habari (MAELEZO) Assah Mwambene aliupongeza umoja huo na kuwataka
kuendelea kuwa daraja muhimu la kuipasha jamii mambo yote ya msingi bila
kuvunja misingi ya kitaifa ikiwemo kulinda maslahi ya taifa.
“Kwanza
kabisa, niwapongeze, COMNETA kwa kuanzisha umoja wenu huu, na kuwapo
kwangu hapa leo kunanifunza mengi, hivyo kwa yale yote mulioniomba nami,
nitayafikisha kwa wahusika na kuyafanyia kazi” alisema, Mwambene.
Aidha,
akijibu maswali mbali mbali ya wajumbe yaliyokuwa yakitolewa kwenye
mkutano huo, Mwambene aliwahakikishia kuwa Serikali inatambua mchango wa
vyombo vya habari na inatarajia kupeleka muswada wa sheria ya vyombo
vya habari kwenye Bunge lijalo.
“Muswada wa habari upo tayari, tunatarajia utapelekwa Bungeni katika
kikao kijacho mwezi Desemba ili kujadiliwa.Tunaamini Kamati husika ya
Bunge itawakaribisha wadau wa tasnia ya habari ili kutoa mawazo yao
katika muswada huo kabla haujafikishwa bungeni,” alisema.
Mkurugenzi
wa Idara ya Habari (MAELEZO) Assah Mwambene akitoa risala wakati
akifungua mkutano wa siku nne wa COMNETA unaoendelea mjini Bagamoyo mkoa
wa Pwani.
Akidokeza
juu ya yaliyomo ndani ya muswada huo, Mwambene alisema umebainisha wazi
ulazima wa wamiliki wa vyombo vya habari kuwakatia bima za afya na
usalama kazini waajiriwa wao pamoja na suala la maslahi stahiki kwa
waandishi wa habari. Muswada huo pia umependekeza kiwango cha elimu kwa
mwandishi wa habari kiwe shahada ya kwanza.
Kwa
upande wake, Makamu Mwenyekiti wa COMNETA, Bw. Felician Nchewe aliomba
Serikali ivifikirie vyombo vya Jamii nchini, katika kufikia malengo
yake.
Afisa Mipango Taifa wa Kitengo cha Mawasiliano na Habari na mratibu wa
miradi ya UNESCO, Bw.Yusuph Al-Amin akizungumza mbele ya mgeni rasmi Mkurugenzi
wa Idara ya Habari (MAELEZO) wakati wa ufunguzi wa mkutano wa nne wa
WanaCOMNETA uliofunguliwa rasmi jana wilayani Bagamoyo mkoa wa Pwani.
“Kwa
sasa COMNETA, tumefikia malengo mbali mbali, hivyo tunaiomba sana
Serikali ivifikie vyombo hivi vya Jamii, kama ilivyo kwa wenzetu kupitia
TCRA, kuvisaidia vituo vya Tele Centre kufikia malengo yao” alisema
Nchewe.
Kwa
upande wake, Mkufunzi wa radio za Jamii kutoka UNESCO, Mama Rose Hajj
Mwalimu alisema mkutano huo wa COMNETA wa siku nne, ni wa kuweka mifumo
na mikakati bora ya uendashaji wa vituo hivyo na kuweka maazimio ya
kufanyia kazi. Ambapo uliwahusisha Mameneja na Wakurugenzi kutoka radio
za Jamii (Community Radio) zilizopo nchini.
Mkutano huo unaendelea katika hoteli ya New Palm Tree Village, Bagamoyo.
Meneja wa Redio Kahama FM Marco Mipawa akichangia maoni yake juu ya
sheria ya Magereza wakati wa mkutano wa nne wa COMNETA unaohusisha redio
za Jamii nchini uliofadhiliwa na Shirika la UNESCO kupitia mradi wa
DEP.
Afisa Habari wa Kitengo cha Habari cha Umoja wa Mataifa (UNIC) Bi. Usia Nkhoma Ledama akitoa maoni yake katika mkutano huo
Baadhi
ya washiriki wakisikiliza mada mbalimbali zilizokuwa zikitolewa wakati
wa mkutano wa nne wa COMNETA unaoendelea Bagamoyo mkoani Pwani.
Erick Kalunga kutoka Ubalozi wa Uswiss ambao wanadhamini mradi wa SIDA
akizungumzia furaha yao kuona miradi wanayofadhili inapiga hatua na
kuleta maendeleo kwa jamii.
Mwenyekiti wa Tanzania Telecentre Network (TTN) Bw. Hirnoy Barmeda akizungumzia umuhimu wa Telecentre kwa jamii.
Mkurugenzi
wa taasisi isiyo ya kiserikali ya Barmedas na Jamii Foundation Crystal
Kigoni akifafanua kuhusu taasisi yao isiyo ya Kiserikali
inayojishughulisha na mambo ya ustawi wa Jamiikupitia vyombo vya habari
na Teknohama kwa kuibua mambo yanayotokea mitaani kwa jamii inayozunguka
Redio za Jamii.
Washiriki wa mkutano wa nne wa COMNETA unaoendelea wilayani Bagamoyo mkoani Pwani.
Mkutano wa nne wa WanaCOMNETA ukiendelea katika hoteli ya New Palm Tree wilayani Bagamoyo mkoa wa Pwani.
Mratibu
wa Mtandao wa Jinsia na Habari Tawi la Tanzania (GEMSAT) Bi. Gladness
Hemedi Munuo akiongelea usawa wa jinsia katika Uongozi na Utawala kwa
Redio za Jamii.
