Thursday 13 November 2014

MAJALIWA RUBUYE KAFUNGUKA YA MOYONI KUHUSU MSHIKAMANO ARTS GROUP

MAJALIWA RUBUYE
afisa mipango wa kundi la mshikamano arts group la mpanda katavi  MAJALIWA RUBUYE,kundi linalo fanya vema kwa sasa hapa katavi,ametoa yake ya moyoni juu ya wale wanao sambaza habari kuhusu kundi hili mahiri na lenye mafanikio makubwa hapa mkoani katavi,
MSHIKAMANO ARTS GROUP

COMEDDY ZA MSHIKAMANO NI HATAREE
WAKI SHOOT MOJA YA VIDEO ZAO

 katika ukurasa wake wa face book mr.rubuye ambaye pia ni muajiriwa wa halmashauri hapa mkani katavi ali funguka haya

Hahahahaaaaaaaa! Nimefurahi sana kwa maswali yako na nimelazimika kukujibia hapa japo wewe umeni in box! Huenda wako wengi wenye maswali kama yako dhidi yangu!
Ki ukweli hata mimi niliisikia hiyo radio interview kama uliivyoiita! Lakini mimi naamini ukitukanana na mtoto wote mtaonekana mna akili za kitoto! Mimi naamini kila palipo na nia njema moyoni kuna mkono wa mungu Na kuhusu Mshikamano Arts Group hawajapoa kama unavyodhani,wanaendelea na harakati kama kawaida kwa sababu fulsa walizonazo kama kundi ni nyingi na zinaongezeka kila siku! Ingawa nimedokezewa kuwa “eti”kuna jitihada za wazi kuwadhoofisha hapa mjini (hahahahaaaa!) Niandikapo post hii wako katika ziara ya maonesho maalumu mkoani Rukwa,walianzia Kakese Mpanda tarehe 7/11 ingawa baadhi yao walilazimika kubakia mpanda kwa ajili ya sherehe za LATCU then wakawafuata wenzao, lakini pia wamefanikiwa kutengeneza tamthiria itakayokuwa ikiruka Azam Two kwa jina la MOTO WA YAKA wakishirikiana na Dodo Arts ya Dar-es-salaam kila siku ya alhamis saa tatu usiku,pia kwa mara ya kwanza wameweza kutengeneza komedi ambayo tunaamini itakuwa gumzo hapa mjini! Na mengine mengi ambayo yako sirini,
Kuhusu makundi ya sanaa mimi sijawahi kuwa na bifu na kundi lolote kwa sababu mimi ni mwanaharakati wa masuala ya kijamii na vijana ndio issue yangu kuu! Nashirikiana na kundi la Mshikamano kwa kua ndio kundi ninalofanya nalo kazi lakini nimejaribu mara kadhaa kuwaunganisha wasanii hapa katavi ili washirikiane na kufanya sanaa kuwa kazi yao na si kuendekeza majungu!
Kimsingi nimekuwa nikiwahimiza wasanii wa mshikamano kufanya sanaa kama mradi wao wa maendeleo na si kufanya sanaa ya mashindano ya nani zaidi! Ukiona mtu anafanya sanaa ili akushinde na aonekane mbele ya jamii kwamba yeye ni mkali kuliko wewe huyo hajitambui achana nae we fanya vizuri ili ulipwe vizuri na kazi yako ndio itakutangaza na jamii itajua nani zaidi hata bila kupiga kelele maana hatuuzi sura ila tunauza kazi yetu ya sanaa ili tujikwamue kiuchumi pia!
Kwa kawaida kundi huwa haliyumbi wanaoyumba ni wanakikundi ndio maana hata Tanzania ipo ingawa mawaziri wana badilika kila mara kutokana na sababu mbalimbali! Mimi kazi yangu ni kuratibu kazi ya vijana na kuhakikisha ndoto zao zinatimia,
Nawasisitiza wasanii wote wa mkoa wetu wa katavi kukaa chini na kufikilia zaidi ni jinsi gani wanajikwamua kiuchumi ili wamudu viwango vya kazi zao na kuleta tija waachane na wababaishaji wachache wanaopenda sifa na kujikweza! Na pia wawe na moyo wa kusameheana kwani riziki ya mtu huja kupitia mtu mwingine hivyo nikijenga chuki na wewe sijui mungu amepanga uwe nani kesho! Pia tutendeane vile vimpendezavyo mungu ili mkono wake uwe mbele ya kazi zetu!
Asante sana na mungu akubariki, ada ya mja hunena “uungwana ni vitendo”
MSHIKAMANO KAZINI

