Thursday, 7 November 2013

WASAMBAZAJI WAAKANDAMIZA WASANII WA FILAMU



WASANII wa filamu nchini bado wanaendelea kupokea  kipato kidogo kutoka kwa wasambazaji wa filamu hali iinayopelekea kudumaza  soko la filamu nchini, huku kupelekea wasanii hao kuwa na kipato cha chini.

Hayo yalibainishwa na msanii wa filamu za maigizo nchini Kulwa Kikumba 'Dude' ambapo aliweka wazi kuwa tasnia hiyo inaonekana kukuwa siku hadi siku ingawa wasanii hao bado wanaonekana kuwa masikini kutokana na kipato wanachopata.

Aliweka wazi kuwa mfumo mbaya wa mauzo ya filamu nchini ndio chanzo pekee kinachodidimiza kazi za wasanii hao huku baadhi yao wakikosa soko la filamu hali inayochangia baadhi yao kupotea katika tasnia hiyo.

Alibainisha kuwa wapo baadhi ya wasanii wanaendelea kunufaika kutokana na kazi zao lakini walio wengi wanaendelea kudidimia hadi hapo mfumo wa usambazaji utakapobadilika ndipo ahueni itakapopatikana kwa wasanii wengine.

" Sisi wasanii tumekosa ushirikiano kutokana na baadhi ya wasanii kunufaika na kazi hizo huku wengi kunyonywa na wasambazaji , ila kama tungeweza kushirikiana wasanii wote tukawa tunauza filamu kwa bei zinazolingana na ubora na ghrama ya filamu tungefika mbali" alibainisha Dude

LULU AKANUSHA KUCHUMBIWA


MSANII wa filamu nchini Elizabeth Michael 'Lulu' akanusha taalifa za kuzushiwa za kuchumbiwa na kukalibia kuolewa muda mchache zilizoandikwa na moja ya chombo cha habari jijini.

Lulu amekanusha taarifa hizo ambazo zimeandikwa na gazeti moja la udaku kuwa anatarajia kuolewa hivi karibuni  huku wazazi wake wakiwa tayari wameshapokea mahali.

Akizungumza na katika mahojiano , muigizaji huo ameweka wazi kuwa ameshangazwa na habari hizo ambapo baadhi ya magazeti mengi ya udaku ndiyo yamekuwa yakimwandika kile wanachojisikia.

Aliweka wazi kuwa hajachumbiwa na mwanaume yoyote yule na siku ikitokea amechumbiwa basi kila mtu atajua kwani halitakuwa jambo la kificho tena.

"Sijajua wao wameipata wapi hiyo habari kutoka chanzo kipi, kila kukicha kumekuwa na habari mtu akijisikia kuandika tu anaandika bila hata ya kufikiria leo wameandika nimechumbiwa, kesho wataandika nimeolewa, tena wataandika nimeachwa, kila watakalo lihisi kuandika wanaandika" alieleza Lulu.

Aliweka wazi kuwa kuchumbiwa kuolewa ni vitu ambavyo vimeumbiwa binadamu, vipo kama ukiwa na mpango wa mwenyezi mungu nitachumbiwa.

BAADA YA KUTOKA LUPANGO..... MASOGANGE APIGA ZA NUSU UTUPU

 SIKU chache baada ya kutoka lupango kwa msala wa madawa ya kulevya, ‘video queen grade one’ Bongo, Agnes Gerald ‘Masogange’ ametupia picha za utupu mtandaoni.
Agnes Gerald ‘Masogange’ katika pozi.
Masogange na mwenzake, Melisa Edward walikamatwa nchini Afrika Kusini Julai 5, mwaka huu wakidhaniwa kuwa na madawa haramu ya kulevya na baadaye mahakama kuu ya nchini humo ikawaachia kwa dhamana ikidai unga waliokutwa nao si madawa ya kulevya bali ni mali ghafi zijulikanazo kama Methamphetamine. Baada ya kuachiwa huru, Masogange anayesifika kwa kuwa na figa matata, alitupia picha hizo katika mtandao wa Instagram akiwa amevalia sidiria na nguo ya ndani pekee hali iliyowafanya wafuasi wa mtandao huo wamshangae huku wengi wakimlaumu kuwa alichokifanya hakifanani na maadili ya Mtanzania.
 
