Sunday, 26 January 2014

JUAN MATA: NI RASMI, NI MCHEZAJI MANCHESTER UNITED

KUTAMBULISHWA RASMI JUMATATU JIONI!!

MOYES_n_MATA-1Juan Mata amekamilisha Uhamisho wa Dau la Pauni Milioni 37.1 kutoka Chelsea kwenda Manchester United.
Jana Mata alipimwa Afya yake huko Manchester na kusaini Mkataba unaoaminika kuwa unamalizika Juni 2018.
Mata, Miaka 25, anatarajiwa kucheza Mechi yake ya kwanza hapo Jumanne Uwanjani Old Trafford na Cardiff City kwenye Mechi ya Ligi Kuu England.
Akiongea baada ya kusaini Mkataba, Mata alisema: “Umefika wakati wa changamoto nyingine. Nimefurahi mno kuwa sehemu ya awamu nyingine ya historia ya Klabu hii.”
Aliongeza: “Chelsea ni Klabu kubwa na nia Marafiki wengi kule lakini huwezi kuikataa nafasi ya kujiunga na Manchester United. Ninatarajia kumsaidia Meneja na Timu kupata mafanikio zaidi katika Miaka ijayo!”
Mata anakuwa Mchezaji wa pili kusainiwa na Meneja David Moyes baada kumsaini Marouane Fellaini kutoka Everton  Mwezi Septemba kwa Dau la Pauni Milioni 27.5.
Pia, kwa kumsaini Mata, Man United imevunja Rekodi yao ya kusaini Mchezaji kwa Bei ya juu ambayo iliwekwa Mwaka 2008 walipomsaini Dimitar Berbatov kwa Pauni Milioni 30.
Mata atatambulishwa rasmi kama Mchezaji mpya wa Man United Jumatatu Saa 10 na Nusu Jioni, Saa za Tanzania.

WASIFU:
Jina: Juan Manuel Mata GarcĂ­a
Kuzaliwa: 28 Aprili 1988 (Miaka 25)
Namba ya Jezi: 10

MH. KIKWEMBE ATOA VIFAA VYA MAABARA SEKONDARI YA MWANGAZA

by rahim kassonga (La Captain

Katika jitihada za kukuza na kuendeleza elimu hususani katika masomo ya sayansi, Mbunge wa viti maalum Mkoa wa Katavi kwa tiketi ya CCM mh. Pudenciana Kikwembe ameipatia shule ya sekondari Mwangaza vifaa vya maabara vyenye thamani zaidi ya milioni mbili zikiwemo kemikali


vifaa hivyo vilikabithiwa ijumaa mchana shuleni mwangaza mbele ya mwenyekiti wa Halmashauri ya mji Mpanda mh Enock Gwambasa, Afisa elimu mji, mkuu wa shule mh. Simon Rubange, walimu na wanafunzi


mh kikwembe akiingia mwangaza sekondari
waeni wakisalimiana, nje ya ofisi ya mkuu wa shule
mh. kikwembe akijiandaa kusaini kitabu cha wageni ofisini kwa mkuu wa shule
baadhi ya wanafunzi ambao waliwawakilisha wenzao kupokea msaada huo
mh. kikwembe akitoka kusalimiana na wanafunzi
mh. kikwembe anasisitiza jambo kuhusu mtalaam wa masomo ya sayansi wa
kujitolea kutoka korea kusini ambaye yupo mwangaza sekondari
Mr. Kim mtaalam wa kujitolea wa masomo ya sayansi kutoka korea kusini akitoa neno la shukranii na usia kwa wanafunzi

mh kikwembe akiwahusia wanafunzi kuhusu shule, likini pia alizungumzia umuhimu wa masomo ya sayansi
baadhi ya vifaa vilivyokabidhiwa

baadhi ya vifaa vilivyokabidhiwa

baadhi ya vifaa vilivyokabidhiwa
baadhi ya vifaa vilivyokabidhiwa
mh. akitafakari jambo na pembeni kushoto ni vifaa alivyovitoa

Mkuu wa shule ya sekondari mwangaza akitoa shukrani zake kwa mh. Kikwembe kabla ya kupokea vifaa

