Shule ya msingi Mpanda
inakabiliwa na changamoto mbalimbali
ikiwemo upungufu wa vyumba vya madarasa
na matundu ya vyoo ukilinganisha na idadi ya watoto wanaosoma katika shule hiyo.
Hayo yamebainishwa na mwalimu mkuu
wa shule Bw. Lazaro Jangu wakati
akizungumza na mwandishi wa habari
ofisini kwake amesema kuwa,baadhi ya watoto hulazimika kukaa chini wakati wamasomo hali ambayo
inawawia vigumu walimu kufundisha.
Vilevile amesema kuwa licha ya
madarasa ya kufundishia kuwa machache
wanafunzi wa awali na darasa la
kwanza mpaka sasa wamefikia jumla ya mia
tatu arobaini na mbili ambapo wanabanana na mwalimu kukosa sehemu ya kusimama
wakati akufundisha.
Aidha Bw.Jangu ameomba wazazi kuweza
kuwahimiza wanafunzi ambao mpaka sasa hawajafika shuleni ili kujiunga na
wenzao kwani walio wengi wamekuwa
wakiwatumia watoto wao kwenye shughuli zingine za nyumbani.
SOURCE:TRYPHONE
No comments:
Post a Comment