Monday 16 December 2013

MWANA KABENDE FATAKI ASHUSHA KIPIGO KIKALI KWA BONDIA TOKA DAR

by rahim kassonga (La captain)

Bondia FATAKI toka Mpanda juzi alishushia kipigo cha nguvu bondia Tadeo toka Dar es salaam kwa kumtwanga kwa KO katika raundi ya pili tu tena sekunde za mwanzoni.

Pambano hilo ambalo ni la kwanza kufanyika mkoani Katavi lilisimamiwa na shirikisho la ngumi za kulipwa nchini TPBO.

Said Kassim Chaku ambaye pia ni katibu wa TPBO ndio alikuwa mwamuzi wa pambano hilo ambalo lilitangulia na mapambano mengine mawili na burudani mbalimbali zikiwemo muziki toka kwa vijana wa mkoani katavi na mchezo wa TAI CHI

Majaji wa mapambano yote matatu walikuwa ni Steven Monela bondia na mwanajeshi mstaafu na Rey Mwanauta wote kutoka Katavi
maandalizi ya pambano glove zikiwa tayari kwa ajili ya pambano

ulingo uliandaliwa vema

wasanii D-touch na D-zela wakifanya yao

Ally Bizo akishambulia jukwaa


mkurugenzi wa Pamoja FM Emmanuel mallack akitoa neno 

Balbel King akifanya yake

Balbel King

Bondia kulwa akijiandaa kucheza pambano la utangulizi na Benjamini


Benjamin akiwa tayari kumkabili kulwa



Refarii said Chaku akitoa maelekezo kwa mabondia kabla ya pambano


Ngumi jiwe shurti ukunje sura- chezea masumbwi wewe






Konde sharti litokee mbali

sio kama nakwepa bali navuta kasi ya konde

MC kelly B akijumlisha hesabu na refa CHAKU

benjamin ameshinda kwa pointi 39 dhidi ya 38 za mpinzani wake kwenye uzito wa unyoya


Pambano la pili ambapo Oswald mwenye bukta nyekundu akipambana na Elfaz mwenye Blue

refa yupo makini kwelikweli




Oswald aliibuka kidedea kwa pointi 40 dhidi ya 36 za mpinzani wake

mambo ya TAI CHII

Radical Mnyama akifanya unyama jukwaani, funika mbayaaaaa

kazi ilikuwepo Radical aliwasha moto vibaya yaani mpaka baaaasiiiiii

mwana Kabende Fataki akiingia na wapambe wake

Add caption

Simon Tadeo kama Tyson atoki katikati anakufuata tu

Makonde yaliendelea

Tadeo akijaribu kuinuka bila ya mafanikio baada ya kupokea konde nene toka kwa Fataki

King FATAKI akitia mbwembwe baada ya kumaliza mpinzani wake kwenye raundi ya pili

refa akitangaza mshindi

Steven Monela kocha wa Fataki akimpongeza kijana wake

Ndondi sio ugomvi, baada ya kubondwa mnakuwa marafiki kama kawa, fair play


Fataki akipongezwa na mashabiki wake



Fataki akiwashukuru mashabikimkwa sapoti yao



La Captain akiwa kazini 





wasanii radical na ally bizo wakimpongeza kaka yao fataki

Wednesday 4 December 2013

TABU LEY ROCHEREAU : PROFILE

by zangii ze icon


Tabu Ley: Mshumaa uliozimika kimyakimya *Aacha watoto 68 akiwa na miaka 76

JINA KAMILI : Pascal-Emmanuel Sinamoyi Tabu, ni mwanamuziki nguli wa Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo (DRC).

JINA LA KIMUZIKI : Maarufu kwa jina la Tabu Ley Rochereau.

MWANAMUZIKI WA AINA GANI? Alikuwa ni mwanamuziki wa miondoko ya Afrika ya aina ya Rhumba

AMEFARIKI : Amefariki Dunia Novemba 30, mwaka huu

AMEZALIWA : Tabu Ley alizaliwa Novemba 13, kati ya mwaka 1937 katika mji wa Bagata kwenye nchi iliyokuwa ikijulikana kama Congo ya Ubelgiji (Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo).

ANAWATOTO WANGAPI? Anawatoto 68 ambao amezaa na wanawake tofautitofauti.