NI HAYO TUU KAZI KWENU WADAU TOA COMENT YAKO HAPA CHINI

Thursday 23 October 2014

MSANII DIAMOND AHOJIWA POLISI, ASALIMISHA MAGWANDA YA JESHI, AACHIWA KWA DHAMANA

MSANII wa Muziki wa Kizazi kipya nchini,Naseeb Abdul  maarufu kama Diamond Platnumz amehojiwa na Jeshi la Polisi baada ya kuonekana na mavazi halisi ya Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) katika Tamasha la Fiesta lililofanyika jijini Dar mwishoni mwa wiki.
Diamond amejikuta hapo  siku moja tu baada ya Meneja wake Babu Tale kukamatwa  jana kwa kuhojiwa na kulala mahabusu kuhusiana na matumizi hayo ya mavazi ya kijeshi katika onyesho la Fiesta.
Habari zinasema Diamond naye alijisalimisha mwenyewe polisi ambako baada ya mahojiano aliachiwa kwa dhamana. Magwanda aliyokuwa nayo aliyakabidi polisi wakati uchunguzi ukiendelea.

Kumekucha!!! HAYA HAPA MAGAZETI YOTE YA LEO ALHAMIS OKTOBA 23,2014-UDAKU,MICHEZO & HARD NEWS


.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.

TAMKO RASMI LA SERIKALI KUHUSU TETESI ZA KUWA NA MGONJWA MWENYE EBOLA NCHINI!

Utangulizi 
Mnamo tarehe 18 Oktoba 2014, Wizara ilipokea taarifa kutoka Ofisi ya Mganga Mkuu wa Mkoa wa Mwanza ya kuwepo kwa mgonjwa aliyehisiwa kuwa na ugonjwa wa Ebola. Mgonjwa huyu aliyekuwa na umri wa miaka 17, jinsia ya Kike na mkazi wa kijiji cha Bupandwa Tarafa ya Kahunda Wilaya ya Sengerema, alilazwa akiwa na dalili za homa kali, manjano, kutokwa na damu sehemu mbalimbali za mwili.
Mgonjwa huyu alilazwa katika Kituo cha Afya Mwangika tarehe 15 hadi 16 Oktoba, 2014 ambapo pia alionekana kuwa vimelea vya ugonjwa wa Malaria kabla ya kuhamishiwa Hospitali Teule ya Wilaya ya Sengerema mnamo tarehe 17 oktoba 2014 na kufariki duniani siku hiyo hiyo muda wa saa 3.30 usiku.
Hata hivyo, mgonjwa huyu hakuwa na historia ya kusafiri kwenda nchi zilizoathirika na ugonjwa wa Ebola na hakuwahi kupokea mgeni kutoka nchi hizo ndani ya siku ya 21 zilizopita.
Hatua zilizochukuliwa ni pamoja na; 
i.Sampuli ya damu ya mgonjwa kwa ajili ya uchunguzi wa Kimaabara ilipokelewa tarehe 18 Oktoba, 2014. Matokeo ya awali dhidi ya magonjwa ya jamii ya ebola yakiwa ni pamoja na Dengue na Chikungunya yanaonyesha kuwa mgonjwa hakuwa na magonjwa haya. Uchunguzi wa kimaabara bado unaendelea na Wizara itatoa taarifa rasmi pindi utakapokamilika.
ii.Mgonjwa alihudumiwa katika chumba maalumu kilichotengwa ambapo wahudumu pamoja na walioshughulikia mazishi yake walivaa vifaa kinga (PPE)
iii.Wataalamu pamoja na ndugu waliomhudumia mgonjwa kabla ya mauti kumfika wametengwa na wapo kwenye uangalizi maalumu
Mwongozo wa utambuzi wa ugonjwa huu (Standard Case Definition) unaeleza kwamba ili mgonjwa aweze kuhusiwa kuwa na ugonjwa wa Ebola anatakiwa akidhi vigezo ifuatavyo:
i. Dalili za awali ni homa kali ya ghafla, kulegea mwili, maumivu ya misuli, kuumwa na kichwa, na kutokwa na vidonda kooni. Mara nyingi dalili hizi hufuatiwa na kutapika, kuharisha,kutokwa na vipele vya ngozi, kwa baadhi ya wagonjwa hutokwa na damu ndani na nje ya mwili
ii.Awe amesafiri kwenda sehemu zilizothibitishwa kuwa na ugonjwa wa ebola ndani ya kipindi cha wiki 3
iii. Kugusa majimaji kutoka kwa mgonjwa, maiti au mnyama anayehisiwa au kuthibitishwa kuwa na ugonjwa wa Ebola.
HitimishoWizara inapenda kuwatoa hofu wananchi kuwa hadi sasa HAKUNA MGONJWA yeyote aliyethibitishwa kuwa na virusi vya ugonjwa wa Ebola hapa nchini. Hata hivyo uchunguzi wa kina wa Kimaabara unaendelea na taarifa itatolewa baada ya majibu kupatikana.

