Tuesday, 29 October 2013

RAY C AWA BONDIA,AMTWANGA HUYU DADA WA BONGO MOVIE.

BY ZANGII ZE ICON


KATIKA hali ya kushangaza, siku chache baada ya kuripotiwa kupona na kuacha matumizi ya madawa ya kulevya, mwanamuziki Rehema Chalamila ‘Ray C’ anadaiwa kugeuka mwanamasumbwi na kumpa kipigo mwigizaji Nuru Nassoro ‘Nora’,.Kwa mujibu wa shuhuda wetu, tukio hilo lilijiri wiki iliyopita ndani ya studio moja ya kurekodia muziki iliyopo Kinondoni, Dar ambapo wawili hao walikutana walipokwenda kurekodi ngoma zao.
Ilidaiwa kuwa akiwa studio hapo, Nora alikutana na Ray C ambaye pia alizama mahali hapo bila mawasiliano na prodyuza anayemtengenezea ngoma mpya.


Chanzo hicho kilipasha kuwa baada ya Ray C kuingia studio hapo alimkuta prodyuza huyo akiandaa ngoma ya Nora ambapo alihoji kilichompeleka mwigizaji huyo mahali hapo.

Ilidaiwa kuwa prodyuza huyo ambaye jina halikupatikana alimwambia Ray C kuwa Nora alifika kurekodi wimbo wake.

Ilisemekana kuwa Ray C hakuridhishwa na majibu hayo, akaomba asikilizishwe ngoma hiyo ya Nora lakini baada ya kusikiliza ilidaiwa kwamba Ray C aliiponda mbele ya Nora, jambo ambalo mwigizaji huyo hakufurahishwa nalo.
Ilidaiwa kuwa Nora alipandwa hasira na kujikuta akimjibu mbovu Ray C.

Habari ziliendelea kutiririka kuwa siku hiyo walimalizana kwa kusonyana na siku iliyofuta walikutana tena studio hapo ambapo Ray C alidaiwa kutinga akiwa ‘masanga’.
Ilisemekana kuwa alipomuona Nora alianza kumpa vijembe, jambo lililosababisha Nora kushikwa hasira ndipo wakavaana na kuzichapa.

Hata hivyo, ilidaiwa kuwa Ray C ndiye aliyeibuka bingwa wa ndondi hizo kwa kumtwanga Nora hadi kumvimbisha jicho kabla ya maprodyuza na watu wengine kufanya kazi ya ziada kuwaamulia.
Ilisemekana kuwa baadaye Ray C alitolewa nje ndipo akahamishia hasira kwenye gari la Nora aina ya Toyota Vitz kisha akalivunja kioo na kutambaa zake.

Baada ya kupenyezewa ‘niuz’ hizo tulimtafuta Nora ambaye alikiri kutokea kwa sekeseke hilo huku akibainisha namna alivyoumizwa jicho lake na kuvunjiwa kioo cha pembeni cha gari lake.
Aliongeza kuwa siku hiyo alipoteza pochi wakati wa ugovi huo.

“Ray C alinikuta studio nikifanya wimbo, kilichonishangaza baada ya kuniona tu alibadilika ghafla.
“Nilijua angenishauri kwa kuwa ndiyo ninaanza gemu kumbe mwenzangu alifikiria vingine,” alisema Nora na kuongeza:
“Mbali na kuniumiza jicho lakini alinifanyia mambo ya ajabu sana, kama kusingekuwa na watu wa kutuamulia basi chochote kingetokea.

“Sikwenda kuripoti polisi. Niliamua kusamehe kwa sababu kuna watu walinisihi niachane naye kwa sababu bado kuna mambo yanamwendesha. 

Kwa upande wake Ray C alitafutwa kwa kila njia kupitia simu ya mkononi na kumvizia studio lakini hakupatikana hivyo juhudi za kumpata zinaendelea.


Monday, 28 October 2013

VIWANJA MISUNKUMILO

by rahim kassonga (La Captain)


Wananchi wa Kata ya Misunkumilo Wilaya ya Mpanda Mkoani Katavi wameulalamikia Uongozi wa Kata yao kwa kushindwa kufuatilia viwanja walivyo takiwa kugawiwa na Idara ya Ardhi.

Wananchi hao wamesema kuwa Augosti mwaka huu Idara ya Ardhi ilifanya tathmini ya  viwanja kwa ajili ya kupanga mpangilio maalumu wa kuacha nafasi ya barabara za Mitaa lakini mpaka sasa hawajarudi kwajili ya kugawa viwanja hivyo.

Aidha wananchi hao wamesema kuwa kutokana na kufuatilia na kukaa kwa muda mrefu baadhi ya wananchi wameanza kujenga ili waweze kuishi katika nyumba zao kwasababu wamechoka kukaa kwenye nyumba za kupanga.