Video queen grade one Bongo, Agnes Gerald ‘Masogange’.
“Sasa huu upuuzi gani unatuwekea humu, kwani kila kitu unachofanya ni lazima sisi tuone? Hivi kwa nini mastaa wa Bongo wanapenda kujirahisi kiasi hiki?” alihoji mmoja wa wafuasi wa mtandao huo. Pamoja na wadau wengi kuonesha kukerwa na picha hizo, Masogange hakujali, aliwajibu kuwa kama hawataki kuziona picha hizo wamuondoe kwenye listi ya marafiki mtandaoni humo kwani siyo lazima. “Hii ni akaunti yangu, nina uhuru wa kuweka picha za aina yoyote. Kama mtu anaona nimemkera basi ‘aniblok’ maana hapa nimevaa mavazi ya kuogelea sasa mlitaka nivae pensi niogelee nayo? Simuogopi mtu…,” aliandika Masogange.

HII NI LAANA...!! MISS UTALII NA MSANII WA BONGO MOVIE WANASWA WAKISAGANA LIVE...CHEKI PICHA HAPA

Fathiya" Mrembo wa Facebook" na Suzi Magoti mshiriki kwenye filamua Ngema akimvua nguo mrembo huyo kuanza tendo.
Katika hali isiyokuwa ya kawaida na kusikitisha matendo ya aibu kwa wasanii wetu yameendelea kushika kasi kama moto wa tipa baada ya blog hii makini kunasa picha nyingine za wasanii hawa wakusagana live bila chenga.
  Tumefanikiwa kupata picha hizi ambazo ni baadhi tu licha ya kwamba kuna CD nzima ya picha hizo tunazo kabatini na kuna taarifa kuwa pia kuna CD ya Viedo kabisa ambayo ndani yake kuna mambo ya kutisha.
tunakuahaidi siku mbili hizi itakuletea tuki hilo moja kwa moja kupitia blog hii pamoja na kuzimwaga picha hizo zaidi. Habari zaidi zilisema kuwa wasanii hao ambao mmoja alikuwa mshiriki Miss Utalii mwaka huu na mwingine ni staa kwenye filamu ya msanii Manaiki Sanga ambayo bado haijatoka na ndiye kwenye video hiyo anaonekana fundi wa kumbonyeza mwenzake.
Bofya hapo chini kuangalia picha hizo...




JINI KABULA ANYWA SUMU KISA PENZI LA CHUZ...

  Nyota wa Tamthiliya ya Jumba la Dhahabu, Miriam Nyafulwa Jolwa ‘Jini Kabula’ aliwahi kunywa sumu ambayo haikujulikana mara moja huku chanzo kikiwa ni ugomvi wa kimapenzi na mzazi mwenzake, Tuesday Kihangala ‘Chuz’. Akizungumza na mwandishi wetu mwanzoni mwa wiki hii, Chuz alisema tukio hilo lilijiri mwaka 2011 nyumbani kwake, Makongo jijini Dar na kwamba  siku hiyo hataisahau kutokana na jinsi alivyochanganyikiwa na hali ilivyokuwa. Aidha, Chuz alisema walikuwa na ugomvi mdogo tu wa kimapenzi jambo ambalo alitarajia kuwa lingeisha kwa amani. Lakini tofauti na matarajio yake, kila dakika iliyokuwa ikiondoka Kabula alizidi kupandisha mori kama si maruhani. Alisema muda mfupi baadaye, Jini Kabula  alivunja vioo vya gari lake kwa kutumia mawe kitendo kilichompa sababu Chuz kumpeleka polisi (hakutaja jina la kituo). Hata hivyo, Chuz aliendelea kushusha ‘vesi’ kuwa baada ya siku mbili, Jini Kabula alitolewa kwa dhamana huku yeye  akidhani kuwa yameisha lakini Kabula aliendeleza ‘libeneke’ ambapo alifika nyumbani  kwake na kujifungia ndani kisha akanywa dawa ambazo zilidaiwa kuwa ni sumu kali. “Nilipokuta mlango umefungwa nilianza kubisha hodi bila mafanikio. Niliamua kwenda polisi, wakaja na kuvunja mlango na kumkuta akiwa amelala chali huku akiwa anatokwa na povu jingi kinywani,” alisema Chuz.
Baadaye walimpa huduma ya kwanza kabla ya kumkimbiza hospitali (jina tunalo) kwa matibabu zaidi. Hata hivyo, baada ya kutibiwa, Chuz aliomba yaishe kwa amani.
“Kaka sitaisahau siku hiyo, ilikuwa  mbaya sana kwangu. Jini Kabula alikuwa kabadilika kabisa, alidhamiria kujiua kweli. “Nashukuru hamkupata habari hiyo lakini ilinichanganya sana,” alisema Chuz.
Mwandishi alimtafuta Jini Kabula kwa njia ya simu ili kuthibitisha juu ya habari hizo ambapo baada ya kusomewa madai hayo alianza kwa kucheka na kujibu:
“Duh! Wewe ni kiboko, umezipata wapi hizo habari? Lakini sipendi kuzungumzia mambo ya zamani, muulize vizuri aliyekwambia.”