SAFARI YAKE YA MUZIKI : Alikuwa kiongozi wa bendi ya muziki wa dansi iitwayo Orchestre Afrisa International na alikuwa mmoja wa waimbaji wa Afrika wenye mvuto na mtunzi mahiri.

ALIFANYA VITU GANI KUBORESHA MUZIKI WAKE : Akiwa pamoja na mpiga gita mashuhuri Dkt. Nico Kasanda, Tabu Ley alikuwa mwasisi wa mtindo wa soukous (Rumba ya Afrika) na muziki wake aliufanya kuwa wa kimataifa kwa kutia vionjo vya muziki wa asili wa Congo na rhumba la Cuba, Caribbean na Latin America.

MTU MASHUHURI WA CONGO : Tabu Ley au ukipenda Rochereau, anaelezewa kama 'mtu mashuhuri' wa Congo ambaye, pamoja na Rais Mobutu Sese seko, waliweka historia ya Afrika katika karne ya 20."

JINA ALILOPEWA KUTOKANA NA KAZI YAKE : Kutokana na umahiri wake katika muziki wa rhumba, Tabu Ley aliwahi kupewa jina la "Elvis wa Afrika" na gazeti la 'Times' la Los Angeles nchini Marekani.

MBALI NA MUZIKI ALIKUWA MWANASIASA : Baada ya kuangushwa utawala wa Mobutu, Tabu Ley pia aliingia katika siasa.

JUMLA YA NYIMBO ALIZOTUNGA : Wakati wa enzi zake, Tabu Ley aliweza kutunga nyimbo mpaka 3,000 na kutoa albamu 250.

ALIANZA MUZIKI LINI?: Tabu Ley au Rochereau, alianza kazi ya muziki mwaka 1956 wakati alipoimba pamoja na Joseph Kabasele Yampanya 'Pepe Kalle' akiwa na bendi yake ya African Jazz.

Baada ya kumaliza kidato cha sita, Tabu Ley aliamua kuwa mwanamuziki wakati wote. Tabu Ley alitoa wimbo uitwao 'Cha Cha' kusherehekea uhuru wa Congo kutoka Ubelgiji mwaka 1960.

ALIFANYA MUZIKI NA WASANII GANI? Wimbo huu wa 'Cha Cha' ulitungwa na Pepe Kalle, ambapo ulimpaisha Tabu Ley na kupata umaarufu kwa haraka sana. Tabu Ley alibaki na bendi ya African Jazz mpaka mwaka 1963 wakati yeye na Dkt. Nico Kasanda walipounda bendi yao, African Fiesta.

ALIFUNGUA BENDI: Miaka miwili baadaye, Tabu Ley na Dkt. Nico walisambaratika na Tabu Ley akaunda bendi yake ambayo ilikuwa ikijulikana kama African Fiesta National, na pia ilijulikana kama African Fiesta Flash.

Bendi ya African Fiesta National ilikuwa moja ya bendi zenye mafanikio makubwa katika historia ya muziki wa Afrika, ikirekodi nyimbo kali kama 'Afrika Mokili Mobimba'.

WIMBO GANI ULIOVUNJA REKODI YA MAUZO ? Wimbo Wa 'Afrika Mokili Mobimba' ilivunja rekodi ya mauzo kwa kuuza nakala milioni moja mwaka 1970.

Wakati huo, Papa Wemba na Sam Mangwana walikuwa miongoni mwa wanamuziki waliotakatisha kundi la African Fiesta National.

JINA GANI LA JUKWAA ALILOCHUKUA? Tabu Ley alichukua jina la jukwaa la 'Rochereau' kutoka kwa Generali wa Jeshi la Ufaransa, Pierre Denfert-Rochereau, ambaye alisoma naye shule moja na kulipenda jina lake.

SAFARI YA BENDI : Mwaka 1970, Tabu Ley aliunda bendi ya Orchestre Afrisa International, Afrisa ikiwa ni mchanganyiko kati ya jina Afrika na Isa, alama ya muziki wake.

Akiwa pamoja na Franco Luambo Makiadi wa TPOK Jazz, Afrisa ikawa moja ya bendi kubwa barani Afrika. Walirekodi vibao kama 'Sorozo', 'Kaful Mayay', 'Aon Aon', na 'Mose Konzo'.