Pinda amtambia Lowassa

JINA la Waziri Mkuu, Mizengo Pinda, limeanza kutumiwa na baadhi ya makada wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) kukusanya na kugawa fedha kwa kile kinachoitwa “mbio wa kusaka urais.”
Taarifa zilizolifikia gazeti hili zinasema kuwa wajumbe hao wamesema mbio za Pinda kusaka urais zimekuwa na kishindo kikuu kwa sababu ya sera yao kwamba “pesa itaongea.”
Baadhi yao wamefika mahali pa kumtambia Mbunge wa Monduli, Edward Lowassa, ambaye naye anatajwa kuwania urais, huku mmoja wa wapambe wake akisema, “Walidhani wao ndio wana pesa tu. Sasa tutawaonyesha kazi.”
Tanzania Daima lina taarifa kwamba Pinda ndiye tishio jipya la Lowassa, na katika hatua ya kwanza ameshauriwa atumie fedha ya kutosha kufikia wajumbe wengi wa Halmashauri Kuu ya Taifa ya Chama Cha Mapinduzi, wanaojulikana kama Wanec.
Inafahamika kwamba, kwa muda mrefu, Lowassa ndiye amekuwa na nguvu kubwa miongoni kwa wanec wa mikoa mingi.
Ili kukabiliana na nguvu hiyo, timu ya Pinda inadaiwa kuteua familia moja yenye madaraka makubwa ya kisiasa jijini Dar es Salaam, kushika mikoba yake. Taarifa zinasema mume akipita huku, mke anapita kule.
“Kazi ya kwanza waliyo nayo ni kulainisha wanec ambao ndio wapiga kura za maoni watarajiwa. Lengo ni kuvuta kasi ya waliomtangulia, ambao walishakuwa na mitandao imara ya wafuasi ndani ya NEC,” anadai mnec mmoja ambaye anadai kushuhudia matukio kadhaa ya makundi ya watu kupewa fedha kwa jina la Pinda.