Afisa elimu mji akitoa shukrani zake na kuwahusia wanafunzi hasa wa kike umuhimu wa kusoma na kumtolea mfano mh. Kikwembe kwa ni mwanamke mwenye PHD




Mh Enock Gwambasa , meya akisisitiza jambo kwa wanamwangaza

Mh. Meya akitoa shukrani kwa mh kikwembe

Mh. Pudenciana Kikwembe mbunge viti maalum

baadhi ya walim wakisiliza kwa makini maelekezo na maagizo


Thursday, 23 January 2014

DAFTARI LA WAPIGA KURA LIBADILISHWE = CHADEMA

Tanzania ikiwa inaelekea katika uchaguzi mkuu,chama cha demokrasia na maendeleo(CHADEMA),kimeitaka serikali kubadilisha daftari la kudumu la kupiga kura kabla ya mchakato wa maoni juu ya katiba mpya kukamilika ili kuwawezesha watanzania wengi kupiga kura kwenye chaguzi mbalimbali za serikali za mitaa.
Uchaguzi wa serikali za mitaa utafanyika October mwaka huu ambapo chama hicho kimeanza ziara nchi nzima lengo likiwa ni kutoa elimu juu ya umuhimu wa kupiga kura katiba mpya na kujiimarisha kwenye majimbo.
Chadema kimesema,uamuzi  wa kufanya ziara nchi nzima unakuja kufuatia kuwepo kwa matukio mengi ya kihistoria kwa mwaka huu wa 2014 yakiwemo ya uchaguzi pamoja na bunge la katiba.

Aidha kimesema,iwapo serikali itaendelea na mchakato wa katiba kabla ya kuboresha daftari hilo,chama hicho kitachukua hatua kadhaa ikiwepo ya kutoshiriki katika zoezi zima la upatikanaji wa katiba mpya.

Wednesday, 22 January 2014

Shule ya msingi  Mpanda  inakabiliwa na changamoto mbalimbali  ikiwemo upungufu wa vyumba vya madarasa  na matundu ya vyoo ukilinganisha na idadi ya watoto  wanaosoma katika shule hiyo.
Hayo yamebainishwa na mwalimu mkuu wa shule Bw. Lazaro Jangu wakati akizungumza na mwandishi wa habari  ofisini kwake amesema kuwa,baadhi ya watoto hulazimika  kukaa chini wakati wamasomo hali ambayo inawawia vigumu walimu kufundisha.
Vilevile amesema kuwa licha ya madarasa ya kufundishia kuwa machache  wanafunzi wa awali  na darasa la kwanza  mpaka sasa wamefikia jumla ya mia tatu arobaini na mbili ambapo wanabanana na mwalimu kukosa sehemu ya kusimama wakati akufundisha.
Aidha Bw.Jangu ameomba wazazi  kuweza kuwahimiza wanafunzi ambao mpaka sasa hawajafika shuleni ili kujiunga na wenzao  kwani walio wengi wamekuwa wakiwatumia watoto wao kwenye shughuli zingine za nyumbani.

SOURCE:TRYPHONE

FIFA yaonya Brazil kuhusu maandalizi ya kombe la dunia

by rahim kasoonga
Uwanja wa Curitiba nchini Brazil ambao haujakamilika kuambatana na kanuni za FIFA
Shiriksho la mchezo wa soka duniani FIFA, limetoa onyo kwa utawala nchini Brazil, kuwa mji wa kusini wa Curitiba huenda ukaondolewa miongoni mwa miji itakayoandaa fainali ya kombe la dunia, kutokana na kuchelewesha kwa shughuli za ujenzi.

Katibu Mkuu wa FIFA, Jerome Valcke, amesema kuwa ukarabati katika uwanja huo unaendelea kwa mwendo wa pole sana.