Hata hivyo Mtendaji wa Kata hiyo January Kayungilo amesema kuwa Idara ya Ardhi imeshafanya tathmini, hiyo amewaomba wananchi  kusubiri shughuli ya kuanza kugawa viwanja hivyo kwaajili ya kuvilipia ili waweze kujenga nyumba zao pia amewataka wananchi hao kuwa wavumilivu katika suala hilo.

EDITOR:TIDA SAIDEA

tutatumia umeme wa gesi asilia na makaa ya mawe;Prof.Sospeter Muhongo

by rahim kassonga (La Captain)Waziri wa Nishati na madini Pr.Sospeter Muhongo  amesema Serikali imedhamiria kutumia gesi asili na makaa ya mawe pamoja na vyanzo vingine vya kuzalisha umeme ili kuwawezesha wananchi zaidi ya asilimia 30 kutumia Nishati hiyo ya umeme ifikapo mwaka 2015.

Akiwa Mjini Mpanda katika siku yake ya kwanza ya kukagua utekelezaji wa mradi wa umeme katika maeneo ya vijijini kwa kiwango cha zaidi ya asilimia 10 toka asilimia chini ya 7 za sasa ambapo Pr.Muhongo amesema lengo la wananchi kukabiliana na tatizo la umaskini ifikapo mwaka 2025 haliwezi kukamilika ikiwa Nishati ya umeme haitazalishwa kwa wingi.

Akizungumza na Viongozi wa Serikali wa Mkoa wa Katavi Pr.Muhongo amesema kuwa kwa kutambua umuhimu wa Nishati ya umeme kwa maendeleo ya Taifa na ukuzaji wa uchumi kwa mtu mmoja mmoja Serikali imeweka nia ya kweli kuhakikisha uzalishaji wa Nishati hii muhimu unaongezeka.


Taarifa ya Mkuu wa Mkoa wa Katavi Mh.Rajabu Lutengwe imeeleza mikakati ya Serikali Mkoani humu kushirikiana na wakala wa mradi wa kusambaza umeme vijijini ambapo kiasi cha shilingi bilioni 10 zitatumika kusambaza umeme katika vijiji 14.

Mazishi ya baba mzazi wa Wema Sepetu ni jumatano hii ....Rais Kikwete na mama Salma watoa mkono wa pole

 BY ZANGII ZE ICONBalozi Isaac Abraham Sepetu ambaye ni baba yake mzazi na Wema Sepetu, anatarajiwa kuzikwa Jumatano hii visiwani Zanzibar. Mwili wa marehemu utasafirishwa kesho asubuhi kuelekea visiwani humo.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Jakaya Kikwete na mkewe Mama Salma, leo wameungana na watu wengi wa karibu wa familia ya Wema kuwapa pole wafiwa akiwemo mama yake, Bi. Mariam Sepetu. 
 
Balozi Sepetu alifariki jana baada ya kuugua kwa muda mrefu maradhi ya kisukari na kiharusi na alikuwa amelazwa kwenye hospitali ya TMJ jijini Dar es Salaam.

  
Balozi Sepetu aliwahi kuwa Naibu Waziri wa Mambo ya Nchi za Nje mnamo miaka ya 1970 wakati wa utawala wa awamu ya kwanza chini ya Mwalimu Julius KambaragE Nyerere. 
 
Vilevile, aliwahi kuwa balozi nchini Urusi tangu mwaka 1982 wakati wa utawala huohuo wa Nyerere. Hadi anafariki, Mzee Sepetu alikuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya Mamlaka ya Uwekezaji wa Vitega Uchumi Zanzibar.

Anakubalika Kwa Sauti Na Umbo Lake, Rihanna Ndani Ya Vazi La Kuogelea.Tazama Picha zaidi ya nne hapa!! JINI KABULA AAMUA "KUOKOKA"...ASHINDA NA BIBLIA

MWANADADA anayefanya vizuri kunako gemu la filamu Bongo, Miriam Jolwa ‘Jini Kabula’ ameamua kubadili mfumo wa maisha kwa kusoma Biblia kila wakati.
 
Miriam Jolwa ‘Jini Kabula’.
Paparazi wetu alimnasa Jini Kabula nyumbani kwake Sinza akiwa anasoma Biblia na alipoulizwa kulikoni amekuwa mtu wa kushinda nyumbani na siyo kupiga misele kama alivyozoeleka, alitiririka:
“Nimeamua kubadili mfumo wa maisha yangu niliyokuwa nikiishi zamani ya kuendekeza starehe, nimemrudia Mungu wangu na mara nyingi nashinda ndani kwangu nikisoma Biblia kwa sababu Mungu ndiye rafiki wa kweli,” alisema Jini Kabula.