Habari za ndani zinasema mtandao huo unafadhiliwa na matajiri na wawekezaji kadhaa wanaowekeza katika maeneo nyeti, akisaidiwa na baadhi ya watendaji wa serikali katika wizara nyeti ambayo imekuwa na migogoro mingi kwa miaka tisa mfululizo. Wanakusanya fedha kutoka kwa matajiri hao.
Baadhi ya wawekezaji wanaofahamika hadi sasa ni waziri mmoja mwenye makeke na majivuno na katibu wake mkuu, ambao wanadiwa kukusanya fedha kutoka kwa wawekezaji wa rasilimali za nchi ambazo zimekuwa zinaleta mvutano na utata kati ya serikali na wananchi, kiasi cha kuchafua hali ya kisiasa katika mikoa kadhaa ya Kusini mwa Tanzania.
Yumo pia tajiri mmoja anayemiliki mabasi, mbunge mmoja wa Zanzibar na mzazi wa mbunge mmoja mwenye asili ya Kiasia, ambao wote kwa pamoja ni wawekezaji katika biashara ya sukari.
Zipo taarifa kuwa mkubwa wanayempigania amesaidia kurahisisha wapate vibali ya kuingiza sukari kwa wingi. Wamo pia wamiliki wa super market moja maarufu ambayo imekuwa na utata katika miezi ya karibuni.
Ili kuwasilisha fedha hizo kwa wahusika, zinatumika fursa, sehemu na staili mbalimbali katika kugawiana pesa.
Miongoni mwa matukio makubwa yanayotajwa yanayohusisha wapambe na wanec hao ni haya yafuatayo:
Tarehe 20 Oktoba 2014, katika jengo moja la kisasa, jijini Dar es Salaam, jirani na Hospitali moja maarufu yenye kutafiti na kuibu magonjwa sugu nchini, mke wa mshika mikoba alikodi ofisi ambayo aliitumia kukutana na wanec kadhaa na kuwagawia fedha.
Miongoni mwao ni wanec kutoka Kigoma Vijijini, Shinyanga na Bungeni, ambao kila mmoja walipewa dola za Kimarekani 600, sawa na sh. milioni moja ya Kitanzania.
Majina ya wanec hao tunayahifadhi kwa sasa. Tarehe hiyo hiyo, vijana kadhaa wa UVCCM kutoka Ilala, nao walikutana na mshika mikoba huyo, akawagawia sh. 200,000 kila mmoja.
Tarehe 16 Oktoba 2014, katika majengo ya NHC Dodoma, nyumbani kwa mbuge mmoja wa Viti Maalumu kutoka Singida, mke wa mshika mikoba huyo anadaiwa kupokea sh. milioni 24 kutoka ofisi moja ya umma, iliyo chini ya mabosi hao wa wizara waliotajwa. Inasemekana fedha hizo zililetwa kwa agizo la katibu mkuu husika, baada ya fungu la awali walilokuwa wamesafiri nalo kwenye mabegi kuisha.
Baada ya kupokelewa na mshika mikoba, alikabidhiwa mnec mmoja kutoka Mbozi, akazigawa kwa baadhi ya wanec kutoka Zanzibar.
Tarehe 14 Oktoba 2014, wapambe hao na mshika mikoba walikutana nyumbani mwa kigogo mkubwa serikalini, Masaki, Dar es Salaam, wakawezesha wanec kadhaa kutoka Dar es Salaam, Tanga, Pwani na Zanzibar, kiasi cha sh. milioni moja kila mmoja.
Baadaye, katika hoteli moja maarufu nje kidogo ya mji wa Dodoma, na nyingine maarufu katikati ya mji, katika siku ya kwanza ya kikao cha NEC, wanec wapatao 42 wanadaiwa kupokea sh. 200,000 kila mmoja kutoka kwa mshika mikoba huyo na mkewe.
Kati ya tarehe 15 hadi 18 Oktoba 2014, mshika mikoba huyo na mkewe waligawa fedha kwa wanec kwa viwango vya sh.300,000; 500,000 na 700,000. Makatibu wa Wilaya wanadaiwa kupewa sh.150,000 hadi 300,000.
Tarehe 18 Oktoba 2014, asubuhi kabla ya wajumbe kuondoka, wanec kadhaa kutoka Mkoa wa Kagera wanadaiwa kupokea sh. milioni moja kila mtu.
