Waziri wa Nishati na madini Pr.Sospeter Muhongo amesema
Serikali imedhamiria kutumia gesi asili na makaa ya mawe pamoja na vyanzo
vingine vya kuzalisha umeme ili kuwawezesha wananchi zaidi ya asilimia 30
kutumia Nishati hiyo ya umeme ifikapo mwaka 2015.
Akizungumza na Viongozi wa Serikali wa Mkoa wa Katavi Pr.Muhongo amesema kuwa kwa kutambua
umuhimu wa Nishati ya umeme kwa maendeleo ya Taifa na ukuzaji wa uchumi kwa mtu
mmoja mmoja Serikali imeweka nia ya kweli kuhakikisha uzalishaji wa Nishati hii
muhimu unaongezeka.
Taarifa ya Mkuu wa Mkoa wa Katavi Mh.Rajabu Lutengwe imeeleza mikakati ya Serikali Mkoani humu
kushirikiana na wakala wa mradi wa kusambaza umeme vijijini ambapo kiasi cha
shilingi bilioni 10 zitatumika kusambaza umeme katika vijiji 14.
No comments:
Post a Comment