HUU NDO UJANJA WA DIAMOND NA UZEMBE WA ALI KIBA ..

Hata kama sio shabiki wa diamond ila kuna kitu lazima uwe kinakuvutia kutoka kwake.Unaweza kujitahidi kumchukia labda kutokana na skendo zake za nje ya muziki wake ila ukirudi kwenye muziki wake nadhani anastahili kuwa pale alipo.
Kuanzia muonekane wake mpaka anavyoweza kuji-brand kimataifa na anavyojua kucheza na akili za mashabiki.

Wasanii wengi wa bongo flava wana tabia ya kurithika kwa mafanikio yao ila Diamond toka atoke na Kamwambie mwaka 2009 mpaka 2013 amezidi kwenda juu bila kuonyesha kusuasua wala kutetereka.
Angalia video ya number 1.Wimbo unaweza sema ni wa kawaida kabisa ukilinganisha na mbagala, kamwambie au nitarejea ila akili ya kwenda kufanya video cape town,south africa kumeifanya nyimbo iwe number 1 kama jina lake lilivyo.

Ushawahi kujiuliza Ali kiba yupo wapi pamoja na kuwa kila mtu anajua ni mkali kuliko diamond?Ali kiba toka atoe my everything mwisho wa mwaka jana amepotea hata video ajatoa.Tukaja kumuona kwenye kidela na Abdu kiba bila kurefusha maneno Ali anashindwa kuufanya mziki wake kama mashabiki wake wanavyotarajia labda pengine angekuwa anafukuzana na diamond ila matokeo yake vijana wake kama Rich mavoko na Dimpoz ndio wapo nyuma ya Diamond huku Ali akibaki msanii mkali ambae ameshindwa kuendelea kutuonyesha ukali wake sijui anawaza nini!

Ushawahi kujiuliza kama ule wimbo wa airtel hands across the world waliopiga wakina r.kelly,fall ipupa,2 face kama nafac ile angeipata diamond leo angekuwa wapi?
Diamond leo anatuletea remix ya number 1 f.t Davido kila mtu anaisubiri kwa hamu ila Ali alishindwa hata kutuletea remix ya Dushelele f.t Fally ipupa pamoja kukaa nae wiki nzima wakifanya wimbo pamoja.
Diamond ni mjanja anaejua biashara ya mziki ilivyo labda pengine ni management yake inayomsimamia.Diamond kaweza kuubadilia mziki wetu kwa kiasi chake leo ndio msanii anaelipwa pesa nyingi kwa show.

Nampenda ali kiba,naipenda sauti yake,anajua mziki kuliko Diamond ila Ali ameshindwa kubadilika na kukubali soko la mziki linataka nini.