Ametaja suala hilo kama la muhimu na kuwa FIFA itatangaza katika kipindi cha mwezi mmoja ujao ikiwa mji huo wa Curitiba utasalia kama moja ya miji itakayokuwa mwenyeji wa fainali hizo.
Huku ikiwa imesalia chini ya miezi mitano kabla ya fainali hizo kuanza viwanja sita kati ya kumi na mbili vinavyohitajika vimekamilika.

source: bbc sports

Tuesday, 21 January 2014

WAZIRI MIZENGO KAYANZA PETER PINDA ATOA PIKIPIKI 44 KWA SHULE ZA SEKONDRI NA VITUO VYA AFYA

by rahim kassonga (La Captain)

Katika kuboresha huuma kwa wananchi, Mbunge wa jimbo la Katavi na waziri mkuu wa Tanzania Mh. Mizengo Pinda wmetoa pikipiki 44 kwa vituo vya afya, shule za sekondari na makatibu wa CCM.


baadhi ya wawakilishi waliopokea pikipiki hizo wakijaribu pikipiki zilizotolewa na mh Pinda

Mmoja wa maafisa ajiribu kuwasha pikipiki zilizotolewa na mh.Pinda

wawakilishi wa taasisi zilizokabidhiwa pikipiki wakizichagua na kuchagua pikipiki zao

baadhi ya pikipiki zilizotolewa kwa taasisi na mh. waziri mkuu Pinda

mh.Charles Kanyanda mwakilishi wa waziri mkuu ambaye ndio aliyekabidhi pikipiki hizo, na kusema kuwa pikipiki hizo zitumike kwa kazi za kijamii zilizokusudiwa ili zisaidie jamii.

Kanyanda alisisitiza kuwa kwa yeyote atakayebadili matumizi ya pikipiki hizo basi atanyang'anya na kupewa watu wengine

Ndg. Emmanuel Chaula, katibu wa wawakilishi wa vituo vilivyopewa pikipiki akikabidhi risala kwa mgeni rasmi mh. Charles Kanyanda mwakilishi wa wazir mkuu

mwakilishi wa waziri wa mkuu akikabidhi kadi ya pikipiki kwa mmoja wa wawakilishi

wawakilishi wa vituo vilivyopata pikipiki wakikagua pikipiki walizopewa 

Mbali na pikipiki hizo pia wawakilishi hao walipatiwa mafunzo ya usalama barabarani ambapo walilipiwa gharama za mafunzo hayo na kulipiwa leseni ambavyo vyote kwa  3,200,000.
aidha, wawakilishi hao wameashwa kufuata vema kanuni za usalama barabarani na kuzitunza vizuri pikipiki hizo pia wameaswa wasizitumie kama bodaboda bali zikafanye kazi iliyokusudiwa tu.

Sunday, 19 January 2014

Serikali yawabeba waliofeli kidato cha pili

Dar es Salaam. Wakati Watanzania wakisubiri matokeo ya kidato cha pili mwaka 2013, imebaini kuwa Serikali imetoa agizo kwamba wanafunzi wote waliofeli mtihani huo kuendelea na masomo ya kidato cha tatu, huku wakisoma mafunzo ya kurudia mtihani wa kidato cha pili.
Licha ya matokeo hayo kutotangazwa hadi sasa, imebainika kuwa waliofaulu mtihani huo uliofanywa Oktoba 7 hadi 21 mwaka jana ni asilimia 62 tu, asilimia 31 wakitakiwa kukariri (kurudia) kidato cha pili mwaka huu, huku asilimia saba wakishindwa mtihani huo kwa mara ya pili.
Jumla ya wanafunzi 531,457 walitajwa na Wizara ya Elimu mwaka jana kuwa watafanya mtihani huo.
Uamuzi huo wa Serikali ni tofauti na ule uliotolewa na Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi, Dk Shukuru Kawambwa Novemba 4, mwaka 2012, kwamba kuanzia wakati huo mtihani wa kidato cha pili utakuwa ni wa mchujo na kwamba atakayefeli atatimuliwa.
Dk Kawambwa alisema matokeo ya mtihani wa kidato cha pili yatatumika kama kigezo cha kuchuja na kukariri kidato cha pili kwa watahiniwa watakaoshindwa kufikia wastani wa ufaulu wa alama 30.
Alisema mtahiniwa ataruhusiwa kukariri kidato cha pili mara moja tu na endapo mtahiniwa atashindwa mtihani kwa mara ya pili kwa mwaka utakaofuatia, itabidi aendelee na elimu ya sekondari nje ya mfumo rasmi.
Gazeti hili limeiona barua iliyoandikwa Januari 16 mwaka huu na Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi na kusainiwa na Katibu Mkuu wake, Profesa Sifuni Mchome, kwenda kwa wadau wa elimu nchini, wakiwamo maofisa elimu wa mikoa na Chama cha Wamiliki wa Vyuo na Shule Binafsi (Tamongsco).
Katika barua hiyo, wizara hiyo imewataka wadau hao kuhakikisha kuwa wanafunzi watakaofeli mtihani huo, wanaendelea na masomo ya kidato cha tatu.
“Matokeo ya kidato cha pili yamepokewa na kufanyiwa uchambuzi ili kupata taswira ya taifa. Taarifa ya matokeo hayo imebaini kuwa watahiniwa waliofanya mtihani na kufaulu ni sawa na asilimia 62 tu,” inaeleza sehemu ya barua hiyo na kuongeza;
“Hali hii inaonyesha kuwa asilimia 31 ya wanafunzi watatakiwa kukariri kidato cha pili, 2014. Wale walioshindwa kwa mara ya pili ambao ni asilimia saba wanatakiwa kuendelea na masomo nje ya mfumo rasmi.”
Barua hiyo inaeleza kuwa wanafunzi waliofaulu kwa wastani wa alama 20 na kuendelea waendelee na masomo ya kidato cha tatu mwaka 2014, wakati awali Serikali ilitoa tamko kuwa watakaoshindwa kufikisha alama 30 watatimuliwa.