Ney Wa Mitego Aswekwa Sero Baada Kuvaa Sare Za Polisi.


by zangii ze icon 
Rapper Ney Wa Mitego ameniambia kuwa hii picha hapo juu tukio hilo limetokea Jana wakati wana shoot video ya wimbo wake Unaofanya vizuri kwa sasa kwenye radio stations ' Salam Zao'.


Ney Wa Mitego Amesema ' Nikweli nilitupwa sero jana baada ya raia wasio julikana kuleta fujo eneo la kazi yangu  kwasababu kulikuwa na waigizaji waliokuwa na sare za polisi. Watu hao sijuani nao na walijitambulisha kama askari na kutaka kujua kwanini natumia sare za polisi kwenye video yangu bila kibali. hicho ndio kitu kilichopelekea nikapelekwa polisi.

Mitego ameendela kusema kuwa baada ya kuka sero kwa dakika kama 15 mkuu wa kituo alikuja na kusikiliza tatizo hilo na ndio aliachiwa huru baada ya kutoa maelezo kuhusu tukio hilo na sare hizo kuonekana uraiani.

Ney aliwekwa sero Kwenye kituo cha polisi Urafiki kilichopo Manzese na wiki ijayo video hii itaonekana kwenye vituo vya televison Tanzania.


HIKI NDICHO KINACHOENDELEA KWENYE MSIBA YA BABA MZAZI WA WEMA SEPETU HUKO SINZA JIJINI DAR


by zangii ze icon

Wema Sepetu akiwa katika hali ya majonzi baada ya kufiwa na baba yake mzazi
Mama mzazi wa Wema akiwa na simanzi baada ya kuondokewa na mumewe mzee Sepetu.
  

Kajala Masanja (kushoto), Wema Sepetu (katikati) na Zamaradi Mketema (kulia) wakiwa katika hali ya majonzi nyumbani kwao Wema Sepetu, Sinza - Mori jijini Dar.Kajala Masanja (kushoto) na Wema Sepetu (katikati) wakiangua vilio. Kulia Zamaradi akijaribu kumtuliza Wema.

Ndugu wa karibu wa marehemu akiwa na simanzi nzito
STAA wa sinema za Kibongo na Miss Tanzania 2006 Wema Isaac Sepetu, bado yuko kwenye wakati mgumu baada ya leo asubuhi kupatwa na msiba mkubwa wa kuondokewa na baba yake mzazi Balozi Isaac Abraham Sepetu aliyefariki asubuhi ya leo.
Kwa sasa kuna watu wengi wamefika kumjulia hali maeneo ya Sinza, Mori jijini Dar, rafiki yake wa karibu Kajala Masanja na Zamaradi Mketema wapo bega kwa bega kuwa naye karibu na vilio vimetawala kila kona ya familia ya marehemu Balozi Sepetu.
Bado haijafahamika mazishi yanafanyika lini maana wanasubuliwa watoto wa Marehemu Tunnu Sepetu na Sunna Sepetu ambao wanaishi nchini Marekani, lakini kuna tetesi kuwa huenda mazishi hayo yakafanyika siku ya Ijumaa.
Mama mzazi wa Wema bado yuko kwenye hali ya huzuni baada ya kufiwa na mume wake ambaye amedumu nae kwa miaka mingi kabla ya kupatwa na mauti asubuhi ya leo katika hospitali ya TMJ jijini Dar. Mpaka mauti yanamfika, marehemu alikuwa akisumbuliwa na kisukari pamoja na kiharusi.

RAIS AFRICA MASHARIKI ATATEKWA NA CLUB KULIPULIWA.


by ZANGII ZE ICON
Yule Mchungaji Maarufu kutoka Nigeria Ambae hutabiri mambo mbalimbali na kweli yakatokea  TB Joshua leo ametoa utabiri mpya ambao unahusisha Africa Mashariki.

...ameonyeshwa rais mmoja Africa Mashariki atatekwa na ameonyeshwa watu wakiwa club wanacheza then wanalipukiwa na nchi iyo ni jirani na Kenya, Angalizo, amesema siyo kenya tena,je itakuwa nchi gani? 

Misa ya jana jumapili ndo kasema, na amesema ataendelea kuomba ili jumatano na alhamisi ijayo aonyeshwe ni rais gani na nchi gani.

BABA MZAZI WA LOVENESS DIVA WA CLOUDS AULA TFF SASA NDIO MRITHI WA TENGA
Baada ya uchaguzi uliofanyika kwenye ukumbi wa NSSF Water front kumpata Rais mpya wa TFF kati ya Athumani Nyamlani na Jamal Malinzi, hatimaye TFF imepata Rais mpya ambaye ni Jamal Malinzi.
Mashuhuda waliokuwepo hapo ukumbini wanasema kwamba mpinzani wa Jamal Malinzi alitoka kabla ya utaratibu mzima wa uchaguzi kuisha. Baada ya matokeo kutangwaza Jamal Malinzi alimzidi kura Athumani Nyamlani na hatimaye kupata nafasi ya kumrithi Leodigar  Tenda.

