Sunday 23 March 2014

KOCHA RHINO ALIA WANATABORA WANAWAMALIZA


by kassonga




SIKU moja baada ya kukumbana na kipigo cha mabao 3-0 kutoka kwa Yanga, Kocha Mkuu wa Rhino, Jumanne Chale amesema wako baadhi ya wadau we mkoa we Tabora wanachangia timu hiyo kutofanya vizuri.

Chale amesema amekuwa akishangazwa na kuona baadhi ya mashabiki au wadau wa soka katika mkoa huo wakifanya kila juhudi kuzisaidia timu za wageni.


“Wanaona Yanga, Simba au timu nyingine ndiyo wanapaswa kuzisaidia. Lakini wanasahau wao wako hapa Tabora.
“Hata kuziona timu nyingine ni kwa kuwa Rhino iko ligi kuu. Ikiteremka wataziona wapi Yanga na Simba, kweli inanishangaza sana,” alisema akionyesha kutokukubaliana na suala hilo.

Tuesday 4 March 2014

HIZI NDIO SHULE ZETU KATAVI MPANDA PICHA MOJA YA SHULE KATA YA KABUNGU WILAYA YA MPANDA

                                            Haya ndio madarasa ya shule ya Kabungu
                                           Hili ndio darasa zuri kuliko yote na ni la awali ( CHEKECHEA )
                                          Ofisi ya walimu. mwalimu akiendelea na kazi za kiofisi
                                             Vyoo vinavyoonekana kuto kutumika muda mrefu