Amka Ali huyu Diamond hakuwezi ila usipokuwa makini utajikuta nyuma ya rich,barnaba,dimpoz na ben pol maana mziki sio kuimba peke yake mziki ni biashara pia

Monday, 4 November 2013

Kesi dhidi ya Morsi kuanza leo Misri

by rahim kassonga (La Captain)

Wameshitakiwa kwa kosa la kuchochea mauaji ya waandamanaji wakati wa vurugu za kisiasa nje ya ikulu ya Rais mwezi Disemba mwaka jana.
Vikosi vya usalama vimedhibiti hali ya usalama baada ya wafuasi wa Morsi kuitishia kufanya maandamano makubwa.
Morsi aliondolewa uongozini kwa nguvu za jeshi mwezi Julai baada ya maandamano ya kila mara kufanyika kupinga utawala wake.
Rais aliyeng’olewa mamlakani nchini Misri, Mohammed Morsi anatarajiwa kufikishwa mahakamani leo pamoja na vigogo wengine 14 wa chama cha Muslim Brotherhood, wakati kesi yake itakapoanza kusikilizwa mjini Cairo.
Ingawa alishinda urais kwa njia ya demokrasia, wakati wa uongozi wake wa zaidi ya mwaka mmoja, Morsi hakuelewana sana na taasisi nyingi za serikali.
Baada ya kupinduliwa na jeshi, maandamano yalifanyika kila kulipokucha mjini Cairo na makubwa zaidi yalikuwa ya wafuasi wake kukesha karibu na kasri la rais wakitaka Morsi aachiliwe.
Polisi walaisababisha mamia ya vifo vya wafuasi hao walipovunja maandamano yao kwa nguvu.
Serikali ya muda pia imekuwa ikiwasawa na kuwakamata wanachama wa Muslim Brotherhood, chama chake Morsi.
Serikali pia imeharamisha vyama vyote vya kisiasa huku ikiwakamata mamia ya viongozi wa mashirika hayo.
Wafuasi wake wanasema kuwa alipinduliwa na jeshi na sasa anakabiliwa na kesi ya kisiasa.
Mashirika ya kutetea haki za binadamu, yameituhumu maafisa wa usalama kwa kufanya kazi yao bila uwajibikaji.


Sunday, 3 November 2013

Mourinho kimyaa abamizwa na Newcastle 2 - 0


Newcastle wakiwa katika uwanja wao nyumbani wa St. James Park jumamosi hii wameisambaratisha Chelsea kwa jumla ya magoli 2 -0 katika mechi ya ligi kuu ya England.

Newcastle walianza kusherekea ushindi baada ya kupata goli la kuongoza katika dakika ya 67 lililofungwa kwa kichwa cha kuchumpa na Yoan Gouffran.
Wakicheza kwa kujiamini Loic Remmy wa Newcastle alizidi kupigilia mwiba mkali kwa mashabiki wa Chelsea pale alipopachika goli la pili katika dakika 89.
Kwa matokeo hayo Newcastle sasa itakuwa na point 14 huku na Chelsea ikibakiwa na pointi 20.

Tuesday, 29 October 2013

RAY C AWA BONDIA,AMTWANGA HUYU DADA WA BONGO MOVIE.

BY ZANGII ZE ICON


KATIKA hali ya kushangaza, siku chache baada ya kuripotiwa kupona na kuacha matumizi ya madawa ya kulevya, mwanamuziki Rehema Chalamila ‘Ray C’ anadaiwa kugeuka mwanamasumbwi na kumpa kipigo mwigizaji Nuru Nassoro ‘Nora’,.



Kwa mujibu wa shuhuda wetu, tukio hilo lilijiri wiki iliyopita ndani ya studio moja ya kurekodia muziki iliyopo Kinondoni, Dar ambapo wawili hao walikutana walipokwenda kurekodi ngoma zao.
Ilidaiwa kuwa akiwa studio hapo, Nora alikutana na Ray C ambaye pia alizama mahali hapo bila mawasiliano na prodyuza anayemtengenezea ngoma mpya.


