Thursday 23 January 2014

DAFTARI LA WAPIGA KURA LIBADILISHWE = CHADEMA

Tanzania ikiwa inaelekea katika uchaguzi mkuu,chama cha demokrasia na maendeleo(CHADEMA),kimeitaka serikali kubadilisha daftari la kudumu la kupiga kura kabla ya mchakato wa maoni juu ya katiba mpya kukamilika ili kuwawezesha watanzania wengi kupiga kura kwenye chaguzi mbalimbali za serikali za mitaa.
Uchaguzi wa serikali za mitaa utafanyika October mwaka huu ambapo chama hicho kimeanza ziara nchi nzima lengo likiwa ni kutoa elimu juu ya umuhimu wa kupiga kura katiba mpya na kujiimarisha kwenye majimbo.
Chadema kimesema,uamuzi  wa kufanya ziara nchi nzima unakuja kufuatia kuwepo kwa matukio mengi ya kihistoria kwa mwaka huu wa 2014 yakiwemo ya uchaguzi pamoja na bunge la katiba.

Aidha kimesema,iwapo serikali itaendelea na mchakato wa katiba kabla ya kuboresha daftari hilo,chama hicho kitachukua hatua kadhaa ikiwepo ya kutoshiriki katika zoezi zima la upatikanaji wa katiba mpya.

No comments:

Post a Comment