Kama ulikuwa hujui ni kwamba  Rais huyu wa TFF Jamal Malinzi ndiyo baba wa Diva Loveness wa Ala za Roho ya Clouds FM

Diamond kuja na video ya 'Number One Remix'


Diamond amefunguka kuhusu kuwepo kwa video hiyo kupitia Instagram, ambapo ameonesha pia nia ya kuwaalika watu ambao wanapenda kuwa sehemu ya video hiyo, ‘Do you wanna be a part ov it..? Aliuliza Diamond.
Kwa maelezo ya Diamond aliyoyaweka jumamosi kwenye Instagram, video hiyo ilitakiwa kufanyika jana jumapili, lakini hakuna taarifa za kufanyika video hiyo hapo jana, huenda video hiyo ikafanyika leo.
C.E.O wa Wasafi, aliweka picha inayoonesha yuko studio na 'Skelewu hit maker' Davido wakiipika remix ya Number One.
"[ @ ] diamondplatnumz I said NGOLOLO Dance, and he said Nah man! SKELEWU Dance... then we decided to put it in a song....and show each other what we gat, we are on tommorow for the new Video #NumberOneRemix @Diamondplatnumz ft @lifeofdavido .. Do you wanna be a part ov it...?" Aliandika Diamond.

Saturday, 26 October 2013

Ofisi ,usafiri,nyumba za wafanyakazi vyazorotesha huduma za elimu

by rahim kassonga (La Captain)


KATAVI
Chama cha walimu (CWT) Wilaya ya Nsimbo Mkoani Katavi  kimetoa changamoto wanazo kabiliana nazo na malengo ambayo wanatarajia kufanya ili kuimarisha chama hicho.

Akiongea na Mpanda Fm Mwenyekiti wa chama hicho Mwl. Kenedi Simsokwe amesema kuwa mazingira ya uendeshaji ni magumu kwakutokuwa na Ofisi ya chama,usafiri,nyumba za wafanyakazi na baadhi ya wanachama kuto kufikisha marejesho shuleni.

Aidha Mwenyekiti huyo ameongeza kuwa  malengo ambayo wanayo ni kuongeza huduma zaidi kwa wanachama kwa kuwatembelea mara kwa mara na kujenga ofisi ya chama ili kuweza kufanya kazi kwa ufasaha.

Hata hivyo Simsokwe amesema kuwa anaiomba serikali iwatambue na kuwathamini walimu kwa kuwaongezea posho kama inavyo fanya kwa watumishi wengine wa umma sambamba na kuboresha mazingira ya kazi kwa kufanya hivyo watakuwa wameinua kiwango cha elimu Mkoani hapa . 
SOURCE:DAWATI
EDITOR:IRENE TEMU

Friday, 25 October 2013

MAJANGA KWENYE ELIMU, WANAFUNZI 471, MADAWATI 39, MADARASA 4, WAPI SERIKALIII !!!!!

by rahim kassonga (La Captain)


Shule ya msingi Ilebula iliyopo Kata ya Kabungu Wilaya ya Mpanda vijijini wametoa changamoto wanazo kabiliananazo katika mazingira ya shule ikiwemo upungufu wa madarasa,madawati na nyumba za walimu.

Akiongea na Mpanda Fm Mwalimu Mkuu wa shule hiyo Moses Mathias Makalawa amesema kuwa shule hiyo ina upungufu wa vyumba vya madarasa ambapo shule nzima ina madarasa manne hali inayopelekea wanafunzi kusomea chini ya mti na wengine katika ofisi za walimu.

Makalawa ameongeza kuwa shule hiyo ina wanafunzi 471 ambapo madawati katika shule nzima ni 39 ambayo hayakidhi idadi ya wanafunzi na kupelekea wengine kukaa chini huku walimu wakiishi mbali na mahali pa kazi kutokana na shule hiyo kumiliki nyumba mbili za walimu.

Hata hivyo  mwalimu Makalawa ametoa wito kwa serikali kutatua changamoto hizo ili kuongeza ufaulu katika shule hiyo na kufanikisha mpango wa Big Result Now ulioanzishwa na serikali.
NANDO APEWA NAFASI YA KIPEKEE KUSHIRIKI TENA BIG BROTHER AFRICA YA MWAKANI 2014.

by zangii ze icon After being disqualified from the recently concluded BBA The Chase show, Nando Khan (also known as Ammy Nando) has gotten himself another chance at the game!


Word reaching us right now is that, he will be representing Tanzania in the 9th season of the Big Brother Africa show, tagged BBA Stars.

Reliable sources also reveal that he has accepted the offer and will be back in the house come next year.

The Tanzania rep got disqualified shortly after his fight with Ghana's Elikem.

Nando is rumored to have apologized to Elikem during the finale party.

