Thursday, 8 May 2014

Sura ya Alicia Keys kuiuza perfume ya Givenchy


Mshindi wa tuzo za Grammy, Alicia Keys amepata mchongo kwa mara ya kwanza na kuiuza bidhaa ya urembo ambapo amesainiwa kuwa kisura kwenye perfume ya Givenchy.
Kwa mujibu wa WWD, mwimbaji huyo ataanza kuonekana kwenye perfume hiyo kuanzia Setember mwaka huu.View image on Twitter
So proud to be part of the @ParfumsGivenchy family! Much love & Divine energy! Love forever, Alicia

Maana ya wimbo mpya wa Victoria Kimani aliowashirikisha Ommy Dimpoz na Diamond 'Prokoto' unatoka May 14Mwimbaji wa label ya Chocolate City, Victoria Kimani amewashirikishwa Ommy Dimpoz na Diamond kwenye wimbo wake anaotarajia kuuachia May 14, unaitwa bokodo ‘Prokoto’.
Wakali hao wameutengeneza wimbo huo kwa kuunganisha lugha mbili ambazo ni Kiswahili na Kiingeza ili kutengeneza kitu ambacho kuwashika mashabiki wao kwa ujumla.
Prokoto haina maana ila ni neno tu la kutunga ambalo limetumika kama alivyozoea kufanya Dully Sykes kwenye nyimbo zake nyingi.
“Prokoto ni jina la kubuni tu ambalo itakuwa style mpya ya uchezaji, watu wataona itakavyotoka video ambayo tunatarajia kushoot very soon.” Ommy Dimpoz ameiambia Bongo5.
Ommy Dimpoz ameeleza kuwa ‘Prokoto’ ni wimbo mkali sana wa kuchezeka ambao anaamini kwa kutumia lugha hizo mbili wimbo huo utaishika Afrika nzima.
Victoria Kimani yuko Tanzania na inawezekana akawa anaendelea na mchakato wa kushoot video ya Prokoto..

MIRROR AFANYA COLLABO NA CHAMELEONE MIRROR AFANYA COLLABO NA CHAMELEONEMsanii wa muziki wa kizazi kipya nchini kutoka kampuni ya Endless Fame Films iliyopo chini ya Wema Sepetu, Mirror amefanya collabo na msanii mkubwa Afrika Mashariki  Jose Chameleone ambapo hivi karibuni itakamilika.

Wawili hao wamerekodi wimbo huo kwenye studio za AM Records chini ya producer Manecky Jumapili iliyopita 

Mirror ameiambia Pro-24 Blog kuwa alifanikiwa kumpata Chameleone na kumshirikisha kwenye wimbo wake huo baada ya kukutanishwa na meneja wake (Mirror) waliyekutana na Chameleone kwenye tuzo za KTMA zilizofanyika Jumamosi kwenye ukumbi wa Mlimani City. 

Amesema kesho yake alifanikiwa kumsikilizisha baadhi ya nyimbo zake na Chameleone akamshauri warekodi wimbo mpya kabisa. 

“Kila kitu tumeshamaliza ni wimbo unasubiri kufanyiwa finishing tu uwe tayari,” amesema. 

“ I am so happy kwanza ni ndoto yangu kwasababu Chameleone ni msanii mkubwa ambaye mimi nimeanza kumwangalia, kumsikiliza tokea niko mdogo so nilikuwa na dream kufanya naye kazi siku moja. Nafikiri na yeye pia amenikubali kama ni msanii mchanga ambaye ndio ninatoka sasa hivi. I am so proud kwanza kufanya nyimbo naye na nyimbo ni kali, watu wategemee kitu kikubwa sana,” amesema Mirror.

Saturday, 3 May 2014

Masaa machache kabla ya KTMA 2014, tuzo za tatu kwa ukubwa Afrika, nani mshindi? 'Itafahamika leo'


Dakika zinahesabika kabla tukio zima la utoaji tuzo za muziki za Tanzania, Kilimanjaro Tanzania Music Awards 2014 lianze kushuhudiwa na mashabiki wengi waliopiga kura huku joto likipanda kwa baadhi ya wasanii, nani atashinda tuzo katika kipengele husika?
Swali hilo litajibiwa masaa machache yajayo ambapo kila kipengele kitasomwa na mshindi atatajwa huku tukisubiri kuona nani ataondoka na vikombe vingi zaidi (trophies).
Tuzo hizi ni muhimu sana kwa kila msanii aliyetajwa kwenye kipengele husika kwa kuwa ni tuzo kubwa zinazoshika nafasi ya tatu Afrika kwa kuzingatia kuwa nafasi ya kwanza inashikwa na KORA, nafasi ya pili ni tuzo za MAMA (MTV Africa Music Awards).
Kama ilivyo kawaida, tuzo hizo zitapambwa na burudani ya kipekee kutoka kwa wasanii mbalimbali.
 Akiongea katika kipindi cha Sun Rise cha 100.5 Times Fm, Meneja wa bia ya Kilimanjaro, George Kavishe aliahidi kuwa kutakuwa na burudani ya kipekee hata zaidi ya ile ya mwaka jana iliyokuwa gumzo pale wasanii wakongwe walipoimba nyimbo za wasanii wa kizazi kipya huku wasanii wa kizazi kipya wakiperform nyimbo za wasanii wakongwe.
Utoaji wa tuzo hizo utaoneshwa Live kupitia vituo vitatu vya runinga chini na kupitia tovuti ya Kilimanjaro Premium Lager.
Mitandao ya kijamii pia itakuwa sehemu kubwa ya media. Fuatilia Times Fm katika Twitter  @timesfmtz na katika instagram @timesfmtz ama Facebook Times Fm Tz.