Wananchi wa Kata ya Misunkumilo Wilaya ya Mpanda Mkoani Katavi
wameulalamikia Uongozi wa Kata yao kwa kushindwa kufuatilia viwanja walivyo
takiwa kugawiwa na Idara ya Ardhi.
Wananchi hao wamesema kuwa Augosti
mwaka huu Idara ya Ardhi ilifanya tathmini ya
viwanja kwa ajili ya kupanga mpangilio maalumu wa kuacha nafasi ya
barabara za Mitaa lakini mpaka sasa hawajarudi kwajili ya kugawa viwanja hivyo.
Aidha wananchi hao wamesema kuwa kutokana na kufuatilia na
kukaa kwa muda mrefu baadhi ya wananchi wameanza kujenga ili waweze kuishi
katika nyumba zao kwasababu wamechoka kukaa kwenye nyumba za kupanga.
Hata hivyo Mtendaji wa Kata hiyo January Kayungilo amesema kuwa Idara ya Ardhi imeshafanya tathmini, hiyo
amewaomba wananchi kusubiri shughuli ya
kuanza kugawa viwanja hivyo kwaajili ya kuvilipia ili waweze kujenga nyumba zao
pia amewataka wananchi hao kuwa wavumilivu katika suala hilo.
EDITOR:TIDA SAIDEA
No comments:
Post a Comment