“Wanafunzi waliofaulu kwa wastani wa alama 20 hadi 39 wapewe mafunzo rekebishi ‘Remedial class’ wakiwa kidato cha tatu,” inaeleza sehemu ya barua hiyo.
source mwananchi

MAWAZIRI WAPYA: serikali ya Kikwete

 
Saada Mkuya (Wizara ya Fedha), Hussein Mwinyi (Wizara ya Ulinzi), Mathias Chikawe (Wizara ya Mambo ya Ndani), Dk Titus Kamani (Wizara ya Mifugo) na Lazaro Nyalandu (Wizara ya Maliasiri na Utalii), Wengine wapya ni Dk Rose Migiro (Wizara ya Katiba na Sheria), Dk Seif Selemani Rashid (Wizara ya Afya).

MANAIBU WAPYA: 
Naibu Mawaziri wapya ni Ummy Mwalimu (Muungano), Mwigulu Nchemba na Adam Malima (Fedha), Jenista Mhagama (Wizara ya Elimu), Manaibu Mawaziri wengine katika mabadiliko hayo ni Juma Nkamia (Wizara ya Habari), Pindi Chana (Wizara ya Jinsia), Amos Makala (Wizara ya Maji), Charles Kitwanga (Wizara ya Madini) ,George Simbachawene (Wizara ya Ardhi na Makazi)…
source mwananchi

Murray asonga mbele Australian Open

by rahim kasoonga

Murray angali anapona kutokana na upasuaji aliofanyiwa mgongoni
Mchezaji wa Tennis Andy Murray ameonyesha wazi kuwa na yeye yumo mbioni kuwania ubingwa wa mashidnano ya tennis ya Australian Open baada ya kumbwaga Feliciano Lopez katika raundi ya tatu ya mashindano hayo yanayoendelea nchini Australia.
Muingereza huyo akicheza kwenye mashindano yake ya pili tangu kufanyiwa upasuaji , alishinda seti zake zote kwa poiti 7-6 (7-2) 6-4 6-2 katika ukumbi wa Hisense na kuwa miongoni mwa wachezaji bora kumi na sita.
Katika mechi itakayofuata, Murray atapambana na Stephane Robert.
Murray, mwenye umri wa miaka 26, atacheza mechi hiyo wengi wakiwa wanamuunga mkono aweze kushinda. Hata hivyo amepuuza nafasi yake ya kuweza kushinda taji lengine Jumapili ijayo.
"nimeweza kupona vyema, baada ya mechi zote,'' alisema Murray. '' mara kwa mara mimi husikia uchungu lakini kwa ukubwa sina matatizo sana.''
Kusinda mechi mbili mfululizo, katika ufunguzi wa mashindano hayo, ni jambo la kumtia motisha Lopez.
Lopez, mwenye umri wa miaka 32, alimpa Murray mazoezi wakati wa mechi yao ya kwanza katika joto kali la nyuzo 20 ikilinganishwa na nyuzi joto 40 za siku za kwanza za michuano hiyo.
sourece: bbc

Friday, 17 January 2014

WABONGO 8 KUCHEZESHA MECHI ZA CAF



Watanzania wanane wameteuliwa kuchezesha mechi mbili za marudiano za raundi ya awali za Ligi ya Mabingwa Afrika na Kombe la Shirikisho zitakazochezwa wikiendi ya Februari 14 na 16 mwaka huu.