ALIVUMBUA VIPAJI VIPYA : Katikati ya miaka ya 1980, Tabu Ley aliweza kugundua kipaji cha mwanadada mwimbaji na mcheza shoo, M'bilia Bel, ambaye alichangia sana kuipaisha bendi ya Orchestre Afrisa International.

M'bilia Bel alikuwa mwimbaji mwanamke wa kwanza wa muziki wa soukous, ambaye alijipatia umaarufu Afrika yote.

MAISHA YA MAPENZI : Tabu Ley na M'bilia Bel baadaye walifunga ndoa na kupata mtoto mmoja. Mwaka 1988 Tabu Ley alimuibua mwanamuziki mwingine wa kike ajulikanaye kama Faya Tess.

Kuona Faya Tess ananyanyuka kwa kasi,  M'bilia Bel aliamua kuondoka katika bendi hiyo na kuendelea kufanya vizuri katika kazi za muziki akiwa kivyake.

Baada ya M'bilia Bel kuondoka, mvuto wa bendi ya Afrisa pamoja na ule wa wapinzani wao TPOK Jazz uliendelea kufifia kutokana na mashabiki kugeukea mtindo mpya wa muziki wa soukous wenye kasi zaidi.

Baada ya utawala wa Rais Mobutu Sese Seko kuanzishwa katika Congo, Rochereau akachukua jina la 'Tabu Ley' kama sehemu ya kampeni ya Mobutu kuwafanya wananchi wa Zaire kuwa na majina ya asili.

SABABU ZILIZOMFANYA ATOROKE: Hata hivyo, mwaka 1988 Tabu Ley alitoroka na kwenda kuishi uhamishoni nchini Ufaransa.

Mwaka 1985, Serikali ya Kenya ilipiga marufuku muziki wa kigeni kuchezwa kwenye Redio ya Taifa.

Baada ya Tabu Ley kutunga wimbo 'Twende Nairobi', aliouimbwa na M'bilia Bel, kumsifu Rais wa Kenya wakati huo, Daniel Arap Moi katazo hilo mara moja likaondolewa.

Mapema 1990 Tabu Ley aliishi kwa muda mfupi Kusini ya California nchini Marekani. Alianza kutengeneza muziki wake kuwa wa kimataifa zaidi na kuingiza lugha ya Kingereza na kuongeza staili za kucheza kuwa za kimataifa zaidi kama vile Samba.

Rochereau aliona kupata mafanikia kwa kutoa albamu kama Muzina, Exil Ley, Africa worldwide na Babeti soukous.

Utawala wa Mobutu ulipiga marufuku albamu yake ya mwaka 1990 iitwayo 'Trop, C'est Trop' ambayo aliiona kama inamchafua. Mwaka 1996, Tabu Ley alishiriki katika albamu iitwayo Gombo Salsa iliyotolewa na bendi ya Africando.

Wimbo wa 'Paquita' kutoka albamu ya Gombo ni moja ya wimbo uliowahi kurekodiwa mwishoni mwa miaka ya 1960 na bendi ya African Fiesta.

Wakati Rais Mobutu Sese Seko alipoondolewa madarakani mwaka 1997, Tabu Ley alirudi Kinshasa na kupewa Uwaziri katika serikali mpya ya Rais Laurent Kabila.

Kutokana na kifo cha Laurent Kabila, Tabu Ley kisha alijiunga na Bunge teule la mpito lililoundwa na Joseph Kabila, mpaka lilipovunjwa baada ya kuundwa kwa taasisi za mpito.

CHEO ALICHOPATA : Novemba 2005, Tabu Ley aliteuliwa kuwa Kaimu Gavana Kinshasa, nafasi aliyopewa kutokana na chama chake cha Congolese Rally for Democracy, kutokana na makubaliano ya amani 2002.

AMESHWAHI KUWA WAZIRI : Tabu Ley aliyewahi pia kuwa Waziri wa Utamaduni, inasemekana amezaa watoto 68 na wanawake tofauti tofauti, akiwemo rapa mashuhuri wa Ufaransa, Youssoupha.

Rochereau amekufa akiwa na umri wa miaka 76 katika Hospitali ya Mtakatifu Luc mjini Brussels, Ubelgiji ambako alikuwa akipata matibabu ya ugonjwa wa kiharusi uliomkumba mwaka 2008.