Thursday 9 January 2014

YANGA YAENDA KUWEKA KAMBI UTURUKI





Timu ya Yanga inatarajiwa kuweka kambi ya siku 14 nchini Uturuki kwa ajili ya kujiandaa na mzunguko wa pili wa Ligi Kuu Bara na Klabu Bingwa Afrika.


Kikosi kizima cha Yanga chini ya Kocha Boniface Mkwasa, kinaondoka leo baada ya kufanya mazoezi ya mwisho kwenye Uwanja wa Bora jijini Dar.

Kambi hiyo itakuwa jijini Antalya ambako Yanga iliwahi kuweka kambi chini ya Kocha Ernie Brandts aliyetimuliwa.
 
Uongozi wa Yanga ulitangaza kwenda kuweka kambi nje ya nchi mara baada ya kichapo cha mabao 3-1 dhidi ya Simba kilichosababisha kutimuliwa kwa kocha Ernie Brandts na Championi likawa la kwanza kuandika.

Yanga ambayo inaondoka nchini kesho Alhamisi, ipo chini ya kocha msaidizi, Boniface Mkwasa, ambaye amekuwa akiwapa mazoezi mazito pamoja na kocha wa makipa, Juma Pondamali.

 Mwenyekiti wa Kamati ya Usajili ya Yanga, Abdallah Bin Kleb, alisema wanahitaji kukaa nje kwa muda wa wiki mbili ili kukinoa kikosi chao waweze kujiandaa na mzunguko wa pili na michuano ya kimataifa.

“Tunatarajia kuwa nje kwa muda wa siku 14, lengo letu kubwa ni kubadili mazingira na kuwaweka sawa wachezaji kisaikolojia.
“Kuhusu mechi za kirafiki si lazima sana ila tukizipata tutacheza na kocha mpya atakayepatikana ndiye atakayeamua juu ya michezo anayohitaji,” alisema Bin Kleb.

No comments:

Post a Comment