KATAVI
Chama cha walimu (CWT) Wilaya ya Nsimbo Mkoani Katavi kimetoa changamoto wanazo kabiliana nazo na
malengo ambayo wanatarajia kufanya ili kuimarisha chama hicho.
Akiongea na Mpanda Fm Mwenyekiti wa chama hicho Mwl. Kenedi Simsokwe amesema kuwa mazingira
ya uendeshaji ni magumu kwakutokuwa na Ofisi ya chama,usafiri,nyumba za
wafanyakazi na baadhi ya wanachama kuto kufikisha marejesho shuleni.
Aidha Mwenyekiti huyo ameongeza kuwa malengo ambayo wanayo ni kuongeza huduma
zaidi kwa wanachama kwa kuwatembelea mara kwa mara na kujenga ofisi ya chama
ili kuweza kufanya kazi kwa ufasaha.
Hata hivyo Simsokwe
amesema kuwa anaiomba serikali iwatambue na kuwathamini walimu kwa kuwaongezea
posho kama inavyo fanya kwa watumishi wengine wa umma sambamba na kuboresha
mazingira ya kazi kwa kufanya hivyo watakuwa wameinua kiwango cha elimu Mkoani
hapa .
SOURCE:DAWATI
EDITOR:IRENE TEMU
No comments:
Post a Comment