Waamuzi hao walioteuliwa na Shirikisho la Mpira wa Miguu Afrika (Caf) ni Israel Mujuni atakayechezesha mechi ya MABINGWA kati ya Rayon Sport ya Rwanda na AC Leopards ya Congo itakayofanyika Kigali RWANDA.

Mujuni atasaidiwa na Josephat Bulali, Samwel Mpenzu na Ramadhan Ibada, wakati Kamishna wa mechi hiyo atakuwa Jean Marie Hicuburundi wa Burundi.

Naye Waziri Sheha ataongoza jopo lingine kwenye mechi ya SHIRIKISHO kati ya FC MK ya Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo (DRC) na El Ahly Atbara ya Sudan. Mechi hiyo itachezwa jijini Kinshasa.


Sheha atasaidiwa na Ferdinand Chacha, John Kanyenye na Israel Mujuni. Kamishna wa mechi hiyo ni Chayu Kabalamula kutoka Zambia.

Friday, 10 January 2014

KUELEKEA KOMBE LA DUNIA: UCHAMBUZI WA TIMU

by rahim kassonga (La captain)
TIMU YA ARGENTINA
Argentina ni timu nzuri sana , na wanakocha bora safari hii wakiwa chini ya Alejandro Sabella na wanawachezaji bora kwenye kila idara
Mfumo wanaotumia wakumchezesha Messi chiini zaidi unaweza usiwe mzuri sana, nadhani kama wangemchezesha mbele zaidi wangefanya vema sana .
Kuna swali juu ya beki wao wa kati na golikipa Sergio Romero, lakini kwa uimara wa washambuliaji wao wanaweza kufanya vyema na hata kunyakua kombe la Dunia.

STYLE & FORMATION:
Argentina wanatumia mfumo wa 4-3-3 ingawa wakiwa ugenini hutumia  5-3-2
Mfumo wao humfanya Messi acheze kama namba 10 nyuma ya washambuliaji wawili Sergio Aguero na Gonzalo Higuain ambao hutanua sana uwanja.
Lakini wana Angel Di Maria anayetumiwa kama kama kiungo ambaye kidogo huongeza nguvu pia kwenye ulinzi.
STRENGTHS:
Wachezaji mahiri mahiri wane, Los Cuatro Fantasticos - the Fantastic Four of Di Maria, Aguero, Higuain and Messi, ambao wanauwezo wa kucheza timu yeyote duniani
Mess amekuwa akiimarika kwenye timu ya taifa, kitu kinachoonesha kwamba kama atakuwa fiti, anawezakufanya mashindano yhaya kuwa yake na kumwongezea nafasi ya kuwa mchezaji bora wa dunia wa muda wote
WEAKNESSES:
Timu haina uwiano mzuri kiufundi na haina walinzi mahiri
Goalkeeper Sergio Romero hafanyi vema na timu yake ya Monaco, huku  left-back Marcos Rojo, wa Sporting, na centre-back Federico Fernandez wa Napoli hawana uzoefu kwenye mashindano makubwa.

KEY PLAYER

Licha ya kukebehiwa kwa kutofanya vema na timu ya taifa kama anavyofanya na timu yake ya  Barcelona kwa kucheza mechi 16 za mashindano bila kufunga kocha  Alejandro Sabella alimwita Messi mwaka 2011alipoteuliwa na amekuwa ni tegemeo lake.
Messi mwenye miaka 26, amebadilika na anatoa matumaini ameshafunga magoli 20 kwenye mechi 20 alizoichezea Argentina.