Msanii wa bongo movie anusurika kuliwa KIBOGA.....Alizidisha pombe na kujikuta chooni akiwa mtupu.

Muigizaji wa filamu za kibongo anayejulikana kwa jina la Danny Cloud  maarufu  kama  Danny mtoto wa mama  ambaye  alipata  umaarufu  wa  jina  hilo  kupitia  filamu ya mtoto wa mama  amenusurika  kubakwa ( kuliwa kiboga ) 

Akizungumza  na  mpanda fm, rafiki wa karibu wa msanii huyo  alidai kwamba  Danny  alikuwa maeneo ya Bilcanas  ambapo  alipewa  ofa  ya  pombe  na  jamaa  zake...

Rafiki huyo  alidai  kuwa, baada  ya  kupewa  ofa  hiyo  adimu, msanii  huyo  alianza  kuiparamia  pombe mfano  wa  mtu  mwenye  kiu  kali  ya  maji, hali  iliyomfanya  asijitambue  na  kuanza  kuvua  nguo...

"Kuna  wakati Danny  alinyanyuka  na  kuelea  chooni  huku  akipepesuka...Alipofika  huko  alidondoka  na kulala  huko huko chooni, hali  iliyowafanya   vibaka  watake  kumla  kiboga"...Alisema  huyo rafiki  yake  na  kuongeza:

"Baada  ya  kimya  kirefu, ilibidi  tukamwangalie  ambapo  tuliwakurupusha  vijana  watatu  wakiwa  wameshamvua  nguo"

MAZISHI YA NYAISANGAH... MAMIA WAMLILIA CHALZ HILLARY


by zangii ze icon
Stori: Waandishi Wetu
VILIO vilitawala juzi Jumanne wakati nguli katika utangazaji Bongo, Julius Nyaisangah ‘Uncle J’ akiagwa, lakini wengi walionekana kumlilia zaidi swahiba wake wa karibu, Charles Hillary ‘Chalz Hillary’.
Jopo la waandishi wetu lililofika mapema katika Viwanja vya Leaders Club, Kinondoni, Dar katika Ibada ya kumuaga marehemu, lilishuhudia mijadala ikiendelea katika makundi kuhusu upweke alioachwa nao Hillary.
Kwa sasa Hillary ni mtangazaji katika Shirika la Utangazaji la Uingereza (BBC) lenye makao yake makuu, jijini London.
 
Charles Hillary ‘Chalz Hillary’.
Mwandishi mmoja mwandamizi aliyekataa jina lake kutajwa, alisikika akisema; “Nilimsikia Charles Hillary akihojiwa BBC, alilia sana, akasema lazima aje amzike rafiki yake, lakini mpaka sasa sijamuona. Masikini, kama namuona vile, atakuwa na hali mbaya.”
Mwingine alisema: “Inawezekana amechelewa ndege lakini kama atafanikiwa kuja, anaweza kukodisha ndege ndogo ikamuwahisha  Tarime kwenye mazishi, maana anazikwa

HESHIMA
Watangazaji na wadau wa habari nchini waliofika viwanjani hapo waliipongeza serikali kwa heshima kubwa waliyompa marehemu Nyaisangah kwa kuomba shughuli za kuagwa kwa mwili wake ifanyike pia Dar es Salaam, ambako alikuwa na marafiki wengi.

Mgeni rasmi alikuwa ni Makamu wa Rais, Dk. Ali Gharib Bilal ambaye alitoa salamu zake za rambirambi na kuwataka wanafamilia na wanahabari wote kuwa na moyo wa subira katika kipindi hiki kigumu.
VINGOZI WENGINE
Mbali na Dk. Bilal, vingozi wengine waliohudhuria shughuli hiyo ni pamoja na Mbunge wa Hai na Mwenyekiti wa taifa we Chadema, Freeman Mbowe, Mkuu wa Wilaya ya Bahi, Betty Mkwasa na viongozi wengine.

Mbali na hao, Mwenyekiti wa wamiliki wa vyombo vya habari (MOAT) Dk. Reginald Mengi, Mwenyekiti wa Jukwaa la Wahariri, Absalom Kibanda, John Kitime ambaye aliwawakisha wanamuziki wote na Mkurugenzi wa Aset, Asha Baraka.
WATANGAZAJI 
Ukiacha waandishi wa habari wa magazeti mbalimbali waliohudhuria, pia walikuwepo watangazaji wengi wa kizazi cha sasa na wale waliowahi kufanya kazi na marehemu Radio Tanzania Dar es Salaa (RTD – sasa TBC Taifa) na Radio One.
Baadhi yao ni pamoja na Rainfred Masako, Mikidadi Mahamud, Enock Ngombare Mwiru, Misanya Bingi, Masoud Masoud, Abdallah Mwaipaya, Betty Mkwasa, Godwin Gondwe, Issac Gamba, Allan Lawa na Abdallah Majura.
SAFARI YA TARIME
Baada ya shughuli ya kumuaga Uncle J, taratibu nyingine ziliendelea ambapo alitarajiwa kusafirishwa kwa ndege ya kukodi kwenda Tarime, Mara kwa maziko yaliyopangwa kufanyika juzi Jumatano.

