Wednesday 26 February 2014

LIGI YA MKOA WA KATAVI YAMALIZIKA; ZAWADI ZAKABIDHIWA

by rahim kassonga (La Captain)

Ligi ya mkoa wa katavi imemalizika hii leo, kwa mchezo mmoja ambao ulikuwa wa kukamilisha ratiba baada ya jana timu ya Mpanda United kuibuka bingwa wa ligi hiyo baada ya kufikisha jumla ya point 10 katika ligi ndogo ya mzunguko wa pili ambayo ilikuwa na jumla ya timu tano.

kombe la bingwa wa mkoa

kaimu katibu mkuu wa karefa (katikati ) akiwa na mgeni rasmi Galius Mgawe
 Katika mchezo wa leo ambao uliwakutanisha Majalila FC toka Ifukutwa  na timu ya Mbugani ya Kakese, Mbugani waliendelea kuthibitisha kuwa vibonde wa mzunguko wa pili baada ya kukubali kipigo cha goli 4 -0.


kocha wa majalila akitoa maelekezo kwa wachezaji wake
 Magoli ya Majalila leo yalifungwa na WEMA SADOCK  aliyefunga magoli 2 ktk dakika ya 27 na 55, wakati mengine yalifungwa na MAULID SAID dk 47 na HILALI SAID 86.


mchezaji wa majalila akipiga faulo

mashabiki wakifurahia burudani ya mpira
 Mbugani walipata penati katika dk za mwishoni za mchezo lakini katika hali isiyotegemewa jalala MAULID alipaisha penati hiyo na kuifanya mbugani kushindwa kupata hata goli moja katika mzunguko wa pili ikiruhusu magoli 15 baada ya kufungwa 5 na timu za majalila na Polisi Katavi goli 1 dhidi ya Mpanda Utd na magoli 4 dhidi ya Majalila


wachezaji wa mbugani wakiwa wamekata tamaa baada ya kukosa penati
 Baada ya mchezo ya mchezo huo timu zote zilikabidhiwa mpira mmoja mmoja na bingwa kukabidhiwa kikombe na mgeni rasmi GALIUS MGAWE ambaye pia ndio aliyetoa zawadi hizo
kapteni wa mbugani akipokea zawadi kutoka kwa mgeni rasmi

shije luvinza kapeni wa majalila akipokea mpira 

mwakilishi wa washindi wa pili timu ya makanyagio akipokea mpira

mwakilishi wa polisi akipokea mpira

mwakilishi wa mpanda united akipokea mpira


Geofrey Augustino maarufu kama KANYOKA akiwa amebeba kombe la ubingwa wa mkoa
MSIMAMO WA LIGI YA KATAVI MZUNGUKO WA PILI

1
MPANDA UNITED
10
2
POLISI KATAVI
7
3
MAKANYAGIO FC
5
4
MAJALILA FC
4
5
MBUGANI FC
0
kapteni wa mpanda united akipokea kombe toka kwa mgeni rasmi

No comments:

Post a Comment