Chanzo hicho kilipasha kuwa baada ya Ray C kuingia studio hapo alimkuta prodyuza huyo akiandaa ngoma ya Nora ambapo alihoji kilichompeleka mwigizaji huyo mahali hapo.

Ilidaiwa kuwa prodyuza huyo ambaye jina halikupatikana alimwambia Ray C kuwa Nora alifika kurekodi wimbo wake.

Ilisemekana kuwa Ray C hakuridhishwa na majibu hayo, akaomba asikilizishwe ngoma hiyo ya Nora lakini baada ya kusikiliza ilidaiwa kwamba Ray C aliiponda mbele ya Nora, jambo ambalo mwigizaji huyo hakufurahishwa nalo.
Ilidaiwa kuwa Nora alipandwa hasira na kujikuta akimjibu mbovu Ray C.

Habari ziliendelea kutiririka kuwa siku hiyo walimalizana kwa kusonyana na siku iliyofuta walikutana tena studio hapo ambapo Ray C alidaiwa kutinga akiwa ‘masanga’.
Ilisemekana kuwa alipomuona Nora alianza kumpa vijembe, jambo lililosababisha Nora kushikwa hasira ndipo wakavaana na kuzichapa.

Hata hivyo, ilidaiwa kuwa Ray C ndiye aliyeibuka bingwa wa ndondi hizo kwa kumtwanga Nora hadi kumvimbisha jicho kabla ya maprodyuza na watu wengine kufanya kazi ya ziada kuwaamulia.
Ilisemekana kuwa baadaye Ray C alitolewa nje ndipo akahamishia hasira kwenye gari la Nora aina ya Toyota Vitz kisha akalivunja kioo na kutambaa zake.

Baada ya kupenyezewa ‘niuz’ hizo tulimtafuta Nora ambaye alikiri kutokea kwa sekeseke hilo huku akibainisha namna alivyoumizwa jicho lake na kuvunjiwa kioo cha pembeni cha gari lake.
Aliongeza kuwa siku hiyo alipoteza pochi wakati wa ugovi huo.

“Ray C alinikuta studio nikifanya wimbo, kilichonishangaza baada ya kuniona tu alibadilika ghafla.
“Nilijua angenishauri kwa kuwa ndiyo ninaanza gemu kumbe mwenzangu alifikiria vingine,” alisema Nora na kuongeza:
“Mbali na kuniumiza jicho lakini alinifanyia mambo ya ajabu sana, kama kusingekuwa na watu wa kutuamulia basi chochote kingetokea.

“Sikwenda kuripoti polisi. Niliamua kusamehe kwa sababu kuna watu walinisihi niachane naye kwa sababu bado kuna mambo yanamwendesha. 

Kwa upande wake Ray C alitafutwa kwa kila njia kupitia simu ya mkononi na kumvizia studio lakini hakupatikana hivyo juhudi za kumpata zinaendelea.


Monday, 28 October 2013

VIWANJA MISUNKUMILO

by rahim kassonga (La Captain)


Wananchi wa Kata ya Misunkumilo Wilaya ya Mpanda Mkoani Katavi wameulalamikia Uongozi wa Kata yao kwa kushindwa kufuatilia viwanja walivyo takiwa kugawiwa na Idara ya Ardhi.

Wananchi hao wamesema kuwa Augosti mwaka huu Idara ya Ardhi ilifanya tathmini ya  viwanja kwa ajili ya kupanga mpangilio maalumu wa kuacha nafasi ya barabara za Mitaa lakini mpaka sasa hawajarudi kwajili ya kugawa viwanja hivyo.

Aidha wananchi hao wamesema kuwa kutokana na kufuatilia na kukaa kwa muda mrefu baadhi ya wananchi wameanza kujenga ili waweze kuishi katika nyumba zao kwasababu wamechoka kukaa kwenye nyumba za kupanga.

Hata hivyo Mtendaji wa Kata hiyo January Kayungilo amesema kuwa Idara ya Ardhi imeshafanya tathmini, hiyo amewaomba wananchi  kusubiri shughuli ya kuanza kugawa viwanja hivyo kwaajili ya kuvilipia ili waweze kujenga nyumba zao pia amewataka wananchi hao kuwa wavumilivu katika suala hilo.