Thursday, 24 October 2013

MAMA KANUMBA ATAKA MCHUNGAJI AKAMATWE


by zangii ze icon
Stori: zangii koroboy
SIKU chache baada ya mchungaji aliyejitambulisha kwa jina moja la Mayanga kuibuka na kudai ndiye amewaua Steven Kanumba na Hussein Mkiety ‘Sharo Milionea’, mama mzazi wa Kanumba, Flora Mtegoa ametaka jamaa huyo akamatwe mara moja na kufikishwa kwenye vyombo vya dola.
Mchungaji Mayanga (mwenye kipaza sauti) akitoa ushuhuda kuwa ndiye aliyewaua Steven Kanumba na Hussein Mkiety ‘Sharo Milionea’.
Mbali na kudai kumuua Kanumba na Sharo, Mchungaji Mayanga alidai kabla ya kuokoka kuwa alihusika na vifo vya watu milioni 605 wakiwemo wasanii wa Kundi la Five Stars wapatao 14 na mwanamuziki James Dandu ‘Mtoto wa Dandu’ kwa njia za kichawi.
Mara baada ya gazeti la Amani toleo namba 782 la Oktoba 17, mwaka huu kuripoti habari hiyo, mama Kanumba alipelekewa nakala yake nyumbani ambapo baada ya kuisoma, ndipo alipoona kuna kila sababu ya mchungaji huyo kukamatwa kwa kuwa atakuwa amehusika moja kwa moja na kifo cha mwanaye Kanumba. “Mama Kanumba alipata mshtuko mkubwa siku ile alipoliona lile gazeti, maskini alikuwa tayari ameanza kusahau machungu ya kuondokewa na mwanaye,” kilisema chanzo kilicho karibu na mama Kanumba.
Mama mzazi wa Kanumba, Flora Mtegoa.
Mara baada ya chanzo hicho kupenyeza habari hizo, paparazi wetu alimtafuta mama Kanumba ili kumuuliza alipokeaje habari za mchungaji huyo ambapo alipopatikana, alitiririka; “Naiomba serikali imkamate huyo mchungaji, maana yeye si amesema amemuua mwanangu, sasa iweje aendelee kutanua mtaani wakati ameweka wazi kuwa amemuua mwanangu. “Imeniuma sana, ameamsha machungu ambayo tayari nilianza kuyasahau. Huyo mchungaji akamatwe na sheria imchukulie hatua stahiki,” alisema mama Kanumba.
 
Marehemu Steven Kanumba.
Hata hivyo, katika ushuhuda alioutoa mchungaji huyo, alijitabiria kuwa ipo siku atakamatwa na kufungwa kutokana na siri za vigogo ambao aliwapa utajiri kwa nguvu za giza. “Nina siri za watu wengi sana, nikiwaambia mtaogopa na nchi itatikisika. Najua siku moja watu watanikamata na kunifunga pingu kwa siri nilizonazo, lakini kamwe siogopi kwa kuwa Bwana ameniongoza,” alisema.
Juzi gazeti hili lilifanya jitihada za kumtafuta mama Sharo Milionea, Zainabu Mkiete lakini hakupatikana kwani simu yake iliita bila ya kupokelewa. Mchungaji huyo alipotafutwa naye simu yake iliita bila kupokelewa.

SOMA HABARI YA MCHUNGAJI ALIYEDAI KUWAUA SHARO, KANUMBA: HAPA

JOKATE: DIAMOND ALITAKA TUZAE


by zangii zen icon
Stori: Mwandishi Wetu
MTANGAZAJI maarufu Bongo, Jokate Mwegelo ‘Kidoti’ amefunguka kuwa aliyekuwa mpenzi wake, Nasibu Abdul ‘Diamond’ alitaka wazae kipindi walipokuwa wapenzi.
Jokate Mwegelo ‘Kidoti’.
Jokate alifunguka hayo juzikati alipokuwa akifanya mahojiano maalum na mapaparazi , pamoja na kufunguka mengi, alibainisha kuwa Diamond huwa anapenda watoto kwenye uhusiano.
Nasibu Abdul ‘Diamond’.
“Mh! Diamond anapenda kuzaa, tena siyo kwangu tu wanawake wake wote huwa nasikia anataka kuzaa nao,” alisema Jokate.

WATANZANIA WANUSURIKA KIKAANGONI TUSKER PROJECT FAME


WASHIRIKI wanaowakilisha nchi ya Tanzania katika mashindano ya Tusker Project Fame msimu wa sita yanayofanyika nchini Kenya wamenusurika kuingia kikaongoni wiki hii.

