Tuesday 1 July 2014

TID amtusi Ray C baada ya kumuomba wazungumze, "B**ch leave me alone...'


Mmiliki wa Top Band, TID amegeuka mbogo baada Ray C kumuomba kupitia Instagram wazugumze.
Mwimbaji huyo ambaye anadaiwa kuwa mmoja wa wasanii wanaotumia dawa za kulevya huenda alihisi Ray C anataka kumletea habari za kumsaidia kuachana na matumizi ya dawa hizo kupitia Methadone.
“Come let’s talk Tid ur the best musian in east Africa pls lets talk @tidmnyama.” Aliandika Ray C.
Ingawa Ray C hakufafanua katika comment yake aliyoiweka kwenye post ya picha ya TID inayotambulisha Refix ya wimbo wake ‘Asha ‘ uliofanywa na Lamar,  TID aliporomosha matusi akimtaka aachana nae kabisa.
“B*tch leave me alone am not ur type also I don’t need shit from you. Ur mistake is urs nakuomba can u just f**k off, help ur boyfriend, I have never liked you, full stop.”Ameandika TID
Hata hivyo mashabiki walioandika comments zao walimshambulia tena TID kutokana na kile alichomjibu Ray C ambaye hakutaja kabisa nia ya kutaka kuzungumza na Mnyama TID.

TRA waanza rasmi ukaguzi na urasimishaji wa kazi za muziki na filamu


Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) imetangaza kuanza rasmi ukaguzi na urasimishaji wa kazi za muziki na filamu kwa kubandika stika maalum kwenye kazi za wasanii hao.
Taasisi za serikali zilizopewa jukumu la kurasimisha kazi za sanaa ya muziki na filamu zimeanza kukagua na kukamata kazi zote ambazo hazina sifa ya kuuzwa ndani au kupelekwa nje ya nchi. 
Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na TRA kwa kuzingatia sheria ya ushuru wa bidhaa iliyofanyiwa marekebisho mwaka 2012 na kupitishwa kwa kanununi zake mwaka 2013, inamtaka kila mfanyabiashara wa kazi za muziki na filamu kuhakikisha kuwa bidhaa yake ina stempu ya ushuru wa bidhaa inayotolewa na TRA kabla ya kusambazwa.
Taarifa hiyo imefafanua kuwa wasanii wote wa muziki wanapaswa kupitia hatua zote za awali kwa kuipeleka kazi yao BASATA, COSOTA kabla ya kuifikisha TRA kwa ajili ya kununua stempu/stika maalum ya utambulisho wa ushuru.
Kwa wasanii wa filamu wanapaswa kupitisha kazi zao kwenye bodi ya filamu na COSOTA kabla ya kufika TRA kununua stika.
Imeeleza kuwa zoezi hilo litafanyika kwa kazi zote za ndani na za nje ya nchi na kwamba zitatofautiana rangi tu za stempu/stika zitakazoitambulisha.
-Filamu kutoka nje ya nchi-rangi ya kijani (green)
-Muziki toka nje ya nchi –rangi bluu (blue)
=Filamu zinazotengenezwa ndani ya nchi-Zambarau (violet)
-Muziki wa ndani ya nchi –rangi ya pink
“Stempu hizi zitapatikana ofisi za idara ya fedha, makao makuu TRA. Kila kazi yaani CD, DVD au kanda zitatolewa stempu mbili zenye namba moja katika mtiririko maalum wa namba (serial number). Stempu moja hubandikwa katika kasha na nyingne kwenye CD/DVD au Kanda. Utaratibu unamtaka mhusika anaehitaji stempu kuwasilisha maombi tofauti kwa kila kazi husika. Hairuhusiwi kuwekwa stempu zilizoombwa kwa ajili ya kazi moja kwenye kazi nyingine hata kama kazi hizo zimetolewa na mzalishaji au msambazaji mmoja.” Inaeleza taarifa hiyo.

Mke wa T.I amkimbia Floyd Mayweather kwenye BET Red Carpet


Mke wa rapper T.I, Tiny hakutaka ugomvi mwingine utokee kwenye tuzo za BET baada ya kumkimbia kiaina bondia Mayweather aliyekuwa anajaribu kumuita.
Video iliyochukuliwa na na Hip Hollywood inamuoenesha Floyd Mayweather akijaribu kumuita Tiny wakati wapo wote kwenye red carpet, lakini Tiny anaonesha kushitukia na kukatisha interview yake haraka kisha akaondoka.
Bado Mayweather alionesha nia ya kutaka kumgusa mkono lakini Tiny aliendelea kuchapa mwendo na kujiunga na T.I.
Hata hivyo baada ya kuingia ukumbini, mchekeshaji Chris Rock ambaye alikuwa MC  aliendelea kufanya utani kuhusu ugomvi wa T.I na Mayweather uliotokea mwezi mmoja uliopita baada ya Mayweather kuonekana akiwa na Tiny kwenye picha kadhaa kitendo ambacho hakikumfurahisha kabisa rapper huyo.

