Sunday 26 January 2014

JUAN MATA: NI RASMI, NI MCHEZAJI MANCHESTER UNITED

KUTAMBULISHWA RASMI JUMATATU JIONI!!

MOYES_n_MATA-1Juan Mata amekamilisha Uhamisho wa Dau la Pauni Milioni 37.1 kutoka Chelsea kwenda Manchester United.
Jana Mata alipimwa Afya yake huko Manchester na kusaini Mkataba unaoaminika kuwa unamalizika Juni 2018.
Mata, Miaka 25, anatarajiwa kucheza Mechi yake ya kwanza hapo Jumanne Uwanjani Old Trafford na Cardiff City kwenye Mechi ya Ligi Kuu England.
Akiongea baada ya kusaini Mkataba, Mata alisema: “Umefika wakati wa changamoto nyingine. Nimefurahi mno kuwa sehemu ya awamu nyingine ya historia ya Klabu hii.”
Aliongeza: “Chelsea ni Klabu kubwa na nia Marafiki wengi kule lakini huwezi kuikataa nafasi ya kujiunga na Manchester United. Ninatarajia kumsaidia Meneja na Timu kupata mafanikio zaidi katika Miaka ijayo!”
Mata anakuwa Mchezaji wa pili kusainiwa na Meneja David Moyes baada kumsaini Marouane Fellaini kutoka Everton  Mwezi Septemba kwa Dau la Pauni Milioni 27.5.
Pia, kwa kumsaini Mata, Man United imevunja Rekodi yao ya kusaini Mchezaji kwa Bei ya juu ambayo iliwekwa Mwaka 2008 walipomsaini Dimitar Berbatov kwa Pauni Milioni 30.
Mata atatambulishwa rasmi kama Mchezaji mpya wa Man United Jumatatu Saa 10 na Nusu Jioni, Saa za Tanzania.

WASIFU:
Jina: Juan Manuel Mata GarcĂ­a
Kuzaliwa: 28 Aprili 1988 (Miaka 25)
Namba ya Jezi: 10

No comments:

Post a Comment