Washiriki hao walionusurika kuingia katika kikaango hicho ni Hisia, pamoja na Angel, ambapo wameonesha hali ya matumaini ya kuendelea kuwepo na kufanya vizuri katika mashindano hayo.

Washiriki walioingia katika kingao hiko ni pamoja na Fess (kenya), Jennifer (Kenya),  Mishel (Kenya)Undercover Brother (Uganda), hali inayoonesha hati hati ya washiriki wa nchi ya Kenya.

Akielezea sababu ya washiriki hao kuingia katika kikaangoni 'Probation' jaji mwenye machachari Ian Mbugua alieleza kuwa shindano hilo halitafuti wasanii wa kawaida bali wenye vipaji na uwezo mkubwa zaidi Afrika Mashariki.

"Kwao hiyo  ni changamoto kuingia ndani ya probation mashindano haya hatutafuti wasanii wa kawaida tu ,bali tunatafuta wasanii wenye uwezo mkubwa, hivyo ili kujitoa kikaangoni lazima waongeze juhudi" alisema Ian

Wema Sepetu atumia milioni 13 kuibadili ngozi yake akiwa China baada ya kuharibiwa sana na Mkorogo


IMEVUJA! Kumbe ile safari ya nchini China ya Miss Tanzania 2006, Wema Sepetu ‘Madam’ lengo lilikuwa kubadili ngozi ya mwili wake katika mwonekano mpya ambayo ilishaharibika kwa mkorogo.
 
Wema Sepetu ‘Madam’.
 
Kwa mujibu wa chanzo chetu makini, staa huyo aliingia nchini humo na mdogo wake aitwaye Bite ambaye kazi yake kubwa ilikuwa kufanya mawasiliano na nyumbani, Tanzania endapo lingetokea baya wakati wa zoezi hilo.
 

KWA NINI ALIAMUA KUDILI NA NGOZI?
Mpashaji wetu aliliambia Amani kwamba, Wema alichoshwa na ‘vijembe’ vya watu mbalimbali wakiwemo wabaya wake kuwa ngozi yake imebabuka kwa kutumia mkorogo kupitiliza.
 
Miguu ya Wema Sepetu ‘Madam’ kabla ya kubadili ngozi.
 
“Kuna wakati Wema alikuwa akikosa amani kutokana na maneno ya watu, wengine waliokuwa wakimrushia vijembe ni masupastaa wenzake, ndiyo maana akaamua kwenda China kubadili ngozi yake iwe na mwonekano mpya,” kilisema chanzo.

Habari zaidi zilidai kwamba, supastaa huyo hakupenda kabisa Wabongo wajue kuwa yupo China kubadili ngozi, hata baadhi ya magazeti yalipoandika amekwenda kujirusha na msanii wa Bongo Fleva, Nasibu Abdul ‘Diamond’ alimshukuru Mungu siri yake imesitirika.

UBADILISHAJI WA NGOZI WATUMIA SAA 12
Kwa mujibu wa chanzo chetu, Wema aliingia kwenye kliniki ya ngozi katikati ya mwezi Oktoba, saa 3:12 asubuhi na shughuli ikamalizika saa 2:25 usiku.
 
“Alikaa kliniki toka saa tatu na dakika kumi na mbili asubuhi hadi saa mbili na dakika ishirini na tano usiku,” kilisema chanzo.
 
MADAKTARI WAMWONYA
Habari zaidi zinaeleza kuwa, madaktari waliokuwa wakimfanyia zoezi hilo walipomaliza walimuonya kutorudia tena kutumia mikorogo au aina yoyote ya losheni zenye kubabua ngozi, kama vile carolite.
 
SEHEMU ZILIZOHARIBIKA SANA
Kwenye mwili wa Wema, sehemu zenye mikunjo kama nyuma ya magoti, kukaribia makwapa, mapajani na mbele ya viwiko ndizo ziliongoza kwa kuharibika hali iliyokuwa ikimfanya mara nyingi ashindwe kuvaa sketi za vimini.
 

SHILINGI MILIONI 13 ZAYEYUKA
Katika zoezi hilo, Wema ambaye pia ni msanii wa filamu za Bongo na bosi wa Kampuni ya Filamu ya Endless Fame Production ya jijini Dar, ametumia shilingi za Tanzania, milioni 13 ikiwa ni pamoja na nauli yake na Bite kwenda China na kurudi, malazi na chakula.
 
APEWA DAWA YA KUZUIA KUZEEKA MAPEMA
Baada ya ubadilishaji huo wa ngozi, Wema alipewa dawa ambazo zitamsaidia kutozeeka mapema.
 
AONYWA MATUMIZI YA SIGARA NA KUTOLALA KWA WAKATI
Mbali na dawa hizo, staa huyo alionywa na matumizi ya sigara aina yoyote ile na kujipanga upya kwenye suala la kulala mapema ili apate usingizi wa kutosha.
 