EDITOR:TIDA SAIDEA

tutatumia umeme wa gesi asilia na makaa ya mawe;Prof.Sospeter Muhongo

by rahim kassonga (La Captain)



Waziri wa Nishati na madini Pr.Sospeter Muhongo  amesema Serikali imedhamiria kutumia gesi asili na makaa ya mawe pamoja na vyanzo vingine vya kuzalisha umeme ili kuwawezesha wananchi zaidi ya asilimia 30 kutumia Nishati hiyo ya umeme ifikapo mwaka 2015.

Akiwa Mjini Mpanda katika siku yake ya kwanza ya kukagua utekelezaji wa mradi wa umeme katika maeneo ya vijijini kwa kiwango cha zaidi ya asilimia 10 toka asilimia chini ya 7 za sasa ambapo Pr.Muhongo amesema lengo la wananchi kukabiliana na tatizo la umaskini ifikapo mwaka 2025 haliwezi kukamilika ikiwa Nishati ya umeme haitazalishwa kwa wingi.

Akizungumza na Viongozi wa Serikali wa Mkoa wa Katavi Pr.Muhongo amesema kuwa kwa kutambua umuhimu wa Nishati ya umeme kwa maendeleo ya Taifa na ukuzaji wa uchumi kwa mtu mmoja mmoja Serikali imeweka nia ya kweli kuhakikisha uzalishaji wa Nishati hii muhimu unaongezeka.


Taarifa ya Mkuu wa Mkoa wa Katavi Mh.Rajabu Lutengwe imeeleza mikakati ya Serikali Mkoani humu kushirikiana na wakala wa mradi wa kusambaza umeme vijijini ambapo kiasi cha shilingi bilioni 10 zitatumika kusambaza umeme katika vijiji 14.

Mazishi ya baba mzazi wa Wema Sepetu ni jumatano hii ....Rais Kikwete na mama Salma watoa mkono wa pole

 BY ZANGII ZE ICON



Balozi Isaac Abraham Sepetu ambaye ni baba yake mzazi na Wema Sepetu, anatarajiwa kuzikwa Jumatano hii visiwani Zanzibar. Mwili wa marehemu utasafirishwa kesho asubuhi kuelekea visiwani humo.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Jakaya Kikwete na mkewe Mama Salma, leo wameungana na watu wengi wa karibu wa familia ya Wema kuwapa pole wafiwa akiwemo mama yake, Bi. Mariam Sepetu. 
 
Balozi Sepetu alifariki jana baada ya kuugua kwa muda mrefu maradhi ya kisukari na kiharusi na alikuwa amelazwa kwenye hospitali ya TMJ jijini Dar es Salaam.

  
Balozi Sepetu aliwahi kuwa Naibu Waziri wa Mambo ya Nchi za Nje mnamo miaka ya 1970 wakati wa utawala wa awamu ya kwanza chini ya Mwalimu Julius KambaragE Nyerere. 
 
Vilevile, aliwahi kuwa balozi nchini Urusi tangu mwaka 1982 wakati wa utawala huohuo wa Nyerere. Hadi anafariki, Mzee Sepetu alikuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya Mamlaka ya Uwekezaji wa Vitega Uchumi Zanzibar.

Anakubalika Kwa Sauti Na Umbo Lake, Rihanna Ndani Ya Vazi La Kuogelea.Tazama Picha zaidi ya nne hapa!!



 



JINI KABULA AAMUA "KUOKOKA"...ASHINDA NA BIBLIA

MWANADADA anayefanya vizuri kunako gemu la filamu Bongo, Miriam Jolwa ‘Jini Kabula’ ameamua kubadili mfumo wa maisha kwa kusoma Biblia kila wakati.
 