Nakaaya: Baada ya kupata mtoto amenipa nguvu ya kufanya muziki tena


Mwimbaji aliyefanya vizuri kwenye game na nyimbo kama Mr. Politician, Nakaaya Sumari amerudi tena kwenye game na kuachia wimbo mpya unaoitwa Blessing ambao amesema ni maalum kwa ajili ya mtoto wake.
Akiongea na Bongo Dot Home ya 100.5 Times Fm, Nakaaya ambaye aliwahi kushiriki mashidnano ya kuimba ya Tusker Project Fame, amesema kuwa alikuwa amekata tamaa na muziki lakini baada ya kumpata mwanae amepata nguvu ya kurudi tena kwenye game.
“Baada ya kumpata mwanangu imenipa changamoto na imenipa motisha ya kufanya muziki wangu tena. Kwa sababu kuna time ilifika nikawa nimeshindwa kufanya muziki tena nilikuwa sitamani tena kufanya muziki na nilikuwa nimeachana nao.” Amesema Nakaaya. #
Akifafanua kuhusu hilo amesema aliona kuwa ni bora afanye muziki wake ambao mwanae atakapokuwa na kuanza kuelewa atajivunia badala ya kusimuliwa kuwa mama yake alikuwa anafanya muziki.
Amesema tayari ameshakamilisha albam yake aliyoipa jina la Blessing na wanasubiri wakamilishe video na kisha waendelee kuachia wimbo mmoja mmoja.

Nikki Mbishi aeleza sababu za kuisogeza mbele project ya Ufunuo na collabo aliyofanya na Collo


Rapper wa Tamaduni music, Nikki Mbishi ambaye aliwafanya mashabiki wake waisubiri kwa hamu siu ya June 16 ambayo ilikuwa inaonekana kwenye akaunti zake za Twitter na jina project yake ya ‘Ufunuo’.
Nikki Mbishi ameeleza kuwa tarehe hiyo ilikuwa tarehe ya kuzaliwa ya mwanae Malcom amapo alikuwa ameiweka kama siku muhimu kwake.
Hata hivyo rapper huyo ameeleza kuwa alilazimika kutotoa Ufunuo siku hiyo kwa kuwa rapper mwenzake One The Incredible alikuwa amepanga kauchia mradi wake June 11 kwa hiyo ratiba ingekuwa nzuri kibiashara.
“Ile tarehe ilikuwa tarehe ya kuzaliwa kwa Malcom kwa hiyo niliiweka tu vile lakini nilikuwa najua siwezi kufanya hivyo kwa sababu One pia alitangaza kutoa kazi yake. Kwa hiyo One angetoa tarehe 11 mwezi wa 6 na mimi nikatoa tarehe 16 mwezi wa 6 ingekuwa sio biashara ni utoto kwa kuwa tungekuwa tunashindana sisi wenyewe kuuza.” Amesema Nikki Mbishi.
Hata hivyo, kutokana na sababu zilizo juu ya uwezo wao, One The Incredible pia alishindwa kutoa kazi yake kama ilivyopangwa.
Nikki Mbishi amewaahidi mashabiki wake kuwa mwisho wa mwaka huu ni lazima aitoe albam ya Ufunuo kwa ajili yao.
Katika hatua nyingine, Nikki ameeleza kuhusu collabo waliyofanya na King wa Rap Kenya, Collo kuwa ilikuwa ngoma waliyofanya pamoja mwaka jana na imekaa pending kwa muda mrefu huku kichwani kwake kukiwa na mipango tofauti na kwamba hana uhakika kama ataichia hivi karibuni.

Mashabiki wamshambulia Amber Rose kwa kumtaja Wiz Khalifa kuwa mwanaume mwenye mvuto zaidi duniani


Kuna msemo wa Kiswahili uliozoeleka kuwa muwamba ngoma huvutia kwake. Wazungu wenyewe wanasema uzuri upo kwenye macho ya anaeangalia kitu hicho.
Baadhi ya mashabiki ambao hawaamini hayo yaliyoandikwa hapo juu wamemshambuli kwa kejeli mrembo Amber Rose baada ya kupost picha ya mpenzi wake rapper Wiz Khalifa kwenye Instagram na kumtaja kuwa mwanaume mwenye mvuto zaidi duniani.
“The sexiest man on Earth.” Aliandika Amber Rose.
Wengine walisema kuwa amewatukana wanaume kama Trey Songz.
 “Speaking as a man and an inhabitant of earth I take offence to that statement."  Aliandika shabiki mmoja anaetumia jina la deanxod.
Wengine waliandika comments zenye matusi pia.

Justin Bieber atoa msaada katika ajali ya gari iliyowahusisha watoto wa Mayweather


Justin Bieber aambaye amewahi kuingia katika matukio ya ajali ya gari mara kadhaa, Jumapili iliyopita aligueka kuwa msamalia mwema na kutoa msaada wa haraka kwa watoto wa bondia Floyd Mayweather waliopata ajali ya gari.
Kwa mujibu wa TMZ, muda ambao watoto hao wanapata ajali ya gari huko Los Angeles, Floyd alikuwa kwenye tukio la red Carpet ya tuzo za BET na alipewa taarifa kwa njia ya simu na Justin Bieber.
Inaelezwa kuwa magari mengi yaligongana katika eneo hilo na kuhusisha gari walilokuwemo watoto wa Mayweather.
Justin alikuwa katika eneo hilo na alikimbia kwenye tukio hilo na kuwachukua watoto hao haraka na aliwaeleza polisi kuwa ni watoto wa rafiki yake.
Watoto hao hawakupata majeraha makubwa, mtoto mmoja alichanika kidogo kwenye mdomo wa chini na Justin aliamua kuwafariji kwa kuwaimbia wimbo wake mpya kabla hajawapeleka kwa baba yao.
Inaelezwa kuwa baada ya kuwafikisha watoto hao kwa Floyd. Justin alirudi katika eneo hilo na kuwaarifu polisi kuwa watoto hao wameshafika kwa baba yao.