MTU WA KUMWANGALIA

Angel Di Maria, kasiyake uwanjani, ufuni na nidhamuviliwafanya Real Madrid kucheza karata ya kumtoa Mesut Ozil na kumwacha yeye, wakati wakimsajili Gareth Bale.
Angel Di Maria,  25  anasifa zote za kucheza kwenye nafasi ya winga wa kushoto

THE BOSS

Alejandro Sabella alipata nafasi baada ya kuisaidia  Estudiantes  kushinda ubingwa wa Copa Libertadores.
Ni mchezaji wa zamani wa Sheffield United ya Uingereza, alikuwa sehemu ya benchi la ufundi la Argentina mwaka 98 nchini  France na ametumia muda wake mwingi wa kufundisha kama kocha msaidizi wa Daniel Passarella.

HOW THEY QUALIFIED

Argentina's qualifying campaign

  • 7 Oct 2011 W 4-1 v Chile (h)
  • 11 Oct 2011 L 0-1 v Venezuela (a)
  • 11 Nov 2011 D 1-1 v Bolivia (h)
  • 15 Nov 2011 W 2-1 v Colombia (a)
  • 2 Jun 2012 W 4-0 v Ecuador (h)
  • 7 Sep 2012 W 3-1 v Paraguay (h)
  • 11 Sep 2012 D 1-1 v Peru (a)
  • 12 Oct 2012 W 3-0 v Uruguay (h)
  • 16 Oct 2012 W 2-1 v Chile (a)
  • 22 Mar 2013 W 3-0 v Venezuela (h)
  • 26 Mar 2013 D 1-1 v Bolivia (a)
  • 7 Jun 2013 D 0-0 v Colombia (h)
  • 11 Jun 2013 D 1-1 v Ecuador (a)
  • 10 Sep 2013 W 5-2 v Paraguay (a)
  • 11 Oct 2013 W 3-1 v Peru (h)
  • 15 Oct 2013 L 2-3 v Uruguay (a)
Wamedungwa kwa mara ya kwanza na  Venezuela, na kutoa sare nyumbani na Bolivia wakati walifungwa mchezo wa mwisho ambao haukuwa na umuhimu sana kwao dhidi ya Uruguay kwani walikuwa wamekwishafuzu.

WORLD CUP RECORD

Mabingwa mwaka 1978 na 1986, washindi wapili mwaka 1930 na 1990, wameshindwa kufika nusu fainali katika mashindano matano ya mwisho.

Fifa ranking: 3                                                                  

Thursday, 9 January 2014

YANGA YAENDA KUWEKA KAMBI UTURUKI





Timu ya Yanga inatarajiwa kuweka kambi ya siku 14 nchini Uturuki kwa ajili ya kujiandaa na mzunguko wa pili wa Ligi Kuu Bara na Klabu Bingwa Afrika.


Kikosi kizima cha Yanga chini ya Kocha Boniface Mkwasa, kinaondoka leo baada ya kufanya mazoezi ya mwisho kwenye Uwanja wa Bora jijini Dar.

Kambi hiyo itakuwa jijini Antalya ambako Yanga iliwahi kuweka kambi chini ya Kocha Ernie Brandts aliyetimuliwa.
 
Uongozi wa Yanga ulitangaza kwenda kuweka kambi nje ya nchi mara baada ya kichapo cha mabao 3-1 dhidi ya Simba kilichosababisha kutimuliwa kwa kocha Ernie Brandts na Championi likawa la kwanza kuandika.

Yanga ambayo inaondoka nchini kesho Alhamisi, ipo chini ya kocha msaidizi, Boniface Mkwasa, ambaye amekuwa akiwapa mazoezi mazito pamoja na kocha wa makipa, Juma Pondamali.

 Mwenyekiti wa Kamati ya Usajili ya Yanga, Abdallah Bin Kleb, alisema wanahitaji kukaa nje kwa muda wa wiki mbili ili kukinoa kikosi chao waweze kujiandaa na mzunguko wa pili na michuano ya kimataifa.

“Tunatarajia kuwa nje kwa muda wa siku 14, lengo letu kubwa ni kubadili mazingira na kuwaweka sawa wachezaji kisaikolojia.
“Kuhusu mechi za kirafiki si lazima sana ila tukizipata tutacheza na kocha mpya atakayepatikana ndiye atakayeamua juu ya michezo anayohitaji,” alisema Bin Kleb.