MENEJA WAKE ATINGA CHINA KUHAKIKI NGOZI
Habari zaidi zikawekwa wazi kwamba, Wema alimwita meneja wake, Martin Kadinda kwa lengo la kuhakiki mwonekano mpya wa ngozi ya staa huyo.
 
Juzi, Amani lilimtafuta Dk. George wa zahanati maarufu ya Sino iliyopo Sinza Mapambano (Kwawachina) ambapo alisema warembo wengi hubadili ngozi kwa mtindo wa plastic surgery, mara nyingi sehemu yenye mikunjo au kuharibika hukatwa na kuvutwa, kama mtu alishaanza kuzeeka huonekana kijana.
 
“Nchi maarufu kwa kubadili ngozi ni Thailand, lakini China na Afrika Kusini zimeanza  kutoa huduma hiyo.
 
“Hapa nchini bingwa wa masuala ya ngozi ni Profesa Masawe, zamani alikuwa Muhimbili kwa sasa ana kituo chake upanga Dar,” alisema Dk. George.
 
Kuhusu madhara, Dk. George alisema hayako wazi sana inategemea maisha ya mtu ya kila sikiu.

MENEJA WA WEMA AZUNGUMZA
Baada ya gazeti hili kuzinyaka habari hizo, lilimtafuta meneja wa Wema, Martin Kadinda alipoulizwa alikiri kwenda China kwa ajili ya kuhakiki mwonekano mpya wa ngozi ya ‘Beautiful Onyinye’ huyo na kusema kuwa ilikuwa lazima bosi wake afanyiwe hivyo kwa sababu bosi ni kioo cha jamii.
 
“Unajua Wema ni kioo cha jamii, hivyo si vyema watu kumsema kwa kitu kidogo kuhusu ngozi yake kwani hata yeye alikuwa hapendezwi nayo. Lakini nashukuru sana kwa sasa ana mwonekano mpya wa ngozi.

“Nilikwenda kuhakikisha kama ngozi yake kwa sasa inaweza kuwa na mwonekano mpya, ni kweli wamefanikiwa madaktari. Wamempa masharti kadhaa, kama kulala sana,  lakini pia wamempa dawa nyingine,” alisema Kadinda.
 

WEMA MWENYEWE SASA
Baada ya kuzungumza na Kadinda, Amani lilimuendea hewani Wema ili kumsikia na yeye kuhusu kubadili ngozi nchini China.

Amani: Mambo Wema, za China?
Wema: Salama tu, niambie.
 
Amani: Hapa kuna habari kuwa safari yako ya China ilikuwa kwa ajili ya matengenezo ya ngozi yako, vipi ni habari za kweli?
Wema: Ah! Sasa ngozi yangu imekuaje kwani?

Amani: Inasemekana una mwonekako mpya wa ngozi, ile ya kwanza hukuipenda kwa sababu ya kujeruhiwa na mkorogo.
Wema: (kimya kidogo) oke, sikupenda kulizungumzia hilo kwa sasa lakini ndiyo hivyo kama ulivyosikia.

Amani: Unaweza kuniambia ni shilingi ngapi umetumia?
Wema: Mh! Mbona unanikaba koo jamani? Kama shilingi 
milioni 13 pamoja na gharama za usafiri.

Amani: Nashukuru sana Wema.
Wema: Karibu sana.

Chanzo: Gazeti la Amani, toleo la leo

Wastara Juma afichua siri.....Adai kioo kilimfanya amvulie nguo SajukiWastara   amefichua  siri kwamba kioo ndicho kilisababisha aanzishe uhusiano wa mapenzi na marehemu Juma Issa Kilowoko ‘Sajuki’ aliyefariki Januari 2, mwaka huu..
 
Wastara aliweka bayana kuwa marehemu Sajuki ambaye alikuwa mumewe, hakuwahi kumtongoza lakini kioo ndiyo kilikuwa chanzo kilichosababisha wajikute wameingia dhambini kwa mara ya kwanza.
 
Akizungumza na mpanda fm, Wastara alisema kuwa siku hiyo walikuwa wakifanya mazoezi ya filamu moja (hakutaja jina) nyumbani kwake na Sajuki alikuwa muongozaji wa sinema hiyo.
 
“Ilikuwa ni usiku wa manane tukiwa nyumbani kwangu tukifanya mazoezi ya filamu moja, sasa ilikuwa ni scene ya mapenzi tukawa mbele ya kioo huku tumekumbatiana.
 
“Tukaendelea hivyoo, mmh! Sasa tulivyokitazama, tukahisi tunaendana. Tukaendelea kujifanyia tathmini na ghafla tukajikuta tunafanya kweli, kioo kilisababisha tukajikuta tunafanya mapenzi,” alisema Wastara kwa uso wa aibu..