Shiriksho la mchezo wa soka duniani FIFA, limetoa onyo kwa utawala nchini Brazil, kuwa mji wa kusini wa Curitiba huenda ukaondolewa miongoni mwa miji itakayoandaa fainali ya kombe la dunia, kutokana na kuchelewesha kwa shughuli za ujenzi.
Katibu Mkuu wa FIFA, Jerome Valcke, amesema kuwa ukarabati katika uwanja huo unaendelea kwa mwendo wa pole sana.
Ametaja suala hilo kama la muhimu na kuwa FIFA itatangaza katika kipindi cha mwezi mmoja ujao ikiwa mji huo wa Curitiba utasalia kama moja ya miji itakayokuwa mwenyeji wa fainali hizo.
Huku ikiwa imesalia chini ya miezi mitano kabla ya fainali hizo kuanza viwanja sita kati ya kumi na mbili vinavyohitajika vimekamilika.
source: bbc sports
No comments:
Post a Comment