Miriam Jolwa ‘Jini Kabula’.
Paparazi wetu alimnasa Jini Kabula nyumbani kwake Sinza akiwa anasoma Biblia na alipoulizwa kulikoni amekuwa mtu wa kushinda nyumbani na siyo kupiga misele kama alivyozoeleka, alitiririka:
“Nimeamua kubadili mfumo wa maisha yangu niliyokuwa nikiishi zamani ya kuendekeza starehe, nimemrudia Mungu wangu na mara nyingi nashinda ndani kwangu nikisoma Biblia kwa sababu Mungu ndiye rafiki wa kweli,” alisema Jini Kabula.

Ney Wa Mitego Aswekwa Sero Baada Kuvaa Sare Za Polisi.


by zangii ze icon 
Rapper Ney Wa Mitego ameniambia kuwa hii picha hapo juu tukio hilo limetokea Jana wakati wana shoot video ya wimbo wake Unaofanya vizuri kwa sasa kwenye radio stations ' Salam Zao'.


Ney Wa Mitego Amesema ' Nikweli nilitupwa sero jana baada ya raia wasio julikana kuleta fujo eneo la kazi yangu  kwasababu kulikuwa na waigizaji waliokuwa na sare za polisi. Watu hao sijuani nao na walijitambulisha kama askari na kutaka kujua kwanini natumia sare za polisi kwenye video yangu bila kibali. hicho ndio kitu kilichopelekea nikapelekwa polisi.

Mitego ameendela kusema kuwa baada ya kuka sero kwa dakika kama 15 mkuu wa kituo alikuja na kusikiliza tatizo hilo na ndio aliachiwa huru baada ya kutoa maelezo kuhusu tukio hilo na sare hizo kuonekana uraiani.

Ney aliwekwa sero Kwenye kituo cha polisi Urafiki kilichopo Manzese na wiki ijayo video hii itaonekana kwenye vituo vya televison Tanzania.


HIKI NDICHO KINACHOENDELEA KWENYE MSIBA YA BABA MZAZI WA WEMA SEPETU HUKO SINZA JIJINI DAR


by zangii ze icon

Wema Sepetu akiwa katika hali ya majonzi baada ya kufiwa na baba yake mzazi




Mama mzazi wa Wema akiwa na simanzi baada ya kuondokewa na mumewe mzee Sepetu.
  

Kajala Masanja (kushoto), Wema Sepetu (katikati) na Zamaradi Mketema (kulia) wakiwa katika hali ya majonzi nyumbani kwao Wema Sepetu, Sinza - Mori jijini Dar.



Kajala Masanja (kushoto) na Wema Sepetu (katikati) wakiangua vilio. Kulia Zamaradi akijaribu kumtuliza Wema.

Ndugu wa karibu wa marehemu akiwa na simanzi nzito
STAA wa sinema za Kibongo na Miss Tanzania 2006 Wema Isaac Sepetu, bado yuko kwenye wakati mgumu baada ya leo asubuhi kupatwa na msiba mkubwa wa kuondokewa na baba yake mzazi Balozi Isaac Abraham Sepetu aliyefariki asubuhi ya leo.
Kwa sasa kuna watu wengi wamefika kumjulia hali maeneo ya Sinza, Mori jijini Dar, rafiki yake wa karibu Kajala Masanja na Zamaradi Mketema wapo bega kwa bega kuwa naye karibu na vilio vimetawala kila kona ya familia ya marehemu Balozi Sepetu.
Bado haijafahamika mazishi yanafanyika lini maana wanasubuliwa watoto wa Marehemu Tunnu Sepetu na Sunna Sepetu ambao wanaishi nchini Marekani, lakini kuna tetesi kuwa huenda mazishi hayo yakafanyika siku ya Ijumaa.
Mama mzazi wa Wema bado yuko kwenye hali ya huzuni baada ya kufiwa na mume wake ambaye amedumu nae kwa miaka mingi kabla ya kupatwa na mauti asubuhi ya leo katika hospitali ya TMJ jijini Dar. Mpaka mauti yanamfika, marehemu alikuwa akisumbuliwa na kisukari pamoja na kiharusi.

RAIS AFRICA MASHARIKI ATATEKWA NA CLUB KULIPULIWA.


by ZANGII ZE ICON
Yule Mchungaji Maarufu kutoka Nigeria Ambae hutabiri mambo mbalimbali na kweli yakatokea  TB Joshua leo ametoa utabiri mpya ambao unahusisha Africa Mashariki.