Hali hii ndiyo ilimfanya Makamu Mwenyekiti wa CCM Phillip Mangula, wakati anawasilisha taarifa ya kamati ya maadili kwenye NEC, akasema kwamba amegundua kuwa pale Dodoma kumezuka ATM mpya. Alionya kuwa wahusika wataitwa na kuonywa.
Kutokana na makeke ya wapambe hawa wanaotumia jina la Pindi kugawa fedha, zipo taarifa kwamba tayari kamati ya maadili imemuita na kumuonya waziri mkuu kuhusiana na tuhuma hizi.
Kauli za wahusika
Gazeti hili lilipomuuliza Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM, Nape Nnauye, kuhusu ukweli wa taarifa hizo, alisema: “Mimi nazisikia kutoka kwako, kama mmeziokota bafuni au chooni mtajua ninyi lakini mimi ndiyo nazisikia kutoka kwako,”
Mnec kutoka Kigoma alipoulizwa kuhusu fedha hizo, alikanusha, lakini alikiri kwamba juzi alikuwa katika jengo jirani na Hospitali ya Ocean Road.
Alisema jengo lile ni la ofisi, na kwamba alienda katika moja ya ofisi ya jengo hilo kwa shughuli zake binafsi. Alikana kukutana na mke wa mshika mikoba huyo, lakini akasisitiza kuwa alikwenda pale kwa shughuli zake binafsi.
Katika hatua ya kujichanganya, Mnec huyo aliuliza kama kuna taarifa zozote zinazomuhusu. Alipoelezwa kuwa zipo bila kujua ni taarifa gani, alianza kujitetea kuwa kwa nafasi yake, yeye ni mtu mdogo asiyeweza kuhusishwa katika makundi ya wawania urais kupitia CCM.
“Mimi ni mtu mdogo sana tena mkulima wa mihogo kutoka Kigoma. Hayo makundi ni ya watu wakubwa. Kwanza hata pombe sinywi sasa nitakaa nao wapi?”alihoji.
Alipoulizwa sababu ya kujitetea kuwa hayupo katika makundi hayo ilihali mwandishi hajamueleza kama habari aliyonayo inahusiana na makundi ya urais, Mnec huyo aliomba kukutana na mwandishi katika hoteli ya Harare Inn, Dar es Salaam, jambo ambalo halikutekelezwa na mwandishi.
Mnec mwingine atokaye Shinyanga, alipoulizwa kuhusu fedha alizopokea juzi, alisema mwandishi amemfananisha na mtu mwingine, kwani yeye hahusiki.
Alipoulizwa ataje mtu aliyefananishwa naye, aliomba mwandishi ampigie simu baadaye kwa kuwa muda huo alikuwa katika mkutano. Jitihada za gazeti hili kumpigia simu hazikuzaa matunda baada ya namba yake kuita bila kupokewa na wakati mwingine simu ilikatwa.
Mnec wa Tabora alidai kwamba hajawahi kufika katika jengo hilo kwa ajili ya kupokea fedha kutoka kwa mke wa mshika mikoba wa Pinda.
Alisema kuwa tangu alipopata ajali hajaweza kufanya shughuli yoyote hata kuhudhuria vikao vya kamati ya bunge vilivyoanza juzi jijini Dar es Salaam, na kwamba kwa muda huo alikuwa katika Hospitali ya Taifa Muhimbili kwa ajili ya kufanyiwa vipimo vya afya.
“Ninyi si mnajua kuwa ninaumwa nilipata ajali ya gari hata gazeti lenu liliandika ajali hiyo sasa iweje niende huko wakati sijaanza kutoka? Lakini nikwambie wewe ni mtu wa pili kunipigia simu na kuniuliza swali hilo wa kwanza ni kaka yangu Hussein nikamueleza kuwa sijaenda kuchukua fedha kwa mtu yeyote yule,” alisema.
Mshika mikoba na mkewe simu zao hazikupatikana kabisa hewani kwa siku nzima ya jana.

UEFA CHAMPIONS::ARSENAL WALEEE WAITANDIKA ANDERCHT GOLI 2 KWA 1