Mshauri wa UNESCO, Balozi mstaafu Mh. Celestine Liundi akisisitiza umuhimu wa kuhubiri amani kwa redio za Jamii nchini.
Meneja wa mradi wa DEP kutoka UNESCO Courtney Ivins akibadilishana mawazo na Mwenyekiti
wa COMNETA ambaye pia ni Mkurugenzi wa Redio ya Jamii ya Wilayani
Karagwe ya FADECO Bw.Joseph Sekiku kwenye mkutano wa WanaCOMNETA
unaoendelea wilayani Bagamoyo mkoa wa Pwani.
Mkurugenzi
wa Idara ya Habari (MAELEZO) Bw. Assah Mwambene katika picha ya pamoja
na WanaCOMNETA mara baada ya kufungua mkutano wa nne wa COMNETA wilayani
Bagamoyo.
Mkurugenzi wa Idara ya Habari (MAELEZO) Assah Mwambene katika picha ya pamoja na Bodi ya COMNETA.
Mkurugenzi
wa Idara ya Habari (MAELEZO) Assah Mwambene (kulia) akibadilishana
mawazo na Mshauri wa UNESCO, Balozi mstaafu Celestine Liundi (katikati)
pamoja Mkufunzi wa Mafunzo hayo ambaye pia ni Mjumbe ya wadhamini
COMNETA Bw. Gervas Mushiro (kushoto)
Monday, 18 November 2013
THE VOICE OF KATAVI: KATAVI SPORTS BONANZA
THE VOICE OF KATAVI: KATAVI SPORTS BONANZA: by rahim kassonga
Tamasha kubwa la aina yake na la kwanza la michezo limefanyika leo wilayani Mpanda mkoani Katavi kwa kushir...
Tamasha kubwa la aina yake na la kwanza la michezo limefanyika leo wilayani Mpanda mkoani Katavi kwa kushir...
KATAVI SPORTS BONANZA
by rahim kassonga
Tamasha kubwa la aina yake na la kwanza la michezo limefanyika leo wilayani Mpanda mkoani Katavi kwa kushirikisha michezo mbalimbali ikiwemo,mpira wa miguu kwa wanawake,wanaume na watoto,mpira wa pete,mpira wa wavu,riadha ,kukimbia na magunia,kufukuza kuku,mbio za walemavu na kushindana kunywa soda.
Tamasha hilo lililofanyika katika viwanja vya azimio lilianza saa tatu asubuhi na kumalizika saa kumi na mbili jioni ambapo kamanda wa polisi mkoa wa katavi,Dhahiri Kidavashari ndiye alikuwa mgeni rasmi ambapo alitia baraka katika tamasha hilo kwa kupiga penati na kumfunga muhandisi Frank John wa Tanroad.
Katika hotuba yake kamanda Kidavashari alisisitiza kuwa michezo ni afya,michezo ni ajira lakini pia michezo inaleta undugu kwani inawakusanya watu pamoja na kuongeza kuwa kama michezo ikitumika vizuri inapunguza uhalifu.
kikosi cha msakila |
kikosi cha shule ya Uhuru |
timu ya Msakila na Uhuru wakikaguliwa na waamuzi |
Afisa michezo halmashauri ya mji-Revocatus Kalunde akifungua Bonanza |
waamuzi wa mchezo wa ufunguzi, Daudi (kushoto), Ngalla (katikati) na Kaburu (kulia) wakiingia uwanjani tayari kwa mchezo wa ufunguzi |
vijana wa msakila wakisalimiana kabla ya mchezo |
kibatari nishati, the super MC akisherehesha
|
mchezaji wa Msakila akimiliki mpira |
vijana wa Msakila wakimpongeza mwenzao baada ya kufunga goli |
wanafunzi wa Msakila wakishangilia baada ya mpira kwisha na kuibuka washindi |
Ulinzi ulikuwa wa kutosha |
timu ya netiboli ya halmashauri ya wilaya ikifanya mazoezi kabla ya kuanza kwa mchezo huo |
pasha..pasha..pasha |
Timu ya vijana ikipokea maelekezo toka kwa mwalimu wao |
Timu za netiboli zikipokea maelekezo kabla ya kuanza kwa mchezo
KIVUMBI KIMEANZA
huwezi amini hadi mapumziko walikuwa wamefungana 16-16
Mkubwa ni mkubwa, mwishowe Halmashauri ya wilaya waliibuka na ushindi |
SARAKASI
mambo ya sarakasi pia yalikuwepo, ilikuwa noumaaa sanaaaaaaaaaaaaaaa
WATU WENGIIIIIIIIIIIII
watoto kwa wakubwa, wanawake kwa wanaume
KUFUKUZA KUKU
mtu aliondoka na bonge la jogoo, ilikuwa nouma sanaa, weka mbali na watoto
wanaume wakijiandaa kufukuza kuku |
refarii akitoa maelekezo |
kuku anapasha |
HATIMAE JAMAA KAJIPATIA KITOWEO, kiroho safi
BURUDANI KADHAA ZILITO;EWA, mshikamano arts group nao waliwasha moto
RIADHA MITA 400 KINAMAMA ilikuwa sooo,
HATARII SANAAA, jamaa akionesha mautundu kwa kucheza na baiskeli huwezi amini, mshikaji alivyotembelea tairi moja
KWENYE VOLLEYBALL NAKO PALIKUWA HAPATOSHI
veta na katavi walioneshana kazi
WEKA MBALI NA WATOTO, mbio za magunia zilifunika
kazi imeanza |
huyu jamaa nouma sana, achana nae |
soka la wanawake |
Subscribe to:
Posts (Atom)