...ameonyeshwa rais mmoja Africa Mashariki atatekwa na ameonyeshwa watu wakiwa club wanacheza then wanalipukiwa na nchi iyo ni jirani na Kenya, Angalizo, amesema siyo kenya tena,je itakuwa nchi gani? 

Misa ya jana jumapili ndo kasema, na amesema ataendelea kuomba ili jumatano na alhamisi ijayo aonyeshwe ni rais gani na nchi gani.

BABA MZAZI WA LOVENESS DIVA WA CLOUDS AULA TFF SASA NDIO MRITHI WA TENGA




Baada ya uchaguzi uliofanyika kwenye ukumbi wa NSSF Water front kumpata Rais mpya wa TFF kati ya Athumani Nyamlani na Jamal Malinzi, hatimaye TFF imepata Rais mpya ambaye ni Jamal Malinzi.
Mashuhuda waliokuwepo hapo ukumbini wanasema kwamba mpinzani wa Jamal Malinzi alitoka kabla ya utaratibu mzima wa uchaguzi kuisha. Baada ya matokeo kutangwaza Jamal Malinzi alimzidi kura Athumani Nyamlani na hatimaye kupata nafasi ya kumrithi Leodigar  Tenda.

Kama ulikuwa hujui ni kwamba  Rais huyu wa TFF Jamal Malinzi ndiyo baba wa Diva Loveness wa Ala za Roho ya Clouds FM

Diamond kuja na video ya 'Number One Remix'


Diamond amefunguka kuhusu kuwepo kwa video hiyo kupitia Instagram, ambapo ameonesha pia nia ya kuwaalika watu ambao wanapenda kuwa sehemu ya video hiyo, ‘Do you wanna be a part ov it..? Aliuliza Diamond.
Kwa maelezo ya Diamond aliyoyaweka jumamosi kwenye Instagram, video hiyo ilitakiwa kufanyika jana jumapili, lakini hakuna taarifa za kufanyika video hiyo hapo jana, huenda video hiyo ikafanyika leo.
C.E.O wa Wasafi, aliweka picha inayoonesha yuko studio na 'Skelewu hit maker' Davido wakiipika remix ya Number One.
"[ @ ] diamondplatnumz I said NGOLOLO Dance, and he said Nah man! SKELEWU Dance... then we decided to put it in a song....and show each other what we gat, we are on tommorow for the new Video #NumberOneRemix @Diamondplatnumz ft @lifeofdavido .. Do you wanna be a part ov it...?" Aliandika Diamond.

Saturday, 26 October 2013

Ofisi ,usafiri,nyumba za wafanyakazi vyazorotesha huduma za elimu

by rahim kassonga (La Captain)


KATAVI
Chama cha walimu (CWT) Wilaya ya Nsimbo Mkoani Katavi  kimetoa changamoto wanazo kabiliana nazo na malengo ambayo wanatarajia kufanya ili kuimarisha chama hicho.

Akiongea na Mpanda Fm Mwenyekiti wa chama hicho Mwl. Kenedi Simsokwe amesema kuwa mazingira ya uendeshaji ni magumu kwakutokuwa na Ofisi ya chama,usafiri,nyumba za wafanyakazi na baadhi ya wanachama kuto kufikisha marejesho shuleni.

Aidha Mwenyekiti huyo ameongeza kuwa  malengo ambayo wanayo ni kuongeza huduma zaidi kwa wanachama kwa kuwatembelea mara kwa mara na kujenga ofisi ya chama ili kuweza kufanya kazi kwa ufasaha.

Hata hivyo Simsokwe amesema kuwa anaiomba serikali iwatambue na kuwathamini walimu kwa kuwaongezea posho kama inavyo fanya kwa watumishi wengine wa umma sambamba na kuboresha mazingira ya kazi kwa kufanya hivyo watakuwa wameinua kiwango cha elimu Mkoani hapa . 
SOURCE:DAWATI
EDITOR:IRENE TEMU